Kitambulisho cha Matangazo

Kitambulisho cha matangazo ni kitambulisho cha kipekee, kinachoweza kubadilishwa na kufutwa na mtumiaji kwa ajili ya kutangaza. Kitambulisho hiki kinatolewa na Huduma za Google Play. Kitambulisho hiki huwapa watumiaji udhibiti bora na kuwapa wasanidi programu mfumo rahisi, ili waendelee kuchuma mapato ya programu zao. Huwawezesha watumiaji kuweka upya au kufuta kitambulishi chao

Sasisho la huduma za Google Play la mwaka 2021

Kama sehemu ya sasisho la Huduma za Google Play mwishoni mwa 2021, kitambulisho cha matangazo kitaondolewa mtumiaji anapofuta kitambulisho cha matangazo katika mipangilio ya Android. Majaribio yoyote ya kufikia kitambulishi yatapokea mifuatano ya sufuri badala ya kitambulishi. Ili kusaidia wasanidi programu na watoa huduma za matangazo/takwimu katika juhudi za kutii na kuheshimu chaguo la mtumiaji, wataweza kupokea arifa za ufutaji wa kitambulisho cha matangazo. Ikiwa ungependa kujaribu mfumo wa arifa uliotajwa, jaza fomu hii.

Hatua hii ya kusambaza huduma za Google Play itaathiri programu zinazotumika kwenye vifaa vya Android 12 kuanzia mwishoni mwa mwaka 2021 na itaendelea kuathiri programu zinazotumika kwenye vifaa vyote vinavyotumia Google Play kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022. Kwa hali za matumizi muhimu yasiyo ya matangazo kama vile takwimu na uzuiaji wa ulaghai, tumia Kitambulisho cha Kundi la Programu.

Pia, programu zikisasisha mifumo inayolenga kuwa Android 13 au mifumo ya baadaye itatakiwa kubainisha ruhusa ya kawaida ya huduma za Google Play kwenye faili ya maelezo kama ifuatavyo:

<uses-permission android:name="com.google.android.gms.permission.AD_ID"/>

Baadhi ya SDK, kama vile Google Mobile Ads SDK (play-services-ads) huenda tayari zimetangaza ruhusa hii kwenye faili ya maelezo ya maktaba ya SDK. Ikiwa programu yako inatumia SDK hizi kama vitegemezi, ruhusa ya AD_ID kwenye faili ya maelezo ya maktaba ya SDK itaunganishwa na faili kuu ya maelezo ya programu yako kwa chaguomsingi, hata kama hutatangaza ruhusa hii moja kwa moja kwenye faili kuu ya maelezo ya programu yako. Pata maelezo zaidi kuhusu uunganishaji wa faili za maelezo kwenye Tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Ruhusa hii itatekelezwa kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022 kwa vifaa vyote. Angalia hati ya API ili upate maelezo zaidi.

Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu bora za vitambulishi mahususi.

Kupata kitambulisho cha matangazo

Ili upate kitambulisho cha matangazo katika programu zako, unaweza kutumia API ya Kitambulisho cha matangazo.

Masharti ya sera

Sera ya Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play inahitaji kuwa masasisho yote na programu mpya zinazopakiwa kwenye Google Play zitumie kitambulisho cha matangazo (kinapopatikana kwenye kifaa) badala ya vitambulishi vyovyote vingine kwa madhumuni yoyote ya matangazo. Una wajibu wa kuhakikisha kwamba programu zako zinatii sera zinazohusu matumizi yake, pamoja na sera zote za Google Play.

Programu zinazoendelea kutumia kitambulisho kingine tofauti na kitambulisho cha matangazo huenda zikapokea onyo la ukiukaji wa sera kupitia tovuti ya mchapishaji au anwani ya barua pepe iliyotumika kusajili akaunti. Ukipokea onyo, lazima uhakikishe kwamba APK zozote zilizochapishwa zinatii mwongozo unaohusiana na kitambulisho cha matangazo wa Sera ya Mpango wa Wasanidi Programu. Kama unatumia SDK ya tangazo ya masoko mengine, tafadhali wasiliana na mtengenezaji wa SDK ili upate toleo jipya ambalo linatii sera hii mpya.

Maelezo ya ziada

Kunja Zote Panua Zote

Vitambulishi vingine, vikiwemo Kitambulisho cha Android

Upatikanaji

Vitambulishi vingine bado vinapatikana kwa sababu kuna matukio mbalimbali ya matumizi ambayo hayahusiani na utangazaji. Kama mpango wa muda mrefu, tutatathmini fursa za ziada ili kuwapa watumiaji udhibiti wenye maelezo zaidi juu ya vitambulishi gani vingine ambavyo hutolewa kwa watu au mashirika mengine. Tutakutaarifu kuhusu hili kwa haraka na mapema tutakapokuwa na ufafanuzi.

Kwa madhumuni yasiyo ya matangazo

Unaweza kutumia vitambulishi vingine kama tu una sera ya faragha na unashughulikia data kwa mujibu wa Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu na sheria zote zinazotumika za faragha katika maeneo unayosambaza programu zako.

Kulenga vifaa visivyo na kitambulisho cha matangazo

Wakati kitambulisho cha matangazo hakipo, programu yako inaweza kurejea kutumia kitambulishi kingine au unachokimiliki, alimradi:

Ukiukaji wa Kitambulisho cha matangazo

Tafadhali thibitisha ikiwa programu kwenye orodha yako zinatii mwongozo wa sera ya kitambulisho cha matangazo. Wasanidi programu wataarifiwa kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa ukiukaji kupitia arifa ya tahadhari katika Dashibodi ya Google Play au maonyo ya barua pepe yatakayotumwa kwenye anwani ya barua pepe iliyotumika kusajili akaunti ya msanidi programu.

Ikiwa una maswali ya ziada, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu ukiukaji wa sera ya kitambulisho cha matangazo.

Kubadilisha kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako
  1. Kwenye kifaa chako cha Android, nenda kwenye Mipangilio.
  2. Gusa Faragha > Matangazo.
  3. Gusa Badilisha kitambulisho cha matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.
Kufuta kitambulisho cha matangazo cha kifaa chako
  1. Kwenye kifaa chako cha Android, nenda kwenye Mipangilio.
  2. Gusa Faragha > Matangazo.
  3. Gusa Futa kitambulisho cha matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.

Kidokezo: Kitambulisho chako cha matangazo kitafutwa lakini programu zinaweza kuwa na mipangilio yake inayoweza kuathiri aina za matangazo unayoona.

Kwenye baadhi ya matoleo ya zamani ya Android
  1. Fungua Mipangilio.
  2. Gusa Faragha > Mipangilio ya KinaMatangazo
  3. Washa Jiondoe kwenye Mipangilio ya Kuweka Mapendeleo ya Matangazo kisha uthibitishe mabadiliko uliyofanya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6908857047781001975
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false