Kuandikisha programu yako kwenye mfumo mbadala wa utozaji

Mipangilio hii inatumika tu ukishafanya uhamishaji ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji. Iwapo hauko tayari kujijumuisha kwenye API za mfumo mbadala wa utozaji, endelea kufanya mabadiliko kwenye hali yako ya kujiandikisha kupitia fomu ya kujiandikisha badala ya kupitia Dashibodi ya Google Play.

Huku chaguo zetu za mfumo mbadala wa utozaji zikiendelea kupanuka na kubadilika, tumeanza kuwapa wasanidi programu mipango kadhaa ili kuwezesha mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji. Kama sehemu ya mchakato wa kujiunga, ni lazima uandikishe programu yako kupitia Dashibodi ya Google Play. Mchakato huu unahusisha kutambua programu, nchi au maeneo yanayostahiki ambako utakuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji na aina ya mpango unaotaka kuutumia.

Muhtasari

Unaweza kudhibiti programu ambazo zimeandikishwa na kujumuishwa ili kutumia chaguo za mfumo mbadala wa utozaji na kuchagua kutoka katika mipango iliyopo kuligana na kila programu kwa kila soko linalostahiki kwenye ukurasa wa Mfumo mbadala wa utozaji (Weka mipangilio ya > Mfumo mbadala wa utozaji) kwenye Dashibodi ya Google Play.

Pata maelezo zaidi kuhusu chaguo za mfumo mbadala wa utozaji kwenye Google Play.

Kuandikisha programu yako

Ili uandikishe programu yako, lazima kwanza ukamilishe hatua za kuanza mchakato kujiunga za mfumo mbadala wa utozaji zinazohitajika kama ilivyobainishwa ndani ya kila mpango husika.

Kabla hujaanza:

  • Soma makala haya kwa umakini ili uhakikishe kuwa unafahamu kwa kina mipango yetu ya chaguo mbadala la utozaji.
  • Kabla ya kuuza usajili kupitia chaguo za mfumo mbadala wa utozaji, hakikisha kuwa maelezo yako ya mawasiliano yamesasishwa kwa kila programu.
  • Baadhi ya vipimo vya kuripoti vinapatikana tu kwa miamala ya mfumo wa utozaji wa Google Play. Huenda tusingeweza kutoa vipengele na vipimo fulani kwa kutumia data kutoka katika chaguo za mfumo mbadala wa utozaji.

Kuandikisha programu yako:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mfumo mbadala wa utozaji (Weka mipangilio > Mfumo mbadala wa utozaji).
  2. Tafuta programu unayotaka kuandikisha kisha ubofye Dhibiti kwenye jedwali. Hatua hii hufungua ukurasa wa mipangilio ya Uchumaji wa Mapato wa programu husika.
  3. Nenda chini hadi sehemu ya "Mfumo mbadala wa utozaji" kisha ubofye Weka chaguo la mfumo mbadala wa utozaji.
  4. Teua chaguo la utozaji:
    • Chaguo mbadala la utozaji: Teua chaguo hili ili uwapatie watumiaji chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play.
    • Mfumo mbadala wa utozaji pekee: Teua chaguo hili ili utoe mfumo mbadala wa utozaji unaojitegemea bila kutoa mfumo wa utozaji wa Google Play.
  5. Bofya + Nchi au eneo ili kuchagua nchi au maeneo yanayostahiki ambayo ungependa kutumia chaguo hili la malipo.
  6. Ukishamaliza kuchagua nchi au maeneo, bofya Tekeleza.
  7. Karibu na "URL ya udhibiti wa usajili," weka kiungo cha kudhibiti usajili, ambacho kinaweza kutolewa kwa watumiaji wanapoomba. Kiungo chako cha udhibiti wa usajili ndicho kitakachotumiwa na watumiaji ili kudhibiti mzunguko wa muda wa usajili ikiwa, kwa mfano, watahitaji kubadilisha mipangilio ya usajili wao. Ikiwa hupangi kuuza usajili, weka "Haitumiki".
    • Muhimu: Iwapo una viungo tofauti vya udhibiti wa usajili kwa kila nchi au eneo, ni lazima uandikishe programu yako iwe katika chaguo tofauti kwa kila nchi.
  8. Chaguo mbadala la utozaji pekee: Katika sehemu ya "Bango la njia za kulipa", toa bango la nembo zinazowakilisha njia za kulipa zinazotumiwa na chaguo la mfumo mbadala wa utozaji. Ikiwa tayari una bango, bofya ili uipakie au dondosha faili yako. Ikiwa huna, unaweza kubofya Pakua kiolezo cha bango la njia za kulipa.
  9. Chaguo mbadala la utozaji pekee: Chagua kisanduku cha kuteua cha "Njia za ziada za kulipa" ikiwa ungependa kuonyesha lebo ya "na zaidi" baada ya picha ya bango. Hii inaonyesha kuwa zaidi ya njia tano za kulipa zinatumika zikiwa ni pamoja na zile zilizo kwenye bango.
  10. Bofya Tekeleza.

Angalia maelezo na udhibiti mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji

Unaweza kudhibiti mipangilio yako ya mfumo mbadala wa utozaji ikijumuisha uandikishaji wa kiwango cha programu na maelezo ya wasifu, kwenye ukurasa wa Mfumo mbadala wa utozaji (Weka mipangilio > Mfumo mbadala wa utozaji).

Bofya sehemu inayofuata hapa chini ili uipanue au uikunje.

Angalia maelezo ya ankara ya mfumo mbadala wa utozaji wa kieneo

Ili kutazama maelezo ya ankara ya mfumo mbadala wa utozaji wa kieneo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mfumo mbadala wa utozaji (Weka mipangilio > Mfumo mbadala wa utozaji).
  2. Unaweza kuchagua kichupo ili uone maelezo ya malipo yanayohusiana na kichupo hicho, kama vile kiasi unachodaiwa, miamala, ankara na hati na mipangilio.

Kudhibiti mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji

Ili udhibiti mipangilio yako ya mfumo mbadala wa utozaji:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Mfumo mbadala wa utozaji (Weka mipangilio > Mfumo mbadala wa utozaji).
  2. Tafuta programu unayotaka kuandikisha kisha ubofye Dhibiti kwenye jedwali. Hatua hii hufungua ukurasa wa mipangilio ya Uchumaji wa Mapato wa programu husika.
  3. Teua chaguo la malipo:
    • Chaguo mbadala la utozaji: Teua chaguo hili ili uwapatie watumiaji chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play.
    • Mfumo mbadala wa utozaji pekee: Teua chaguo hili ili utoe mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji badala ya mfumo wa utozaji wa Google Play.
    • Si kwenye Mfumo mbadala wa utozaji: Teua chaguo hili ili urudi kwenye Malipo kupitia Google Play au kuacha kuchuma mapato kwenye programu yako katika nchi hizi mahususi.
  4. Bofya + Nchi au eneo ili uchague nchi au maeneo yanayostahiki ambayo ungependa kusasisha chaguo hili la malipo.
  5. Ukishamaliza kuchagua nchi au maeneo, bofya Tekeleza.
  6. Karibu na "URL ya udhibiti wa usajili", sasisha kiungo chako cha kudhibiti usajili ikihitajika, ambacho kinaweza kutolewa kwa watumiaji wanapoomba. Ikiwa hupangi kuuza usajili, weka "Haitumiki".
    • Muhimu: Iwapo una viungo tofauti vya udhibiti wa usajili kwa kila nchi au eneo, ni lazima uandikishe programu yako iwe katika chaguo tofauti kwa kila nchi.
  7. Chaguo mbadala la utozaji pekee: Katika sehemu ya "Bango la njia za kulipa", toa bango lililosasishwa la nembo zinazowakilisha njia za kulipa zinazotumiwa na chaguo la mfumo mbadala wa utozaji, ikihitajika.
  8. Chaguo mbadala la utozaji pekee: Chagua kisanduku cha kuteua cha "Njia za ziada za kulipa" ikiwa ungependa kuonyesha lebo ya "na zaidi" baada ya picha ya bango. Hatua hii inaonyesha kwamba njia zaidi za kulipa zinatumika pamoja na zile zilizo kwenye bango.
  9. Bofya Tekeleza.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6167925559393003018
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false