Kugundua mapema matatizo kwenye programu kupitia ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa

Ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa hukusaidia kubaini matatizo yanayoweza kuwepo kwenye mabadiliko unayopanga kufanya kwenye programu yako, kabla ya kuyatuma ili yakaguliwe. Baadhi ya matatizo yanaweza kuwa makubwa na ni sharti yatatuliwe kabla uweze kutuma mabadiliko unayopanga kufanya ili yakaguliwe.

Muhtasari

Unaweza kupata kipengele cha ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji, katika sehemu ya "Mabadiliko ambayo bado hayajatumwa ili kufanyiwa ukaguzi". Unaweza tu kuona sehemu hii ikiwa umefanya mabadiliko kwenye programu yako tangu mara ya mwisho ilipotumwa ili kufanyiwa ukaguzi.

Ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa hufanywa kiotomatiki kila unapofanya mabadiliko kwenye programu yako. Unaweza kuangalia hali ya ukaguzi kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji, ila unapaswa kukumbuka yafuatayo:

  • Baadhi ya ukaguzi hufanywa kwa muda mrefu kuliko mwingine, kwa hivyo huenda ukaona muda unaokadiriwa ili ukaguzi ukamilike.
  • Si lazima usubiri hadi ukaguzi ukamilike ili uweze kutuma mabadiliko uliyotekeleza yafanyiwe ukaguzi. Unaweza kutuma mabadiliko wakati wowote na tutakamilisha michakato hii ya ukaguzi kabla ya kutuma mabadiliko uliyofanya ili yakaguliwe.

Matatizo yataonekana punde tu yanapogunduliwa. Bofya Angalia matatizo ili upate maelezo kuhusu kila tatizo.

Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wetu wa kukagua programu katika Chuo cha Google Play.

Angalia mfano ulio kwenye skrini wa ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa

Kudhibiti matatizo yanayotambuliwa

Tunafanya ukaguzi ili kubaini matatizo ya aina tofauti. Tutatoa maelezo kuhusu kila tatizo, pamoja na viungo ili kukusaidia kuyatatua au upate maelezo zaidi kuhusu mada husika. Unaweza kutatua matatizo moja kwa moja kwenye Dashibodi ya Google Play, huku matatizo mengine yakihitaji mabadiliko ya kiufundi kwenye programu yako, hali ambayo huenda ikahitaji kuwa ubuni na upakie toleo jipya la programu.

Baadhi ya matatizo ni sharti yarekebishwe ili uweze kuendelea. Mengine yanaweza kuahirishwa kwa kuchagua Puuza tatizo. Ili upuuze tatizo, ni sharti ufumbue sababu ya kufanya hivyo kwa kuchagua sababu moja au zaidi, kwa mfano, "Tayari nina mipango ya kutatua tatizo hili" au "Tatizo hili si sahihi." Maelezo haya yatawekwa kwenye Kumbukumbu ya shughuli na tutatumia jibu lako kusaidia kuboresha hali ya kutegemewa kwa shughuli zetu za ukaguzi.

Jibu lako halitaathiri matokeo ya ukaguzi wa programu yako, lakini ikiwa tatizo linafanya programu isifanye kazi, huenda programu yako ikakataliwa wakati wa ukaguzi kwa kutotii sera za Google Play zinazohusiana na ubora wa programu (kama vile sera ya Utendakazi wa Chini Zaidi).

Ukipuuza matatizo bila kuyatatua baadaye, huenda yakatokea tena siku zijazo.

Angalia mfano ulio katika skrini wa tatizo lililotambuliwa

Ruhusa zinazohitajika ili kupuuza matatizo

Ni watumiaji walio na mojawapo ya ruhusa hizi pekee ndio wanaoweza kupuuza matatizo:

Hizi ni ruhusa zile zile zinazotumiwa katika vipengele vingine kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji, ikiwa ni pamoja na uchapishaji unaodhibitiwa, ili usilazimike kubadilisha ruhusa za watumiaji ulizokabidhi kwa sasa.

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini mnaweka mchakato huu mpya wa ukaguzi?

Tunataka kukupa maoni ya mapema kuhusu matatizo yoyote hatari kwenye mabadiliko uliyopanga kufanya ili kuhakikisha kuwa programu yako inafanya kazi vizuri kwa watumiaji. Pia, ukaguzi huu unakusaidia kuepuka makosa ya kawaida yanayoweza kusababisha mabadiliko yakataliwe wakati wa ukaguzi.

Je, michakato hii ya ukaguzi ni mipya?

Huwa tunafanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa programu zinatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu na kwamba zinafanya kazi vyema kwenye vifaa vya watumiaji. Sasa tunaonyesha baadhi ya matatizo haya mapema kwenye Dashibodi ya Google Play, pamoja na baadhi ya ukaguzi mpya kabisa wa ubora, kama vile matatizo ya uoanifu wa programu kwenye matoleo mapya kabisa ya Android, ili uokoe muda.

Je, michakato ya ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa ni sawa na mchakato uliopo wa kukagua programu?

Hapana. Ukaguzi huu hufanywa kabla ya programu yako ufanyiwe mchakato wa ukaguzi

Je, ni ukaguzi upi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa hutekelezwa?

Tunafanya baadhi ya ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa kwenye programu yako. Baadhi ya mifano ya ukaguzi ni pamoja na kuhakikisha masasisho yako yana maelezo yote muhimu ndani ya ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera na mipango > Maudhui ya programu) na kubaini idadi ya juu ya matukio ya programu kuacha kufanya kazi kwenye baadhi ya vifaa au matoleo ya Android.

Je, ukaguzi huu huchukua muda gani?

Mchakato yote ya ukaguzi huchukua muda usiozidi dakika 15 kupata matokeo lakini kwa kawaida huchukua muda mfupi zaidi. Unaweza kuchagua Tuma ili ikaguliwe wakati michakato ya ukaguzi inaendelea na bado hatujapata tatizo lolote. Tutamaliza kufanya ukaguzi na kutuma mabadiliko uliyofanya kiotomatiki ili yakaguliwe ikiwa hatutapata matatizo yoyote.

Je, ukaguzi huu unafanya kazi vipi kupitia API?

Kwa sasa, michakato mingi ya ukaguzi inafanywa tu kwenye tovuti ya Dashibodi ya Google Play, huku kikundi kidogo kikifanywa kupitia API. Ukaguzi unaoleta matokeo karibu papo hapo utafanywa kupitia API, lakini ule unaochukua muda mrefu hauwezi kufanywa kupitia API.

Je, ninaweza tu kuchagua kupuuza matatizo yote?

Hapana, unahitaji kufanya baadhi ya ukaguzi ili uweze kuchapisha kwenye Google Play na huwezi kuupuuza. Mifano ni pamoja na kukosekana kwa maelezo ya maudhui ya programu na taarifa nyingine kuhusu programu yako.

Je, mnatumia vipi majibu ninayochagua baada ya kupuuza tatizo?

Tutatumia majibu haya kutusaidia kuelewa ikiwa tumefanya kila kitu kwa usahihi au ikiwa tumekosea ili kuboresha hali ya kutegemewa kwa shughuli zetu za ukaguzi na kuelewa jinsi unavyochukulia michakato hii ya ukaguzi. Jibu lako halitaathiri matokeo ya ukaguzi wa programu yako, lakini ikiwa tatizo linafanya programu isifanye kazi, huenda programu yako ikakataliwa kwa kutotii sera za Google Play zinazohusiana na ubora wa programu (kama vile sera ya Utendakazi wa Chini Zaidi).

Iwapo nitafaulu michakato yote ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa, bado ninaweza kutofaulu mchakato wa ukaguzi wa programu?

Ndiyo, inawezekana ukafaulu ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa na bado usifaulu mchakato wa ukaguzi wa programu ambao ni wa kina zaidi kuliko michakato ya ukaguzi unaofanywa kabla ya programu kukaguliwa tunaoonyesha moja kwa moja kwenye Dashibodi ya Google Play.

Ni nini hufanyika ikiwa nitatuma mabadiliko ili yakaguliwe kabla ya mchakato wa ukaguzi kukamilika?

Mchakato wa ukaguzi utaendelea kufanywa na mabadiliko uliyofanya yatatumwa kiotomatiki ili yakaguliwe baada ya ukaguzi kukamilika, mradi hakuna matatizo hatari yatakayotambuliwa.

Je, matatizo yote yanayotambuliwa huwa sahihi?

Tunajitahidi kupata usahihi, lakini baadhi ya matatizo huenda yasiwe sahihi kutokana na hali zao za kiufundi. Unaweza kupuuza matatizo haya na uchague sababu inayofaa ili utupatie maoni.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11713486178093631133
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false