Fanya majaribio ya kuboresha bei za bidhaa za ndani ya programu

Unaweza kufanya majaribio ya bei katika Dashibodi ya Google Play ili upanue mkakati wako wa bei katika masoko yanayochipua au ujaribu viwango tofauti vya bei katika masoko yako ya msingi ili ujipatie mapato zaidi.

Muhtasari

Majaribio ya bei hukuruhusu ufanye Majaribio ya A/B na kutumia matokeo ili kurekebisha bei za programu yako kwa usahihi na kwa uhakika kulingana na uwezo wa kununua katika masoko tofauti duniani. Unaweza pia kutumia majaribio ya bei ili kujaribu viwango tofauti vya bei dhidi ya bei elekezi katika masoko yako ya msingi ili ujipatie mapato zaidi. Kuweka viwango bora vya bei za bidhaa zako za ndani ya programu katika nchi/maeneo tofauti huhakikisha unatumia mkakati bora wa bei kwenye programu yako ili uendelee kuongeza mapato huku ukiendelea kuwavutia watumiaji wapya. Kwa kuwa kipengele hiki kinatokana na mauzo na bei za bidhaa za ndani ya programu, ni sharti uwe muuzaji na msanidi programu ili ukitumie.

Tayarisha na ufanye jaribio la bei

Sehemu zilizo hapa chini zinatoa mwongozo na maelezo muhimu kuhusu kuandaa na kufanya majaribio ya bei na kuelewa matokeo yake.

Kabla ya kuanza

Panua na usome kila sehemu hapa chini kabla ya kuanza kuweka mipangilio ya jaribio la bei katika Dashibodi ya Google Play.

Masharti ya msingi
Maelezo muhimu

Maelezo ya jumla

  • Majaribio hufanyika katika kiwango cha programu pekee; huwezi kufanya majaribio katika programu nyingi.
  • Muda wa juu zaidi unaoruhusiwa wa jaribio ni miezi sita, kisha bei zitarejea kuwa bei za awali. Bei pia zitarejea kuwa za awali baada ya siku 14 zikishakuwa muhimu kitakwimu.
  • Unaweza kufanya jaribio la bidhaa za ndani ya programu zisizozidi 1000 katika jaribio moja.
  • Huwezi kutekeleza jaribio moja ukitumia bidhaa za ndani ya programu zinazoingiliana na nchi zinazoingiliana hadi angalau siku 30 baada ya kumalizika kwa jaribio la kwanza.
  • Huwezi kusitisha majaribio. Unaweza tu kuyafanya au kuyasimamisha kabisa. Huwezi kuanzisha tena jaribio ukishalisimamisha.

Vikomo vya nchi/eneo

  • Unaweza kufanya jaribio moja kwa wakati mmoja katika nchi/eneo lolote husika. Kwa mfano, ikiwa tayari unafanya jaribio nchini Norwe, huwezi kufanya jaribio lingine huko ukitumia bidhaa tofauti isipokuwa ukomeshe jaribio la kwanza na uanzishe lingine.
  • Ni sharti bei inayojaribiwa iwe katika viwango vya bei vilivyobainishwa kwa ununuzi wa ndani ya programu. Ikiwa asilimia ya bei iko nje ya kiwango cha bei kilichobainishwa cha nchi/eneo hilo kama sehemu ya jaribio, asilimia hiyo ya bei itakoma kiotomatiki katika thamani ya kikomo.
  • Unaweza kutumia hadi vibadala viwili vya bei na bei elekezi kwa kila jaribio.
  • Majaribio yanatekelezwa tu katika nchi/eneo lililochaguliwa na si katika maeneo yenye kodi tofauti yanayohusiana. Kwa mfano, ukifanya jaribio nchini Ufaransa, jaribio hili halitajumuisha maeneo ya Ufaransa yanayohusiana (Guyana ya Ufaransa, Polinesia ya Ufaransa, Guadalupe, Martinique, Mayotte, New Caledonia, Riyunioni, Saint Barthélemy, Saint Martin, Saint Pierre na Miquelon, Wallis na Futuna).

Mabadiliko katika bidhaa za ndani ya programu

  • Huwezi kubadilisha bei ya bidhaa ya ndani ya programu iliyotumika katika jaribio linaloendelea. Ili ubadilishe bei, ni sharti ukomeshe jaribio hilo. Kumbuka yafuatayo:
    • Kanuni hii haifuatwi wakati unafanya majaribio mawili na unatumia matokeo ya jaribio la kwanza. Au, iwapo bidhaa yako ya ndani ya programu imeunganishwa na kiolezo cha bei, unaweza kubadilisha bei za bidhaa za ndani ya programu katika nchi ambazo hujazifanyia majaribo.
    • Ukiweka mipangilio ya bidhaa mpya ya ndani ya programu wakati jaribio linaendelea, haitajumuishwa katika jaribio hilo.

Kutekeleza majaribio na kutumia majibu

  • Unaweza kuweka bei za majaribio wakati wowote. Hata hivyo, tunapendekeza usubiri hadi matokeo yawe muhimu kitakwimu na uweke tu mabadiliko ya bei yenye utendaji bora kuliko kikundi chako cha bei elekezi.
  • Huwezi kuongeza nchi au maeneo zaidi au bidhaa kwenye jaribio linaloendelea kwa sasa.
  • Ikiwa bidhaa yako moja au zaidi zimeunganishwa kwenye kiolezo cha bei, hatua ya kuweka bei itasasisha bei za nchi au eneo la jaribio lako na kutenganisha bidhaa hizi kwenye kiolezo au violezo.
Istilahi za majaribio

Majaribio yanatumia kwa wingi istilahi za takwimu. Ikiwa hufahamu istilahi hizi, unaweza kurejelea faharasa hapa chini.

Istilahi Ufafanuzi Madokezo
Viwango vya kutegemeka

Kiwango cha thamani kinachoonyesha ukosefu wa uhakika iwapo matokeo ni muhimu au si muhimu kitakwimu.

Hii ni ishara kuu ya kutumia kufasili matokeo ya jaribio. Umuhimu wa kitakwimu hubainishwa wakati viwango vya kutegemeka havikutani katika 0.

Huenda hii isionekane siku chache za kwanza kutokana na viwango vya chini vya data.

Kiwango cha kutegemeka

Uwezekano ambapo tofauti iliyoonekana kati ya kibadala na thamani elekezi ni 'ndivyo'.

Mfano: Kiwango cha kutegemeka cha 90% kitamaanisha kuwa 10% ya muda ambao tofauti ilionekana huenda ilitokea kinasibu. Yaani, kuna uwezekano wa chini ya 10% kuwa data inayofanyiwa majaribio ingeweza kutokea iwapo hakuna tofauti kati ya thamani elekezi na kibadala.
  • Tunatumia jackknife (zana ya takwimu inayoruhusu ukadiriaji wa kibadala kwa kuchukua sampuli upya) ili kukokotoa viwango vya kutegemeka na kisha tunatumia jaribio la uwezekano wa mfululizo wa mseto ili kudhibiti kiwango kilichozidishwa kisicho cha kweli kwenye ufuatiliaji endelevu.
  • Kiwango chaguomsingi cha kutegemeka ni 90%, lakini unaweza kuchagua kati ya 70% na 99%. Baada ya kukichagua wakati wa kuweka mipangilio ya jaribio, hakitabadilika katika kipindi cha jaribio
  • Huwezi kubadilisha kiwango chako cha kutegemeka ukishaanzisha jaribio lako.
  • Viwango vya kutegemeka vinavyotumika sana ni 95%, 90% na 99%; viwango vya kutegemeka vya juu zaidi vinahitaji data zaidi, kwa hivyo, inamaanisha kuwa matokeo ya jaribio yana uwezekano mkubwa wa kuwa na uhakika.
  • 50% itamaanisha uwezekano wa 50:50 kuwa jaribio si sahihi (sawa na kurusha sarafu).
Elekezi Kibadala halisi cha jaribio (chenye ununuzi wa ndani ya programu wa bei halisi) katika upande wa jaribio. Bei elekezi huonekana na sehemu ya hadhira ya jaribio ikiwa imebainishwa wakati wa kuweka mipangilio na watumiaji wote nje ya jaribio.
Matokeo ya jaribio Matokeo ya jaribio lako. Matokeo yanayoweza kupatikana yameorodheshwa kwenye sehemu ifuatayo.
Si kweli Wakati tukio hasi limeainishwa visivyo kuwa chanya.

Tunapotambua kuwa tofauti kati ya bei elekezi na jaribio ni muhimu kitakwimu (chanya) lakini tofuati kati ya bei elekezi na jaribio si muhimu kitakwimu (hasi), inachukuliwa si kweli.

Kiwango cha hali isiyo kweli ni uwiano wa idadi ya matukio yasiyo kweli na jumla ya matukio hasi.

Bidhaa za ndani ya programu

Bidhaa ambazo wateja hutozwa mara moja.

Bidhaa za ndani ya programu zinaweza kujumuisha vipengee kama vile bidhaa pepe (kwa mfano, viwango au vipengee maalum vya mchezo) na huduma zinazolipishwa ndani ya programu yako kwenye Google Play.

Unaweza kuchagua bidhaa moja au nyingi za ndani ya programu, hadi kikomo cha 2,000. Kwa ujumla, data nyingi inamaanisha muda mchache wa kutambua tofauti kati ya bei elekezi na vibadala, ikiwa kuna tofauti.

Kufanya majaribio ya mabadiliko ya bei katika bidhaa nyingi kunaweza kupunguza uwezekano wa bidhaa fulani kulemea na kupunguza uuzaji wa zingine.

Athari ya chini inayotambulika (MDE)

Kiwango unachochagua wakati unaweka mipangilio ya jaribio lako inayoashiria kiwango cha maboresho unayotaka jaribio lako litambue. Unaweza kuchukulia hii kama kuamua jinsi ambavyo ungependa jaribio lako litambue vitu kwa kina, hivyo kuathiri muda uliokadiriwa hadi kufikia hali ya umuhimu kitakwimu. Baada ya kuchagua MDE yako, utaona kadirio la muda ambao itachukua kupata matokeo yenye umuhimu kitakwimu kulingana na data ya kihistoria ya uteuzi wako.

Kwa mfano, MDE ndogo inamaanisha jaribio lenye utambuzi wa kina linalosababisha muda mrefu zaidi uliokadiriwa wa kukokotoa umuhimu wa kitakwimu.

  • MDE chaguomsingi ni asilimia 30, lakini unaweza kuchagua nyongeza za asilimia 5 kuanzia asilimia 5 hadi asilimia 50.
  • Huwezi kubadilisha MDE yako ukishaanzisha jaribio lako.
  • MDE inaathiri tu muda uliokadiriwa wa kukokotoa hali ya umuhimu kitakwimu kulingana na data ya kihistoria au tunapobaini kuwa bei elekezi au ya vibadala ni sawa katika jaribio. Kwa maelezo zaidi, angalia matokeo yanayoweza kupatikana ya jaribio.
  • Ikiwa unafanya majaribio ya bidhaa mpya ambazo hazina data ya kihistoria, muda uliokadiriwa wa kukokotoa hali ya umuhimu kitakwimu hautakuwa sahihi.

Athari ya upya Hali ambapo, watumiaji wanaweza kupendelea au kujaribu kipengele kipya (kama vile bidhaa mpya au kiwango cha bei), hata kama kipengele hicho si bora au hakivutii zaidi ya kipengele cha awali. Katika hali hii, umaarufu kwa kawaida hushuka kadri muda unavyosonga. Majaribio yanayoisha haraka huenda yakakabiliwa na athari za upya. Tunapendekeza utumie kwa wiki zilizokadiriwa hadi ufikie ukokotoaji wa hali ya umuhimu kitakwimu ili kuzingatia athari hii.
Umuhimu kitakwimu Katika jaribio la A/B, hii hubaini kama tofauti kati ya bei elekezi na kibadala ni halisi au inatokea kibasibu.

Ikiwa kiwango cha kutegemeka hakijumuishi thamani ya sifuri katika athari, tunachukulia kuwa haya ni matokeo muhimu kitakwimu. Katika hali hii, athari ni tofauti kati ya bei elekezi na kibadala.

Unaweza kuona baadhi ya mifano inayoonekana ya viwango vya kutegemeka katika sehemu ya Maswali yanayoulizwa sana.

Kibadala Kibadala cha bei halisi ya jaribio upande wa jaribio. Kibadala huwa ongezeko la bei au kupungua kwa bei halisi ya ununuzi wa ndani ya programu.

Weka mipangilio ya jaribio

Wakati unaweka mipangilio ya jaribio, tunapendekeza ujumuishe bidhaa zote za ndani ya zinazoweza kubadilishwa katika programu yako (kama vile sarafu za ndani ya mchezo) katika jaribio ili kupunguza matukio ya bidhaa fulani kulemea na kupunguza uuzaji wa zingine.

Kabla ya kuanza: Viwango vya chini vya data

Ikiwa unatumia viwango vya chini vya data, huenda usiwe na data ya kutosha ya kubaini matokeo ya jaribio. Kwa mfano, ikiwa unafanya jaribio la bidhaa mpya, urefu wetu uliokadiriwa wa jaribio na tahadhari huenda zisiwe sahihi. Katika hali hii, huenda ukaona tahadhari katika Dashibodi ya Google Play kuwa kiwango cha chini sana cha data kinatabiriwa katika kipindi cha muda ulichochagua. Ukipata ujumbe wa kiwango cha chini cha data, huenda usiwe na data ya kutosha kutekeleza jaribio au huenda usiweze kuboresha vigezo vya jaribio lako. Hivi ni baadhi ya vitendo vinavyopendekezwa vya kutatua matatizo ya kiwango cha chini cha data.

Hata hivyo, ikiwa unafanya jaribio la muda mrefu zaidi, ni muhimu kuzingatia kuwa huenda matokeo yakaathiriwa na vigezo vya kiuchumi kama vile mabadiliko ya kimataifa ya sarafu kadri muda unavyosonga.

Sehemu ya 1: Weka maelezo

Ili kuongeza maelezo ya jaribio lako, fanya yafuatayo:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Majaribio ya bei (Chuma mapato > Majaribio ya bei).
  2. Bofya Unda jaribio.
  3. Katika sehemu ya "Weka maelezo", weka jina la jaribio na maelezo mafupi ya jaribio lako (si lazima).
    • Kumbuka: Jina na maelezo mafupi ya jaribo lako hayaonekani kwa watumiaji.
  4. Chagua nchi/maeneo ambako ungependa kufanyia majaribio.
    • Muhimu: Majaribio yanatekelezwa tu katika nchi/eneo lililochaguliwa na si katika maeneo yake yanayohusiana. Kwa mfano, ukichagua Ufaransa, majaribo ya bei yatatekelezwa tu nchini Ufaransa na si katika maeneo yake yanayohusiana kama vile Guiana ya Ufaransa.
  5. Ukitumia menyu kunjuzi ya Bidhaa, chagua bidhaa za ndani ya programu ambazo ungependa kufanyia majaribio. Orodha kunjuzi inaonyesha majina, vitambulisho na bei za bidhaa za ndani ya programu.
    • Muhimu: Ukichagua bidhaa ya ndani ya programu ambayo imeunganishwa na kiolezo cha bei, kiolezo cha bei kitafungwa kwa muda wote wa jaribio la bei.
  6. Chagua tarehe ya kuanza. Jaribio lako litaanza saa sita usiku, saa za eneo la PT tarehe uliyochagua. Unaweza kuratibu jaribio lako lianze wakati ujao.
  7. Bofya Endelea ili uendelee kuweka mipangilio ya jaribio lako kwa kuweka vibadala.

Kulingana na data ya kuweka mipangilio ya jaribio lako, tukitabiri viwango vya data yako vitakuwa chini mno na havitaweza kufikia hali ya umuhimu kitakwimu, utaona tahadhari. Katika hali hii, tunapendekeza ufanye marekebisho ili uhakikishe unakusanya data ya kutosha kufikia hali ya umuhimu kitakwimu. Ili kuona hatua zinazofuata, angalia Hatua zinazopendekezwa kwa viwango vya chini vya data.

Hatua zinazopendekezwa kwa viwango vya chini vya data

Mapendekezo yafuatayo yatasaidia kubadilisha viwango vya data vinavyohitajika ili kufikia hali ya umuhimu kitakwimu ili muda wa jaribio ufupishwe.

Hatua ya kuweka mipangilio ya jaribio

Hatua inayopendekezwa
Sehemu ya 1: Weka maelezo Ongeza idadi ya nchi/maeneo katika jaribio.
Sehemu ya 1: Weka maelezo Fanya jaribio la bidhaa zote za ndani ya programu au uongeze idadi ya bidhaa za ndani ya programu.
Sehemu ya 2: Weka vibadala Punguza idadi ya vibadala kutoka viwili kuwa kimoja.
Sehemu ya 2: Weka vibadala

Fanya jaribio kwa kupunguza bei kwa asilimia kubwa (punguza bei).

Kumbuka: Hatua hii haitaathiri makadirio ya mwanzo lakini husaidia wakati jaribio linaendelea.
Sehemu ya 3: Dhibiti mipangilio Ongeza ukubwa wa hadhira kwa kila kibadala (kwa mfano, 50% kuwa elekezi na 50% kuwa inayojaribiwa).
Sehemu ya 3: Dhibiti mipangilio

Ongeza athari ya chini inayotambulika.

Kumbuka: Hii huathiri majaribo ambayo bei elekezi na vibadala ilikuwa na utendaji sawa.

Sehemu ya 3: Dhibiti mipangilio Punguza kiwango cha kutegemeka.

Sehemu ya 2: Weka vibadala

Katika sehemu ya "Weka vibadala", unaweza kuongeza na kuondoa vibadala vya bei. Ni sharti jaribio lako la bei liwe na angalau kibadala kimoja. Ili uweke vibadala:

  1. Ukitumia menyu kunjuzi, chagua Ongeza bei au Punguza bei, na uweke asilimia unayotaka kutumia kwenye chaguo lako. Kumbuka yafuatayo:
    • Ni sharti uweke nambari kamili.
    • Ukichagua Punguza bei, ni sharti uweke thamani kati ya 1 na 99.
    • Ukichagua Ongeza bei, ni sharti uweke thamani kati ya 1 na 999.
  2. Baada ya kuweka kibadala, kiwango chako cha bei elekezi na kiwango cha bei ya kibadala vitaorodheshwa kwenye ukurasa. Unaweza kubofya Angalia bei za bidhaa kwa maelezo zaidi, ikiwa ni pamoja na majina na vitambulisho vya bidhaa, maeneo yenye kodi tofauti (ikiwa yapo) na taarifa za kodi. Hapa unaweza kuona mabadiliko halisi ya asilimia ya bei baada ya kutumia kiwango cha kubadilisha sarafu na mitindo ya bei za nchi mahususi.
  3. Bofya + Weka kibadala kingine na urudie hatua za awali ikiwa unataka kujumuisha vibadala vingi katika jaribio lako. Kiwango cha bei elekezi na kiwango cha bei ya kibadala vitaorodheshwa kwenye ukurasa.
  4. Bofya Inayofuata ili uendelee kuweka mipangilio ya jaribio lako kwa kuweka mipangilio ya jaribio lako iwe mahususi zaidi.

Sehemu ya 3: Dhibiti mipangilio

Katika sehemu ya "Dhibiti mipangilio", unaweza kuweka vigezo vyako vya ulengaji ili jaribio lako liwe mahususi zaidi. Ili udhibiti mipangilio ya jaribio lako:

  1. Weka hadhira ya jaribio lako. Hii ni asilimia ya watumiaji ambao watakuwa kwenye jaribio. Idadi ya watumiaji itagawanywa kwa usawa katika thamani elekezi na vibadala vyako. Kumbuka kuwa watumiaji walio nje ya jaribio pia wataona bei halisi (elekezi) lakini hawatajumuishwa katika uchanganuzi wa jaribio.
    • Kumbuka: Ni sharti uweke nambari kamili kati ya 1 na 100.
  2. Weka kiwango cha kutegemeka. Hatua ya kupunguza kiwango cha kutegemeka itaongeza uwezekano wa kupata matokeo yasiyo kweli, lakini pia itapunguza muda wa kutekeleza jaribio.
  3. Weka kiwango cha chini cha athari inayoweza kutambulika. Hii inaashiria kiwango cha maboresho ambacho ungependa jaribio lako litambue. Unaweza kuchukulia hii kama kuamua jinsi ungependa jaribio lako litambue vitu kwa kina. Hii itarekebisha muda wako unaokadiriwa hadi ukokotoaji wa hali ya umuhimu kitakwimu.
  4. Chuja vigezo vyako vya ulengaji ili uimarishe jaribio lako. Unaweza kuona muda uliokadiriwa hadi hali ya umuhimu kitakwimu ikokotolewe kama mwongozo kulingana na mipangilio yako.

Sehemu ya 4: Anzisha jaribio lako

Sasa uko tayari kuanzisha jaribio lako. Wakati wa jaribio, bei zitabadilika kwa bidhaa za ndani ya programu na nchi au maeneo yaliyochaguliwa. Unaweza kutamatisha jaribio lako wakati wowote.

  1. Kabla ya kuanzisha jaribio lako, thibitisha kuwa unaelewa yafuatayo:
    • Jaribio linaweza kuathiri mapato ya programu yako. Kumbuka kuwa bila tokeo lililo muhimu kitakwimu, tokeo lolote hasi au chanya la mapato huenda lisiwe na maana, kwa hivyo tungependekeza usubiri hadi jaribio lifikie hali ya umuhimu kitakwimu.
    • Hutaweza kubadilisha bei za bidhaa za ndani ya programu ulizochagua wakati jaribio linaendelea.
    • Kutumia matokeo ya jaribio kutaathiri nchi/maeneo yote yaliyojumuishwa na bidhaa za ndani ya programu.
  2. Bofya Thibitisha na uanzishe.

Si lazima: Tamatisha jaribio lako

Unaweza kutamatisha jaribio lako wakati wowote.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Majaribio ya bei (Chuma mapato > Majaribio ya bei).
  2. Fungua jaribio unalotaka kutamatisha.
  3. Bofya Tamatisha jaribio.

Ukishatamatisha jaribio lako, bei za majaribio zitarejea ziwe bei halisi kwa nchi/maeneo na bidhaa za ndani ya programu husika. Utakomesha jaribio na uchanganuzi.

Ikiwa umeratibu jaribio la wakati ujao, unaweza kulighairi pia kwa kufuata hatua za awali. Majaribio yanayoghairiwa ndani ya saa 24 kabla ya tarehe ya kuanza iliyoratibiwa, wakati mwingine yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi.

Kuangalia matokeo ya jaribio na kutumia vibadala

Ni muhimu ufahamu matokeo tofauti yanayoweza kupatikana ya jaribio na jinsi yanavyoathiri programu yako na mkakati wake wa bei. Soma sehemu hii kwa umakini kabla ya kutumia matokeo.

Angalia na uchanganue matokeo ya jaribio yako

Wakati matokeo yako yanachukuliwa kuwa muhimu kitakwimu, yatapatikana kwenye ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio lako na utatumiwa arifa kupitia ujumbe katika Kikasha chako.

Angalia matokeo yako

Fungua jaribio lako ili uone matokeo na uchanganuzi. Nenda kwenye ukurasa wa Majaribio ya bei (Chuma mapato > Majaribio ya bei) na ubofye kishale cha kulia karibu na jaribio lako ili uangalie ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio.

Matokeo yanaonyeshwa karibu na sehemu ya juu ya ukurasa. Panua sehemu ya Matokeo yanayoweza kupatikana ya jaribio ili uangalie matokeo tofauti na maana yake. Chini ya matokeo ya jaribio, unaweza kuangalia maelezo mafupi yanayofafanua matokeo. Kwa mfano, unaweza kuona "Kibadala cha [X] kilikuwa na utendaji bora zaidi," juu ya ufafanuzi mfupi wa matokeo ya jaribio, ambao unaweza kusema kitu kama vile " Kibadala cha [X] kilifanikisha mapato mengi zaidi." Katika hali ambapo kibadala kililingana na bei elekezi au kilikuwa na utendaji mzuri kuliko bei elekezi, unaweza kubofya Tumia kibadala cha [X] ili utumie kibadala hicho na usasishe bei ya bidhaa ya ndani ya programu ipasavyo. Ili upate maelezo zaidi, angalia Tumia vibadala.

Kumbuka: Majaribio huisha kiotomatiki siku 14 baada ya matokeo kubainishwa, au unaweza kubofya Tamatisha jaribio ili ulitamatishe mara moja.

Kidokezo: Unaweza kutumia bei za majaribio wakati wowote lakini tunapendekeza usubiri hadi baada ya matokeo kuwa na umuhimu kitakwimu na utumie tu mabadiliko ya bei yenye utendaji bora kuliko kikundi chako cha bei elekezi.

Angalia data ya kuthibitisha

Chini ya matokeo, jedwali linaonyesha data ambayo matokeo ya takwimu yametokana nayo. Jedwali hilo linaorodhesha vibadala, mapato, mapato yakilinganishwa na bei elekezi (na mapato yakilinganishwa na bei elekezi katika asilimia) na viwango vya kutegemeka kwa vibadala vyako. Ikiwa ungependa kuelewa vipimo tofauti kwenye ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio, panua sehemu ya Ufafanuzi wa vipimo.

Chini ya jedwali katika sehemu ya "Data ya kuthibitisha", unaweza kutazama data kwa kina. Chati inaonyesha mapato yakilinganishwa na maelezo ya bei elekezi ya tarehe ya hivi karibuni inayopatikana kuwa chaguomsingi. Katika mwonekano huu, eneo lenye rangi linawakilisha viwango vya kutegemeka; chati hii inakuruhusu kuangalia mabadiliko ya viwango vya kutegemeka kadri muda unavyosonga. Unaweza kurekebisha muda na tarehe ulizochagua ukitumia vichujio vya muda na tarehe katika sehemu ya juu kulia mwa chati.

Unaweza pia kuonyesha vipimo vifuatavyo ukitumia kichujio cha vipimo katika sehemu ya juu kushoto mwa chati: Mapato, Oda, Wanunuzi, Uwiano wa wanunuzi, ARRPU (vipimo hivi pia vimefafanuliwa katika sehemu ya Ufafanuzi wa vipimo). Ukichagua kipimo kingine, chati haitaonyesha viwango vya kutegemeka, kwa kuwa viwango hivi vinatokana na mapato.

Ili uone maelezo zaidi ya kiwango cha bidhaa, unaweza pia kutuma matokeo ya jaribio lako katika faili ya CSV. Unaweza kuangalia sehemu, muundo na mifano ya faili ya CSV ya kutuma kwa kupanua sehemu ya Ufafanuzi wa vipimo (kutuma katika CSV).

Kidokezo: Unaweza kubofya Angalia mipangilio ya jaribio ili uone maelezo ya mipangilio ya jaribio, ambayo unaweza pia kuchuja kulingana na kibadala au kulingana na nchi/eneo. Hii inaweza kukusaidia ukumbuke haraka vigezo vya jaribio lako.

Tumia vibadala

Kabla ya kutumia kibadala, kumbuka yafuatayo:

  • Iwapo bidhaa yako moja au zaidi za ndani ya programu zimeunganishwa na kiolezo cha bei, kutumia kibadala kutasasisha bei za nchi/eneo la jaribio lako na kutenganisha bidhaa hizi za ndani ya programu na kiolezo/violezo.
  • Unaweza tu kuweka kibadala kwa bidhaa zote za ndani ya programu na nchi au maeneo katika jaribio lako. Tunakokotoa umuhimu kitakwimu katika mpangilio wote wa majaribio na kwa hivyo hatuwezi kukuhakikishia matokeo na majibu sawa ikiwa umetumia tu baadhi ya nchi au maeneo na bidhaa za ndani ya programu katika mpangilio wako.

Ikiwa vibadala vyako vinalingana au vina utendaji mzuri zaidi ya bei yako elekezi, unaweza kusasisha bei yako kwa kutumia kibadala husika:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Majaribio ya bei (Chuma mapato > Majaribio ya bei).
  2. Bofya Tumia kibadala karibu na kibadala unachotaka kutumia.

Bei ya programu yako itasasishwa jinsi ilivyowekwa katika kibadala. Jaribio lako litaisha kiotomatiki siku 14 baada ya matokeo kubainishwa, au unaweza kubofya Tamatisha jaribio ili utamatishe mara moja.

Matokeo yanayoweza kupatikana ya jaribio

Kuna matokeo mengi yanayoweza kupatikana katika jaribio. Matokeo ya jaribio yatabaini hatua zako zinazofuata.

Matokeo ya jaribio Maana Madokezo/mapendekezo
Kibadala cha [X] kilikuwa na utendaji bora Kibadala cha [X] kimekuwa na umuhimu kitakwimu kwa kuzalisha matokeo yenye manufaa yakiwa na ongezeko kubwa zaidi katika mapato. Tumia kibadala cha [X] , kwa kuwa kilikuwa na utendaji mzuri sana ikilinganishwa na bei yako elekezi na vibadala vingine.
Vibadala vyote viwili vilikuwa na utendaji bora kuliko bei elekezi Vibadala vyote viwili vilipata mapato zaidi kuliko bei elekezi. Kagua matokeo na uchague kibadala cha kutumia. Utaamua kibadala cha kutumia.
Vibadala na bei elekezi vilikuwa na utendaji unaolingana Hakuna kibadala kilichopata mapato ya juu zaidi kuliko bei elekezi. Jaribio lako limekusanya data ya kutosha na matokeo ya vibadala na bei elekezi yanalingana.
Bei elekezi ilikuwa na utendaji bora zaidi Bei elekezi ilipata utendaji wa juu zaidi kuliko vibadala vyote viwili. Hii inaashiria kuwa viwango vyako vya bei vya sasa kwa nchi na bidhaa za majaribio tayari vimeboreshwa. Endelea kutumia bei elekezi kwa bidhaa na nchi za jaribio.
Data zaidi inahitajika Jaribio lako linaendelea. Data zaidi inahitajika ili kubainisha matokeo muhimu kitakwimu. Nenda kwenye hatua zinazopendekezwa kwa viwango vya chini vya data ili kubaini hatua zinazofuata.
Matokeo yasiyohitimishwa Jaribio lako limesitishwa mapema au limefikia kikomo cha muda wa jaribio wa miezi sita. Data zaidi inahitajika ili kubainisha matokeo muhimu kitakwimu. Jaribu kutekeleza jaribio jipya ukitumia mipangilio tofauti. Nenda kwenye hatua zinazopendekezwa kwa viwango vya chini vya data ili kubaini hatua zinazofuata. Huenda hii ni ishara kuwa wanunuzi hawajali bei za bidhaa za ndani ya programu katika nchi/maeneo ya jaribio.
Ufafanuzi wa vipimo

Jedwali hili linaorodhesha vipimo kutoka kwenye ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio lako.

Kipimo Ufafanuzi
Mapato ya bidhaa zote Mapato yote kutoka kwa watumiaji wa jaribio walionunua bidhaa za ndani ya programu ndani na nje ya jaribio katika kipindi mahususi cha muda.
Wastani wa mapato kwa kila mtumiaji anayelipa (ARPPU) Mapato yote ya bidhaa za ndani ya programu yakigawanywa kwa idadi ya wanunuzi wa kipekee (watumiaji walionunua bidhaa za ndani ya programu angalau mara moja ndani na nje ya jaribio) katika kipindi mahususi cha muda wa jaribio. Kipimo hiki kitakusaidia kuelewa umuhimu wa wanunuzi katika biashara yako.
Uwiano wa wanunuzi (siku 28)

Asilimia ya wanaotumia programu yako kila mwezi walionunua angalau bidhaa moja ya ndani ya programu wakati wa jaribio, ikiwa ni pamoja na bidhaa za ndani ya programu kutoka nje ya jaribio.

Kumbuka: Hiki ni kipimo muhimu katika kuelewa kushawishika kwa wanunuzi na kuongeza idadi ya watumiaji wanaolipia huduma yako.

Wanunuzi Watumiaji mahususi wanaonunua angalau bidhaa moja ya ndani ya programu kwa bei ya jaribio katika kipindi mahususi cha muda.
Mapato kutokana na watumiaji wapya waliosakinisha Mapato yote kutoka kwa watumiaji waliosakinisha programu kwa mara ya kwanza kwenye kifaa chochote baada ya tarehe ya kuanza jaribio na kuona bei ya jaribio kwa mara ya kwanza. Kumbuka kuwa baadhi ya watumiaji hujiondoa ili wasishiriki data hii na Google.
Maagizo Idadi ya ununuzi wa bidhaa za ndani ya programu za jaribio uliofanyika wakati wa jaribio katika kipindi mahususi cha muda.
Mapato Mapato yote kutoka kwa watumiaji walionunua bidhaa za ndani ya programu katika jaribio katika kipindi mahususi cha muda.
Ufafanuzi wa vipimo (utumaji wa CSV)

Jedwali hili linaorodhesha sehemu, muundo na mifano ya ufafanuzi wa vipimo vilivyotumwa kama faili ya CSV.

Sehemu

Muundo Mifano na madokezo
Tarehe Mfuatano

Tarehe 23 Machi 2023

Tarehe ya oda kulingana na Saa za Eneo la Pasifiki (katika muundo wa DD MMM YYYY).

Kitambulisho cha SKU Mfuatano

treasure_chest_for_new_users

Kitambulisho cha kipekee cha bidhaa ya ndani ya programu kilichobainishwa na msanidi programu.

Jina la Bidhaa Mfuatano

sarafu, usajili wa kila mwezi, na kadhalika.

Jina la bidhaa ya ndani ya programu lililobainishwa na msanidi programu.

Nchi Mfuatano

BR, US, FR na na kadhalika.

Msimbo wa kipekee wa nchi wa vipimo husika vya bidhaa za ndani ya programu.

Upande wa Jaribio Mfuatano

ELEKEZI, A, B

Upande wa jaribio wa vipimo husika vya bidhaa za ndani ya programu.

Sarafu ya Msanidi Programu

Mfuatano

USD, EUR, THB, na kadhalika.

Sarafu iliyotumika kwa oda. Hii ni sarafu ya nchi ulimo inayotumiwa kukulipa.

Mapato Nambari

2794.60

Jumla ya mapato yote ya bidhaa mahususi za ndani ya programu (kwa kuzingatia tarehe, nchi na upande wa jaribio).

Mapato Kutokana na Watumiaji Wapya Waliosakinisha Nambari

577.20

Mapato yote kutoka kwa watumiaji waliosakinisha programu kwa mara ya kwanza kwenye kifaa chochote baada ya tarehe ya kuanza jaribio na kuona bei ya jaribio kwa mara ya kwanza (kuzingatia bidhaa mahususi ya ndani ya programu, kuzingatia tarehe, nchi na upande wa jaribio.) Kumbuka kuwa baadhi ya watumiaji hujiondoa ili wasishiriki data hii na Google.

Maagizo Nambari

240

Jumla ya oda za bidhaa mahususi za ndani ya programu (kwa kuzingatia tarehe, nchi na upande wa jaribio).

Wanunuzi Nambari

197

Jumla ya wanunuzi wa bidhaa mahususi (kwa kuzingatia tarehe, nchi na upande wa jaribio). Wanunuzi ni watumiaji walionunua bidhaa mahususi ya ndani ya programu wakati wa jaribio.

Maswali yanayoulizwa sana

Kunja yote Panua yote

Majaribio hutekelezwa katika nchi/maeneo gani?

Nchi/maeneo yanastahiki majaribio ya bei iwapo yatatimiza vigezo vifuatavyo:

  • Nchi/maeneo ambako tayari umesambaza toleo (ikiwa ni pamoja na matoleo ya jaribio la ndani).
  • Nchi/maeneo ambako sarafu ya nchi ulimo inatumika.
Ni kwa nini sioni data yoyote kwenye ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio langu?

Ikiwa viwango vya data ni vya chini, hamna data inayopatikana. Pia, baadhi ya data inayoonyeshwa kwenye ukurasa wa uchanganuzi wa jaribio lako inaweza kuchelewa kwa hadi siku saba.

Je, ninaweza kutumia bidhaa za ndani ya programu zilizounganishwa na violezo vya bei?

Ndiyo. Kumbuka kuwa ukifanya jaribio lenye bidhaa ya ndani ya programu iliyounganishwa na kiolezo cha bei, bei za nchi/eneo la jaribio zitafungwa kwa kipindi chote cha jaribio. Hata hivyo, bado unaweza kubadilisha bei za nchi/maeneo mengine.

Ukiamua kutumia bei mpya baada ya kuisha kwa jaribio lako, bidhaa zote za ndani ya programu ulizofanyia majaribio hutenganishwa na violezo vya bei husika na kiolezo cha bei hakitabadilishwa. Iwapo unataka kutumia matokeo ya majaribio bila kutenganisha bidhaa zako za ndani ya programu na violezo vya bei, nenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa Kiolezo cha bei (Mipangilio > Violezo vya bei) na usasishe bei hapo.

Ili upate maelezo zaidi, angalia violezo vya bei.

Je, ninaweza kujaribu bei zilizo chini au juu zaidi ya vikomo vya sasa vya kila nchi?

Hapana, bei za majaribio zinaweza kufanyiwa majaribio ndani ya vikomo vya bei ya juu na chini vilivyobainishwa katika kila nchi/eneo. Unapoweka mabadiliko ya bei wakati wa kuweka mipangilio ya jaribio, ikiwa mabadiliko ya bei yamefikia kikomo cha juu au chini, itachukua kiotomatiki bei hiyo ya chini au ya juu. Ili ukague orodha yetu ya viwango vya bei na sarafu zinazoruhusiwa kulingana na nchi, angalia Maeneo yanayoruhusiwa kwa ajili ya usambazaji kwa watumiaji wa Google Play.

Je, ninahitaji kutumia Maktaba ya Malipo kupitia Google Play 5 ili niweze kutekeleza majaribio ya bei?

Hapana; iwapo umejumuishwa kwenye toleo lolote la mfumo wa utozaji wa Google Play, unaweza kufanya majaribio ya bei.

Je, ninawezaje kuona iwapo mtumiaji alifanya ununuzi katika kibadala badala ya bei elekezi?

Oda zote za jaribio huonekana katika ripoti za fedha za kila mwezi zinazoweza kupakuliwa (ripoti ya makadirio ya mauzo na ripoti ya mapato). Unaweza kuona bidhaa za ndani ya programu za jaribio zilizonunuliwa kwa bei elekezi na za vibadala katika nchi/maeneo unakofanyia jaribio lako la bei.

Je, ninaweza kutumia jaribio la A/B na majaribio ya bei kwa wakati mmoja?

Tunapendekeza kuwa usifanye kwa pamoja majaribio ya A/B ili upate matokeo yanayokufaa zaidi. Kwa mfano, Firebase hufanya kazi tofauti na majaribio ya bei katika Dashibodi ya Google Play na ukatizaji wowote katika bidhaa mahususi za ndani ya programu unaweza kuathiri uhakika wa matokeo ya jaribio.

Unatumia mbinu gani kubaini hali ya umuhimu kitakwimu?

Tunatumia jackknife (zana ya takwimu inayoruhusu ukadiriaji wa kibadala kupitia kuchukua sampuli upya) ili kukokotoa viwango vya kutegemeka na kisha tunatumia jaribio la uwezekano wa mfululizo wa mseto ili kudhibiti kiwango kilichozidishwa kisicho cha kweli kwenye ufuatiliaji endelevu. Umuhimu wa kitakwimu hubainishwa wakati viwango vya kutegemeka havikutani katika sifuri.

Ninahitaji ruhusa gani ili nitumie zana ya majaribio ya bei?

Ni sharti uwe na ruhusa za Kudhibiti upatikanaji dukani na Kuangalia data ya kifedha ili watumie majaribio ya bei.

Kwa nini jaribio langu limekoma?

Jaribio hukoma kiotomatiki siku 14 baada ya kufikia hali ya umuhimu kitakwimu au katika kikomo cha juu cha muda unaoruhusiwa wa jaribio wa miezi sita. Hatutamatishi jaribio katika muda uliokadiriwa uliowekwa katika mipangilio ya jaribio, badala yake tunalitamatisha baada ya tofauti ya hali umuhimu kitakwimu kutambuliwa, ndani ya siku 14 zilizotolewa za kutumia bei mpya kabla bei haijarudi kuwa bei halisi.

Je, inawezekana kuwa mtumiaji (anayetumia akaunti na kifaa sawa) anaweza kuona bei tofauti za kila siku baada ya jaribio kuanza?

Hapana, haiwezekani. Mtumiaji ataweza kuona bei moja tu katika kipindi cha jaribio.

Je, ninaweza kuweka nchi/maeneo zaidi katika jaribio linaloendelea?

Hapana, haiwezekani kwa sababu jaribio limeshaanza kukusanya matokeo kwa kutumia vigezo ulivyochagua awali. Unaweza kufanya jaribio la pili sambamba ukitumia nchi/maeneo ya ziada uliyochagua, au unaweza kutamatisha jaribio la sasa na uanzishe jaribio jipya. Kumbuka kuwa iwapo kuna bidhaa za ndani ya programu na nchi/maeneo yanayoingiliana, utahitaji kusubiri kwa siku 30 kabla ya kuanzisha jaribio jipya.

Ni kwa nini ninashindwa kurudufisha matokeo sawa na ya majaribio yangu ya bei?

Hali ya umuhimu kitakwimu inakokotolewa katika nchi/maeneo yote kwa pamoja na bidhaa zilizotumika katika jaribio badala ya kandokando kwa kila mseto. Ikiwa ungependa kurekebisha bei katika nchi/eneo mahususi, tunapendekeza uchague tu nchi/eneo hilo katika mipangilio ya jaribio.

Je, bado ninaweza kutumia kibadala baada ya jaribio kukomeshwa au kuisha?

Ndiyo, unaweza kutumia kibadala hata baada ya bei kurejea katika bei halisi.

Ni kwa nini baadhi ya majaribio yana matokeo yasiyokamilika?

Iwapo bidhaa za ndani ya programu za jaribio lako hazizalishi mapato ambayo ni tofauti sana na mapato yako ya bei elekezi au data haitoshi, matokeo yanachukuliwa kuwa hayajakamilika. Kwa matokeo haya, inawezekana kuwa wanunuzi hawajali bei zote mbili.

Je, kwa ujumla inashauriwa kutekeleza jaribio lenye bidhaa moja ya ndani ya programu kwa wakati mmoja au bidhaa nyingi za ndani ya programu?

Kwa jumla, sampuli kubwa huwa na ufanisi zaidi. Ikiwa bidhaa moja ya ndani ya programu unayopanga kufanyia jaribio ni moja ya bidhaa maarufu kabisa kwa wanunuzi wengi, basi inaweza kuwa vyema kufanyia jaribio bidhaa hiyo ya ndani ya programu pekee. Vinginevyo, tunahimiza kufanyia majaribio bidhaa nyingi za ndani ya programu pamoja ili kuongeza ufanisi wa jaribio lako.

Iwapo una bidhaa nyingi za ndani ya programu ambazo zinaweza kubadilishwa kwa kiwango fulani (kwa mfano, USD 0.99 kwa sarafu 60 za ndani ya programu na USD 4.99 kwa sarafu 300 za ndani ya programu), basi tunakuhimiza ujaribu bidhaa zote za ndani ya programu kwa pamoja ili kuepuka matukio ya bidhaa moja kulemea na kupunguza uuzaji wa nyingine.

Je, ninapaswa kutekeleza majaribio na kibadala kimoja au viwili?

Kwa ujumla tunapendekeza majaribio ya kibadala kimoja ukitumia bidhaa zako za ndani ya programu zenye bei halisi kuwa bei elekezi na bidhaa zako za ndani ya programu zenye punguzo kuwa bei ya kibadala. Jaribio la vibadala viwili lina bidhaa zako za ndani ya programu zenye bei halisi kuwa bei elekezi na bidhaa sawa za ndani ya programu katika viwango viwili tofauti vya bei. Inaweza kuwa vigumu kufasiri matokeo ya majaribio kama haya, na majaribio ya vibadala viwili yanachukua muda zaidi ya majaribio yenye kibadala kimoja kufikia hali ya umuhimu kitakwimu.

Ninapaswa kufasiri vipi viwango vya kutegemeka vya jaribio langu?

Ikiwa kiwango cha kutegemeka hakijumuishi thamani ya sifuri katika athari, tunachukulia kuwa haya ni matokeo muhimu kitakwimu. Katika hali hii, athari ni tofauti kati ya bei elekezi na kibadala.

Huu ni mfano wa jinsi viwango vyako vya kutegemeka vinavyoweza kuonekana ukiwa na tokeo chanya kamilifu:

CI_conclusive_positive

Huu ni mfano wa jinsi viwango vyako vya kutegemeka vinavyoweza kuonekana ukiwa na tokeo hasi kamilifu:

CI_conclusive_negative

Huu ni mfano wa jinsi viwango vyako vya kutegemeka vinavyoweza kuonekana ukiwa na tokeo lisilo kamilifu linalohitaji data zaidi:

CI_not_conclusive

Je, Google inawapa wasanidi programu ulinzi wowote dhidi ya matukio yanayotokana na tofauti za bei?

Ndiyo, tunafuatilia kudanganya kwa kuonyesha eneo bandia la mtumiaji na kuchukua hatua za kupunguza athari kwa wasanidi programu wetu na bidhaa zao.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8397237439516321958
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false