Ongeza au ujaribu faili za upanuzi za APK

Kuanzia Agosti 2021, programu mpya zitatakiwa kuchapishwa kwa kutumia Android App Bundle kwenye Google Play. Programu mpya zenye ukubwa wa zaidi ya MB 200 zinaweza kutumia Play Asset Delivery au Utumaji wa Vipengele vya Google Play.

Kuanzia tarehe 30 Juni 2023, Google Play haitaruhusu tena masasisho ya programu ya televisheni kwa kutumia APK. Masasisho yote ya programu ya televisheni lazima yachapishwe kwa kutumia Android App Bundle (AAB).

Ili upate maelezo zaidi, soma makala ya Mustakabali wa Android App Bundles umewadia, kwenye Blogu ya Wasanidi Programu wa Android.

Kama programu yako inahitaji hifadhi ya zaidi ya MB 100, unaweza kutumia faili za upanuzi ili kuhifadhi vipengee zaidi vya APK. Unaweza kuhifadhi faili mbili za upanuzi kwa kila programu. Kila faili ya upanuzi inaweza kuwa na ukubwa usiozidi GB 2.

Faili za APK zina kiwango cha juu cha ukubwa wa faili, kulingana na toleo la Android ambalo APK yako hutumia:

  • MB 100 - APK zinazolenga Android toleo la 2.3 na matoleo mapya zaidi (Kiwango cha API cha 9-10 na 14 na juu zaidi)
    • Ni sharti watumiaji wawe na toleo la programu ya Duka la Google Play la 5.2 au toleo jipya zaidi ili kusakinisha APK za MB 100.

Faili za upanuzi hupangishwa bila gharama ya ziada. Panapowezekana, Google Play hupakua faili za upanuzi wakati programu zinasakinishwa au kusasishwa. Katika baadhi ya matukio, programu yako itahitaji kupakua faili zake za upanuzi.

Ikiwa ukubwa uliobanwa wa APK yako (ikiwa ni pamoja na faili za upanuzi) unazidi MB 200 wakati wa kupakua, watumiaji wataona kidirisha chenye tahadhari inayowapendekezea watumie Wi-Fi kupakua programu yako.

Kidokezo: Kwa kuchapisha programu yako ukitumia Android App Bundle, unaweza kuunda na kuwasilisha programu ndogo na zinazofaa zaidi ili watumiaji wazisakinishe.

Aina ya faili za upanuzi

Unapotumia faili za upanuzi, faili moja ndiyo faili kuu na nyingine ni faili ya ziada ya hiari. Faili za ziada za hiari kwa kawaida hutumika kwa masasisho madogo kwenye faili kuu.

Faili za upanuzi zinaweza kuwa aina yoyote ya faili na huhifadhiwa kwenye eneo la hifadhi inayoshirikiwa (kwa mfano: Kadi ya SD au sehemu inayopachikwa kutumia USB) ambapo programu yako inaweza kuzifikia. Kila URL ya faili ya upanuzi inayotolewa ni ya kipekee kwa kila upakuaji.

Kudhibiti faili za upanuzi

Kuweka au kubadilisha faili za upanuzi

Unaweza kupakia faili za upanuzi mpya au uweke zilizopo kwenye APK katika toleo la rasimu.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu yako.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, nenda kwenye Toleo > Toleo la umma.
  4. Kwenye ukurasa wa Toleo la umma, utaona menyu kujunzi yenye "Programu za kawaida, Programu zinazofunguka papo hapo pekee na Ddhibiti aina za matoleo.
  5. Chagua Dhibiti aina ya toleo.
  6. Utaona orodha ya APK zinazohusishwa na toleo lako. Karibu na msimbo wa toleo husika, chagua aikoni ya kuweka
  7. Chagua kama unataka kupakia faili mpya au kuambatisha faili ya upanuzi iliyopo.
    • Ikiwa APK haijachapishwa, unaweza kubadilisha au kuondoa faili ya upanuzi kwa kuchagua faili nyingine au Hakuna faili ya upanuzi. Huwezi kuondoa faili za upanuzi kwenye toleo lililopo.
  8. Chagua Hifadhi.
Kuondoa faili za upanuzi

Huwezi kuondoa faili za upanuzi kwenye toleo lililopo. Ikiwa hutaki tena kujumuisha faili za upanuzi kwenye APK yako, unda toleo lenye APK mpya ambalo halina faili ya upanuzi.

Kwa APKs ambazo hazijachapishwa, unaweza kubadilisha faili za upanuzi wakati wowote.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play.
  2. Chagua programu yako.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, nenda kwenye Toleo> Matoleo ya programu.
  4. Karibu na aina ya toleo unalotaka kusasisha, nenda kwenye Dhibiti.
  5. Utaona orodha ya APK zinazohusishwa na toleo lako. Karibu na msimbo wa toleo husika, chagua aikoni ya kuweka
  6. Chagua kishale cha chini Kishale cha menyu kunjuzi.
  7. Chagua Hakuna faili ya upanuzi > Hifadhi.
Kujaribu faili za upanuzi

Kabla ya kuchapisha programu yako, hakikisha kuwa unajaribu utekelezaji wa faili ya upanuzi.

Huwezi kujaribu faili za upanuzi za APK kwa kutumia rasimu ya programu. Ili ujaribu faili za upanuzi za APK, sharti uchapishe APK yako kwenye toleo linalopatikana.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15557423352310605239
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false