Thibitisha na uendelee kutumia viungo mahususi

Ukitumia ukurasa wa Viungo mahususi (Kuza > Viungo mahususi) kwenye Dashibodi ya Google Play, unaweza:

  • Kudhibiti mipangilio ya viungo vyako mahususi na kuongeza ushiriki zaidi kwenye maudhui ya ndani ya programu. 
  • Angalia hali ya uambatishaji wako kati ya tovuti na programu na uone mahali panapohitaji uboreshaji kwa kuweka viungo mahususi kwenye URL zako zinazotembelewa zaidi. 
  • Unaweza kutumia marekebisho ili uweke, uzime na urekebishe matatizo kwenye viungo mahususi, bila kuchapisha toleo jipya la programu.

Ikiwa umeunganisha akaunti ya Google Ads, unaweza kuangalia kampeni ambazo zinatumia viungo mahususi, kupata maarifa kuhusu watu unaowafikia na kukagua matoleo ya kurusa zako za kutua zinazotumia viungo mahususi.

Muhtasari wa viungo mahususi

Viungo mahususi ni URL za mpango wowote zinazowaelekeza watumiaji kwenye sehemu maalum ya programu badala ya tovuti. Wasanidi programu wanaweza kuunda viungo mahususi kwa kuweka vichujio vya utaratibu wa kuratibu vinavyowaelekeza watumiaji kwenye shughuli sahihi katika programu zao.

Ukurasa wa Viungo mahususi hurahisisha mchakato wa kuunda, kudumisha na kuthibitisha viungo mahususi. Ukurasa huu una vichupo viwili:Mipangilio ya programu na URL za Wavuti. Kichupo cha Mipangilio ya programu hutoa muhtasari wa mipangilio ya toleo la programu yako na viungo mahususi vinavyohusika. Unaweza kutumia kichupo hiki:

  • Kuangalia muhtasari rahisi lakini wenye maelezo ya kina kuhusu mipangilio ya viungo mahususi vilivyo kwenye toleo la programu ulilochagua.
  • Kubaini kwa muhtasari matatizo ya mipangilio ya viungo mahususi, ili uweze kuyatatua mapema zaidi.
  • Kuunda na kuchapisha marekebisho, kuzima na kurekebisha matatizo kwenye viungo mahususi, bila kuchapisha toleo jipya la programu.

Kichupo cha URL ya Wavuti huonyesha maelezo yanayohusiana na utendaji wa programu yako kwenye wavuti, kama vile URL zako muhimu zaidi zilizotambuliwa kwenye wavuti na vikoa vilivyobofya zaidi kutoka kwenye kampeni zako zilizounganishwa za Google Ads pamoja na maelezo ya hali. Unaweza kutumia kichupo hiki:

  • Kuangalia ni kampeni gani za utangazaji zina viungo mahususi na upate maarifa kuhusu ufikiaji wa watumiaji wa viungo mahususi (ikiwa una akaunti iliyounganishwa ya Google Ads).
  • Kukagua kwanza matoleo yenye viungo mahususi ya kurasa zako za kutua, ambayo yinaweza kulinganishwa upande kwa upande na toleo la wavuti.
  • Kuangalia orodha ya URL zako muhimu zaidi za wavuti pamoja na hali ya kuwa na viungo mahususi.
  • Kugundua fursa ulizokosa za kuweka kiungo mahususi kwenye maudhui na kuongeza kushiriki kwa watumiaji.
Ukurasa wa Viungo mahususi pia una kipengele thabiti cha utafutaji ili uweze kuangalia kwa urahisi orodha yako kamili ya njia, vikoa na mipango maalum.​

Vipengele vya ukurasa wa viungo mahususi

Sehemu zilizo hapa chini zinaelezea vipengele na utendaji wa ukurasa wa Viungo mahususi.

Vipengele vya jumla

Hivi ni vipengele vya jumla ambavyo unaweza kuona na kutumia katika vichupo vyote viwili kwenye ukurasa wa Viungo mahususi. Bofya sehemu ili uipanue au uikunje.

Kiteua programu

Unaweza kuchagua toleo la programu unalotaka kukagua viungo vyake mahususi kwa kutumia kiteua toleo la programu kilichopo kwenye sehemu ya juu kulia mwa ukurasa. Unaweza kuchagua toleo lolote la programu linalotumika kwenye kikundi chochote (toleo la umma, jaribio la watumiaji mahususi au jaribio la ndani). Majedwali yataonyesha data ya kiungo mahususi kulingana na toleo la programu ulilochagua.

Kumbuka: unaweza kuchagua kwenye matoleo yote ya programu yako yanayotumika (yaani, matoleo ya programu ambayo bado yanatolewa kwa watumiaji). Huenda ukawa na watumiaji wenye toleo la zamani lililosanikishwa ambalo halitolewi tena. Google Play inachukulia matoleo haya ya programu kuwa yameondolewa, kwa hivyo hutaweza kuchagua matoleo haya.

Marekebisho

Unaweza kuunda na kuchapisha marekebisho ili uweke, uzime na urekebishe matatizo kwenye viungo mahususi, bila kuchapisha toleo jipya la programu. Ukishaunda rekebisho, unaweza kuchagua matoleo yanayotumika ya programu yako ambako litatumika. Kitufe cha Unda rekebisho kipo karibu na kiteuzi cha toleo la programu katika sehemu ya juu kulia ya ukurasa.

Nenda kwenye 'Rekebisha mipangilio ya viungo vyako mahususi' ili upate maelezo zaidi.

Kadi za Mihtasari

Katika sehemu ya juu ya ukurasa, huenda ukaona baadhi ya kadi za muhtasari zenye arifa kuhusu viungo vyako vya moja kwa moja. Kadi hizi huangazia masuala muhimu katika uwekaji wa viungo vyako vya moja kwa moja ili uweze kubaini kwa haraka vipengee unavyohitaji kuzingatia. Huenda kadi za muhtasari zikawa na vidokezo na vitendo tofauti kulingana na maudhui. Kwa mfano, kubofya Angalia vikoa kutachuja baadhi ya majedwali kwenye ukurasa ili kuyaonyesha, ilhali kubofya Pata maelezo zaidi kutakuelekeza kwenye maudhui mahususi katika hati ambayo yatakusaidia kupata maelezo zaidi kutoka kwenye viungo vyako mahususi.

Utafutaji na vichujio

Majedwali yote kwenye ukurasa wa Viungo mahususi yanaweza kutafutwa na kupangwa. Unaweza kutumia mbinu ya kutafuta ili kupata matokeo yanayohusiana na orodha kamili ya njia, vikoa na mipango maalum inayohusiana na toleo la programu yako. Mbinu ya kupanga hupanga tu data ambayo imepakiwa kwa sasa (kwa chaguomsingi au kulingana na matokeo yako ya utafutaji).

Katika jedwali la Vikoa, unaweza kutafuta vikoa (utafutaji wa kiambishi cha msimbo), na kuchuja kulingana na hali (SAWA, Si SAWA). Unaweza pia kutafuta njia na mipango maalum kwa kutumia mbinu zifuatazo:

  • Tafuta mpango (utafutaji wa kiambishi cha msimbo)
  • Tafuta vikoa (utafutaji wa kiambishi cha msimbo)
  • Tafuta njia (utafutaji wa kiambishi cha msimbo)
  • Tafuta shughuli (utafutaji wa kiambishi cha msimbo)

Kumbuka: Kwa jedwali la Njia, ikiwa utaweka URL kamili (kwa mfano, http://example.com/someStrangePattern) dashibodi itajaribu kulinganisha muundo kulingana na aina ya njia. Angalia mfano huu:

Njia iliyobainishwa katika faili ya maelezo ni mchoro (https://example.com/Some.*Pattern).

Katika hali hii, ukiandika URL kamili, njia hii inarudishwa. Unaweza kutumia utendaji huu kuelewa aina ya vichujio vya utaratibu wa kuratibu na njia zitakazowajibika kushughulikia URL iliyowekwa kwenye kisanduku cha kutafutia.

Kipengele cha utafutaji hupuuza vigezo vya hoja, kwa hivyo unaweza kubandika URL kamili kwenye kisanduku cha kutafutia bila kusababisha matatizo.

Mipangilio ya programu

Kichupo cha Mipangilio ya programu hutoa muhtasari wa kuweka mipangilio ya toleo la programu yako na viungo mahususi vinavyohusika. Sehemu zilizo hapa chini zinaelezea majedwali hayo mawali unayoweza kuona na kutumia kwenye kichupo. Bofya sehemu ili uipanue au uikunje.

Jedwali la vikoa

Jedwali la Vikoa liko kwenye kichupo cha Mipangilio ya programu na huorodhesha vikoa vyote vilivyobainishwa kwenye faili ya maelezo ya programu yako. Linakusaidia kuthibitisha uhusiano kati ya URL zako na programu yako katika kuunda viungo vya programu. Ikiwa programu yako haitumii Viungo vya Programu kwa makusudi, lakini bado ungependa kutumia viungo vya wavuti kwa kuwafanya watumiaji wako waweke mapendeleo katika mipangilio, huenda sehemu hii isikufae zaidi, kwa kuwa vikoa vyako vitashindwa kuhusishwa na programu yako kulingana na muundo.

Iwapo vikoa vyako vina matatizo yoyote, unaweza kuwekelea kiashiria juu ya safu wima ya hali ili uone ni ukaguzi upi hasa haujafanikiwa. Unabofya katika safu mlalo ili uangalie matatizo kwa kina zaidi.

Ikiwa una matatizo kwenye jedwali lako la Vikoa, zifuatazo ni mbinu unazoweza kutumia kuyatatua:

  1. Tumia programu ya uundaji wa JSON katika tangazo lililowekelewa juu ili unakili moja kwa moja maudhui ya faili yako ya assetlinks kwenye kikoa chako, ambacho kitakuwa na maelezo yote muhimu ya kufanya viungo vya programu yako vifanye kazi. Kumbuka yafuatayo:
    • Baada ya kufanya mabadiliko yanayohitajika kwenye faili ya assetlinks na kuipakia kwenye kikoa chako, rudi kwenye ukurasa wa Viungo mahususi kisha ukague ikiwa tatizo hilo limeshatatuliwa.
    • Programu ya uundaji ni nyongeza, kumaanisha kuwa itawajibika kwa chochote ambacho tayari kiko kwenye kikoa chako. Ni salama kabisa kuchukua maudhui yote na kuyabandika jinsi yalivyo (au kupakua faili) — hali hii haitaathiri uoanifu na programu nyingine ambazo huenda unamiliki. Tunaangazia mabadiliko yaliyopendekezwa kwa rangi ya kijani.
  2. Kurekebisha matatizo kwa kutumia kikoa chako haikuhakikishii kuwa watumiaji wote watakuwa na viungo vya programu vilivyothibitishwa. Katika matoleo mengi ya Android (kabla ya toleo la Android 12), uthibitishaji wa vikoa hufanyika wakati wa kusakinisha, kwa hivyo utahitaji kuchapisha toleo jipya la programu yako ikiwa ungependa matoleo yaliyosakinishwa zamani yaanze kupokea viungo vya programu. 
Jedwali la viungo vya faili ya maelezo ya Programu

Jedwali la viungo vya faili ya maelezo ya Programu liko kwenye kichupo cha Mipangilio ya programu na huonyesha data inayohusiana na faili ya maelezo ya programu yako. Google Play huthibitisha vichujio vya utaratibu wa kuratibu na kuvipanga kulingana na njia (kwa viungo vya wavuti). Ikiwa kuna matatizo yoyote, unaweza kubofya kwenye safu mlalo yoyote ili upate maelezo ya kina ya jinsi ya kurekebisha programu yako. Kubofya kwenye njia pia kutaorodhesha viungo vyote vinavyotumika chini ya njia hii. Mchakato huu utakuwa mseto wa mipango (http/https) na vikoa vilivyobainishwa kwa ajili ya vichujio vya utaratibu wa kuratibu ambavyo vina njia na shughuli hii.

Kumbuka: Ili urekebishe matatizo yoyote yaliyoorodheshwa kwenye jedwali la viungo vya faili ya maelezo ya Programu, ni sharti urekebishe faili ya AppManifest.xml na uchapishe toleo jipya la programu yako. Matatizo ya toleo la sasa la programu yako yatasalia, kwa sababu yanahusishwa na toleo la programu ambalo tayari limechapishwa.

Kidokezo: Unaweza kutambua kwamba baadhi ya hati za Android zinazopendekeza kuwa na kichujio tofauti cha utaratibu wa kuratibu kwa kila lebo ya <data>. Hata hivyo, tunapendekeza uhifadhi viungo vyote vya wavuti ambavyo vitanaswa na njia au shughuli sawa chini ya kichujio husika cha utaratibu wa kuratibu ili kuwezesha udhibiti wa faili yako ya maelezo. Kuwa na lebo nyingi za <data> ni hatari kwa sababu zimeunganishwa kwenye mabadiliko yote ya mpango, njia na kikoa. Lakini ikiwa utaweka njia sawa kwa ajili ya viungo vya wavuti (ambapo mipango itakuwa http au https kila wakati), suala hili halina tatizo.

URL za Wavuti

Kichupo cha URL za Wavuti huonyesha ufikiaji wa viungo mahususi (idadi iliyojumlishwa inayoonyesha asilimia ya URL maarufu kutoka kwa vikoa vyako vilivyoidhinishwa, zinazotumia viungo mahususi) na maelezo mengine yanayohusiana na maelezo na utendaji wa programu yako kwenye wavuti, kama vile URL zako muhimu zilizotambaliwa kwenye wavuti na vikoa ambavyo watumiaji walibofya zaidi kutoka kwa kampeni zako zilizounganishwa za Google Ads na maelezo ya hali. Sehemu zilizo hapa chini zinaelezea majedwali hayo mawali unayoweza kuona na kutumia kwenye kichupo. Bofya sehemu ili uipanue au uikunje.

Jedwali lenye idadi kubwa ya walioangalia tangazo (akaunti za Google Ads zilizounganishwa pekee)

Jedwali lenye idadi kubwa ya walioangalia tangazo linapatikana kwenye kichupo cha URL za Wavuti na — Ikiwa una akaunti ya Google Ads iliyounganishwa — huorodhesha vikoa kutoka kwenye kampeni zako za utangazaji ambazo zilipata mibofyo mingi zaidi huku ufikiaji wa watumiaji ukiorodheshwa katika asilimia. Ufikiaji wa watumiaji ni asilimia ya watumiaji waliosakinisha programu yako ambao, baada ya kufuata URL ya wavuti, huamua kutumia ndani ya programu (au huonyeshwa kiteua programu) ikilinganishwa na kuendelea kuwa kwenye wavuti.

Unaweza pia kutazama hali ya kikoa (Kiungo mahususi, Kiungo kisicho mahususi, Matatizo yaliyopatikana). Ukigundua kuwa kuna vikoa ambavyo bado hujawekea viungo mahususi lakini vinapata mibofyo mingi, kuweka viungo mahususi kwenye vikoa hivi kunaweza kuwa fursa nzuri ya kuongeza kushiriki kwa watumiaji kwa kuwaelekeza watumiaji moja kwa moja kwenye programu yako.

Unaweza kubofya safu mlalo yoyote ili upate maelezo ya kina kuhusu kikoa mahususi. Ikiwa URL yako haijawekewa viungo mahususi, unaweza kufuata hatua kwenye skrini ili kuweka mipangilio ya programu yako na kuthibitisha umiliki wa kikoa, au uangalie mwongozo wa wasanidi programu kwa usaidizi zaidi. Ikiwa huduma ipo, unaweza pia kuona onyesho la kukagua picha za skrini upande kwa upande, kuhusu jinsi kikoa chako chenye viungo mahususi kinavyoonekana katika wavuti na kwenye programu yako. Hatimaye, unaweza kuona uchanganuzi wa kina wa ufikiaji wa watumiaji, unaoonyesha matokeo yafuatayo ya watumiaji wanaotarajiwa kwa URL uliyochagua kwenye matoleo yote ya programu yanayoonyeshwa katika asilimia:

  • Watumiaji walioelekezwa kwenye programu
  • Watumiaji walioelekezwa kwenye kiteuzi cha programu
  • Watumiaji walioelekezwa kwenye kivinjari
URL zilizotambaliwa kwenye wavuti

Jedwali la URL zilizotambaliwa kwenye wavuti liko kwenye kichupo cha URL za Wavuti na hukuonyesha URL muhimu zaidi zilizotambaliwa kwenye wavuti, zenye ufikiaji wa watumiaji ulioorodheshwa katika asilimia. Unaweza pia kutazama hali ya kikoa (Kiungo mahususi, Kiungo kisicho mahususi, Matatizo yaliyopatikana). Ukigundua kuwa kuna vikoa ambavyo bado hujawekea viungo mahususi lakini vinapata mibofyo mingi, kuweka viungo mahususi kwenye vikoa hivi kunaweza kuwa fursa nzuri ya kuongeza kushiriki kwa watumiaji kwa kuwaelekeza watumiaji moja kwa moja kwenye programu yako.

Unaweza kubofya safu mlalo yoyote ili upate maelezo ya kina kuhusu kikoa mahususi. Ikiwa URL yako haijawekewa viungo mahususi, unaweza kufuata hatua kwenye skrini ili kuweka mipangilio ya programu yako na kuthibitisha umiliki wa kikoa, au uangalie mwongozo wa wasanidi programu kwa usaidizi zaidi. Ikiwa huduma ipo, unaweza pia kuona onyesho la kukagua picha za skrini upande kwa upande, kuhusu jinsi kikoa chako chenye viungo mahususi kinavyoonekana katika wavuti na kwenye programu yako. Hatimaye, unaweza kuona uchanganuzi wa kina wa ufikiaji wa watumiaji, unaoonyesha matokeo yafuatayo ya watumiaji wanaotarajiwa kwa URL uliyochagua kwenye matoleo yote ya programu yanayoonyeshwa katika asilimia:

  • Watumiaji walioelekezwa kwenye programu
  • Watumiaji walioelekezwa kwenye kiteuzi cha programu
  • Watumiaji walioelekezwa kwenye kivinjari

Rekebisha mipangilio ya viungo vyako mahususi

Unaweza kuunda na kuchapisha marekebisho ili uweke, uzime na urekebishe matatizo kwenye viungo mahususi, bila kuchapisha toleo jipya la programu. Marekebisho hayahifadhiwi ili yatumike katika matoleo ya siku zijazo ya programu yako. Unaweza kuhifadhi mabadiliko haya katika matoleo ya siku zijazo ya programu kwa kusasisha faili ya maelezo ya programu yako.

Ukishaunda rekebisho, unaweza kuchagua matoleo yanayotumika ya programu yako ambako litatumika. Kitufe cha Unda rekebisho kipo karibu na kiteuzi cha toleo la programu katika sehemu ya juu kulia ya ukurasa.

Ili uunde rekebisho:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Viungo mahususi (Kuza > Viungo mahususi).
  2. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, bofya Unda rekebisho
    • Kumbuka: Ukishabofya Unda rekebisho, utaona ujumbe karibu na sehemu ya chini ya ukurasa wa Viungo mahususi ukieleza kuwa "Hali ya rekebisho imewashwa: Hakuna mabadiliko yanayoshughulikiwa". Hali hii itajisasisha kadiri unavyofanya mabadiliko ya mipangilio ya viungo vyako mahususi.
  3. Chagua Weka kiungo cha wavuti ikiwa ungependa kuweka njia mpya kwenye viungo vyako mahususi.
    • Iwapo ungependa kutumia kikoa ambacho bado hakijabainishwa kwenye Faili ya maelezo ya Progamu yako, ni lazima kwanza ubofye Weka kikoa katika jedwali la vikoa. Baada ya kikoa chako kuthibitishwa katika kipengele cha kuwekelea, kitapatikana ili utumie unapoweka viungo vipya vya wavuti. Hata hivyo, hakitaonekana kwenye jedwali la vikoa hadi uchapishe rekebisho ukitumia kikoa hicho. 
      • Kumbuka: Vikoa vilivyowekwa kwa kutumia kitufe cha Weka kikoa vitasalia kuwa sehemu ya mipangilio yako ya matoleo ya siku zijazo.
  4. Fafanua vigezo vya URL kwa kuweka maelezo yanayohitajika:
    • Shughuli: Chagua shughuli ukitumia menyu kunjuzi.
    • Mpango na kupangisha: Chagua mpango na upangishe ukitumia menyu kunjuzi.
    • Njia: Weka URL kamili ambako ungependa kiungo chako mahususi kiwaelekeze watumiaji.
  5. Bofya Weka kwenye rasimu ya rekebisho. Baada ya kuweka kwenye rasimu yako ya rekebisho, utaona ujumbe karibu na sehemu ya chini ya ukurasa ukieleza kuwa "Hali ya rekebisho imewashwa: Badiliko 1 la kiungo mahususi linashughulikiwa". 
  6. (Si lazima) Iwapo ungependa kuweka rekebisho kwenye viungo vingine mahususi, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata mchakato huohuo tena. 
  7. Ukiwa tayari kuchapisha marekebisho yako, bofya Kagua kisha uchapishe.

Unaweza pia kutumia marekebisho ili uzime viungo mahususi. Unapozima kiungo mahususi, watumiaji hawataelekezwa moja kwa moja kwenye programu yako kupitia viungo vinavyohusiana na njia hii, lakini wataona kiteuzi cha programu au kuelekezwa kwenye kivinjari. Ili uzime kiungo mahususi:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Viungo mahususi (Kuza > Viungo mahususi).
  2. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, bofya Unda rekebisho
    • Kumbuka: Ukishabofya Unda rekebisho, utaona ujumbe karibu na sehemu ya chini ya ukurasa wa Viungo mahususi ukieleza kuwa "Hali ya rekebisho imewashwa: Hakuna mabadiliko yanayoshughulikiwa". Hali hii itajisasisha kadiri unavyofanya mabadiliko ya rekebisho lako.
  3. Karibu na njia ambayo ungependa kuzima, bofya Zima.
  4. (Si lazima) Iwapo ungependa kuzima viungo mahususi, unaweza kufanya hivyo kwa kufuata mchakato huohuo tena. 

Ukiwa tayari kuchapisha marekebisho yako, bofya Kagua kisha uchapishe. Kagua kisha uchapishe rekebisho lako ili utumie mabadiliko kwenye toleo la programu ulilochagua.

Maswali yanayoulizwa sana

Ufikiaji wa watumiaji ni nini?

Ufikiaji wa watumiaji ni asilimia ya watumiaji waliosakinisha programu yako ambao, baada ya kufuata URL ya wavuti, huamua kutumia ndani ya programu (au huonyeshwa kiteua programu) ikilinganishwa na kuendelea kutumia wavuti. Kadri asilimia inavyoongezeka, ndivyo watumiaji wengi wanavyopata hali bora zaidi ya kutua. Data huonyeshwa upya mara moja kwa siku.

URL zilizotambaliwa kwenye wavuti ni nini?

URL zilizotambaliwa kwenye wavuti ni orodha ya URL maarufu ambazo tumetambua kuwa muhimu zaidi katika vikoa vyako vilivyothibitishwa. Hizi ni pamoja na kurasa zilizotembelewa na zilizorejelewa zaidi ambazo tunaona watu wengi wakizifungua kwenye wavuti. Kuweka viungo mahususi kwenye URL zako muhimu zaidi za wavuti kutahakikisha ushirikishaji wa juu katika maudhui ya programu yako. Orodha ya URL huonyeshwa upya mara moja kwa siku.

Je, ninaweza kuunganisha vipi akaunti yangu ya Google Ads?

Ili kuona hali ya viungo mahususi za kurasa za kutua kutoka kwenye kampeni zako za Google Ad, unahitaji kwanza kuunganisha akaunti yako ya Google Ads. Ili kufanya hivyo, fuata hatua hizi. Baada ya kuunganisha, URL za kampeni zako za utangazaji zitaonekana kwenye ukurasa wa Viungo mahususi katika Dashibodi ya Google Play.

Ufikiaji wa viungo mahususi ni nini?

Ufikiaji wa viungo mahususi ni idadi iliyojumlishwa inayoonyesha asilimia ya URL maarufu kutoka kwenye vikoa vyako vilivyothibitishwa ambavyo vina viungo mahususi. Ufikiaji wa juu wa viungo mahususi unaweza kukusaidia kuhakikisha kuwa watumiaji wako wanapata hali bora ya matumizi ya bidhaa na huduma zako. Ufikiaji huhesabiwa kulingana na hali ya vifaa vya watumiaji vilivyosakinishwa na huonyeshwa upya kila siku.

Nini hufanyika ninapoongeza kikoa?

Unapoongeza kikoa kilichothibitishwa, Dashibodi ya Google Play itaanza kukuonyesha URL zinazohusiana na kikoa hiki. Kumbuka kwamba hii haitafanyika papo hapo; kunaweza kuwa na kuchelewa kwa takribani siku moja kabla ya kuona URL zozote kutoka kwa kikoa ambacho umeongeza hivi punde. Kumbuka kuwa kwa sasa hakuna njia ya kuondoa vikoa vilivyothibitishwa kwenye orodha.

Nimerekebisha viungo vya assetlinks kufuatia mapendekezo ya Dashibodi ya Google Play, lakini ufikiaji haubadiliki. Kwa nini?

Ufikiaji wa kiungo mahususi hautokani na hali ya sasa ya programu yako, bali hutokana na iwapo watumiaji ambao wamesakinisha programu yako wanaweza kufungua URL fulani au la. Unapobadilisha viungo vyako vya assetlinks au kuongeza vichujio vipya vya utaratibu wa kuratibu, itachukua muda kwa watumiaji wa bidhaa waliosakinisha kuafikiana na mabadiliko haya. Unaweza kuona idadi ya ufikiaji ikibadilika polepole watumiaji wako wanapopokea masasisho yako.

Ni kwa nini baadhi tu ya URL ndizo zina picha za skrini?

Kwa sasa tunajaribu seti ndogo ya URL zinazopatikana kwenye ukurasa wa picha za skrini. Ukiona ujumbe unaosema onyesho la kukagua halipatikani, haimaanishi kuwa kuna tatizo kwenye programu yako. Kwa sasa maonyesho ya kukagua yanapatikana kwa seti ndogo ya URL, lakini tunajitahidi kuongeza ufikiaji wa kipengele hiki katika siku zijazo.

URL hupangwa vipi katika vikundi?

Tulitumia njia ya nasibu kubaini URL ambazo zinapaswa kupangwa kwenye kikundi kimoja. Ikiwa programu yako tayari ina vichujio vya utaratibu wa kuratibu, vitaonekana kila wakati kama vikundi katika kiolesura. Algoriti yetu hupanga tu URL ambazo hazilingani na vichujio vyovyote vya utaratibu wa kuratibu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8310818098570122749
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false