Ukaguzi wa Mapema: Tabia Danganyifu

Toleo Tangulizi la sera (kuanzia Tarehe 31 Agosti, 2024)

Makala haya yanatanguliza mabadiliko katika masasisho ya Aprili 2024 ya sera yetu.

Tunasasisha sera dhidi ya Maudhui ya Hila ili kujumuisha sauti kama mfano wa ziada wa aina ya maudhui yanayodhibitiwa na sera hii.

Ili uangalie makala ya sasa ya "Tabia Danganyifu," tembelea ukurasa huu.

Haturuhusu programu zinazojaribu kuwapotosha watumiaji au kuendeleza mienendo isiyo ya kweli ikiwa ni pamoja na programu zilizobainishwa kuwa haziwezi kufanya chochote. Ni lazima programu itoe ufumbuzi, maelezo na picha au video sahihi ya utendaji wake kwenye sehemu zote za metadata. Programu hazipaswi kujaribu kuiga utendaji au maonyo kutoka mifumo ya uendeshaji au programu zingine. Ni lazima mabadiliko yoyote ya mipangilio ya kifaa yafanywe baada ya kupata idhini ya mtumiaji na yawe rahisi kutenduliwa na mtumiaji.

 

KUNJA ZOTE PANUA ZOTE

Madai Yanayopotosha

Haturuhusu programu zilizo na maelezo au madai ya udanganyifu au yanayopotosha, ikiwa ni pamoja na maelezo, jina, aikoni na picha za skrini.
Mifano ya ukiukaji unaotokea sana
  • Programu zinazowakilisha kwa uongo au zisizobainisha kwa uwazi utendaji wake:
    • Programu inayoeleza kuwa ni mchezo wa mbio za magari katika maelezo na picha zake za skrini, lakini ni mchezo wa chemsha bongo unaotumia picha ya gari.
    • Programu inayodai kuwa ni programu ya kingavirusi, lakini iliyo na mwongozo wa maandishi pekee unaoelezea jinsi ya kuondoa virusi.
  • Programu zinazodai utendaji ambao hauwezi kutekelezwa kama vile programu za kufukuza wadudu, hata zikionyeshwa kama za mzaha, bandia, utani n.k.
  • Programu ambazo hazijapangwa vizuri, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, ukadiriaji au aina ya programu.
  • Maudhui yanayopotosha au ya udanganyifu yanayoweza kuathiri michakato ya kupiga kura au kuhusu matokeo ya uchaguzi.
  • Programu ambazo zinadai kwa njia ya udanganyifu kushirikiana na huluki ya serikali au kutoa au kutekeleza huduma za serikali ilhali hazijaidhinishwa kwa njia sahihi.
  • Programu zinazodanganya kuwa ni programu rasmi za huluki inayotambulika. Majina kama "Programu Rasmi ya Justin Bieber" hayaruhusiwi bila ruhusa au haki zinazohitajika.

(1) Programu hii ina madai ya matibabu au yanayohusiana na afya (Tibu Saratani) ambayo yanapotosha.
(2) Programu hizi zinadai utendaji ambao hauwezi kutekelezwa (kutumia simu yako) kama kifaa cha kupima pumzi.

 

Mabadiliko Danganyifu ya Mipangilio ya Kifaa

Haturuhusu programu zinazofanya mabadiliko ya mipangilio au vipengele vya kifaa cha mtumiaji nje ya programu bila mtumiaji kufahamu na kutoa ridhaa yake. Mipangilio na vipengele vya kifaa vinajumuisha mipangilio ya mfumo au kivinjari, alamisho, njia za mkato, aikoni, wijeti na upangaji wa programu kwenye skrini ya kwanza.

Zaidi ya hayo, haturuhusu:

  • Programu zinazorekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa kwa idhini ya mtumiaji lakini katika njia ambayo si rahisi kutenduliwa.
  • Programu au matangazo yanayorekebisha mipangilio au vipegele vya kifaa kama huduma kwa watu wengine au kwa madhumuni ya utangazaji.
  • Programu zinazopotosha watumiaji kuondoa au kuzima programu za wengine au kurekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa.
  • Programu zinazohimiza au kutoa motisha kwa watumiaji kuondoa au kuzima programu za wengine au kurekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa isipokuwa kama sehemu ya huduma ya usalama inayoweza kuthibitishwa.

 

Kuendeleza Mienendo Isiyo ya Kweli

Haturuhusu programu ambazo zinawasaidia watumiaji kuwapotosha wengine au zina utendaji danganyifu kwa njia yoyote, ikijumuisha: programu ambazo zinatengeneza au kusaidia kutengeneza kadi za vitambulisho, nambari za usalama wa jamii, pasipoti, vyeti, kadi za mikopo, akaunti za benki, na leseni za udereva. Lazima programu ziwe na maelezo sahihi ya ufumbuzi, mada, ufafanuzi na picha/video kuhusu maudhui na/au utendaji wa programu na zinapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na usahihi jinsi inavyotarajiwa na mtumiaji.

Nyenzo za ziada za programu (kwa mfano, vipengee vya mchezo) zinaweza tu kupakuliwa iwapo zinahitajika kwa matumizi ya watumiaji wa programu. Nyenzo zilizopakuliwa ni sharti zitii sera zote za Google Play na kabla ya kuanza kupakua, lazima programu iwatumie watumiaji kidokezo na ibainishe wazi ukubwa wa faili ya kupakuliwa.

Dai lolote kuwa programu inatumika kwa ajili ya "utani", "sababu za burudani" (au maneno kama hayo) halizuii programu kufuata sera zetu.

Mifano ya ukiukaji unaotokea sana
  • Programu zinazoiga tovuti au programu nyingine ili kufanya watumiaji wafichue taarifa za binafsi au za uthibitishaji.
  • Programu ambazo zinaonyesha nambari za simu, anwani (ambazo hazijathibitishwa au halisi) au taarifa zinazoweza kuwatambulisha watu au mashirika bila idhini.
  • Programu ambazo zina utendaji tofauti kulingana na jiografia ya watumiaji, vigezo vya vifaa au data nyingine ambayo mtumiaji anategema ambapo tofauti hizo hazijatangazwa kwa uwazi kwa watumiaji kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.  
  • Programu ambazo hubadilisha matoleo kwa kiasi kikubwa bila kumwarifu mtumiaji (k.m., sehemu ya ‘ni nini kipya’) na kusasisha ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Programu zinazojaribu kubadilisha au kufumba msimbo wa vitendo wakati wa ukaguzi.
  • Programu zilizo na faili za kupakuliwa zinazotokana na Mtandao wa Kuwasilisha Maudhui (CDN) ambazo hazimtumii mtumiaji kidokezo wala kubainisha ukubwa wa faili ya kupakuliwa kabla ya kupakua.

 

Maudhui Yaliyobadilishwa

Haturuhusu programu zinazotangaza au zinazosaidia kuanzisha maelezo au madai ya uongo au ya kupotosha yanayowasilishwa kupitia picha, sauti, video na/au maandishi. Haturuhusu programu zinazobainishwa kuwa zinaeneza au kuendeleza picha, video na/au maandishi ya kupotosha, ambazo zinaweza kusababisha madhara kutokana na tukio nyeti, siasa, masuala ya kijamii au mambo mengine yanayohusu umma.

Programu zinazobadilisha au kuathiri maudhui, zaidi ya marekebisho ya kawaida na yanayokubaliwa kwa uhariri kwa ajili ya ubora au ubayana, lazima zifumbue kwa udhahiri au ziweke alama maalum kwenye maudhui yanayobadilishwa iwapo mtu wa kawaida anaweza kukosa kuelewa kuwa maudhui yamebadilishwa. Hali maalum zinaweza kuwekwa kwa maslahi ya umma au tashtiti au bezo dhahiri.

Mifano ya ukiukaji unaotokea sana
  • Programu zinazomweka mtu mashuhuri kwenye maandamano wakati wa tukio nyeti la kisiasa.
  • Programu zinazotumia watu mashuhuri au maudhui kutoka kwenye tukio nyeti kutangaza uwezo wa kubadilisha maudhui ndani ya ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Programu zinazobadilisha klipu za maudhui ili kuiga matangazo ya habari.

    (1) Programu hii hutoa utendaji wa kubadilisha klipu za maudhui ili kuiga matangazo ya habari na kuweka watu maarufu kwenye klipu bila alama maalum.

 

Uwazi wa Utendaji

Utendaji wa programu yako unapaswa kuwa wazi kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji; usijumuishe vipengele vyovyote vilivyofichwa, visivyotumika au visivyoorodheshwa katika programu yako. Mbinu za kukwepa maoni ya watumiaji kuhusu programu haziruhusiwi. Huenda programu zikahitajika kutoa maelezo ya ziada ili kuhakikisha usalama wa watumiaji, uadilifu wa mfumo na utiifu wa sera.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1917057166570317689
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false