Teknolojia ya rekodi ya makundi ya miamala inapoendelea kubadilika kwa kasi, tunalenga kutoa jukwaa kwa wasanidi programu kustawi katika uvumbuzi na kuimarisha ubunifu wa hali ya juu kwa ajili ya watumiaji.
Kwa madhumuni ya sera hii, tunachukulia maudhui yanayotoka kwenye rekodi ya makundi ya miamala kuwa vipengee vya dijitali vyenye tokeni vinavyolindwa kwenye rekodi ya makundi ya miamala. Ikiwa programu yako ina maudhui yanayotokana na rekodi ya makundi ya miamala, ni lazima utii masharti haya.
Uchumaji wa sarafu za dijitaliHaturuhusu programu zinazochuma sarafu za dijitali kwenye vifaa. Tunaruhusu programu zinazodhibiti kwa umbali uchumaji wa sarafu za dijitali.
|
Masharti ya Uwazi kwa Usambazaji wa Vipengee vya Dijitali vyenye TokeniIwapo programu yako inauza au kuwawezesha watumiaji kujipatia Vipengee vya Dijitali vyenye Tokeni, ni lazima utangaze kupitia fomu ya taarifa ya Vipengele vya Fedha kwenye ukurasa wa Maudhui ya Programu katika Dashibodi ya Google Play. Unapounda bidhaa ya ndani ya programu, lazima uonyeshe katika maelezo ya bidhaa kuwa inawakilisha Kipengee cha Dijitali chenye Tokeni. Kwa mwongozo wa ziada, angalia Kuunda bidhaa ya ndani ya programu. Huwezi kutangaza au kuhimiza mapato yoyote yanayoweza kutokana na kucheza au shughuli za biashara. |
Masharti ya Zaida ya Matumizi ya kanuni na vipengele vya michezo ya NFTKama inavyohitajika katika Sera ya Mashindano, Michezo na Kamari za Pesa Halisi ya Google Play, programu za kamari zinazojumuisha vipengee dijitali vyenye tokeni, kama vile NFT, zinapaswa kukamilisha mchakato wa kutuma maombi. Kwa programu nyingine zote ambazo hazitimizi masharti ya kujiunga kwa programu za kamari na hazijabainishwa katika Majaribio Mengine ya Michezo ya Pesa Halisi, kitu chochote cha thamani ya fedha hakipaswi kukubaliwa badala ya nafasi ya kupata NFT ya thamani isiyojulikana. NFT zinazonunuliwa na watumiaji zinapaswa kutumiwa au kutumika katika mchezo ili kuboresha hali ya utumiaji ya mtumiaji au kuwasaidia watumiaji kuendeleza mchezo. NFT hazipaswi kutumika kuweka dau au kubahatisha ili kupata fursa ya kushinda zawadi zenye thamani ya pesa halisi (ikiwa ni pamoja na NFT zingine).
|