Kupokea arifa za utendaji

Kwenye toleo la wavuti la Dashibodi ya Google Play, unaweza kufuatilia utendaji wa programu yako kupitia arifa.

Jinsi ya kupokea arifa

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Bofya Mipangilio Arifa.
  3. Chagua ambacho ungependa uarifiwe kuhusu kisha ubofye visanduku.
  4. Bofya Hifadhi katika kona ya chini kulia ya ukurasa.

Arifa za programu

Arifa zinatokana na takwimu za programu yako. Ikiwa kuna badiliko kubwa katika viashirio vya utendaji wa programu yako, utapokea barua pepe.

Aina za arifa
Arifa Maelezo
Maoni
  • Programu yako inapopata maoni mapya.
Maoni yaliyosasishwa
  • Mtumiaji anaposasisha maoni ukishayajibu.
ANR na matukio ya programu kuacha kufanya kazi
  • Mabadiliko makubwa katika kundi la ANR au matukio ya programu kuacha kufanya kazi yanapotambuliwa.
Android vitals 
  • Mabadiliko makubwa ya Android vitals yanapotambuliwa.

Arifa kuhusu Huduma za Michezo ya Google Play

Kama ukipokea arifa ya Huduma za Michezo kwenye Google Play, inaweza kuhitaji kwa upande wako uchukue hatua fulani.

Aina za arifa za Huduma za Michezo
Arifa ya Google Maelezo
Matumizi mabaya ya kipengele yamegunduliwa
Kikomo cha ukadiriaji kimepitwa kwa Huduma ya mchezo kwa jina la_mbinu
  • Mchezo wako unatekeleza idadi kubwa kuliko kawaida ya utekelezaji wa API ya huduma za michezo na una kikomo cha ukadiriaji kwa baadhi ya wachezaji.
  • Pata maelezo zaidi kuhusu kutambua kikomo cha ukadiriaji ili uhakikishe kuwa vipengele vya mchezo kama vile mafanikio, alama au mechi vinafanya kazi bila tatizo na upunguze matumizi ya betri ya mchezo wako.
Mchezo wako unakaribia kupita au unapita kikomo cha idadi ya kila siku
  • Mchezo wako unakaribia kupita au unapita kikomo cha idadi ya maombi ya API ya kila siku kwa mchezo.
  • Jambo la kawaida zaidi linalosababisha hili ni urudiaji wa kutekeleza API za huduma za michezo. Angalia na udhibiti kikomo cha idadi ya kila siku ili kuepuka kupita kikomo hiki.
Mipangilio ya mchezo haijachapishwa
  • Ulibainisha mipangilio ya huduma zako za michezo lakini haijachapishwa.
  • Chapisha mabadiliko uliyofanya ili hali za mchezo na vipengele vifanye kazi na kuonekana inavyotarajiwa.
Kitambulisho kisicho sahihi kililichotumiwa kwa (mafanikio | bao za wanaoongoza)
  • Arifa hii huonyeshwa wakati mchezo wako unajaribu kufikia API ya mchezo kwa kutumia kitambulisho cha nyenzo kisicho sahihi.
  • Utekelezaji wa kitambulisho sahihi utahakikisha kuwa kipengele cha mchezo kitaonyesha data sahihi ya mchezaji anapofungua mafanikio au kutoa alama.
  • Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka mipangilio ya ubao wa wanaoongoza na mafanikio.
Nakala za picha
  • Arifa hii huonyeshwa wakati mchezo wako unatumia picha sawa mara nyingi kwenye mafanikio au mbao za wanaoongoza.
  • Ni ufanisi zaidi kutumia picha tofauti ili kutofautisha mafanikio na pau za wanaoongoza.
Utekelezaji usio sahihi umetambuliwa Wachezaji Wengi katika Wakati Halisi au Wachezaji Wengi kwa Zamu: Mchezo huu umeweka mialiko lakini hauruhusu watumiaji kujiunga kwenye mechi kwa kutumia mwaliko. Mbinu hii haipendekezwi kwa sababu inaweza kusababisha hali duni ya utumiaji.

Mafanikio: Mchezo huu umeweka mafanikio katika Dashibodi ya Google Play lakini hautumii mbinu za kufungua SDK. Mbinu hii haipendekezwi kwa sababu inaweza kusababisha hali duni ya utumiaji.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14937087613555641522
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false