Uza programu, bidhaa za ndani ya programu na usajili katika sarafu mbalimbali

Kama upo mahali ambapo usajili wa muuzaji unaruhusiwa, unaweza kuuza programu, bidhaa za ndani ya programu na usajili katika sarafu mbalimbali kupitia Dashibodi ya Google Play.

Ukiwasilisha programu yako mahali panapotumia sarafu ya nchi hiyo, wateja wa Google Play wataona programu ikiuzwa katika sarafu hiyo. Wateja watatozwa kulingana na sarafu ya nchi yao, lakini malipo yatafanywa kwa sarafu inayolingana na taarifa zako za malipo.

Weka bei za programu yako, bidhaa za ndani ya programu na usajili

Ili upate maelezo ya jinsi ya kuweka na kubadilisha bei za programu, bidhaa ya ndani ya programu na usajili, nenda kwenye Weka bei za programu zako.

Malipo

Malipo yatatolewa kwa akaunti yako ya benki katika sarafu inayolingana na maelezo ya akaunti ya malipo. Huwezi kuchagua sarafu ya malipo au kupokea malipo katika sarafu isiyolingana na sarafu inayohusishwa na Akaunti yako ya Google au akaunti yako ya benki ya nchi unakoishi.

Kwenye ukurasa wa Udhibiti wa agizo , utaona sarafu ambayo mnunuzi alitumia kulipia programu na ununuzi wa ndani ya programu. Iwapo sarafu ya agizo hailingani na taarifa zako za malipo, Google itabadilisha thamani iwe katika sarafu yako. Malipo kwa maagizo yaliyofanywa katika sarafu ya mahali ulipo yatafuata ratiba ya kawaida ya malipo.

Viwango vya ubadilishaji fedha

Google hutumia viwango vya kubadilisha pesa vinavyotumika wakati ambapo agizo linafanywa, ili kubadilisha mauzo yaliyotayarishwa katika sarafu ya mnunuzi iwe katika sarafu ya akaunti yako ya Google.

Kiasi hiki cha ubadilishaji husasishwa siku nzima, na ubadilishaji hufanyika kila wakati agizo linapotozwa. Utaona kiwango cha ubadilishaji wa fedha katika risiti yako ya maagizo ya kila programu. Utaona kiwango cha ubadilishaji fedha katika stakabadhi ya malipo ya agizo kwa kila programu.

Kurejesha Pesa

Kwa maagizo yaliyofanywa katika sarafu za nchi alimo mnunuzi, mchakato wa kurejesha pesa utafanyika katika sarafu ile ile ya agizo na mabadiliko katika viwango vya ubadilishaji wa fedha hayataathiri pesa zinazorejeshwa. Kiasi kamili cha pesa zinazorejeshwa kitatumwa kwenye kadi ya mikopo au ya malipo ya mteja wako katika sarafu ya nchi alimo. Pesa zozote zitakazotozwa kwenye maelezo ya akaunti ya malipo kwa ajili ya urejeshaji pesa, zitatumia viwango vya ubadilishaji sarafu vilivyokuwa vikitumika wakati agizo lilifanyika.

Kwa maelezo zaidi, soma kuhusu kurejeshewa pesa na kughairi mauzo.

Kutumika kwa sarafu ya nchi mahususi

Google inapoweka uwezo wa kutumia sarafu mpya ya mnunuzi katika nchi ambayo tayari unasambaza programu yako, tutaweka kiotomatiki bei ya programu yako na bidhaa za ndani ya programu kulingana na bei chaguomsingi, kiwango cha sasa cha ubadilishaji fedha na mfumo wa bei unaotumika katika eneo husika.

Unaweza kukagua bei za programu zako kwenye ukurasa wa Bei ya programu (Chuma mapatoBidhaa > Bei ya programu) katika Dashibodi ya Google Play.

Kuhusu usajili, tutaweka bei kiotomatiki kwa ajili ya usajili wako kulingana na bei uliyoweka kwenye "Nchi au maeneo mapya".  Iwapo umechagua kutoweka mpango wa msingi kwa ajili ya usajili wako au ofa inayopatikana kwenye "Nchi au eneo jipya" usajili wako hautapatikana katika nchi hii mpya.  Ili ubadilishe mipangilio hii:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play na uende kwenye ukurasa wa Usajili (Chuma Mapato > Bidhaa > Usajili).
  2. Karibu na sehemu ya usajili unayohitaji kubadilisha, bofya kishale cha kulia ili uangalie maelezo ya usajili.
  3. Chini ya sehemu ya "Mipango ya msingi na ofa", bofya kishale cha kulia karibu na sehemu ya ofa unayotaka kubadilisha.
  4. Kwenye sehemu ya "Bei na upatikanaji," bofya Dhibiti upatikanaji katika nchi au eneo.
  5. Nenda chini hadi kwenye "nchi au maeneo mengine."
  6. Bofya kishale ili upanue orodha, kisha teua au batilisha uteuzi wa Nchi au maeneo mapya.
  7. Bofya Tekeleza
  8. Bofya Hifadhi mabadiliko.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7655105465053241417
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false