Ili kuweka wazi zaidi makataa ya Kiwango Lengwa cha API, tunaunganisha tarehe hadi tarehe 31 Agosti kila mwaka.
Kuanzia tarehe 31 Agosti 2023:
- Ni sharti programu mpya zilenge Android 13 (Kiwango cha API cha 33) au mpya zaidi; isipokuwa kwa programu za Wear OS, ambazo lazima zilenge Android 11 (Kiwango cha API cha 30) au hadi Android 13 (Kiwango cha API cha 33).
- Ni sharti programu zilizopo zilenge kiwango cha API cha 31 au mpya zaidi ili ziendelee kupatikana kwenye vifaa vya watumiaji vinavyotumia mfumo wa uendeshaji wa Android ulio juu zaidi ya kiwango lengwa cha API cha programu yako. Programu zinazolenga kiwango lengwa cha API cha 30 au chini yake (kiwango lengwa cha API cha 29 au chini yake kwa Wear OS), zitapatikana tu kwenye vifaa vinavyotumia mfumo wa uendeshaji wa Android ulio sawa au chini ya kiwango lengwa cha API cha programu yako.
Kila toleo jipya la Android huleta mabadiliko yanayoboresha hali ya utumiaji, usalama na utendaji wa mfumo wa Android kwa ujumla. Kila programu hubainisha targetSdkVersion
(pia hujulikana kama kiwango lengwa cha API) katika faili ya maelezo. Kiwango lengwa cha API huashiria jinsi programu yako inavyotakiwa kufanya kazi kwenye matoleo tofauti ya Android.
Hali ya kuweka mipangilio kwenye programu yako ili ilenge kiwango cha API ya hivi karibuni huhakikisha kwamba watumiaji wananufaika kutokana na maboresho ya usalama, faragha na utendaji, huku ikiruhusu programu itumike kwenye matoleo ya awali ya Android (hadi toleo la minSdkVersion
lililobainishwa).
Ili kuwapa watumiaji wa Android na Google Play utumiaji salama, Google Play inahitaji programu zote zitimize masharti ya kiwango lengwa cha API yaliyoorodheshwa hapa chini.
Hali zisizofuata masharti haya zinajumuisha:
- Programu binafsi zinazotumiwa tu na watumiaji katika shirika mahususi na zinalenga tu usambazaji wa ndani ya shirika.
- Programu za Android Automotive OS zilizojumuishwa ndani ya kifurushi kimoja zitaendelea kupatikana kwa watumiaji wote wa Google Play.
Ufafanuzi
Programu mpya | Programu ambayo bado haijachapishwa katika Google Play (kwa mfano, programu mpya kabisa). |
Programu iliyopo | Programu ambayo imechapishwa kwenye Google Play. |
Sasisho la programu | Toleo jipya la programu ambalo unawasilisha kwa ajili ya ukaguzi ili lichukue nafasi ya programu iliyopo. |
Masharti ya sasisho la programu
Toleo la mfumo wa uendeshaji wa Android |
Je, programu mpya na masasisho ya programu mpya yatahitajika kulenga kiwango hiki cha API lini? | |
Programu mpya | Masasisho ya programu | |
Android 13 (kiwango cha API cha 33)* |
Tarehe 31 Agosti, 2023 |
Tarehe 31 Agosti, 2023 |
Android 12 (kiwango cha API cha 31) |
Tarehe 31 Agosti, 2022 |
Tarehe 1 Novemba, 2022 |
*Ili kusaidia kurahisisha mabadiliko kwa wasanidi programu, wasanidi programu wataweza kuomba muda zaidi hadi tarehe 1 Novemba.
Kidokezo: Ili upate mwongozo wa kiufundi kuhusu jinsi ya kubadilisha kiwango cha API kinacholengwa na programu yako ili kutimiza masharti haya, rejelea mwongozo wa uhamishaji.
Masharti ya programu ya Wear OS
Toleo la mfumo wa uendeshaji wa Android (Kiwango cha API) |
Je, ni wakati gani mawasilisho ya programu ya Wear OS yanahitajika kulenga Kiwango hiki cha API? | |
Programu mpya | Masasisho ya programu | |
Android 11 (Kiwango cha API cha 30) (hamna mabadiliko) | Tarehe 1 Agosti, 2022 | Tarehe 1 Novemba, 2022 |
Masharti ya upatikanaji wa programu
Kwa sasa, programu zilizopo (kwenye vifaa vya mkononi, Android Auto, Android TV) lazima zilenge kiwango cha API cha 31 au mpya zaidi kufikia tarehe 31 Agosti 2023 (kiwango lengwa cha API cha 30 au mpya zaidi na kiwango lengwa cha 33 kwa Wear OS). Vinginevyo zitaacha kugundulika kwa watumiaji wote wa Google Play ambao vifaa vyao vinatumia matoleo ya mfumo wa uendeshaji wa Android ambayo ni mapya kuliko kiwango cha API kinacholengwa na programu yako, kwa sababu programu yako haikuundwa ili kukidhi viwango vya usalama na ubora ambavyo watumiaji hawa wanavitarajia kutoka kwenye matoleo mapya zaidi ya mfumo wa uendeshaji wa Android.
- Programu zenye kiwango lengwa cha Android 11 (Kiwango cha API cha 30)* au chini yake hazitapatikana kwa watumiaji wapya wanaotumia mfumo wa uendeshaji wa Android wa juu zaidi kuliko kiwango lengwa cha API cha programu baada ya tarehe 31 Agosti 2023.
- Programu zenye kiwango lengwa cha Android 10 (Kiwango cha API cha 29) au chini yake hazitapatikana kwa watumiaji wapya wanaotumia mfumo wa uendeshaji wa Android wa juu zaidi kuliko kiwango lengwa cha API cha programu baada ya tarehe 1 Novemba 2022 au tarehe 1 Mei 2023, iwapo programu yako iliongezewa muda.
*Ili kusaidia kurahisisha mabadiliko kwa wasanidi programu, wasanidi programu wataweza kuomba muda zaidi hadi tarehe 1 Novemba 2023. Utaweza kufikia fomu za kuomba kuongezewa muda za programu yako katika Dashibodi ya Google Play mwanzoni mwa mwezi wa Agosti iwapo umeathirika, kupitia ukurasa wa Hali ya sera kwa kubofya hadi kwenye hitilafu husika.
Hatua za kuchukua ili utii
Programu mpya |
Programu zilizopo |
Unapochapisha programu mpya, ni lazima ulenge API ya 33 au zaidi. |
Ikiwa kiwango lengwa cha API cha programu yako iliyopo ni 31 au zaidi, basi programu yako inatii sera hii. Ikiwa ulengaji wa programu yako iliyopo upo chini ya API ya 31, programu itaacha kupatikana kwa watumiaji wote wa Google Play ambao vifaa vyao vinatumia matoleo ya mfumo wa uendeshaji wa Android ambayo ni mapya kuliko kiwango cha API kinacholengwa na programu zako, kwa sababu programu yako haikuundwa ili kukidhi viwango vya usalama na ubora ambavyo watumiaji hawa wanavitarajia kutoka kwenye matoleo mapya zaidi ya mfumo wa uendeshaji wa Android.
|
Masharti ya Wear OS
Programu mpya |
Programu zilizopo |
Unapochapisha programu mpya, ni sharti ulenge API ya 30 au mpya zaidi hadi Android 13 (Kiwango cha API cha 33). |
Ikiwa kiwango lengwa cha API cha programu yako iliyopo ni 30 au mpya zaidi hadi Android 13 (Kiwango cha API 33), basi programu yako inatii sera hii. Ikiwa ulengaji wa programu yako iliyopo upo chini ya API ya 30, programu itaacha kupatikana kwa watumiaji wote wa Google Play ambao vifaa vyao vinatumia matoleo ya mfumo wa uendeshaji wa Android ambayo ni mapya kuliko kiwango cha API kinacholengwa na programu zako, kwa sababu programu yako haikuundwa ili kukidhi viwango vya usalama na ubora ambavyo watumiaji hawa wanavitarajia kutoka kwenye matoleo mapya zaidi ya mfumo wa uendeshaji wa Android.
|
Maswali yanayoulizwa sana
Kwa programu zinazolenga API ya 30 au ya chini zaidi
Nina programu iliyochapishwa kwenye Google Play ambayo inalenga API ya 30 au ya chini zaidi (kwa Wear OS, programu inayolenga API ya 29 au chini zaidi), ambayo sina mpango wa kuisasisha. Je, nina chaguo gani?
Ikiwa ungependa programu hii iendelee kutumika kwa watumiaji wako waliopo, huhitaji kufanya kitu chochote. Hata hivyo, programu yako haitapatikana katika Google Play kwa watumiaji wapya wanaotumia vifaa vyenye mfumo wa uendeshaji wa Android mpya zaidi ya kiwango lengwa cha programu yako. Itapatikana tu kwa watumiaji wa Google Play wanaotumia vifaa vyenye mfumo wa uendeshaji wa Android wenye Kiwango cha API cha programu yako au chini zaidi.
Kufikia tarehe 1 Agosti, 2023, ni lazima programu yako itimize masharti ya kiwango hiki lengwa cha API, vinginevyo itasitisha kutambulika kwa watumiaji wote wa Google Play ambao vifaa vyao vinatumia matoleo mapya zaidi ya mfumo wa uendeshaji wa Android kuliko kiwango lengwa cha API cha programu yako.
Ikiwa unapanga kusasisha programu yako iwe katika kiwango lengwa kipya zaidi cha API na unahitaji muda zaidi baada ya tarehe 31 Agosti, unaweza kuomba uongezewe muda ili uendelee kusambaza kwa watumiaji wote wa Google Play hadi tarehe 1 Novemba. Fomu ya kuomba kuongezewa muda itapatikana baadaye mwaka huu katika Dashibodi ya Google Play.
Ikiwa ungependa kusitisha matumizi ya programu yako kwa watumiaji wapya hata kwenye vifaa vya zamani, unaweza kubatilisha uchapishaji wa programu yako.
Je, nitapata wapi fomu ya kuongezewa muda ili kuendelea kusambaza programu kwa watumiaji wa Google Play hadi tarehe 1 Novemba, 2023?
Nina programu ambazo sitaki tena zichapishwe kwenye Google Play. Ninaweza kufanya nini?
Je, watumiaji wangu ambao walishapakua programu yangu awali wataathiriwa vipi?
Je, sasisho hili litaathiri upakuaji wa programu?
Je, hali ya utumiaji itakuwaje ikiwa mtumiaji mwenye kifaa kipya zaidi atatembelea kiungo mahususi cha ukurasa wa duka la programu, lakini programu inalenga API ya 30 au ya chini zaidi?
Je, kuna hali zozote zisizofuata kanuni kwa programu zilizopo zinazolenga API ya 30 au ya chini zaidi?
Ndiyo. Hatujumuishi programu ambazo ni za faragha kabisa zinazotumiwa tu na watumiaji katika shirika mahususi na zinalenga tu usambazaji wa ndani ya shirika na programu zinazolenga umbo la Android Automotive OS.