Programu za Afya
Ikiwa programu yako inafikia data ya afya na ni programu ya afya au inatoa vipengele vinavyohusiana na afya, ni lazima itii Sera zilizopo za Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na Sera dhidi ya Matumizi Mabaya ya Vifaa, Faragha na Udanganyifu na Matukio Nyeti, pamoja na masharti yaliyo hapa chini:
- Taarifa Kuhusu Dashibodi:
- Nenda kwenye Ukurasa wa maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu) kwenye Dashibodi ya Google Play kisha uchague aina ambazo programu yako inajihusisha nazo.
- Sera ya Faragha na Masharti ya Ufumbuzi Dhahiri:
- Ni lazima programu yako ichapishe kiungo cha sera ya faragha katika sehemu iliyobainishwa kwenye Dashibodi ya Google Play na kiungo au maandishi ya sera ya faragha ndani ya programu yenyewe. Tafadhali hakikisha kuwa sera yako ya faragha inapatikana kwenye URL inayotumika, inayoweza kufikiwa na umma na isiyo na mipaka pepe (hatukubali PDF) na haiwezi kubadilishwa (kwa mujibu wa Sehemu ya Usalama wa Data).
- Ni lazima sera ya faragha ya programu yako, pamoja na ufumbuzi wowote wa ndani ya programu, ifafanue kwa kina ufikiaji, ukusanyaji, matumizi na kuruhusu ufikiaji wa data ya mtumiaji ambayo ni ya binafsi au nyeti, lakini si tu data iliyofumbuliwa katika sehemu ya Usalama wa Data hapo juu. Kwa utendaji au data yoyote inayodhibitiwa na ruhusa hatari au ruhusa za programu inapotumika, ni sharti programu itimize masharti ya idhini na ufumbuzi dhahiri yanayotumika.
- Ruhusa ambazo hazihitajiki katika utendaji wa msingi wa programu ya afya hazipaswi kuombwa na ruhusa zisizotumika lazima ziondolewe. Ili upate orodha ya ruhusa zinazochukuliwa kuwa katika upeo wa data nyeti inayohusiana na afya, angalia Aina za programu za afya na maelezo ya ziada.
- Iwapo programu yako si programu ya afya kwa msingi, lakini ina vipengele vinavyohusiana na afya na inafikia data ya afya, bado ipo katika upeo wa sera ya Programu za Afya. Inapaswa kumwelezea mtumiaji kwa njia ya wazi uhusiano kati ya utendaji wa msingi wa programu na ukusanyaji wa data inayohusiana na afya (kwa mfano, watoa huduma za bima, programu za michezo zinazokusanya data ya shughuli za mtumiaji kama njia ya kuendeleza uchezaji nk.). Ni lazima sera ya faragha ya programu ionyeshe matumizi haya.
- Masharti ya ziada:
Ikiwa programu yako ya afya inastahiki mojawapo ya hali zifuatazo, ni lazima utii masharti husika pamoja na kuchagua aina inayofaa katika Dashibodi ya Google Play:
- Programu za afya zinazoshirikiana na Serikali: Iwapo una ruhusa kutoka kwa serikali au shirika la afya linalotambuliwa, ya kubuni na kusambaza programu kwa kushirikiana nalo, ni sharti uwasilishe uthibitisho wa kustahiki kupitia Fomu ya Arifa ya Mapema.
- Programu za Kufuatilia Waliotangamana na Aliyeambukizwa au za Hali ya Afya: Ikiwa programu yako ni ya kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa na/au ya hali ya afya, tafadhali chagua “Kuzuia Ugonjwa na Afya ya Umma” kwenye Dashibodi ya Google Play, kisha uweke maelezo yanayohitajika kupitia fomu ya arifa ya mapema hapo juu.
- Programu Zinazoendesha Utafiti Unaohusu Binadamu: Ni lazima programu zinazoendesha utafiti unaohusu afya ya binadamu zifuate sheria na kanuni zote; ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, kupata idhini ya washiriki au, ikiwa washiriki ni watoto, zipate idhini kutoka kwa mzazi au mlezi wao. Programu za Utafiti wa Afya zinapaswa pia zipate idhini kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Mashirika (IRB) na/au kamati huru za maadili zinazolingana isipokuwa ziruhusiwe kutopata idhini hii. Uthibitishaji wa idhini kama hizi unapaswa kutolewa ukihitajika.
- Programu za SaMD au Kifaa cha Matibabu: Programu ambazo zinachukuliwa kuwa ni vifaa vya matibabu au SaMD zinapaswa kupata na kuhifadhi barua ya idhini au hati nyingine ya idhini ambayo imetolewa na mamlaka au taasisi ya serikali inayohusika na usimamizi na utiifu wa programu za afya. Uthibitishaji wa idhini kama hizi unapaswa kutolewa ukihitajika.
|