Tunatoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)

Kuanzia tarehe 13 Machi 2024, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji katika eneo la EEA, lazima watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo hapa chini na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API ya mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Kama sehemu ya jitihada za kutii Sheria ya Masoko Dijitali (DMA), tunawapatia wasanidi programu wanaouza huduma au maudhui ya dijitali chaguo la kuwapa watumiaji wao walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) mfumo mbadala wa utozaji kando na ule wa Google Play. Ada za huduma, ambazo hutumika katika uwekezaji wetu kwenye Google Play na Android, zitaendelea kutumika na sharti wasanidi programu walipe Google ada husika za huduma. Kwa maelezo zaidi, angalia chapisho letu kwenye blogu.

Masharti ya Kujiunga

Ili utimize masharti ya kujiunga na mpango huu:

  • Ni lazima programu yako iwe ya michezo au ya kawaida kwenye umbo lolote linalowapatia watumiaji mfumo mbadala wa utozaji katika eneo la EEA.
  • Msanidi programu ni lazima awe biashara iliyosajiliwa.

Masharti

Wasanidi programu wanaoshiriki katika mpango huu ni lazima watii masharti yafuatayo:

  • Wawe biashara iliyosajiliwa.
  • Watoe mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji katika nchi za EEA pekee.
  • Kutimiza masharti yanayofaa ya ulinzi wa mtumiaji.
  • Wawe wanatoa tu mifumo mbadala ya utozaji ndani ya programu.
  • Kutii Kiwango cha Usalama wa Data cha Sekta ya Kadi za Malipo (PCI-DSS) (ikiwa unashughulikia data ya kadi ya mkopo na malipo).
  • Kutoa huduma kwa wateja wanaotumia mfumo mbadala wa utozaji (ikijumuisha bidhaa zozote zinazouzwa kupitia mfumo mbadala wa utozaji) na mfumo mbadala wa utozaji ni lazima ubainishe mchakato wa kupinga miamala ambayo haijaidhinishwa.
  • Kulipa Google ada za huduma zinazotumika. Mtumiaji akinunua kupitia kwa mfumo mbadala wa utozaji, bila kujumuisha chaguo la mtumiaji, ada ya kawaida ya huduma ambayo mtumiaji hulipa itapunguzwa kwa asilimia 3.
  • Jumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, inayorahisisha utekelezaji wa masharti ya hali ya utumiaji na kuripoti. Wasanidi programu ambao hawako tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji wana chaguo la kutekeleza skrini ya taarifa wao wenyewe na kuripoti miamala hadi tarehe 13 Machi 2024.
  • Kabla ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, wasanidi programu wanahitajika kufuata mwongozo wa muda wa hali ya utumiaji ili wadumishe hali thabiti ya utumiaji na kuwasaidia watumiaji kufanya uamuzi sahihi.
  • Tuarifu mapema kuhusu mabadiliko unayokusudia kufanya kwenye mapendeleo yako ya kuandikisha programu, kama vile kuzima au kuwasha kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwenye programu au soko mahususi. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasilisha mabadiliko tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Tafadhali kumbuka kwamba vigezo na masharti vinaweza kubadilika.

Kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji

Ikiwa ungependa kutoa mfumo mbadala wa utozaji na utakuwa unatumia API za mfumo mbadala wa utozaji kuanzia tarehe ya kutoa chaguo hilo, sharti ukamilishe hatua zifuatazo:

  1. Kagua masharti kwenye ukurasa huu ili ubaini iwapo programu zako zinatimiza masharti ya kujiunga.
  2. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango, kupitia kwa usaidizi wa timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo inavyohitajika).
  3. Kamilisha mchakato wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji kama inavyoelezwa kwenye mwongozo huu wa ujumuishaji wa API.
  4. Dhibiti mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji wa Dashibodi yako ya Google Play, ili kujijumuisha au kujiondoa kwenye kila programu yako, kupakia nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  5. Ripoti kwa Google Play miamala yote iliyoidhinishwa inayofanywa na watumiaji wa eneo la EEA, ndani ya saa 24 ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji.
  6. Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwenye API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Ikiwa tayari unashiriki kwenye mpango huo na unahamia kwenye API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kuruka hatua ya 1 na 2 hapo juu. Baada ya kukamilisha hatua zilizoainishwa hapo juu na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Ujumuishaji bila uwekaji otomatiki

Ikiwa ungependa kutoa mfumo mbadala wa utozaji lakini hauko tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, ni sharti ukamilishe hatua zifuatazo ili ujiandikishe mwenyewe:

  1. Kagua masharti kwenye ukurasa huu ili ubaini iwapo programu zako zinatimiza masharti ya kujiunga.
  2. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango kwa usaidizi wa timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo).
  3. Bainisha programu na masoko yanayotimiza masharti, ambapo utakuwa ukitoa mfumo mbadala wa utozaji kwa kutumia fomu ya kujiandikisha ambayo utatumiwa kwa njia ya barua pepe baada ya kujaza fomu ya taarifa ya bili.
  4. Fuata masharti kama yalivyobainishwa kwenye ukurasa huu.
  5. Piga hesabu kamili na uripoti kwa Google Play kiasi cha miamala yote iliyolipwa kupitia mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutuma ankara. Maagizo ya kuripoti kila mwezi yatatolewa kwa wasanidi programu waliojaza fomu ya taarifa na kukamilisha utaratibu wa kuanza ushirikiano wa kimkataba wa mpango huu.
  6. Kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama, jumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, hamisha usajili wowote unaoendelea ambao ulianza ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki na usasishe mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Baada ya kuhamisha usajili unaoendelea na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Ikiwa una maswali yoyote ya ziada, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi hapa.

Maswali yanayoulizwa sana

Je, ni nchi zipi zinazounda nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?
Hivi sasa EEA inajumuisha: Austria, Bulgaria, Denmaki, Estonia, Hangaria, Irelandi, Isilandi, Italia, Jamhuri ya Cheki, Jamhuri ya Saiprasi, Korasia, Lasembagi, Lishenteni, Litwania, Malta, Norwe, Polandi, Romania, Slovakia, Slovenia, Ubelgiji, Ufaransa, Ufini, Ugiriki, Uhispania, Uholanzi, Ujerumani, Ureno, na Uswidi.
Programu yangu imekataliwa hivi karibuni kwa kutotii sera za Malipo ya Google Play. Ninapaswa kufanya nini?

Google haitaondoa au kukataa masasisho ya programu kutoka kwa wasanidi programu wanaoshiriki kwa kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA. Mfumo wa utozaji wa Google Play utaendelea kuhitajika kwa programu na michezo inayosambazwa kupitia Google Play kwa watumiaji walio nje ya EEA isipokuwa mahali ambako wametimiza masharti ya mfumo mbadala wa utozaji.

Ikiwa programu yako inatimiza masharti ya mpango na mengineyo, unapaswa kujaza fomu ya taarifa na uwasilishe sasisho la programu yako. Kumbuka, itatuchukua muda kiasi ili ukamilisha maombi yako. Ikiwa hujatimiza masharti ya kujiunga na mpango huu, utatakiwa usasishe programu yako ili itii sera za Malipo ya Google Play kisha uitume upya.

Kwa sasa ninatoa mfumo wa utozaji wa Google Play. Je, sasa ninaweza kutoa mfumo wa utozaji wa Google Play pamoja na mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?

Ikiwa ungependa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play, jiandikishe kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji ili uwape watumiaji chaguo. Pata maelezo zaidi na ujisajili kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji hapa.

Je, ninawezaje kuwasilisha miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Kuanzia tarehe 14 Novemba 2023, miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji inaweza kuripotiwa kupitia API za mfumo mbadala wa utozaji na ni sharti iripotiwe ndani ya saa 24 ya malipo kuidhinishwa. API hizi zinafanya iwe rahisi kwa wasanidi programu kuripoti na pia kuruhusu miamala kupitia mfumo mbadala wa utozaji ionekane kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Ikiwa bado hujajumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, bado unaweza kuendelea kuripoti miamala wewe mwenyewe hadi terehe 13 Machi 2024. Ukiripoti mwenyewe, unatakiwa uripoti mwenyewe kiasi cha miamala iliyolipwa mara moja kwa mwezi kufikia siku ya 5 ya kazi ya kila mwezi. Kwa mfano, ripoti ya miamala iliyofanywa mwezi Oktoba 2023 itapaswa kuripotiwa kufikia tarehe 7 Novemba 2023. Baada ya kujaza fomu ya taarifa, tutakagua maelezo yako na kukutumia maagizo kuhusu jinsi ya kuripoti miamala yako iliyolipwa na malipo unayopaswa kulipa kwa ajili ya ada za huduma na kodi zozote zinazokatwa.

Ni kwa aina zipi za bidhaa ninaweza kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA?

Mifumo mbadala ya utozaji inaweza kutumika kwa huduma na maudhui dijitali, kama vile usajili na ununuzi wa ndani ya programu.

Kwa nini bado mnatoza ada ya huduma?

Ada ya huduma ya Google Play haijawahi kamwe kuwa ada ya uchakataji wa malipo tu. Huonyesha thamani inayotolewa na mfumo wa Android na Google Play na huendeleza uwekezaji wetu tunaoendelea kufanya katika mfumo wa Android na Google Play, ambao hutuwezesha kubuni vipengele vya watumiaji na wasanidi programu ambavyo watu hutegemea. Tembelea makala hii kwa maelezo zaidi kuhusu ada ya huduma.

Je, mpango huu unaruhusu viungo vya ununuzi wa maudhui dijitali kwa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA)?

Ndiyo, mpango huu unaruhusu wasanidi programu kutumia malipo yanayofanywa kwenye wavuti kama njia mbadala ya kulipa katika mwonekano wa wavuti uliopachikwa ndani ya programu zao. Kama zilivyo njia mbadala nyingine za kulipa, malipo haya yatategemea masharti ya mpango yaliyoorodheshwa kwenye ukurasa huu, ikijumuisha masharti ya usalama, uaminifu wa mtumiaji pamoja na ada ya huduma.

Je, huu ni mpango ni wa lazima?

Hapana, huu ni mpango wa kujijumuisha. Ikiwa hutaki kuwapa watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) mfumo mbadala wa utozaji kwenye Google Play, huhitaji kuchukua hatua yoyote.

Tayari nimejiandikisha kwenye mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji wa eneo la EEA. Je, ninaweza pia kujisajili ili nishiriki kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji?

Ikiwa ulijisajili katika mpango wa (EEA) kabla ya tarehe 1 Septemba, 2022 na ungependa kuwapa watumiaji chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play, utahitaji kuwasilisha upya fomu ya taarifa ili ujiandikishe kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji.

Ikiwa ulijisajili katika mpango wa EEA baada ya tarehe 1 Septemba 2022, huhitaji kuwasilisha upya fomu ya taarifa ili kushiriki kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji. Hata hivyo, utahitajika kutujulisha kwa kuwasilisha fomu ya kujiandikisha ya kifurushi cha programu kilichosasishwa, iwe unatoa chaguo mbadala la utozaji kwa kila moja ya nchi katika eneo la (EEA).

Ikiwa ninapanga kutoa mfumo mbadala wa utozaji au ikiwa tayari nimeutoa, ninapaswa kutimiza masharti ya hali ya utumiaji yaliyobainishwa kwenye ukurasa huu kufikia lini?

Ikiwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji uliowekwa otomatiki, utatimiza masharti ya hali ya utumiaji kwa kujumuisha API za upande wa kiteja. Kuanzia tarehe 14 Machi 2023, wasanidi programu wote wanaoshiriki watahitajika kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji ili kutekeleza skrini ya taarifa na kuripoti miamala.

Ikiwa hauko tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, unahitajika kutekeleza mwongozo wa muda wa hali ya utumiaji.

Nimewasilisha fomu ya kujiandikisha ya kifurushi cha programu, ili kubainisha masoko ambayo yatatumia mpango mbadala wa utozaji bila kujumuisha chaguo kwa mtumiaji kwenye programu yangu. Je, ninawezaje kuarifu Google kuhusu mabadiliko yoyote ya chaguo za kujiandikisha za kifurushi cha programu yangu?

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, unahitaji kuwasilisha fomu ya kujiandikisha ukibadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahsusi kwa kifurushi fulani cha programu. Tafadhali kumbuka kuwa, masasisho yoyote yataanza kutumika tu tarehe moja ya mwezi unaofuata, majira ya (UTC), ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya ada husika za huduma.

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kubadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahususi kwenye kifurushi cha programu fulani kupitia kwa mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Masasisho yoyote yataanza kutumika mara moja ikiwa ni pamoja na ada husika za huduma.

Tayari nimejiandikisha kwenye jaribio kwa programu zangu zisizo za michezo, je, ninahitaji kujisajili tena kwa programu yangu ya michezo ili nishiriki katika jaribio la chaguo mbadala la utozaji?

Hapana. Ikiwa unashiriki kwenye mpango wa jaribio kwa sasa, unaweza kuandikisha programu yako ya michezo ya video katika mpango kupitia Dashibodi ya Google Play na uanze kutoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA. Fuata maagizo ya jinsi ya kuandikisha programu kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi.

Ninawezaje kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji katika maumbo tofauti na vifaa vya mkononi na vishikwambi ninapotoa chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji walio katika eneo la EEA?

API za mfumo mbadala wa utozaji zinaweza kutekelezwa kwa njia sawa kwenye maumbo yote yaliyotimiza masharti. Unaweza kutumia mwongozo ule ule wa ujumuishaji ili upate maagizo ya kina na nyenzo za jinsi ya kuanza.

Ikiwa unapanga kutoa chaguo mbadala la utozaji kwenye kipengele cha Android Auto, tafadhali wasiliana nasi ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanza.

API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yapi? Ninaweza kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji kabla ya kutumia API kuripoti miamala?

Ili kurahisisha hali ya utumiaji ya msanidi programu, API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa ili kujumuishwa na kutumiwa pamoja. API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yafuatayo:

  • Skrini za mfumo mbadala wa utozaji zinazotekelezwa na Google Play, hii inamaanisha kuwa huhitaji kuunda na kutunza skrini ya maelezo wewe mwenyewe.
  • Mchakato wa kuripoti miamala uliorahisishwa, ambao huondoa hitaji la kugusa kwa mikono na hukabili hitilafu za ujumuishaji au ulinganishaji.
  • Miamala ya mfumo mbadala wa utozaji iliyoripotiwa kupitia API itaonyeshwa kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Zaidi ya hayo, pia tumefanya maboresho yafuatayo ili iwe rahisi kwako kuanza kutumia mfumo mbadala wa utozaji:

  • Hali ya kujihudumia katika kudhibiti mfumo mbadala wa utozaji kupitia Dashibodi ya Google Play, kama vile kuwasha na kuzima kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwa kila programu na soko linalotimiza masharti, kudhibiti nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  • Ripoti zinazoweza kuhamishwa za miamala za mfumo mbadala wa utozaji ambazo zimeripotiwa kupitia API zilizo na maelezo ya ziada kama vile kiwango cha ubadilishaji kilichotumika, kitambulisho cha kifurushi cha programu husika na kiwango cha ada ya huduma.
Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji?

Ni rahisi kupanua ujumuishaji wako uliopo wa mfumo wa utozaji wa Google Play ili utumie API za mfumo mbadala wa utozaji. API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa kwa kutumia kanuni na miundo ile ile ya usanifu, sawa na Maktaba yetu ya Malipo kupitia Google Play na API za Msanidi Programu wa Google Play. Hii inamaanisha API hizi zinaoana na usanifu uliopo na timu zako zitakuwa na ufahamu nazo.

Katika mwongozo wetu wa ujumuishaji, tunatoa mwongozo wa kina na nyenzo kuhusu jinsi ya kuanza na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mara moja na unaorudiwa. Kuna vijisehemu vya msimbo vya mfano ya kufanya iwe rahisi kutekeleza. Tunakaribisha maoni kutoka kwa wasanidi programu kuhusu API hizi na nyenzo za ziada ambazo zitakusaidia ukiwa na maswali yoyote au maoni kuhusu API za mfumo mbadala wa utozaji, tafadhali wasiliana nasi hapa.

Tayari ninashiriki kwenye chaguo mbadala la utozaji, ninahitaji kufanya nini ili nianze kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji?

Kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama, ambayo ni tarehe 13 Machi 2024, kamilisha hatua zilizoainishwa kwenye Ujumuishaji wa API za Mfumo Mbadala wa Utozaji. Baada ya kuhamisha usajili wowote unaoendelea kutoka kwenye kipindi cha kuripoti wewe mwenyewe na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Je, ninaweza kuripoti vipi miamala inayorudiwa, kupitia API za mfumo mbadala za utozaji kwa usajili unaoendelea ambao ulianza nilipokuwa nikitoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki?

Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila kuripoti kiotomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwa API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Baada ya kuhamisha, unahitaji tu kuripoti miamala inayorudiwa kupitia API na huhitaji tena kuripoti kupitia mfumo wa kuripoti mwenyewe.

Ikiwa bado hujahamisha usajili unaoendelea, bado unatakiwa kuendelea kuripoti miamala inayorudiwa kupitia maagizo yaliyopo ya kuripoti mwenyewe.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5996144907456535196
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false