Kuwadokezea watumiaji wapate toleo jipya zaidi la programu yako

Unaweza kutumia zana za urejeshaji kwenye Dashibodi ya Google Play kuwadokezea watumiaji walio na toleo la programu lenye hitilafu au la zamani wasasishe ili wapate toleo jipya zaidi linalooana. Kuwapa watumiaji matoleo mapya zaidi ya programu yako kunaweza kusaidia kuboresha hali ya utumiaji na usalama wa programu yako.
Kidokezo: Unaweza pia kuwadokeza watumiaji wasasishe ili watumie toleo jipya zaidi la programu yako kwa kutumia Google Play Developer Publishing API, ambayo hukuwezesha kulenga viwango vyote vya matoleo ya programu pamoja na matoleo mahususi ya programu.

Muhtasari

Iwapo toleo la programu yako linalotumiwa na watumiaji lina hitilafu au limepitwa na wakati, unaweza kutumia Dashibodi ya Google Play kuwadokezea wasasishe toleo hilo. Zana hii ya urejeshaji inaweza kukusaidia hasa ikiwa umegundua tatizo katika toleo la zamani la programu, kama vile hatari za kiusalama.

Unaweza kuanza mchakato huu kwa kuchagua toleo la App Bundle ambako ungependa watumiaji wasasishe. Kisha unaweza kuchagua kigezo chako cha ulengaji, Unaweza kulenga: 

  • watumiaji wote wanaotumia toleo la programu uliloteua;
  • kulingana na nchi/eneo; au
  • kulingana na toleo la Android.

Watumiaji unaolenga wakifungua programu yako, wataona kidokezo kwenye skrini nzima kinachoarifu kuwa programu inahitaji kusasishwa. Kisha watumiaji wanaweza kuchagua kusasisha programu au kuondoa kidokezo. Mtumiaji akiondoa kidokezo, ataona kidirisha kila anapozima na kuwasha upya programu. Vinginevyo, akikubali kusasisha, programu itasasishwa ili kuwa toleo jipya zaidi linalooana.

Ufuatao ni mfano wa jinsi kidokezo cha kusasisha programu kinavyoweza kuonekana kwa watumiaji wa programu yako:

Kumbuka: Picha ni za mifano na zinaweza kubadilika

Kuwadokezea watumiaji kusasisha programu

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuwadokezea watumiaji kusasisha programu kwenye Dashibodi ya Google Play:

  • Sharti pawe na toleo jipya kwa watumiaji katika vikundi vyote vilivyo na toleo la programu ambako ungependa watumiaji wasasishe.
  • Unaweza kughairi kitendo hiki cha urejeshaji wakati wowote. Kughairi sasisho kutaathiri tu watumiaji ambao bado hawajasasisha programu.
  • Unaweza kupanua kigezo chako cha ulengaji wakati wowote.

Masharti ya msingi:

Kuwadokezea watumiaji walio na toleo la programu yako lenye hitilafu au la zamani kusasisha ili kupata toleo jipya zaidi linalooana.

Ili kuwadokezea watumiaji kusasisha programu:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo > Kichunguzi cha App Bundle).
    • Kumbuka: Unaweza pia kuanza urejeshaji kupitia ukurasa wa Muhtasari wa toleo (Toleo > Muhtasari wa toleo). Kwenye sehemu ya "Matoleo mapya zaidi," bofya kishale cha kulia karibu na toleo ambako ungependa watumiaji wasasishe. Hii itafungua ukurasa wa Maelezo kuhusu toleo.
  2. Kwenye sehemu ya juu kulia mwa ukurasa, bofya Zana za urejeshaji kisha uchague Kuwadokezea watumiaji kusasisha programu katika menyu kunjuzi.
  3. Kwenye sehemu ya "Chagua kifurushi," chagua App Bundle ambako ungependa watumiaji watumie kusasisha programu.
    • Kumbuka: Baadhi ya vikundi vilivyo na App Bundle huenda visiwe na matoleo mapya. Ikiwa vipo, vikundi hivi vimeorodheshwa kwenye sehemu ya "Hayapatikani." Unaweza kubofya App Bundle iliyoorodheshwa hapa ili uangalie vikundi ambako hayapatikani.
  4. Baada ya kuchagua App Bundle ya programu yako, bofya Endelea.
  5. Si lazima: Unaweza kubofyaOnyesha maagizo ili kupanua hatua zinazoonyeshwa kwenye skrini ili kujaribu kidokezo chako.
  6. Chagua kigezo cha ulengaji. Unaweza kulenga:
    • watumiaji wote wanaotumia toleo la programu uliloteua;
    • kulingana na nchi/eneo; au
    • kulingana na toleo la Android.

Kumbuka yafuatayo:

  • Ukiteua toleo la Android, ni sharti pia uchague matoleo ya Android unayotaka kujumuisha (unaweza pia kuchagua matoleo yote ya Android).
  • Ukichagua nchi/eneo, ni sharti pia uchague nchi/maeneo unayotaka kujumuisha (unaweza pia kuchagua nchi/maeneo yote).

Unaweza kuangalia idadi ya watumiaji watakaopokea kidokezo cha kusasisha programu kulingana na kigezo cha ulengaji ulichochagua.

  1. Bofya Anzisha kidokezo ili uanze kuwadokezea watumiaji kusasisha programu.

Kudhibiti sasisho lako

Baada ya kuwadokezea watumiaji kusasisha programu, unaweza kutumia zana za urejeshaji kwenye Dashibodi ya Google Play kubadilisha mipangilio ya sasisho lako, kuangalia hatua iliyopiga, au kughairi kitendo cha urejeshaji. Bofya sehemu iliyo hapa chini ili uipanue au uikunje.

Kuangalia hatua ya urejeshaji

Unaweza kuangalia hatua ya urejeshaji wakati wowote. Ili uangalie hatua:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo > Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Kwenye jedwali la matoleo ya programu, chagua kishale cha kulia cha toleo ambalo ungependa kuangalia.
  3. Chagua kichupo cha Urejeshaji.
  4. Angalia hatua kupitia upau wa "Hatua ya urejeshaji". Unaweza kuangalia jumla ya watumiaji wanaolengwa katika urejeshaji, asilimia ya usasishaji iliyokamilika na asilimia iliyosalia.
Kubadilisha sasisho

Ili kubadilisha hatua inayoendelea ya urejeshaji:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Kichunguzi cha App Bundle (Toleo > Kichunguzi cha App Bundle).
  2. Kwenye jedwali la matoleo ya programu, chagua kishale cha kulia cha toleo ambalo ungependa kuangalia.
  3. Chagua kichupo cha Urejeshaji.
  4. Bofya Dhibiti kidokezo cha sasisho kisha uchague Badilisha kwenye menyu kunjuzi.
  5. Fanya mabadiliko muhimu kwenye sasisho lako. Unaweza kurekebisha vigezo vya ulengaji ulivyochagua ulipounda kidokezo cha sasisho.
  6. Hifadhi mabadiliko uliyofanya.

Kumbuka: Hatua ya kubadilisha sasisho itaathiri tu watumiaji ambao bado hawajasasisha programu.

Kumbuka: Zana za urejeshaji kwa sasa hazipatikani kwa programu zinazotumia Uthibitishaji wa Msimbo, Ulinzi Otomatiki wa Uadilifu wa Google Play au Toleo Jipya la Ufunguo.
Pia, baada ya kupata toleo jipya la ufunguo wako wa kuambatisha cheti kwenye programu, hutaweza kutekeleza vitendo vipya vya urejeshaji, lakini bado utaweza kubadilisha na kughairi vitendo vilivyopo. Tunajitahidi kufanya zana za urejeshaji kwa aina hizi za programu zipatikane katika siku zijazo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1580858443434619077
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false