Kuelewa chaguo mbadala la utozaji kwenye Google Play

Muhimu: API za mfumo mbadala wa utozaji zinahitajika ili kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio katika soko zinazotimiza masharti, kufikia tarehe ya mwisho iliyobainisha hapa chini.

Mwaka uliopita, tulianza kuchunguza chaguo pana za malipo kwenye Google Play kwa kutumia jaribio la chaguo mbadala la utozaji, ambalo linawawezesha wasanidi programu wanaostahiki kutoa mfumo wa ziada wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji wao katika masoko mahususi. Jaribio hili hutuwezesha kupata maarifa kutoka kwa wasanidi programu na watumiaji kuhusu ugumu unaotokea katika kutumia chaguo mbadala la utozaji katika masoko mbalimbali kote duniani.

Kadiri jaribio letu linavyoendelea kupanuka na kukua, tumeanza kuwapa wasanidi programu, mipango kadhaa ili kuwezesha mfumo mbadala wa utozaji na kuwapa watumiaji uwezo wa kuchagua. Kila mpango una masharti maalum ya kujiunga kulingana na masharti ya kimaeneo. Ufuatao ni mwongozo wa kubaini mpango/mipango unayoweza kujiandikisha kulingana na eneo unalotaka kutoa chaguo mbadala la utozaji.

Mfano wa kuonyesha wa hali ya utumiaji ya chaguo mbadala la utozaji

Mfano wa kielelezo cha hali ya utumiaji kwa chaguo mbadala la utozaji

Gundua mpango/mipango yetu ya chaguo mbadala la utozaji

Gundua mipango iliyo hapa chini, ambayo hutofautiana kulingana na upatikanaji na masharti ya kimaeneo. Unaweza kuandikisha programu yako katika zaidi ya mpango mmoja. Ikiwa eneo lina chaguo nyingi za mipango, programu yako inaweza tu kuandikishwa katika mpango mmoja kwa kila eneo kwa wakati mmoja. Programu yako inaweza kubadili kati ya mipango ikihitajika, hata hivyo, ni sharti iwasilishwe upya kupitia fomu mpya ya taarifa.

Chaguo mbadala la utozaji — Zaidi ya nchi 35 zinazotimiza masharti, ikiwa ni pamoja na Nchi Washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)

Kwa wasanidi programu wanaotaka kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji katika maeneo yafuatayo:

Australia, Brazili, Indonesia, Japani, Afrika Kusini, Marekani au EEA Austria, Ubelgiji, Bulgaria, Korasia, Jamhuri ya Zechia, Denmaki, Estonia, Ufini, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hangaria, Aisilandi, Ayalandi, Italia, Lativia, Lishenteni, Litwania, Lasembagi, Malta, Uholanzi, Norwe, Polandi, Ureno, Kuprosi, Romania, Slovakia, Slovenia, Uhispania, au Uswidi)

Muhtasari wa jaribio:

  • Ustahiki wa programu:
    • Programu ya michezo au ya kawaida kwenye maumbo yoyote yanayowapatia watumiaji chaguo mbadala la utozaji katika eneo la EEA; au
    • Programu ya vifaa vya mkononi au vishikwambi isiyo ya michezo inayotumiwa na watumiaji katika maeneo mengine yote yaliyoorodheshwa hapo juu.
  • Ada ya huduma: Imepunguzwa kwa asilimia 4 katika miamala ambayo watumiaji hulipa kutumia mfumo mbadala wa utozaji.
  • API za Mfumo Mbadala wa Utozaji ziko tayari: Ndiyo, wasanidi programu wanaoshiriki wanaweza kufanya mchakato wa kuripoti miamala uwe otomatiki kwa kufuata mwongozo wa kujumuisha.
Muhimu: Kuanzia tarehe 13 Machi 2024, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji sharti watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo ambayo yamebainishwa kwenye ukurasa wa jaribio au ukurasa wa mpango wa EEA kisha utembelee mwongozo wa API za mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Pata maelezo kamili kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi ya kuanza kwa kutembelea ukurasa wa jaribio.

Dokezo muhimu: Wasanidi programu walio na watumiaji katika Nchi Washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, pia wana chaguo la kutoa mfumo mbadala wa utozaji bila chaguo la mtumiaji. Hii inamaanisha, wasanidi programu wanaoshiriki ambao wametimiza masharti, wanaweza kutoa mfumo mbadala wa utozaji unaojitegemea bila pia kutoa mfumo wa utozaji wa Google Play. Masharti ya mpango huu wa EEA hutofautiana na jaribio la chaguo mbadala la utozaji. Pata maelezo kamili kwa kutembelea ukurasa wa mpango wa EEA.

Chaguo mbadala la utozaji, Korea Kusini

Kwa wasanidi programu wanaotaka kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji nchini Korea Kusini.

Muhtasari wa mpango:

  • Masharti ya kustahiki kwa programu: Programu za michezo ya video na programu zisizo za michezo za simu au vishikwambi zenye watumiaji nchini Korea Kusini.
  • Ada za Huduma: Zinapunguzwa kwa asilimia 4 kwa miamala ambayo watumiaji hulipa wakitumia mfumo mbadala wa utozaji.
  • API za Mfumo Mbadala wa Utozaji ziko tayari: Ndiyo, wasanidi programu wanaoshiriki wanaweza kufanya mchakato wa kuripoti na kutuma ankara uwe otomatiki kwa kufuata mwongozo wa ujumuishaji.
Muhimu Kuanzia tarehe 2 Agosti 2023, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji nchini Korea Kusini ni sharti watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo yaliyoainishwa kwenye ukurasa wa mpango na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Pata maelezo kamili kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi ya kuanza kwa kutembelea ukurasa wa jaribio kwa chaguo mbadala la utozaji nchini Korea Kusini.

Chaguo mbadala la utozaji — India

Kwa wasanidi programu wanaotaka kutoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji nchini India.

Muhtasari wa mpango:

  • Kustahiki kwa programu:: Programu za michezo ya video na programu zisizo za michezo za simu au kompyuta kibao zenye watumiaji nchini India.
  • Ada za Huduma: Zinapunguzwa kwa asilimia 4 kwa miamala ambayo watumiaji hulipa wakitumia mfumo mbadala wa utozaji.
  • API za Mfumo Mbadala wa Utozaji ziko tayari: Ndiyo, wasanidi programu wanaoshiriki wanaweza kufanya mchakato wa kuripoti na kutuma ankara uwe otomatiki kwa kufuata mwongozo wa ujumuishaji.
Muhimu: Kuanzia tarehe 13 Machi 2024, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji lazima watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo yaliyoainishwa kwenye ukurasa wa mpango na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Pata maelezo kamili kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi ya kuanza kwa kutembelea ukurasa wa jaribio kwa chaguo mbadala la utozaji nchini India

Mambo ya kutarajia wakati wa kujiunga

Kujiunga kwenye mipango yoyote ya chaguo mbadala la utozaji kunahitaji ukubali Sheria na Masharti ya mpango/mipango husika, utoe maelezo ya programu na wasanidi programu yanayoweza kuthibitishwa, na utoe maelezo yanayofaa ili kukamilisha mchakato wa wako wa kujiunga. Maelezo zaidi yametolewa hapa chini.

Hatua ya 1: Kagua masharti

Kagua masharti ya kila mpango kwenye ukurasa wa mpango husika ili kubaini kama programu yako inatimiza masharti ya kujiunga

Hatua ya 2: Kuwasilisha fomu ya taarifa

Kila mpango unahitaji uwasilishaji wa fomu ya taarifa ili kutoa maelezo yanayofaa na kukubali Sheria na Masharti yanayotumika.

Hatua ya 3: Kufungua na kuthibitisha akaunti

Baada ya uwasilishaji wako wa fomu ya taarifa kukaguliwa, timu yetu ya kuanzisha ushirikiano wa kimkataba itakutumia barua pepe kuhusu hatua zinazofuata.

  • Iwapo unahitaji kuunda taarifa za malipo, utahitaji kutoa hati zinazofaa za biashara
  • Ikiwa tayari una taarifa za malipo zinazostahiki au utaarifiwa kuhusu hatua zinazofuata baada ya wasifu wako kuundwa

Hatua ya 4: Andikisha programu zako

Utahitaji kutambua programu na nchi ambazo utatoa chaguo mbadala la utozaji. Unaweza kufanya hivi kupitia fomu ya kujiandikisha ambayo timu yetu ya kuhudumia wanaojiunga itashiriki nawe.

Hatua ya 5: Kukamilisha mchakato wa kujiunga na kushiriki kwenye mpango

Baada ya kuthibitisha kuwa programu yako inatimiza masharti ya kujiunga kwenye mpango husika na umekamilisha hatua zote zinazofaa za kujiandikisha, utapokea barua pepe kutoka Google Play ikithibitisha kuwa umekamilisha mchakato wa kuanza ushirikiano wa kimkataba. Barua pepe hii pia itakuwa na maagizo ya jinsi ya kutekeleza API na kutii masharti ya mpango.

Tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji

API za mfumo mbadala wa utozaji zinahitajika ili kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio katika soko yoyote inayostahiki, kufikia tarehe ya mwisho ya uhamisho ("Terehe ya Kuacha Kuripoti Mwenyewe"). Ili kuanza, fuata ukurasa wa programu ili upate taarifa zaidi kuhusu ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji na masharti ya uhamiaji.

Chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio: API zinazopatikana Terehe ya Kuacha Kuripoti Mwenyewe
Korea Kusini Tarehe 6 Aprili, 2023 Tarehe 2 Agosti, 2023
India Tarehe 14 Novemba 2023 Tarehe 13 Machi 2024
Nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, AU, BR, ID, JP, ZA, US Tarehe 14 Novemba 2023 Tarehe 13 Machi 2024

 

Mfumo mbadala wa utozaji pekee (i.e. bila chaguo la mtumiaji)
kwa watumiaji wa:
API zinazopatikana Terehe ya Kuacha Kuripoti Mwenyewe
Nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya Tarehe 14 Novemba 2023 Tarehe 13 Machi 2024

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1154877218116871691
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false