Masharti ya kujaribu programu kwa akaunti mpya binafsi za wasanidi programu

Mnamo Novemba 2023, tutabadilisha masharti ya kuchapisha programu mpya kwenye Google Play ili kuwasaidia wasanidi programu wafanyie majaribio programu zao, watambue matatizo, wapate maoni na kuhakikisha kwamba kila kitu kiko tayari kabla ya kuchapisha. Mabadiliko haya yatawataka wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa baada ya tarehe 13 Novemba 2023, watimize masharti mahususi ya kufanya majaribio kabla ya kuweza kuchapisha programu zao kwenye Google Play.

Makala haya yanatoa muhtasari wa masharti mapya, muhtasari wa vikundi tofauti vya kujaribu kwenye Dashibodi ya Google Play na hatua ambazo wasanidi programu walio na akaunti za binafsi watatakiwa kuchukua ili kuchapisha programu zao kwenye Google Play.

Tunakuletea masharti ya kufanya majaribio katika akaunti za binafsi zilizofunguliwa mpya

Kufanya majaribio ni sehemu muhimu ya mchakato wa kusanidi programu. Kwa kujaribu programu yako mara kwa mara, unaweza kuthibitisha usahihi wa programu yako, tabia ya utendaji na urahisi wa kutumiwa kabla ya kuichapisha hadharani. Hatua hii inapunguza athari ya matatizo yoyote ya kiufundi au ya hali ya utumiaji na inakusaidia uchapishe toleo bora zaidi la programu yako. Wasanidi programu wanaotumia mara kwa mara zana za kufanya majaribio za Dashibodi ya Google Play kabla ya kuchapisha programu zao wanaweza kutoa hali za utumiaji za ubora wa juu zinazoweza kusababisha ukadiriaji wa juu na mafanikio zaidi kwenye Google Play.

Ili kuwasaidia wasanidi programu wote watoe programu za ubora wa juu, tunaweka masharti mapya ya kufanya majaribio. Wasanidi programu walio na akaunti za binafsi zilizofunguliwa kabla ya tarehe 13 Novemba 2023, watatakiwa kufanyia majaribio programu zao kabla ya programu hizo kustahiki kuchapishwa ili kusambazwa kwenye Google Play. Vipengele fulani kwenye Dashibodi ya Google Play, kama vile Toleo la Umma (Chapisha > Toleo la Umma) na Kujisajili mapema (Chapisha > Kujaribu > Kujisajili mapema), vitazimwa hadi wasanidi programu watimize masharti haya.

Muhtasari wa masharti ya kufanya majaribio

Ikiwa umefungua akaunti mpya ya binafsi ya msanidi programu, lazima utekeleze jaribio la watumiaji mahususi kwenye programu yako na idadi ya chini zaidi ya wachunguzaji 20 waliojijumuisha kwa angalau siku 14 mfululizo zilizopita. Unapotimiza vigezo hivi, unaweza kutuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi kwenye Dashibodi katika Dashibodi ya Google Play ili uweze hatimaye usambaze programu yako kwenye Google Play. Unapoomba, ni lazima ujibu baadhi ya maswali ili kutusaidia tuelewe programu yako, mchakato wake wa kufanyiwa majaribio na iwapo ipo tayari kutolewa kwa umma.

Unaweza kusoma maelezo kuhusu aina tofauti za vikundi vya kufanya majaribio na masharti ya kila kikundi kwa kina zaidi hapa chini na upate maelezo zaidi kuhusu kutuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi.

Kuelewa vikundi tofauti vya kufanya majaribio na masharti yake

Dashibodi ya Google Play inatoa aina tofauti za vikundi vya kujaribu ili uweze kuzidisha kasi ya kufanya majaribio kwa utaratibu na uboreshe programu yako hadi iwe tayari kufikia mabilioni ya watumiaji kwenye Google Play.

  • Kufanya jaribio la ndani: Kabla hujamaliza kusanidi programu yako, unaweza kusambaza haraka miundo yake kwa kikundi kidogo cha wachunguzaji wako unaowaamini. Hatua hii inaweza kukusaidia utambue matatizo na upate maoni ya mapema. Kwa kawaida miundo hupatikana kwa wachunguzaji ndani ya sekunde chache baada ya kuwekwa kwenye Dashibodi ya Google Play. Si lazima ufanye jaribio la ndani, lakini tunapendekeza ufanye hivyo kwanza.
  • Kufanya jaribio la watumiaji mahususi: Katika kufanya jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kushiriki programu yako na kikundi kikubwa cha watumiaji unachodhibiti. Hatua hii inakuwezesha urekebishe matatizo na uhakikishe kwamba programu yako inatii sera ya Google Play kabla ya kuchapisha. Ni lazima utekeleze jaribio la watumiaji mahususi kabla ya kuomba kuchapisha programu yako kwa toleo la umma. Angalau wachunguzaji 20 lazima wajijumuishe kwenye jaribio lako la watumiaji mahususi unapoomba ufikiaji wa umma wakati wa usanidi. Lazima wawe wamejijumuisha kwa siku 14 mfululizo zilizopita. Unaweza kuanzisha jaribio la watumiaji mahususi baada ya kumaliza kusanidi programu yako.
  • Kufanya jaribio la watumiaji wengi: Linakuwezesha uchapishe toleo la kujaribu la programu yako kwenye Google Play. Ukitekeleza jaribio la watumiaji wengi, mtu yeyote anaweza kujiunga na mpango wako wa kujaribu na akupe maoni kwa faragha. Kabla ya kuteua chaguo hili, hakikisha kuwa programu na ukurasa wa programu yako katika Google Play viko tayari kuonekana kwenye Google Play. Unaweza kufanya jaribio la watumiaji wengi ukiwa na ufikiaji wa umma wakati wa usanidi.
  • Toleo la umma: Ambapo unafanya programu yako ipatikane kwa mabilioni ya watumiaji kwenye Google Play. Kabla hujaomba kuchapisha programu yako kwa toleo la umma, unahitaji kutekeleza jaribio la watumiaji mahususi ambalo linatimiza vigezo vyetu. Unapoomba, utahitaji pia kujibu maswali fulani kuhusu jaribio lako la watumiaji mahususi. Unapotuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi, angalau wachunguzaji 20 lazima wawe wamejijumuisha kwenye jaribio lako la watumiaji mahususi. Lazima wawe wamejijumuisha kwa siku 14 mfululizo zilizopita.
Muhtasari wa masharti ya kufanya majaribio kwa kila kikundi

Jedwali lililo hapa linaweza kukusaidia kuangalia au kurejelea haraka kazi ya kila kikundi na masharti (ikiwa yapo) ya kufikia kila kikundi.

Aina za vikundi Madhumuni Masharti ya kufikia kikundi hiki
Kufanya jaribio la ndani Ili usambaze haraka miundo kwa kikundi kidogo cha wachunguzaji wako unaowaamini ili utambue matatizo na upate maoni ya mapema (kabla au baada ya kumaliza kusanidi programu yako). Hamna.
Kufanya jaribio la watumiaji mahususi Ili ushiriki programu yako na kikundi kikubwa cha watumiaji unachodhibiti ili uweze kurekebisha matatizo na kuhakikisha kwamba programu yako inatii sera za Google Play kabla ya kuchapisha. Lazima uwe umemaliza kusanidi programu yako.
Kufanya jaribio la watumiaji wengi

Ili uchapishe toleo la kujaribu programu yako kwenye Google Play — mtu yeyote anaweza kujiunga na jaribio lako na akupe maoni ya faragha.

Lazima uwe umepata uwezo wa kuchapisha kwa toleo la umma ili ufikie jaribio la watumiaji wengi.
Toleo la umma Ili ufanye programu yako ipatikane kwa mabilioni ya watumiaji kwenye Google Play.

Kabla hujatuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi, lazima utekeleze jaribio la watumiaji mahususi na angalau wachunguzaji 20 waliojijumuisha kwa siku 14.

Baada ya kutimiza vigezo, utaweza kutuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi kwa kujibu maswali fulani kuhusu jaribio lako, programu yako na iwapo ipo tayari kutolewa kwa umma kwenye Dashibodi ya Google Play.

Mwongozo na mbinu bora za kufanya jaribio la watumiaji mahususi

Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni, kusanidi na kusambaza programu zako za Android kwenye Google kupitia viungo muhimu vilivyo hapa chini:

Kuandikisha wachunguzaji

Njia ya kawaida zaidi ya kuandikisha wachunguzaji ni kutumia mitandao binafsi na ya kikazi. Unaweza kuwasiliana na marafiki, familia, wafanyakazi wenzako au wenzako unaosoma nao, kwa mfano, na uwaombe wawe wachunguzaji wa beta wa programu yako. Unaweza kuwasiliana na jamii ambapo watumiaji wanaweza kupatikana na uwaandikishe kwa wingi ili wajaribu programu yako. Kwa mfano, ikiwa unasanidi programu ya wapenzi wa CrossFit, zingatia kuwasliana na klabu iliyo karibu nawe au kuwasiliana na watumiaji wako lengwa katika makundi ya mtandaoni. Unaweza pia kuchapisha chapisho kuhusu programu yako kwenye mitandao jamii na uwaombe watu wanaokufuatilia wajisajili ili wajaribu.

Ikiwezekana, unapaswa kuandikisha kikundi cha wachunguzaji tofauti ili utambue hitilafu na matatizo ya urahisi wa kutumiwa ambayo yanaweza kuathiri aina fulani za watumiaji au vifaa. Kwa sababu hiyo, unapaswa pia kuandikisha wachunguzaji ambao unaamini wanawakilisha watumiaji wa baadaye wa programu yako. Kwa mfano, ikiwa unasanidi programu ya kuongeza tija kwa biashara, unapaswa kuandikisha wachunguzaji ambao ni wataalamu wa biashara kutoka sekta mbalimbali ambazo unaamini kwamba programu yako inaweza kuwa maarufu. Kadri watumiaji wako wa kujaribu wanavyokuwa karibu na watumiaji wako lengwa, ndivyo utakavyopata maoni muhimu zaidi.

Kushirikiana na wachunguzaji

Baada ya kuandikisha kikundi cha wachunguzaji wa beta, ni muhimu uwape maagizo ya wazi kuhusu jinsi ya kujaribu programu yako na kuripoti hitilafu. Fahamisha wachunguzaji wako aina ya maoni unayotafuta. Jaribu kuwahimiza wachunguzaji watumie vipengele vingi vya programu yako kadri wawezavyo ili upate maoni ya jumla.

Weka njia ya kuwasilisha maoni au wafahamishe watumiaji wako jinsi wanavyoweza kutoa maoni (kwa mfano, kupitia barua pepe, tovuti au mijadala ya ujumbe). Wachunguzaji wako wanaweza pia kukupa maoni ya faragha kupitia Google Play.

Muhimu: Wasisitizie wachunguzaji wako kwamba wanahitaji kuendelea kushiriki katika jaribio lako la watumiaji mahususi kwa angalau siku 14 mfululizo.

Kukusanya na kuangalia maoni ya watumiaji

Ikiwa una programu inayojaribiwa, unaweza kufikia na kujibu maoni ya watumiaji katika Dashibodi ya Google Play. Ni wewe pekee unayeweza kuona maoni ya watumiaji na hayawezi kuonekana kwenye Google Play.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Maoni ya majaribio (Ukadiriaji na maoni > Maoni ya majaribio).
  2. Amua jinsi utakavyokagua maoni yako.
    • Chuja: Ili uone maoni ya watumiaji wa toleo la beta kulingana na vigezo mahususi (kama vile tarehe, lugha, hali ya jibu, toleo la programu, kifaa na zaidi), chagua kati ya vichujio vilivyopo.
    • Tafuta: Ili utafute maneno mahususi kwenye maoni yaliyowasilishwa, tumia kisanduku cha kutafutia.
Kidokezo: Weka rekodi ya maoni unayopokea. Kurudia kusoma rekodi hii baadaye inaweza kufanya iwe rahisi kwako kutambua matatizo au mada za maoni ya kawaida ambazo ungependa kuzishughulikia kwa kipindi kifupi au cha kudumu ili uboreshe programu yako. Tutakuomba pia ututayarishie baadaye muhtasari wa maoni ya majaribio yako unapotuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi.

Kutekeleza maoni ya watumiaji

Katika kipindi chote cha kujaribu programu yako, unapaswa kushughulikia maoni ya wachunguzaji wako na uhakikishe umerekebisha hitilafu zozote wanazozipata. Hatua hii:

  • Itasaidia kuboresha hali ya utumiaji ya programu yako;
  • kuzidisha uwezekano wa kufaulu kuomba uwezo wa kuchapisha kwa toleo la umma; na
  • kufanya uwe na uwezekano mkubwa wa kuepuka kupata maoni mabaya unapoanza kusambaza programu yako kwenye Google Play.

Majaribio ya kina

Mwongozo ulio kwenye makala haya ni mwanzo tu wa kukusaidia uelewe mambo ya msingi kuhusu majaribio unapojiandaa kusambaza programu yako ya kwanza. Unaweza kugundua nyenzo za kina zaidi za majaribio na mbinu za kuimarisha ubora wa programu yako unapoendelea kupata uzoefu zaidi kama msanidi programu. Kwa mfano, unaweza kupata maelezo kuhusu kujaribu programu kwenye Android na mambo ya msingi kuhusu majaribio kwenye tovuti ya Wasanidi Programu wa Android.

Dashibodi ya Google Play pia inatoa vipengele mbalimbali vinavyoweza kukusaidia utambue matatizo kwenye programu yako. Unaweza kuweka mipangilio na utekeleze ripoti ya kabla ya uzinduzi ili utambue matatizo mapema kabla ya programu yako kuwafikia watumiaji kupitia ripoti ya kina inayoorodhesha matatizo, tahadhari na hitilafu ambazo unaweza kuzichunguza na kuzitatua.

Kutekeleza majaribio ya watumiaji mahususi

Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio na kutekeleza jaribio la watumiaji mahususi kwa kutumia ukurasa huu wa Kituo cha Usaidizi.

Kuomba ufikiaji wa toleo la umma

Baada ya kutimiza masharti ya kufanya jaribio la watumiaji mahususi, unaweza kutuma ombi la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi. Ili uanze:

  1. Nenda kwenye Dashibodi.
  2. Bofya Omba kuchapisha toleo la umma.

Kisha lazima ujibu maswali yafuatayo kuhusu jaribio lako la watumiaji mahususi, programu yako na iwapo ipo tayari kutolewa kwa umma. Maswali haya yamegawanywa katika sehemu tatu:

  • Kuhusu jaribio lako la watumiaji mahususi
  • Kuhusu programu au mchezo wako
  • Utayarifu wa kutoa kwa umma

Unaweza kupata mwongozo wa kutoa maelezo kwa kila sehemu kwa kupanua sehemu zilizo hapa chini.

Sehemu ya 1: Tueleze kuhusu jaribio lako la watumiaji mahususi

Maelezo unayotoa katika sehemu ya "Kuhusu jaribio lako la watumiaji mahususi" yanatusaidia kuhakikisha kwamba programu zimejaribiwa kwa kiwango cha kutosha kabla ya kuchapishwa kwenye Google Play. Hii inatusaidia tuwalinde watumiaji dhidi ya programu za ubora wa chini, kuzuia kuenezwa kwa programu hasidi na kupunguza ulaghai.

Haya ndiyo unahitaji kushiriki ili ujaze sehemu hii:

  1. Tueleze jinsi ilivyokuwa rahisi kwako kuwaandikisha wachunguzaji wa programu yako kwa kuchagua moja ya chaguo zilizoorodheshwa. Hii inatusaidia tuelewe jinsi wasanidi programu wanavyotumia masharti ya majaribio ya Google Play.
  2. Toa maelezo kuhusu maoni uliyopokea kutoka kwa wachunguzaji wakati wa jaribio lako la watumiaji mahususi. Mifano ya maelezo muhimu hapa ni pamoja na:
    • Iwapo wachunguzaji walitumia vipengele vyote vya programu yako
    • Iwapo matumizi ya wachunguzaji wako yalilingana na jinsi unavyoweza kutarajia mtumiaji wa toleo la umma kutumia programu yako na ikiwa sivyo, tofauti unazoweza kutarajia kuona.
  3. Hatimaye, tayarisha muhtasari wa maoni uliyopokea kutoka kwa wachunguzaji, na utujulishe jinsi ulivyokusanya maoni haya.
  4. Bofya Endelea.
    • Muhimu: Ukibofya Futa au ukiondoka bila kuchagua 'endelea' na ukamilishe ombi lako la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi, mabadiliko uliyofanya hayatahifadhiwa.
Sehemu ya 2: Tueleze kuhusu programu au mchezo wako

Maelezo unayotoa katika sehemu ya "Kuhusu programu au mchezo wako" yanatusaidia tupate maelezo zaidi muhimu kuhusu programu au mchezo wako ili tuelewe vizuri programu au mchezo wako. Majibu yako hayaonyeshwi kwenye Google Play na hayataathiri vipengele na huduma unazoweza kufikia kwenye Dashibodi ya Google Play, jinsi programu au mchezo wako unavyoonyeshwa au kustahiki kwako kushiriki katika mipango ya wasanidi programu kwenye Google Play.

Haya ndiyo unahitaji kushiriki ili ujaze sehemu hii:

  1. Tueleze hadhira lengwa ya programu au mchezo wako. Tafadhali toa majibu mahususi kadiri uwezavyo.
  2. Swali la pili linatofautiana kiasi kulingana na iwapo wewe ni msanidi programu au mchezo:
    • Kwa programu: Eleza manufaa ya programu yako kwa watumiaji. Ikiwa huna uhakika kuhusu tunachomaanisha kwa hili, tembelea tovuti ya Wasanidi Programu wa Android ili upate maelezo zaidi kuhusu ubora wa programu kwenye Google Play.
    • Kwa michezo: Fafanua kinachofanya mchezo wako uwe wa kipekee.
  3. Tufahamishe idadi ya watumiaji unaotarajia kusakinisha programu au mchezo wako katika mwaka wake wa kwanza. Chaguo za kiwango ni nyingi, kwa hivyo chagua chaguo ambalo unafikiri linawezekana zaidi. Ni sawa ikiwa hili ni kadirio tu.
  4. Bofya Endelea.
    • Muhimu: Ukibofya Futa au ukiondoka bila kuchagua 'endelea' na ukamilishe ombi lako la ufikiaji wa umma wakati wa usanidi, mabadiliko uliyofanya hayatahifadhiwa.
Sehemu ya 3: Tueleze kuhusu utayari wako wa kuchapisha kwa toleo la umma

Maelezo unayotoa katika sehemu ya "Kuhusu utayari wako wa kuchapishwa kwa toleo la umma" yanatusaidia tuelewe iwapo programu au mchezo wako uko tayari kuchapishwa kwa toleo la umma.

Haya ndiyo unahitaji kushiriki ili ujaze sehemu hii:

  1. Tueleze mabadiliko uliyofanya kwenye programu au mchezo wako kulingana na ulichojifunza wakati wa jaribio lako la watumiaji mahususi.
  2. Eleza jinsi ulivyobaini kwamba programu au mchezo wako uko tayari kuchapishwa kwa toleo la umma.
  3. Bofya Tekeleza.
    • Muhimu: Ukibofya Futa au ukiondoka bila kuomba ufikiaji wa umma wakati wa usanidi, mabadiliko uliyofanya hayatahifadhiwa.

Baada ya kuomba uwezo wa kuchapisha kwa toleo la umma

Baada ya kukamilisha ombi lako la uwezo wa kuchapisha kwa toleo la umma, tutakagua ombi lako. Tukimaliza kukagua, tutamtumia mmiliki wa akaunti taarifa kwa barua pepe. Hii kwa kawaida huchukua siku 7 au chache, lakini wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu.

Ikiwa programu yako haiko tayari kuchapishwa, huenda ukahitajika kuendelea kuijaribu. Mifano ni pamoja na kutokuwa na wachunguzaji 20 waliojijumuisha kwenye jaribio lako la watumiaji mahususi au wachunguzaji wako kutotumia programu yako wakati wa jaribio lako la watumiaji mahususi.

Ikiwa ombi lako litakubaliwa, unaweza kufikia sehemu ya Toleo la Umma (Chapisha > Toleo la Umma) na unaweza kufanya programu yako ipatikane kwa mabilioni ya watumiaji kwenye Google Play iwapo unafikiri iko tayari. Unaweza pia kutumia Jaribio la watumiaji wengi (Chapisha > Jaribio > Jaribio la watumiaji wengi). Tunapendekeza ujaribu programu yako kwa kina kabla ya kuichapisha kwa toleo la umma, na ujaribu mara kwa mara masasisho yoyote ya baadaye unayofanya.

Maswali yanayoulizwa sana

Mnamaanisha nini mnaposema wachunguzaji lazima wajijumuishe kwa siku 14 mfululizo zilizopita kabla sijaomba kuchapisha kwa toleo la umma?

Hii inamaanisha kwamba hatutahesabu wachunguzaji waliojijumuisha, kujaribu kwa chini ya siku 14 kisha kujiondoa. Hata kama watajijumuisha tena ili wawe wamejijumuisha kwa jumla ya siku 14, siku hizi 14 lazima ziwe mfululizo ili zihesabiwe katika kutimiza vigezo vya wachunguzaji 20 waliojijumuisha ambao wamejaribu kwa siku 14 mfululizo.

Je, kuna mbinu nyingine bora zaidi za kujaribu ambazo zinaweza kunifaa?

Endelea kutumia jaribio la watumiaji mahususi unaporekebisha hitilafu na matatizo yaliyoripotiwa na mtumiaji. Kusasisha programu yako katika jaribio la watumiaji mahususi kabla ya kuchapisha kwa toleo la umma ni njia bora ya kupunguza maoni na ukadiriaji wa ubora wa chini.

Unaweza kuwaalika wachunguzaji wako wa jaribio la watumiaji mahususi kwa kikundi cha kuwasiliana kupitia ujumbe, ili maoni yaweze kuonekana kwa wengine. Wachunguzaji wako wanaweza pia kutoa maoni na muktadha wa ziada, ambao utakusaidia kuvipa kipaumbele vipengee vya programu au mchezo wako vya kuboresha.

Zaidi ya kurekebisha hitilafu na matukio ya programu kuacha kufanya kazi, hakikisha umejaribu hali ya jumla ya utumiaji ya programu yako. Pata maelezo zaidi kuhusu ubora wa programu na mchezo kwenye Google Play.

Je, kuna vipengele vingine vyovyote vya Dashibodi ya Google Play ninavyopaswa kuvifahamu ili vinisaidie kufaulu kwenye Google Play?

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya Dashibodi ya Google Play na habari mpya zaidi za Dashibodi ya Google Play kwenye tovuti ya Google Play. Unaweza pia kupata mafunzo ya mtandaoni ya bila malipo, yaliyobuniwa na wataalamu wa Google, kwa ajili ya wasanidi programu wapya na watarajiwa kwenye Chuo cha Google Play.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5755198529472895341
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false