Kufungwa kwa akaunti zisizotumika za wasanidi programu

Akaunti za Wasanidi Programu wa Google Play zinalenga wasanidi programu wanaoendelea kuchapisha na kudumisha programu. Akaunti za wasanidi programu ambazo hazitumiki zitafungwa na ada ya usajili haitarejeshwa.

Ni lini akaunti ya msanidi programu itakuwa haitumiki?

Kuna mipangilio miwili ya vigezo vinavyobaini kama akaunti ya msanidi programu inatumika au la.

Akaunti ya msanidi programu isiyotumika isiyo na programu

  • Akaunti ya msanidi programu ilifunguliwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
  • Haijawahi kutuma programu ikaguliwe.

Akaunti ya msanidi programu isiyotumika yenye programu

  • Akaunti ya msanidi programu ilifunguliwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
  • Programu zote zilizochapishwa (ikijumuisha programu zinazotumika, zilizoondolewa na zilizosimamishwa) kwenye akaunti zina jumla ya usakinishaji usiozidi 1,000 tangu zilipochapishwa.
  • Haijathibitisha namba ya simu na anwani ya barua pepe ya Akaunti ya msanidi programu wa Google Play.
  • Haijatumia Dashibodi ya Google Play katika siku 180 zilizopita.

Nini kitatokea pale ambapo akaunti yangu ya msanidi programu itaacha kutumika?

Akaunti ya msanidi programu inapokidhi mojawapo ya vigezo hapo juu, itatiwa alama ya kufungwa kutokana na kutokutumika. Hili litakapotokea, ujumbe wa barua pepe utatumwa kwa mmiliki wa akaunti ukielezea kuwa akaunti ya msanidi programu itafungwa hivi karibuni. Hili pia litaelezewa vizuri kwenye Dashibodi ya Google Play. 

Barua pepe hii itaonyesha hatua unazoweza kuchukua ili uendelee kutumia akaunti yako ya msanidi programu na tarehe ambayo unapaswa kukamilisha hatua hizi. Kukosa kufuata hatua hizi kutasababisha kufungwa kabisa kwa akaunti yako ya msanidi programu na ada ya usajili haitarejeshwa.

Utatumiwa barua pepe za vikumbusho za kukupatia ilani ya siku 60, 30 na 7.

Je, ninawezaje kuzuia akaunti yangu ya msanidi programu isifungwe?

Ikiwa unapanga kuchapisha au kudumisha programu siku zijazo, zuia akaunti yako isifungwe kwa kukamilisha majukumu yote mawili yafuatayo:

  1. Thibitisha maelezo yako ya mawasiliano:
    1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play.
    2. Nenda kwenye ukurasa wa Maelezo ya akaunti (Programu zote > Maelezo ya akaunti) na ukamilishe uthibitishaji wa barua pepe na namba ya simu.
    3. Bofya Hifadhi.
  2. Tengeneza na uchapishe programu au uchapishe sasisho la programu iliyopo kwenye Google Play
    1. Ingia katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play
    2. Tengeneza na uweke mipangilio ya programu yako ikiwa bado hujafanya hivyo.
    3. Pakia APK au app bundle mpya.

Kumbuka kwamba akaunti yako inaweza kuacha tena kutumika na hali hii ikitendeka utapokea arifa mpya.

Muhimu: Usipokamilisha majukumu yote mawili yaliyo hapo juu kabla ya tarehe iliyobainishwa kwenye barua pepe tuliyotuma kuhusu kufungwa kwa akaunti, akaunti ya msanidi programu itafungwa kabisa na hutarejeshewa ada yako ya usajili.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
219994371110244151
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false