Masharti ya kuthibitisha kifaa kwenye akaunti mpya za msanidi programu

Kuanzia mwanzoni mwa 2024, wasanidi programu walio na akaunti mpya za kibinafsi watahitajika wathibitishe kwamba wanaweza kufikia kifaa halisi cha mkononi cha Android wakitumia programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play kabla ya kuifanya programu yao ipatikane kwenye Google Play.

Hii ni hatua muhimu katika juhudi zetu zinazoendelea za kuboresha imani na usalama wa mtumiaji kwa mabilioni ya watu ambao wanatumia Google Play. Kwa kuwahitaji wasanidi programu wathibitishe kuwa wanaweza kufikia kifaa cha Android, tunaweza kusaidia kuhakikisha kuwa wanaweza kujaribu programu zao ipasavyo kabla ya kuzifanya zipatikane kwa watumiaji. Hii itasaidia kuongeza ubora wa programu kwenye Google Play na kudumisha usalama wa watumiaji.

Kukamilisha uthibitishaji wa kifaa

  1. Ingia katika akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play (toleo la wavuti) kama mmiliki wa akaunti (yaani, ukitumia akaunti ya Google iliyotumiwa kufungua akaunti ya msanidi programu).
  2. Nenda kwenye Ukurasa wa kwanza.
  3. Tafuta jukumu la "Thibitisha kuwa unaweza kufikia kifaa cha mkononi cha Android" kisha ubofye Angalia maelezo.
  4. Changanua msimbo wa QR ili ufungue au uweke programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play kwenye kifaa ambacho ungependa kutumia ili ukamilishe uthibitishaji.
  5. Fungua programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play na uingie katika akaunti kama mmiliki wa akaunti.
  6. Chagua akaunti yako ya msanidi programu.
  7. Gusa Thibitisha kisha ufuate maagizo kwenye skrini.
  8. Baada ya kukamilisha uthibitishaji wa kifaa, jukumu la uthibitishaji wa kifaa cha mkononi halitaonyeshwa tena kwenye Ukurasa wa kwanza katika Dashibodi ya Google Play.

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini siwezi kuona akaunti yangu ya msanidi programu kwenye programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play?

Hii inaweza kuwa ni kwa sababu hukuingia kwa kutumia akaunti sahihi. Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti ukitumia Akaunti ya Google uliyotumia kufungua akaunti yako ya msanidi programu wa Google Play.

Je, ninaweza kutumia kifaa cha aina gani kukamilisha uthibitishaji wa kifaa?

Unaweza kutumia kifaa chochote halisi cha mkononi cha Android kisicho na idhini maalum ya kudhibiti ambacho kinatumia angalau mfumo wa uendeshaji wa Android 10.

Nina vifaa mbalimbali. Je, aina ya kifaa ninachotumia kuthibitisha huzingatiwa?

Unaweza kutumia kifaa chochote halisi cha mkononi cha Android kisicho na idhini maalum ya kudhibiti ambacho kinatumia angalau mfumo wa uendeshaji wa Android 10.

Je, maelezo ya kifaa changu hutumika vipi?

Tunataka kuhakikisha kuwa watu wanaosanidi programu za kutumiwa na watumiaji wa Google Play wana zana za kimsingi wanazohitaji ili wafanikiwe. Tunaweza pia kutumia baadhi ya maelezo ili kusaidia katika juhudi zetu za kuzuia matumizi mabaya.

Je, ninaweza kutumia kifaa kile kile ambacho nimetumia kuthibitisha akaunti tofauti ya msanidi programu?

Ndiyo, unaweza kutumia kifaa kimoja kuthibitisha akaunti nyingi.

Je, uthibitishaji huchukua muda gani?

Uthibitishaji wa kifaa kwa kutumia programu ya vifaa vya mkononi ya Dashibodi ya Google Play unapaswa kuchukua chini ya dakika moja.

Je, ni lazima kiwe kifaa chenye namba ile ile ya simu ya mkononi niliyoweka awali katika mchakato wa kujisajili?

Hapana, namba ya simu ya kifaa kilichotumiwa kuthibitisha haitumiki au kukusanywa kama sehemu ya uthibitishaji wa kifaa.

Je, nitahitajika kuweka kifaa hiki ili kiweze kuthibitishwa tena katika siku zijazo?

Hapana. Tunaweza kukuomba uthibitishe siku zijazo, lakini hutalazimika kutumia kifaa hichohicho.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5512979810744577448
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false