Weka maelezo ya Sehemu ya usalama wa data kwenye Google Play

Sehemu ya Usalama wa Data ya Google Play huwapa wasanidi programu njia ya wazi ya kuonyesha watumiaji iwapo na jinsi wanavyokusanya, kushiriki na kulinda data ya watumiaji, kabla watumiaji hawajasakinisha programu. Wasanidi programu wanahitajika kutuambia kuhusu mbinu za faragha na usalama za programu zao kwa kujaza fomu katika Dashibodi ya Google Play. Kisha maelezo haya huonyeshwa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play.

Makala haya yanatoa muhtasari wa masharti ya Fomu ya usalama wa data, mwongozo wa kujaza fomu na maelezo kuhusu mabadiliko yoyote ya hivi majuzi au yajayo.

Kunja yote Panua yote

Muhtasari

Sehemu ya Usalama wa Data kwenye Google Play ni njia rahisi unayoweza kutumia ili kusaidia watu waelewe aina ya data ya mtumiaji ambayo programu yako hukusanya au kushiriki, na kuonyesha mbinu muhimu za faragha na usalama wa programu yako. Maelezo haya husaidia watumiaji kufanya maamuzi sahihi zaidi wanapochagua programu za kusakinisha.

Ni sharti wasanidi programu wote watangaze jinsi wanavyokusanya na kushughulikia data ya watumiaji kwa programu wanazochapisha kwenye Google Play na kutoa maelezo kuhusu jinsi wanavyolinda data hii kupitia mbinu za usalama kama vile usimbaji fiche. Hali hii ni pamoja na data inayokusanywa na kushughulikiwa kupitia maktaba au SDK zozote za washirika wengine zinazotumiwa katika programu zao. Huenda ukahitaji kurejelea maelezo ya usalama wa data yaliyochapishwa na mtoa huduma wako wa SDK ili upate taarifa. Angalia Faharasa ya SDK ya Google Play ili uone iwapo mtoa huduma wako ametoa kiungo cha mwongozo wake.

Unaweza kutoa maelezo haya kupitia Fomu ya usalama wa data kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu(Sera > Maudhui ya programu) katika Dashibodi ya Google Play. Baada ya kujaza na kuwasilisha Fomu ya usalama wa data, Google Play itakagua maelezo utakayotoa kama sehemu ya mchakato wa ukaguzi wa programu. Maelezo huonyeshwa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ili kusaidia watumiaji waelewe jinsi unavyokusanya na kutuma data kabla ya kupakua programu yako.

Ni wajibu wako pekee kutoa taarifa kamili na sahihi katika ukurasa wa programu yako kwenye Google Play. Google Play hukagua programu kwa kutumia masharti yote ya sera; hata hivyo hatuwezi kufanya uamuzi kwa niaba ya wasanidi programu kuhusu jinsi wanavyoshughulikia data ya mtumiaji. Ni wewe tu uliye na maelezo yote yanayohitajika ili kujaza Fomu ya usalama wa data. Google inapotambua tofauti kati ya utendaji wa programu na ubainishaji wako, huenda tukachukua hatua inayofaa, ikiwa ni pamoja na kitendo cha utekelezaji.

Unaweza kupanua sehemu iliyo hapa chini ili uone jinsi ukurasa wa programu yako katika Google Play utakavyoonekana kwa watumiaji wa Google Play, na arifa na masasisho ambayo watumiaji wanaweza kuona iwapo utafanya mabadiliko fulani katika Sehemu ya Usalama wa Data ya programu yako.

Maelezo yatakayoonyeshwa kwa watumiaji ikiwa programu yako inashiriki data ya watumiaji

Kumbuka: Picha ni mifano na zinaweza kubadilika

Maelezo yatakayoonyeshwa kwa watumiaji ikiwa programu yako haikusanyi au kushiriki data yoyote ya watumiaji

Watumiaji wataona maelezo yafuatayo ikiwa programu yako haikusanyi au kushiriki data yoyote ya watumiaji na makampuni au mashirika mengine:

Watumiaji wataona maelezo yafuatayo ikiwa programu yako haishiriki data yoyote ya watumiaji na makampuni au mashirika mengine:

Kumbuka: Picha ni mifano na zinaweza kubadilika

Je, ni wasanidi programu wapi wanaohitaji kujaza Fomu ya usalama wa data kwenye Dashibodi ya Google Play?

Ni lazima wasanidi programu wote waliochapisha programu kwenye Google Play wajaze Fomu ya usalama wa data, ikijumuisha programu zinazofanyiwa majaribio na watu wachache, watu wengi, au toleo la umma. Hii inajumuisha pia programu zilizotolewa mapema na zilizopakiwa mapema ambazo husasishwa kupitia Google Play.

Programu ambazo zinatumika katika matoleo ya jaribio ya ndani hazijumuishwi kwenye sehemu ya usalama wa data. Huhitaji kujaza Fomu ya usalama wa data kwa programu zinazotumika kwenye kikundi hiki pekee.

Hata wasanidi programu wenye programu zisizokusanya data yoyote ya watumiaji wanapaswa kujaza fomu hii na kuweka kiungo kinachoelekeza kwenye sera zao ya faragha. Hivyo basi, fomu uliyojaza na sera ya faragha zinaweza kuonyesha kuwa hakuna data ya watumiaji inayokusanywa au kushirikiwa.

Huduma za mfumo na programu za matumizi ya faragha hazihitaji kujaza Fomu ya usalama wa data.

Ingawa msanidi programu anahitajika kujaza fomu ya jumla kwa kila programu kama ilivyobainishwa, anaweza kutojumuisha vizalia vya zamani vya programu kwenye fomu. Hii inatumika kwa vizalia vya programu vinavyotumia Toleo la Sdk la 21 au matoleo ya awali ambapo idadi kubwa ya watumiaji (asimilia 90 na zaidi) wanaosakinisha programu wanatumia vizalia vya programu vya Toleo la Sdk la 21 au matoleo mapya zaidi.

Kutayarisha maelezo mapya

Kabla ya kuweka maelezo ya Sehemu ya Usalama wa Data ya Google Play, tunapendekeza kuwa:

Tazama video ya mwongozo ya Fomu ya usalama wa data

Video hii hukuongoza kupitia nyenzo na hatua zote zinazohitajika ili ujaze Fomu ya usalama wa data.

Google Play PolicyBytes - Data safety form walkthrough

Maelezo ambayo wasanidi programu wanafaa kufichua katika Fomu ya usalama wa data

Sehemu hii inafafanua maelezo unayohitaji kufichua katika Fomu ya usalama wa data katika Dashibodi ya Google Play, na kuorodhesha aina za data na madhumuni unayoweza kuchagua.

Maelezo ambayo wasanidi programu wanapaswa kutangaza kwenye aina zote za data

Bofya sehemu zilizo hapa chini ili uzipanue au uzikunje.

Ukusanyaji wa data

"Kusanya" inamaanisha kutuma data kutoka kwenye programu yako iliyo kwenye kifaa cha mtumiaji. Tafadhali zingatia mwongozo ufuatao:

  • Maktaba na SDK: Hii ni pamoja na data ya mtumiaji inayotumwa kutoka kwenye kifaa katika programu yako kupitia maktaba na/au SDK zinazotumika katika programu yako, bila kujali iwapo data inatumwa kwenye seva yako au ya wengine.
  • Mwonekano wa Wavuti: Inajumuisha pia data ya mtumiaji inayokusanywa kutoka kwenye mwonekano wa wavuti ambao umefunguliwa kwenye programu yako, ikiwa programu yako inadhibiti msimbo/utendaji unaotolewa kupitia mwonekano huo wa wavuti.
    • Huna haja ya kubainisha ukusanyaji wa data kutoka kwenye mwonekano wa wavuti ambapo watumiaji wanavinjari wavuti uliofunguliwa.
  • Uchakataji wa muda mfupi: Data ya mtumiaji inayotumwa kutoka kwenye kifaa inayochakatwa kwa muda mfupi inahitaji kujumuishwa katika majibu yako kwenye fomu, ila iwapo inatimiza masharti yaliyo hapa chini, haitafumbuliwa katika Sehemu ya usalama wa data ya programu yako kwenye Google Play.
    • Hali ya kuchakata data "kwa muda mfupi" inamaanisha kufikia na kutumia data wakati imehifadhiwa tu kwenye hifadhi na inahifadhiwa kwa kipindi kinachohitajika ili kushughulikia ombi mahususi katika muda halisi.
    • Kwa mfano, programu ya hali ya hewa inayotuma maelezo ya mahali alipo mtumiaji kutoka kwenye kifaa ili kuleta maelezo ya hali ya hewa ya sasa ya mahali alipo mtumiaji lakini inatumia tu data ya mahali iliyo kwenye hifadhi na haihifadhi data hiyo mara tu ombi limetimizwa, inaweza kuchukulia matumizi yake ya muda ya data ya mahali kama ya muda mfupi. Hata hivyo, kutumia data ili kuunda wasifu wa utangazaji au wasifu mwingine wa mtumiaji hakuwezi kuchukuliwa kuwa jambo la muda mfupi na lazima itangazwe kama mkusanyiko au kushiriki kwa madhumuni yanayofaa.
  • Data ambayo utambulisho wake umefichwa: Ni sharti data ya mtumiaji inayokusanywa kwa njia ya kuficha utambulisho ifumbuliwe. Kwa mfano, ni sharti data inayoweza kuhusishwa tena na mtumiaji ifichuliwe.

Vipengee visivyo katika upeo wa ukusanyaji wa data

Hali zifuatazo za matumizi hazihitaji kufichuliwa kama zinavyokusanywa:

  • Uchakataji au ufikiaji kwenye kifaa: Data ya mtumiaji inayofikiwa na programu yako ambayo inachakatwa tu kwenye kifaa cha mtumiaji na isiyotumwa kutoka kwenye kifaa haihitaji kufichuliwa.
  • Usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho: Data ya mtumiaji inayotumwa kutoka kwenye kifaa, ila isiyoweza kusomwa nawe au mtu yeyote isipokuwa anayetuma na anayepokea kutokana na usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwishohaihitaji kufichuliwa.
    • Si lazima data iliyosimbwa kwa njia fiche iweze kusomwa na huluki yoyote ya kati, ikiwa ni pamoja na msanidi programu, na anayetuma na anayepokea pekee ndiye anayeweza kuwa na funguo zinazohitajika.
Kuruhusu ufikiaji wa data

"Kuruhusu ufikiaji" inamaanisha kuhamisha data ya mtumiaji iliyokusanywa kutoka kwenye programu yako hadi kwa wahusika wengine. Hii ni pamoja na data ya mtumiaji iliyohamishwa:

  • Kutoka kwenye kifaa, kama vile uhamishaji wa kutoka kwenye seva hadi seva nyingine. Kwa mfano, ukituma data ya mtumiaji inayokusanywa na programu yako kutoka kwenye seva yako kwenda kwenye seva ya wengine.
  • Uhamishaji kwenye kifaa kwenda kwenye programu nyingine. Kuhamisha data ya mtumiaji kutoka programu yako kwenda kwenye programu nyingine moja kwa moja kwenye kifaa. Katika hali hii, ni sharti ufichue maelezo ya kuruhusu ufikiaji wa data kwenye ubainishaji wako wa Sehemu ya usalama wa data hata ikiwa programu yako haitumi data kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji.
  • Kutoka kwenye SDK na maktaba ya programu yako. Kuhamisha data inayokusanywa moja kwa moja kutoka programu yako kwenye kifaa cha mtumiaji kwenda kwa wengine kupitia maktaba na/au SDK zilizojumuishwa katika programu yako.
  • Katika mwonekano wa wavuti ambao umefunguliwa kupitia programu yako.Kuhamishia data ya mtumiaji kwa wengine kupitia mwonekano wa wavuti ambao umefunguliwa katika programu yako, ikiwa programu yako inadhibiti msimbo/utendaji unaotolewa kupitia mwonekano huo wa wavuti.
    • Huhitaji kubainisha maelezo ya kuruhusu ufikiaji wa data kutoka kwenye mwonekano wa wavuti ambapo watumiaji wanavinjari wavuti huria.

Aina zifuatazo za uhamishaji wa data hazihitaji kufumbuliwa kama "kuruhusu ufikiaji":

  • Watoa huduma. Kuhamisha data ya mtumiaji kwenye "mtoa huduma" anayeichakata kwa niaba ya msanidi programu.
    • "Mtoa huduma" inamaanisha asasi inayochakata data ya mtumiaji kwa niaba ya msanidi programu na kulingana na maagizo ya msanidi programu.
  • Madhumuni ya kisheria. Kuhamisha data ya mtumiaji kwa madhumuni mahususi ya kisheria, kama vile kujibu wajibu wa kisheria au maombi ya serikali.
  • Kitendo kinachoanzishwa na mtumiaji au ufumbuzi dhahiri na idhini ya mtumiaji. Kuhamishia data ya mtumiaji kwa wengine kulingana na kitendo mahususi kinachoanzishwa na mtumiaji, ambapo mtumiaji anatarajia data ishirikiwe, au kulingana na ufumbuzi dhahiri wa ndani ya programu na idhini inayotimiza masharti yaliyobainishwa katika Sera yetu ya Data ya Mtumiaji.
  • Data iliyofichwa. Kuhamisha data ya mtumiaji ambayo imefichwa kikamilifu ili isihusishwe tena na mtumiaji mahususi.

Mhusika wa kwanza na wengine.

  • "Mhusika wa kwanza" inamaanisha shirika la msingi ambalo lina wajibu wa kuchakata data inayokusanywa na programu, ambalo kwa kawaida ni shirika linalochapisha programu kwenye Google Play na kuonekana kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.
    • Mhusika wa kwanza ana wajibu wa kuwaelezea watumiaji kwa njia dhahiri shirika ambalo kimsingi linawajibikia uchakataji wa data inayokusanywa na programu.
  • "Wahusika wengine" inamaanisha shirika lolote isipokuwa mhusika wa kwanza au watoa huduma wake.
Kushughulikia data

Pia unweza kufumbua ikiwa kila aina ya data iliyokusanywa na programu yako "inahitajika" au "si ya lazima." "Si ya lazima" ni pamoja na uwezo wa kujijumuisha au kujiondoa kwenye ukusanyaji data. Kwa mfano, unaweza kubainisha aina ya data kama "si ya lazima" ambapo mtumiaji ana udhibiti wa ukusanyaji wake na anaweza kutumia programu bila kutoa data hiyo; au ambapo mtumiaji anachagua iwapo atatoa aina hiyo ya data mwenyewe. Ikiwa utendaji wa msingi wa programu yako unahitaji aina ya data, unapaswa kuibbainisha kama "inahitajika."

Unaweza kubainisha kuwa programu yako ikusanye data fulani kwa hiari ikiwa tu watumiaji wote - bila kujali kifaa au eneo - wanaweza kujiondoa, kujiunga au kutoa maelezo kwa hiari ili kukusanya data.

Mifano ya ukusanyaji wa data kwa hiari ni pamoja na:

  • Programu ya mitandao jamii ya muziki inayouliza tarehe ya kuzaliwa ya mtumiaji kwa ajili ya matangazo, mawasiliano, ila maelezo haya hayahitajiki - mtumiaji bado anaweza kujisajili bila kutoa maelezo haya.
  • Data ya mtumiaji inayokusanywa tu wakati mtumiaji anaingia katika akaunti ambapo watumiaji wana uwezo wa kutumia programu bila kuingia katika akaunti.
Ufumbuzi mwingine wa programu na data

Sehemu ya Usalama wa Data pia ni fursa ya kuonyesha mbinu za faragha na usalama za programu yako kwa watumiaji wako. Kwa mfano, unaweza kuangazia maelezo yafuatayo:

  • Usimbaji fiche wa data inapotumwa: Ni data inayokusanywa au kushirikiwa na programu yako kwa kutumia usimbaji fiche inapotumwa ili kulinda uhamishaji wa data ya mtumiaji kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji wa hatima kwenda kwenye seva.
    • Baadhi ya programu zimeundwa ili kuwawezesha watumiaji kuhamisha data kwenda kwenye tovuti au huduma nyingine. Kwa mfano, huenda programu ya kutuma ujumbe ikawapa watumiaji chaguo la kutuma ujumbe kupitia mtoa huduma wao wa simu, ambayo inadumisha mbinu tofauti za usimbaji fiche. Programu hizi zinaweza kubainisha kwenye vifungu vyao vya Usalama wa Data kwamba data inahamishwa kupitia muunganiko salama ili mradi zinatumia kiwango bora cha sekta kusimba data kwa njia fiche na kwa usalama wakati inasafiri kati ya kifaa cha mtumiaji na programu ya seva.
  • Mbinu ya ombi la ufutaji: Je, programu yako inatoa njia kwa watumiaji kuomba ufutaji wa data yao?
Imejikita kufuata Sera ya familia (itapatikana mwezi Machi 2022 kwenye programu zinazotumika)

Ni lazima programu zinazolenga hadhira ya watoto zifuate masharti ya Google Play ya programu za familia. Ikiwa programu yako ni ya aina hii na umeikagua na kuhakikisha kuwa inatii Masharti ya programu za familia, unaweza kuchagua kuonyesha beji kwenye Sehemu yako ya usalama wa data inayobainisha kuwa "Umejikita kufuata Sera ya Familia ya Google Play."

Ili uonyeshe beji hii, nenda kwenye sehemu ya "Mbinu za usalama" ya Fomu yako ya usalama wa data kisha ubofye Nenda kwenye hadhira na maudhui ili ujijumuishe

Ukaguzi huru wa usalama (kinapatikana kwa programu zote)

Unaweza kuchagua kubainisha kwenye Fomu yako ya usalama wa data kwamba programu yako imethibitishwa kwa njia huru kulingana na viwango vya usalama wa kimataifa. Ukaguzi huu unaofanywa na kulipiwa na wasanidi programu si wa lazima. Kupitia MASA (Tathmini ya Usalama wa Programu ya Vifaa vya Mkononi) wasanidi programu wanaweza kufanya kazi moja kwa moja na Maabara Yaliyoidhinishwa na Google ili kutathmini programu zao kwa mujibu wa MASVS ya OWASP (Kiwango cha Uthibitishaji wa Usalama wa Programu ya Vifaa vya Mkononi). Wahusika wengine wanaofanya ukaguzi wanafanya hivyo kwa niaba ya msanidi programu.

Iwapo ungependa kushiriki, unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Maabara Iliyoidhinishwa na Google ili kuanza mchakato wa kufanya majaribio. Mara tu maabara itakapothibitisha kuwa programu yako inakidhi masharti yote ya usalama, unaweza kuchagua kuonyesha beji kwenye sehemu yako ya usalama wa Data inayoeleza kuwa umekamilisha "Ukaguzi Huru wa Usalama."

Maabara Yaliyoidhinishwa yana sehemu maalumu ya weledi kuhusu usalama wa programu za vifaa vya mkononi na hutoa uwezo wa kina wa majaribio ya usalama na utumiaji. Maabara haya pia yanatii kiwango cha ISO 17025 au kiwango sawa kinachotambuliwa kwenye sekta. Ikiwa unakidhi vigezo na ungependa kuwa mshirika wa maabara, tafadhali jaza na utume fomu hii pamoja na maelezo ya kampuni yako.

Muhimu: Huenda ukaguzi huu huru usitumike kuthibitisha usahihi na ukamilifu wa ubainishaji wako wa Usalama wa Data. Hata ukitumia zana za wengine kuchunguza vidhibiti vya usalama wa programu yako, ni wajibu wako kufanya ubainishaji sahihi na kamili katika ukurasa wa programu yako kwenye Google Play.

Beji ya Unified Payments Interface (UPI)

Unified Payments Interface (UPI) ni mfumo wa uhamishaji wa pesa papo hapo, uliosanidiwa na Shirika la Malipo la Taifa la India (NPCI), huluki inayodhibitiwa na RBI. Ikiwa kwa sasa unatumia mfumo huu wa uhamishaji wa pesa, unaweza kuchagua kuubainisha kwenye Fomu yako ya usalama wa data. Iwapo ungependa kushiriki au una maswali, unaweza kuwasiliana na NCPI moja kwa moja ili upate masharti ya kuidhinishwa kwa programu yako. Programu zenye uidhinishaji huu zinaweza kustahiki kuonyesha beji kwenye kurasa zao za programu katika Google Play, inayothibitisha kuwa NPCI imeidhinisha utekelezaji wa UPI wa programu hii. Beji itaonyesha "Inatoa Huduma za Malipo kupitia UPI," na haitaonekana kwa watumiaji isipokuwa uashirie kwa kujijumuisha kwenye Fomu ya usalama wa data katika Dashibodi ya Google Play. Beji inaonekana tu kwa watumiaji wa Google Play wanaoishi nchini India.

Aina za data na madhumuni

Bofya sehemu zilizo hapa chini ili uzipanue au uzikunje.

Aina za data

Wasanidi programu wataombwa kutoa mbinu za ukusanyaji, kushiriki na mbinu nyingine kwa aina mbalimbali za data ya mtumiaji, pamoja na madhumuni ya matumizi ya data hiyo.

Aina Aina ya data Maelezo

Mahali

Eneo linalokadiriwa

Eneo halisi kilipo kifaa au mtumiaji ndani ya eneo linalozidi au linalolingana na kilomita tatu za mraba, kama vile jiji kubwa ambapo mtumiaji yupo, au eneo linalotolewa na ruhusa ya Android ya ACCESS_COARSE_LOCATION.

Eneo mahususi

Eneo halisi kilipo kifaa au mtumiaji ndani ya eneo lisilozidi au linalolingana na kilomita tatu za mraba, kama vile eneo linalotolewa na ruhusa ya Android ya ACCESS_FINE_LOCATION.
Taarifa binafsi Jina Mtumiaji anavyojiita, kama vile jina lake la kwanza au la mwisho au jina wakilishi.
Anwani ya barua pepe Anwani ya barua pepe ya mtumiaji.

Vitambulisho vya Mtumiaji

Vitambulishi vinavyohusiana na mtu anayeweza kutambulishwa. Kwa mfano, kitambulisho cha akaunti, nambari ya akaunti au jina la akaunti. 

Anwani

Anwani ya barua pepe ya mtumiaji, kama vile barua pepe au anwani ya nyumbani.

Nambari ya simu

Nambari ya simu ya mtumiaji.

Mbari na kabila

Maelezo kuhusu mbari au kabila la mtumiaji.

Imani za kidini au siasa

Maelezo kuhusu imani za kidini au kisiasa za mtumiaji.

Mwelekeo wa kijinsia

Maelezo kuhusu mwelekeo wa ngono wa mtumiaji.

Maelezo mengineyo

Taarifa binafsi nyinginezo kama vile tarehe ya kuzaliwa, utambulisho wa kijinsia, hali ya kuwa mwanajeshi mstaafu n.k.

Maelezo ya fedha

Maelezo ya malipo ya mtumiaji

Maelezo kuhusu akaunti za fedha za mtumiaji, kama vile nambari ya kadi ya mikopo.

Historia ya ununuzi

Maelezo kuhusu ununuzi au miamala iliyofanywa na mtumiaji.

Alama ya kuweza kulipa mikopo

Maelezo kuhusu alama ya mtumiaji ya kuweza kulipa mikopo.

Maelezo mengine ya fedha

Maelezo mengine yoyote ya fedha kama vile mshahara au madeni ya mtumiaji.

Afya na siha

Maelezo ya afya

Maelezo kuhusu afya ya mtumiaji, kama vile dalili au rekodi za matibabu.

Maelezo ya siha

Maelezo kuhusu siha ya mtumiaji, kama vile mazoezi au mazoezi mengineyo ya mwili.

Ujumbe

Barua pepe

Barua pepe za mtumiaji, ikiwa ni pamoja na mada za barua pepe, mtumiaji, wapokeaji na maudhui ya barua pepe

SMS au MMS

SMS za mtumiaji, ikiwa ni pamoja na mtumaji, wapokeaji na maudhui ya ujumbe

Ujumbe mwingine wa ndani ya programu

Aina nyingine yoyote ya ujumbe. Kwa mfano, ujumbe wa papo hapo au maudhui ya gumzo.

Picha na video

Picha

Picha za mtumiaji.

Video

Video za mtumiaji.

Faili za sauti

Rekodi za sauti

Sauti ya mtumiaji kama vile ujumbe wa sauti au rekodi ya sauti.

Faili za muziki

Faili za muziki za mtumiaji.

Faili zingine za sauti

Faili zingine zozote za sauti zinazoundwa au kutolewa na mtumiaji.

Faili na hati

Faili na hati

Faili au hati za mtumiaji, au maelezo yoyote kuhusu faili au hati zake kama vile majina ya faili.

Kalenda

Matukio ya kalenda

Maelezo kutoka kwenye kalenda ya mtumiaji kama vile matukio, vidokezo vya matukio na watakaohudhuria.

Anwani

Anwani

Maelezo kuhusu anwani za mtumiaji kama vile majina ya anwani, historia ya ujumbe na maelezo ya grafu ya mitandao jamii kama vile majina ya watumiaji, upya wa anwani, mara ambazo anwani zimetumika, muda wa mawasiliano au rekodi ya simu zilizopigwa.

Shughuli kwenye programu

Matumizi ya programu

Maelezo kuhusu jinsi mtumiaji anavyotumia programu. Kwa mfano, idadi ya mara ambazo wanatembelea ukurasa au sehemu wanazogusa.

Historia ya mambo uliyotafuta ndani ya programu

Maelezo kuhusu utafutaji wa mtumiaji kwenye programu yako.

Programu zilizosakinishwa

Maelezo kuhusu programu zilizosakinishwa kwenye kifaa cha mtumiaji.

Maudhui mengine ya watumiaji

Maudhui mengine yoyote yaliyozalishwa na mtumiaji ambayo hayajaorodheshwa hapa au katika sehemu nyingine yoyote. Kwa mfano, wasifu wa mtumiaji, madokezo au majibu ya wazi ya mtumiaji.

Vitendo vingine

Shughuli au vitendo vingine vya mtumiaji katika programu havijaorodheshwa hapa kama vile uchezaji na idadi ya ishara za imenipendeza na chaguo za kidirisha.

Kuvinjari kwenye wavuti

Historia ya kuvinjari kwenye wavuti

Maelezo kuhusu tovuti alizotembelea mtumiaji.

Utendaji na maelezo ya programu

Kumbukumbu za kuacha kufanya kazi

Data ya rekodi ya matukio ya kuacha kufanya kazi ya programu yako. Kwa mfano, idadi ya mara ambazo programu yako imeacha kufanya kazi au maelezo mengine yanayohusiana moja kwa moja na matukio ya kuacha kufanya kazi.

Uchunguzi

Maelezo kuhusu utendaji wa programu yako. Kwa mfano, muda wa matumizi ya betri, muda wa kupakia, muda wa kusubiri, kasi ya picha au uchunguzi wowote wa kiufundi.

Data nyingine ya utendaji wa programu

Data nyingine ya utendaji wa programu ambayo haijaorodheshwa hapa.

Kifaa au vitambulisho vingine

Kifaa au vitambulisho vingine

Vitambulishi vinavyohusiana na kifaa, kivinjari au programu mahususi. Kwa mfano, nambari ya IMEI, Anwani ya MAC, kitambulisho cha kifaa cha Widevine, kitambulisho cha kusakinisha cha Firebase au kitambulishi cha matangazo.
Madhumuni
Mdhumuni ya data Maelezo Mfano
Utendaji wa programu Inatumika kwenye vipengele vinavyopatikana katika programu Kwa mfano, kuwasha vipengele vya programu au kuthibitisha watumiaji.
Takwimu

Inatumiwa kukusanya data kuhusu jinsi watumiaji wanavyotumia programu yako, au jinsi inavyofanya kazi

Kwa mfano, kuangalia idadi ya watumiaji wanaotumia kipengele mahususi, kufuatilia hali ya programu, kuchunguza na kurekebisha hitilafu au matukio ya programu kuacha kufanya kazi, au kuboresha utendaji wa baadaye.
Mawasiliano ya msanidi programu Inatumika kutuma habari au arifa kuhusu programu au msanidi programu. Kwa mfano, kutuma arifa za programu ili kuwaarifu watumiaji kuhusu sasisho muhimu la usalama au kuwaarifu watumiaji kuhusu vipengele vipya vya programu.
Utangazaji au uuzaji Inatumika kuonyesha au kulenga matangazo au mawasiliano ya matangazo au kupima utendaji wa matangazo Kwa mfano, kuonyesha matangazo katika programu yako, kutuma arifa za programu ili kutangaza bidhaa na huduma zingine au kushiriki data na washirika wa matangazo.
Kuzuia ulaghai, usalama na kutii

Inatumika kwa ajili ya kuzuia ulaghai, madhumuni ya usalama au utii wa sheria.

Kwa mfano, kufuatilia majaribio yasiyofaulu ya kuingia katika akaunti ili kutambua shughuli za ulaghai.

Ubinafsishaji Inatumika kuweka mapendeleo kwenye programu yako, kama vile kuonyesha maudhui yanayopendekezwa au mapendekezo.

Kwa mfano, kupendekeza orodha za kucheza kulingana na mazoea ya kusikiliza ya mtumiaji, au kuwasilisha habari za maeneo kulingana na eneo la mtumiaji.

Usimamizi wa akaunti Inatumika kwa ajili ya mpangilio au usimamizi wa akaunti ya mtumiaji na msanidi programu. Kwa mfano, kuwaruhusu watumiaji kuunda akaunti au kuweka maelezo kwenye akaunti anazotoa msanidi programu kwa ajili ya matumizi katika huduma zake, kuingia katika akaunti ya programu au kuthibitisha vitambulisho vyao.

Kujaza Fomu ya usalama wa data katika Dashibodi ya Google Play

Unaweza kutueleza kuhusu mbinu za usalama na faragha kwenye programu yako katika Fomu ya usalama wa data kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu katika Dashibodi ya Google Play.

Muhtasari

Kwanza, utaulizwa iwapo programu yako inakusanya au kushiriki aina fulani za data ya mtumiaji. Hapa ndipo unapotujulisha iwapo programu yako inakusanya au kushiriki aina zozote zinazohitajika za data ya mtumiaji. Ikiwa inafanya hivyo, utaulizwa maswali fulani kuhusu mbinu zako za faragha na usalama. Ikiwa huna uhakika kuhusu mojawapo ya maswali haya, unaweza kuhifadhi fomu yako kama rasimu wakati wowote na uirejelee baadaye.

Kisha, utajibu maswali fulani kuhusu kila aina ya data ya mtumiaji. Ikiwa programu yako inakusanya au kushiriki aina zozote zinazohitajika za data ya watumiaji, utaombwa uzichague. Kwa kila aina ya data, utaulizwa maswali kuhusu jinsi data inavyotumika na kushughulikiwa.

Kabla ya kuwasilisha, utaona onyesho la kukagua la kitakachoonyeshwa kwa watumiaji kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Baada ya kuwasilisha, maelezo utakayotoa yatakaguliwa na Google kama sehemu ya mchakato wa ukaguzi wa programu.

Mchakato wa Google wa ukaguzi haujabuniwa ili kuthibitisha usahihi na ukamilifu wa taarifa za usalama wa data yako. Ingawa tunaweza kutambua tofauti fulani katika ubainishaji wako na tutachukua hatua zinazofaa za utekelezaji tunapofanya hivyo, ni wewe tu uliye na maelezo yote yanayohitajika ili kujaza Fomu ya usalama wa data. Ni wajibu wako pekee kutoa taarifa kamili na sahihi katika ukurasa wa programu yako kwenye Google Play.

Jaza na uwasilishe fomu yako

Unapokuwa tayari kuanza, yafuatayo ni maagizo ya jinsi unavyojaza na kuwasilisha Fomu ya usalama wa data katika Dashibodi ya Google Play:

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera> Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "Usalama wa data", chagua Anza.
  3. Kabla hujaanza kujaza fomu, soma sehemu ya "Muhtasari". Sehemu hii inatoa maelezo kuhusu maswali utakayoulizwa na maelezo utakayohitaji kutoa. Utakapomaliza kusoma na kuwa tayari kuanza, chagua Inayofuata ili uende kwenye sehemu inayofuata.
  4. Katika sehemu ya "Usalama na ukusanyaji wa data", kagua orodha ya aina zinazohitajika za data ya mtumiaji unazohitaji kufichua. Ikiwa programu yako inakusanya au kushiriki aina zozote zinazohitajika za data ya mtumiaji, chagua Ndiyo. Kama sivyo, chagua Hapana.
  5. Ikiwa umechagua Ndiyo, thibitisha yafuatayo kwa kujibu Ndiyo au Hapana:
    • Iwapo data yote ya mtumiaji inayokusanywa na programu yako inasimbwa kwa njia fiche inapotumwa au la.
    • Iwapo unatoa njia ambayo watumiaji wanatumia kuomba data yao ifutwe au la.
  6. Chagua, Inayofuata ili uende kwenye sehemu inayofuata.
  7.  Katika sehemu ya "Aina za data", chagua aina zote za data ya mtumiaji zinazokusanywa na kushirikiwa na programu yako. Utakapomaliza, chagua Inayofuata ili uende kwenye sehemu inayofuata. Ni sharti [ukamilishe sehemu hii kulingana na mwongozo ulio hapo juu wa kukusanya na kushiriki data.
  8. Katika sehemu ya "Kutumia na kushughulikia data", jibu maswali kuhusu jinsi data inavyotumiwa na kushughulikiwa kwa kila aina ya data ya mtumiaji ambayo programu yako inakusanya au kushiriki. Karibu na kila aina ya data ya mtumiaji, chagua Anza ili ujibu maswali. Utakapomaliza, chagua Inayofuata ili uende kwenye sehemu inayofuata.
    • Kumbuka:Unaweza kubadilisha aina za data ya mtumiaji zinazochaguliwa kwa kurudi kwenye sehemu iliyotangulia na kubadilisha uteuzi wako.
  9. Baada ya kujibu maswali yote, sehemu ya "Ukaguzi wa ukurasa wa programu katika Google Play hukagua maelezo yatakayoonyeshwa kwa watumiaji kwenye Google Play kulingana na majibu utakayotoa. Kagua maelezo haya.
  10. Ukiwa tayari kuwasilisha fomu yako uliyojaza, chagua Wasilisha. Ikiwa ungependa kurudi nyuma na kubadilisha maelezo fulani, unaweza kuchagua Rudi nyuma ili urekebishe majibu yako. Ikiwa huna ukahika na maelezo fulani, unaweza kuchagua Hifadhi kama rasimu na urejee kwenye fomu baadaye. Ukichagua Ondoa mabadiliko, utahitaji kuanza kujaza fomu tena.

Pakia na utume majibu ya fomu yako

Unaweza kutuma majibu ya fomu yako kwenye faili ya CSV. Unaweza pia kupakua sampuli ya CSV, kujaza fomu nje ya mtandao na kupakia fomu uliyojaza kutoka CSV.

Bofya hapa ili upakue sampuli ya CSV.

Elewa muundo wa CSV

CSV ina safu mlalo moja kwa kila jibu. Majibu ya maswali ya jibu moja na ya maswali ya kuchagua jibu moja yanapatikana katika safu mlalo kadhaa, kulingana na idadi ya chaguo zinazopatikana. Ili ujibu swali, weka NDIVYO au SIVYO katika kisanduku husika katika safu wima ya "thamani ya jibu" au unaweza kuacha kisanduku hicho bila chochote ikiwa swali si la lazima au ikiwa unajibu swali linalohitaji kuchagua jibu moja. Safu wima ya "Masharti ya jibu" inaonyesha iwapo ni lazima ujibu na inaweza kuwa na thamani zifuatazo:

  • SI LAZIMA: Halihitajiki, unaweza kuacha tupu.
  • LINAHITAJIKA: Ni lazima ujibu, ni sharti uweke thamani ya jibu
  • MULTIPLE_CHOICE: Unaweza kuweka thamani ya jibu la NDIVYO kwenye angalau mojawapo ya chaguo kwa kitambulisho cha swali husika. Si lazima ujaze majibu yote.
  • SINGLE_CHOICE: Unaweza kuweka thamani ya jibu la NDIVYO kweye mojawapo ya chaguo za majibu kwa kitambulisho cha swali husika. Si lazima ujaze majibu yote.
  • MAYBE_REQUIRED: Linahitajika tu wakati masharti fulani yametimizwa, k.m. kulingana na jibu la swali lililotangulia

Jedwali lililo hapa chini linatoa mfano wa sehemu za "Jina" na "Maeneo yanayokadiriwa" za Fomu ya usalama wa data. Lina:

  • Swali la kuchagua jibu moja
  • Swali linalohitaji jibu
  • Swali ambalo si lazima ujibu

Kitambulisho cha swali
(kinachoweza kusomwa kwa mashine)

Jibu
(linaloweza kusomwa kwa mashine)
Thamani ya jibu Masharti ya jibu Lebo ya maswali yanayofaa binadamu
PSL_DATA_
TYPES_
PERSONAL
PSL_NAME NDIVYO MULTIPLE_
CHOICE
Taarifa binafsi
Jina
...        
PSL_DATA_
TYPES_
LOCATION
PSL_
APPROX_
LOCATION
NDIVYO MULTIPLE_
CHOICE
Mahali
Eneo linalokadiriwa
...        
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
PSL_DATA_USAGE_
COLLECTION_AND_
SHARING
PSL_DATA_
USAGE_ONLY_
COLLECTED
NDIVYO MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na kushughulikia data (Jina)
Je, data hii inakusanywa, kushirikiwa au vyote?
Inakusanywa
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
PSL_DATA_USAGE_
COLLECTION_AND_
SHARING
PSL_DATA_
USAGE_ONLY_
SHARED
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na kushughulikia data (Jina)
Je, data hii inakusanywa, kushirikiwa au vyote?
Inashirikiwa
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
PSL_DATA_USAGE_
EPHEMERAL
  NDIVYO MAYBE_
REQUIRED
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, data hii inachakatwa kwa muda mfupi?
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_USER_
CONTROL
PSL_DATA_
USAGE_USER_
CONTROL_
OPTIONAL
NDIVYO SINGLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, data hii inahitajika kwenye programu yako au watumiaji wanaweza kuchagua iwapo inakusanywa?
Watumiaji wanaweza kuchagua iwapo data hii inakusanywa
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_USER_
CONTROL
PSL_DATA_
USAGE_USER_
CONTROL_
REQUIRED
  SINGLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, data hii inahitajika kwenye programu yako au watumiaji wanaweza kuchagua iwapo inakusanywa?
Inahitaji kukusanya data (watumiaji hawawezi kuzima ukusanyaji huu wa data)
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_APP_
FUNCTIONALITY
NDIVYO MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Utendaji wa programu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_ANALYTICS NDIVYO MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Takwimu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_DEVELOPER_
COMMUNICATIONS
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Mawasiliano ya msanidi programu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_FRAUD_
PREVENTION_
SECURITY
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Kuzuia ulaghai, usalama na kutii
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_ADVERTISING   MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Utangazaji au uuzaji
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_
PERSONALIZATION
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Kuweka mapendeleo
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
COLLECTION_
PURPOSE
PSL_ACCOUNT_
MANAGEMENT
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inakusanywa? Chagua yote yanayotumika.
Usimamizi wa akaunti
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_APP_
FUNCTIONALITY
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Utendaji wa programu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_ANALYTICS   MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Takwimu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_DEVELOPER_
COMMUNICATIONS
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Mawasiliano ya msanidi programu
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_FRAUD_
PREVENTION_
SECURITY
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Kuzuia ulaghai, usalama na kutii
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_
ADVERTISING
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Utangazaji au uuzaji
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_
PERSONALIZATION
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Kuweka mapendeleo
PSL_DATA_USAGE_
RESPONSES:
PSL_NAME:
DATA_USAGE_
SHARING_
PURPOSE
PSL_ACCOUNT_
MANAGEMENT
  MULTIPLE_
CHOICE
Kutumia na Kushughulikia data (Jina)
Je, ni kwa nini data hii ya mtumiaji inashirikiwa? Chagua yote yanayotumika.
Usimamizi wa akaunti
Tuma kwenye faili ya CSV
  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera> Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "Usalama wa data", chagua Anza.
  3. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, chagua Tuma kwenye faili ya CSV.
Pakia kutoka kwenye faili ya CSV

Muhimu: Majibu ambayo tayari yamewekwa katika fomu yako yatabatilishwa utakapopakia faili ya CSV.

  1. Fungua Dashibodi ya Google Play kisha uende kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu (Sera> Maudhui ya programu).
  2. Chini ya "Usalama wa data", chagua Anza.
  3. Karibu na sehemu ya juu kulia kwenye ukurasa, chagua Pakia kwenye faili ya CSV.

Baada ya kuwasilisha Fomu yako ya usalama wa data

Baada ya kuwasilisha, maelezo utakayotoa yatakaguliwa na Google kama sehemu ya mchakato wa ukaguzi wa programu.

Hadi kufikia tarehe 20 Julai 2022, unaweza kuendelea kuchapisha masasisho ya programu kwa muda bila kujali iwapo tunapata hitilafu kwenye maelezo uliyofichua. Ikiwa hakuna hitilafu, programu yako itaidhinishwa na hutahitaji kufanya chochote. Ikiwa kuna hitilafu, utahitaji kurejesha hali ya Fomu yako ya usalama wa data kuwa "Rasimu" katika Dashibodi ya Google Play ili uchapishe sasisho la programu yako. Tutatumia pia mmiliki wa akaunti ya msanidi programu barua pepe, Ujumbe wa kikasha katika Dashibodi ya Google Play na kuonyesha maelezo haya kwenye ukurasa wa Hali ya sera (Sera > Hali ya sera).

Baada ya tarehe 20 Julai, 2022, programu zote zitahitajika kujaza Fomu sahihi ya usalama wa data inayofichua mbinu zake za kukusanya na kushiriki data (ikiwa ni pamoja na programu zisizokusanya data yoyote ya mtumiaji).

Muundo usio wa lazima wa SDK

Ikiwa wewe ni mtoa huduma za SDK, unaweza kubofya sehemu iliyo hapa chini ili uangalie muundo unaoweza kutumia kuchapisha mwongozo kwa ajili ya watumiaji wa programu yako. 

Wasanidi programu watahitajika kufichua mbinu za usalama, kukusanya na kushiriki data ya programu zao kama sehemu mpya ya usalama wa data katika Google Play. Ili kusaidia wasanidi programu katika kuunda uwazi wa usalama na data ya mtumiaji, mwongozo ulio hapa chini unaweza kutumika kuchapisha mwongozo wa SDK kwa wasanidi programu wanaojumuisha SDK yako katika programu zao.

Google Play inachapisha muundo huu usio wa lazima kwa wasanidi programu wa SDK ili uutumie unapokufaa, ila unaweza kutumia muundo wowote au usitumie muundo kulingana na mahitaji ya watumiaji wako.

Muundo usio wa lazima wa SDK
[Jina la SDK]
SDK / kipengele cha SDK kinachoweza kukusanya au kushiriki data

Aina ya data ambayo SDK inafikia na kukusanya

Kumbuka: Zingatia kutoa maelezo sahihi ya kiufundi yatakayowasaidia wateja wako kubaini ni ipi kati ya ufafanuzi wa Sehemu ya Usalama wa Data katika Google Play kuhusu aina za data utatumika kwenye data ambayo SDK yako inakusanya. Katika hali fulani, unaweza kufurahia kutumia ufafanuzi wa Sehemu ya Usalama wa Data (k.m., "eneo linalokadiriwa") kwa sababu aina ya data inayotumika ni dhahiri na haitegemei vipengele vya ziada. Katika hali fulani, ufafanuzi wa aina ya data unaweza kutegemea jinsi data husika inavyotumika baada ya kukusanywa au kutegemea ufasiri fulani wa msanidi programu wa ufafanuzi wa Sehemu ya Usalama wa Data katika Google Play. Kwa mfano, anwani za IP zinaweza kutumiwa kwa njia nyingine kudhibitisha eneo au kutoa vitambulishi au kwa madhumuni mengine mbalimbali kulingana na hali ya SDK, utekelezaji wake na programu yoyote na vipengele vingine. 

Kumbuka: Wasanidi programu hawahitaji kubainisha ufikiaji wa data kama ukusanyaji ikiwa inaonekana peke yake kwenye kifaa cha mtumiaji ili mradi data hiyo haitumwi kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji.

Kwa kila aina ya data iliyoorodheshwa:

  1. Fafanua ufikiaji wa data unaohitajika (au wa kiotomatiki) dhidi ya ufikiaji usio wa lazima. "Si lazima" inajumuisha uwezo wa mtumiaji kujiunga au kujiondoa kwenye ukusanyaji wa data.
  2. Je, SDK inatuma data hii kutoka kwenye kifaa?
  3. Fafanua madhumuni ya kukusanya data kisha kuishiriki na kuitumia.
    • Kumbuka:Katika hali nyingi, madhumuni ya kukusanya na kushiriki yanaweza kutegemea matumizi au utekelezaji mahususi wa SDK yako na msanidi programu husika. Zingatia kuweka maelezo yoyote sahihi ya kiufundi hapa yatakayowasaidia wateja wako kubaini madhumuni yatakayotumika na kuelezwa katika sehemu ya usalama ya Programu zao. Kwa mfano, ikiwa SDK yako ina sehemu zisizo za lazima, unapaswa kutoa maelezo haya kwa misingi ya kila sehemu.
  4. Je, SDK hutuma data kwa wengine, ikiwa ni pamoja na programu nyingine zilizo kwenye kifaa cha mtumiaji?  Fafanua madhumuni ya kushiriki maelezo haya.
Kumbuka: Wasanidi programu hawahitaji kufichua kama kushiriki baadhi ya data katika Sehemu ya Usalama wa Data kwenye programu zao katika hali fulani, kwa mfano, data inapotumwa kwa mtoa huduma anayechakata data kwa niaba yake, au ikiwa data inatumwa kwa madhumuni mahususi ya kisheria na katika hali nyingine. Soma Makala ya usaidizi kutoka Dashibodi ya Google Play ili upate maelezo zaidi. Zingatia kuweka maelezo yoyote sahihi ya kiufundi hapa yatakayowasaidia wateja wako wanapotathmini iwapo hali ya kushiriki isiyofuata kanuni inatumika.

Madokezo ya kiwango cha programu [sehemu kamili ya data yoyote inayokusanywa au kushirikiwa]

  1. Je, SDK yako inasimba data kwa njia fiche inapotumwa?
    • Kumbuka: Ikiwa jibu ni tofauti kwenye seti tofauti za data ambazo SDK inakusanya, zingatia kueleza jinsi usimbaji fiche unavyotumika data inapotumwa kwa kila kifungu kinachofaa cha data. Katika Sehemu ya Usalama wa Data katika Google Play, wasanidi programu wanaweza kubainisha usimbaji fiche data inapotumwa ikiwa inatumika kwa data yote ya mtumiaji ambayo programu yao (ikiwa ni pamoja na SDk na maktaba yake) inakusanya na kutuma kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji.
  2. Je, msanidi programu na/au watumiaji wanaweza kuomba kufuta data ya mtumiaji iliyokusanywa?

Maswali yanayoulizwa sana

Kunja yote Panua yote

Ukaguzi na uwasilishaji wa programu

Itakuwaje iwapo nitahitaji muda wa ziada ili kutimiza masharti mapya?

Tumefungua Dashibodi ya Google Play mnamo Oktoba kwa ajili ya uwasilishaji wa Fomu ya usalama wa data na tutatoa muda wa matumizi kabla ya kutimiza masharti wa hadi tarehe 20 Julai, 2022 ambao unapaswa kuwa muda wa kutosha. Kwa wakati huu, hatuna mipango ya kuongeza muda.

Je, programu yangu inaweza kuzuiwa na Google Play kutokana na maelezo ninayowasilisha katika Fomu yangu ya usalama wa data?

Kwa kifupi, ndiyo. Unapaswa kuweka maelezo sahihi yanayoonyesha mbinu za ukusanyaji na ushughulikiaji wa data za programu yako. Utawajibikia maelezo unayotoa. Google Play hukagua programu kwa kuangalia masharti yote ya sera; hata hivyo hatuwezi kufanya uamuzi kwa niaba ya wasanidi programu kuhusu jinsi wanavyoshughulikia data ya mtumiaji. Ni wewe tu uliye na maelezo yote yanayohitajika ili kujaza Fomu ya usalama wa data.

Tukigundua kuwa umewakilisha data ya uongo na inakiuka sera, tutahitaji uirekebishe. Programu zisizotii sera zitategemea utekelezaji wa sera, kama vile masasisho yaliyozuiwa au kuondolewa kwenye Google Play.

Inachukua muda gani ili masasisho ya Usalama wa Data yanayofanywa kupitia Dashibodi ya Google Play yaonekane kwenye Google Play?

Baada ya kuwasilisha programu mpya au sasisho katika programu iliyopo kwenye Dashibodi ya Google Play, inaweza kuchukua muda kiasi ili programu yako iweze kuchakatwa kwa ajili ya uchapishaji wa kawaida kwenye Google Play. Huenda programu fulani zikakaguliwa kwa muda mrefu, hatua ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa muda wa ukaguzi kwa hadi siku 7 au zaidi katika hali za kipekee.

Je, ninaweza kufanya nini ili kutatua iwapo sioni sehemu yangu ya Usalama wa Data ikiwa imechapishwa?

Masasisho ya programu na uwasilishaji mpya lazima utii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu za Google Play. Unaweza kwenda kwenye ukurusa wa Muhtasari wa uchapishaji katika Dashibodi ya Google Play ili uangalie iwapo uwasilishaji wa programu yako bado haujakamilika.

Iwapo sasisho lako jipya lipo tayari na bado huoni fomu ya sehemu ya Usalama wa Data kwenye Google Play, unaweza kuangalia kama uchapishaji unaodhibitiwa umewashwa kwenye Dashibodi ya Google Play. Ukiwasha kipengele cha uchapishaji unaodhibitiwa, toleo lako halitapatikana kwa umma mpaka ulichapishe. Unaweza kusambaza toleo kutoka kwenye ukurasa wa Muhtasari wa uchapishaji. Uwasilishaji ulioidhinishwa utachapishwa na kupatikana kwenye Google Play baada ya kipindi kifupi.

Ikiwa ulisasisha maudhui ya Sehemu ya Usalama wa Data lakini huoni maudhui mapya kwenye Google Play, jaribu kuonyesha upya ukurasa wa programu. Kumbuka kwamba, kutokana na muunganisho wa kifaa na utofauti wa upakiaji wa seva, huenda ikachukua siku kadhaa (katika hali fulani mpaka siku 7) ili sasisho la programu liweze kufikia vifaa vyote. Tunaomba uvumilivu wako wakati Google Play inasajili na kuwasilisha sasisho lako la programu.

Nimewasilisha maelezo kama haya kwenye iOS. Je, ninaweza kutumia tena kiasi gani cha maelezo hayo kwa ajili ya Fomu ya usalama wa data?

Ni vyema kuwa unaelewa vyema kanuni bora za kushughulikia data kwenye programu yako. Fomu ya usalama wa data itaomba maelezo ya ziada na tofauti ambayo huenda hukutumia awali, hivyo basi tungependa utarajie kuwa hali hii bado itahitaji juhudi za timu yako. Uainishaji na mfumo wa Sehemu ya Usalama wa Data kwenye Google Play unaweza kutofautiana na ule unaotumika katika maduka mengine ya programu.

Je, unahakikishaje kuwa wasanidi programu wanashiriki maelezo sahihi? Tumeona kuwa maelezo haya si sahihi kila wakati katika sekta.

Sawa na sera ya faragha au maelezo ya programu kama picha za skrini na maelezo, wasanidi programu wanawajibikia maelezo wanayotoa katika Sehemu yao ya Usalama wa Data. Sera ya data ya mtumiajikwenye Google Play inahitaji wasanidi programu kutoa maelezo sahihi. Tukigundua kuwa msanidi programu amewakilisha data ya uongo na inakiuka sera, tutahitaji msanidi programu airekebishe. Programu zisizotii sera zinategemea utekelezaji wa sera.

Je, Google hudhibiti ikiwa data ninayokusanya inafaa?

Watumiaji wa Google Play wanapaswa kuwa na imani kuwa data yao iko salama. Tunaendelea kuzindua vipengele na sera mpya ili kulinda faragha ya mtumiaji na kuendelea kufanya Google Play kuwa mfumo wa kuaminika kwa kila mtu. Baadhi ya vipengele na sera mpya za Google Play zimeimarisha udhibiti na uwazi kwa mtumiaji. Vingine husaidia kuhakikisha kuwa wasanidi programu wanafikia tu data binafsi inapohitajika kwa ajili ya matumizi ya msingi ya programu. Sera zilizopo za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play kama hizi zina masharti fulani kuhusu udhibiti na uwazi wa data. Programu zisizotii sera za Google Play za Mpango wa Wasanidi Programu zinategemea utekelezaji wa sera.

Je, ninahitaji kusasisha Sehemu yangu ya Usalama wa Data kila baada ya muda gani?

Unapaswa kusasisha Sehemu yako ya Usalama wa Data wakati kuna mabadiliko yanayofaa kwenye kanuni za data ya programu yako. Ni sharti majibu yako ya Fomu ya usalama wa data yawe sahihi na kamili kila wakati.

Je, Sehemu ya Usalama wa Data kwenye Google Play itaathiri upakuaji wa programu?

Sehemu ya Usalama wa Data inaweza kuwasaidia watu kujifanyia uamuzi unaofaa kuhusu programu za kupakua. Inawasaidia pia wasanidi programu kuimarisha uaminifu na kupata watumiaji wengi wenye uhakika kuwa data yao itashughulikiwa kwa umakini. Wasanidi programu wameshiriki kuwa wanataka njia dhahiri za kuwasiliana na watumiaji wao kuhusu kanuni za data.

Kujaza Fomu ya usalama wa data

Itakuwaje iwapo programu yangu ina utendaji tofauti katika matoleo tofauti yanayotumika ya Android?

Google Play ina Fomu moja ya jumla ya usalama wa data na Sehemu ya Usalama wa Data katika ukurasa wa programu katika Google Play kwa kila jina la kifurushi ambayo inafaa bila kujali matumizi, toleo la programu, eneo na umri wa mtumiaji. Yaani, ikiwa yoyote kati ya mkusanyiko, matumizi au viungo vinapatikana katika toleo lolote la programu inayosambazwa sasa kwenye Google Play, mahali popote ulimwenguni, ni sharti uonyeshe maelezo haya kwenye fomu. Kwa hivyo, Sehemu ya Usalama wa Data hufafanua jumla ya data inayokusanywa na kushirikiwa na programu yako kwenye matoleo yake yote yanayosambazwa kwenye Google Play. Unaweza kutumia sehemu ya "Kuhusu programu hii" kutuma maelezo yanayohusu toleo kwa watumiaji wako.

Ninawezaje kuonyesha kuwa tunaweza kuwa na mbinu tofauti katika maeneo tofauti? Kwa mfano, hatutumii maktaba fulani barani Uropa, ila tunaweza kuyatumia katika nchi nyingine.

Kwa wakati huu, tunaangazia uwakilishi wa jumla wa kanuni zako za data kwa kila programu. Sehemu yako ya Usalama wa Data hufafanua jumla ya data inayokusanywa na kushirikiwa na programu yako kwenye matoleo yake yote yanayosambazwa kwenye Google Play. Unaweza kutumia sehemu ya "Kuhusu programu hii" kutuma maelezo yanayohusu toleo kwa watumiaji wako. Sehemu ya Usalama wa Data inajumuisha ufafanuzi wa watumiaji wa Google Play kuwa mbinu za usalama na ukusanyaji wa data katika programu zinaweza kutofautiana kulingana na idadi ya vipengele kama vile eneo.

Je, Sehemu za Usalama wa Data zinadhibitiwa na utaratibu wa idhini kwa watumiaji? Je, ninahitaji kuchukua hatua zozote za ziada na kuunda ufumbuzi dhahiri kwenye programu?

Hapana, Sehemu ya Usalama wa Data inawakilishwa tu kwenye ukurasa wa programu katika Google Play; hakuna ufumbuzi mpya katika mchakato wa kusakinisha programu ya mtumiaji, na hakuna idhini mpya ya mtumiaji inayohusiana na kipengele hiki. Ni sharti wasanidi programu wanaokusanya data binafsi na nyeti watekeleze ufumbuzi wa ndani ya programu na idhini wanapohitajika na Sera iliyopo ya Data ya Mtumiaji kwenye Google Play.

Je, ninawekaje alama kwenye ukusanyaji unaohitajika au usio wa lazima matoleo tofauti ya programu yangu inayoonyesha Sehemu ya Usalama wa Data yanapofanya mambo tofauti?

Sehemu ya Usalama wa Data inafafanua jumla ya data inayokusanywa na kushirikiwa na programu yako kwenye matoleo yake yote yanayosambazwa kwenye Google Play. Ikiwa toleo lolote la programu yako linahitaji ukusanyaji wa data fulani, ni sharti ubainishe ukusanyaji wake kama inavyohitajika katika Sehemu ya Usalama wa Data. Hupaswi kufafanua ukusanyaji kuwa usio wa lazima ikiwa unahitajika kwa watumiaji wowote wa programu yako. Unaweza kutumia sehemu ya "Kuhusu programu hii" kutuma maelezo yanayohusu toleo kwa watumiaji wako.

Je, ninahitaji kubainisha data ikiwa programu yangu inajumuisha ruhusa ila haikusanyi au kushiriki data?

Huhitaji kubainisha hali ya kukusanya au kushiriki data isipokuwa inakusanywa na/au kushirikiwa. Ni sharti programu yako itii Sera zote za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na sera yetu ya Ruhusa na API Zinazofikia Maelezo Nyeti.

Ikiwa aina moja ya data inakusanywa kama sehemu ya aina nyingine, ninafaa kubainisha zote mbili? Kwa mfano, ikiwa nilikusanya Anwani zinazojumuisha anwani ya barua pepe ya mtumiaji, ninafaa kubainisha aina za data ya "Anwani" na "Anwani ya barua pepe"?

Ikiwa unakusanya aina ya data kimakusudi unapokusanya aina nyingine ya data, unapaswa kufichua zote. Kwa mfano, ukikusanya picha za mtumiaji na uzitumie kubainisha sifa za mtumiaji (kama vile ukabila au mbari) unapaswa pia kufichua ukusanyaji wa data ya ukabila na mbari.

Je, ninahitajika kutoa mbinu ya ufutaji? Je, ni sharti utaratibu uwe wa data yoyote na data yote ya mtumiaji?

Sehemu ya Usalama wa Data hutoa mfumo kwa ajili yako kushiriki iwapo unatoa utaratibu wa kupokea maombi ya kufuta data kutoka kwa watumiaji. Kama sehemu ya kujaza Fomu ya usalama wa data, unahitajika kuonyesha ikiwa unatoa utaratibu huo.

Je, kuna aina mahususi ya utaratibu ambao ni lazima nitoe ili kuonyesha kuwa programu yangu inatumia maombi ya kufuta data ya mtumiaji?

Hakuna utaratibu uliobainishwa, hata hivyo ikiwa ni mbinu bora zaidi utaratibu wa ombi unapaswa kugundulika na kufikiwa kwa urahisi na watumiaji. Mifano ya kawaida ya mbinu zinazoonyesha wazi njia ambayo watumiaji wanaweza kuomba kufutwa kwa data inaweza kujumuisha, lakini si tu: vipengele vya ndani ya programu, fomu za mawasiliano au anwani mbadala ya barua pepe maalum.

Je, ninapaswa kuonyesha vipi katika Fomu yangu ya usalama wa data kuwa ninatoa ombi la utaratibu wa kufuta data ambayo inafutwa kiotomatiki au kwa kuficha utambulisho?

Unaweza kuchagua beji ya utaratibu wa ombi la kufuta katika Fomu ya usalama wa data ikiwa:

  • unawapatia watumiaji utaratibu wa kuomba kufutwa kwa data; au
  • unaanzisha kiotomatiki kufuta au kuficha utambulisho wa data iliyokusanywa ndani ya siku 90 za ukusanyaji data.

Unaweza kuchagua beji ya utaratibu wa ombi la kufuta hata kama unahitaji kuhifadhi data fulani kwa sababu halali kama vile kutii sheria au kuzuia matumizi mabaya.

Je, ikiwa utaratibu wa kufuta data ninaotoa haupatikani kwa watumiaji wote duniani —⁠ je, bado ninaweza kuashiria kuwa nimetoa utaratibu wa ombi la kufuta?

Google Play inatoa Fomu moja ya jumla ya Usalama wa Data na Sehemu ya Usalama wa Data katika ukurasa wa programu katika Google Play kwa kila jina la kifurushi ambacho kinafaa kushughulikia kanuni za data kulingana na matumizi yoyote, toleo la programu, eneo na umri wa mtumiaji. Yaani, ikiwa yoyote kati ya kanuni za data zinapatikana katika toleo lolote la programu inayosambazwa sasa kwenye Google Play, mahali popote ulimwenguni, ni sharti uonyeshe maelezo haya kwenye fomu. Kwa hivyo, Sehemu ya Usalama wa Data itafafanua jumla ya data inayokusanywa na kushirikiwa na programu yako kwenye matoleo yake yote yanayosambazwa kwenye Google Play.

Ni mbinu gani zinazoweza kutumika kuficha utambulisho wa data?

Kuna mbinu mbalimbali zinazoweza kuficha utambulisho wa data ili isiweze kuhusishwa na mtumiaji mahususi. Unapaswa kuwasiliana na wataalamu wako wa usalama na faragha ili kutambua mbinu zinazoweza kutumika katika hali yako. Kama mfano, ukurasa huu unafafanua baadhi ya mbinu za kuficha utambulisho wa data zinazotumiwa na Google, kama vile faragha kwa kuchanganya data.

Je, ninafaa kushughulikia vipi ukusanyaji na utumiaji wa Anwani za IP?

Kama ilivyo kwa aina zingine za data, unafaa kufichua unavyokusanya, kutumia na kutuma Anwani za IP kulingana na kanuni na matumizi yake mahususi. Kwa mfano, wasanidi programu wanapotumia Anwani za IP kama njia ya kubainisha mahali, basi aina ya data inapaswa kubainishwa.

Je, ninafaa kufichua vipi jinsi ninavyokusanya na kutuma data ya aina nyingine za vitambulishi?

Kama ilivyo kwa aina zingine za data, unafaa kufichua unavyokusanya, kutumia na kushiriki aina tofauti za vitambulishi kulingana na kanuni na matumizi yako mahususi. Kwa mfano, ukusanyaji wa jina la akaunti linalohusiana na mtu anayetambulika unafaa kubainishwa kuwa "Kitambulishi Binafsi" na ukusanyaji wa kitambulisho cha matangazo cha mtumiaji cha Android kinafaa kubainishwa kuwa "Kifaa au vitambulishi vingine." Mfano mwingine, kitambulishi kinachohusiana na tukio mahususi la ndani ya programu, ila hakihusiani na kifaa, kivinjari au programu mahususi, hakihitaji kufichuliwa kuwa "Kifaa au vitambulishi vingine."

Jinsi ilivyobainishwa hapo juu, ukusanyaji wa kuficha utambulisho wa data unafaa kufichuliwa kwenye utafiti wako chini ya aina husika ya data. Kwa mfano, ukikusanya maelezo ya uchunguzi na kitambulishi cha kifaa, bado unapaswa kufichua ukusanyaji wa "Uchunguzi" katika Fomu yako ya Usalama wa Data.

Je, ni aina gani za shughuli ambazo "watoa huduma" wanaweza kutekeleza?

Mtoa huduma anaweza tu kuchakata data ya mtumiaji kwa niaba yako. Kwa mfano mtoa huduma za takwimu anayechakata data ya mtumiaji kwenye programu yako kwa niaba yako pekee, au mtoa huduma za wingu anayeweka data ya mtumiaji kwenye programu yako kwa matumizi yako, atafuzu kuwa "watoa huduma." Upande mwingine, ikiwa mtoa huduma za SDK anaunda wasifu wa matangazo unaolenga wateja wengi kulingana na data ya programu yako, hiyo haitachukuliwa kama shughuli ya "mtoa huduma" kwa madhumuni ya Sehemu ya Usalama wa Data na huenda ikahitaji kufichuliwa kama "kushiriki" katika Fomu yako ya Usalama wa Data.

Programu yangu inatumia huduma ya nje ya malipo ili kuruhusu miamala ya kifedha. Je, programu yangu inatakiwa kufichua maelezo ya kifedha kama vile maelezo ya kadi ya mikopo kwenye Sehemu yake ya Usalama wa Data?

Inategemea hali ya ujumuishaji wako na huduma ya malipo. Ikiwa programu yako inatumia huduma ya malipo kama vile PayPal, Google Pay, mfumo wa utozaji wa Google Play au huduma zinazofanana ili ukamilishe malipo ya miamala, huna haja ya kubainisha mkusanyiko wa data ambayo huduma ya malipo inakusanya kuhusiana na uchakataji wake wa miamala ya kifedha, kama vile namba ya kadi ya mikopo, ikiwa masharti yafuatayo yametimizwa:

  • Programu yako haifikii kamwe maelezo haya; na
  • Huduma ya malipo inakusanya maelezo haya moja kwa moja kutoka kwa mtumiaji na mkusanyiko unasimamiwa na sheria na masharti ya huduma.

Unapaswa kukagua ujumuishaji wako na huduma ya malipo kwa undani ili kuhakikisha kwamba Sehemu ya usalama wa data ya programu yako inabainisha mkusanyiko wa data zozote zinazofaa na kushiriki ambazo hazitimizi masharti haya. Pia, unapaswa kuzingatia iwapo programu yako inakusanya maelezo mengine ya kifedha, kama vile historia ya ununuzi na iwapo programu yako inapokea data yoyote inayofaa kutoka kwenye huduma ya malipo, kwa mfano kwa madhumuni hatarishi na yenye kupambana na ulaghai.

Programu yangu inaruhusu watumiaji kupakia data zao moja kwa moja kwenye Hifadhi ya Google au Dropbox kwa ajili ya kuhifadhi nakala. Programu yangu haifikii data yoyote kati ya hizi. Je, hilo bado linapaswa kufichuliwa kama “mkusanyiko”?

Inategemea utekelezaji mahususi. Ikiwa mtumiaji anachagua kupakia data zake moja kwa moja kwenye hifadhi yake ya nje au akaunti ya hifadhi ya wingu (kama vile Hifadhi ya Google Play, Dropbox au huduma zinazofanana) na upakiaji huu unasimamiwa na hifadhi ya nje au sheria na masharti ya huduma ya kutoa hifadhi ya wingu na sera ya faragha, na programu yako haikusanyi kamwe au kufikia data husika, hivyo programu yako haihitaji kubainisha mkusanyiko wa data hii.

Je, nifanyeje kusimba data kwa njia fiche inapotumwa?

Unapaswa kufuata viwango bora vya sekta ili usimbe data za programu yako kwa njia fiche inapotumwa. Itifaki za usimbaji fiche wa kawaida zinajumuisha TLS (Usalama wa Mawasiliano Mtandaoni) na HTTPS.

Programu yangu inaruhusu mtumiaji kuunda akaunti au kuweka maelezo kwenye akaunti yake, kwa mfano, siku ya kuzaliwa au jinsia. Je, nifanyeje kubainisha data ambayo mtumiaji huweka kwenye akaunti yake?

Unapaswa kubainisha mkusanyiko wa data hii kwa ajili ya usimamizi wa akaunti, kuashiria (panapohitajika) ukusanyaji wa data ni hiari kwa mtumiaji.

Pia, kama ilivyo kwa aina yoyote ya data iliyokusanywa na programu yako, unapaswa kufichua data hii kwa madhumuni ambayo programu yako inazitumia. Kwa mfano, ikiwa programu yako inaruhusu mtumiaji kuweka siku ya kuzaliwa kwenye akaunti yake na kutumia data hiyo kutuma arifa za programu kwa wakati, programu yako inapaswa kubainisha madhumuni haya pamoja na usimamizi wa akaunti.

Usimamizi wa akaunti unaweza kutumika kushughulikia matumizi ya jumla ya data ya akaunti ambayo si mahususi kwa programu husika. Kwa mfano, ikiwa unatumia maelezo ya akaunti kwa ajili ya kuzuia ulaghai, utangazaji, uuzaji au mawasiliano ya msanidi programu kwenye huduma zako zote, na matumizi haya si mahususi kwa programu yako au shughuli katika programu yako, kubainisha "usimamizi wa akaunti" kama dhumuni la kukusanya data ya akaunti hii itatosha kuangazia matumizi hayo ya jumla katika sehemu yako ya usalama wa Data. Hata hivyo, ni lazima programu yako ibainishe madhumuni yote ambayo programu yenyewe hutumia data. Ikiwa ni mbinu bora, tunapendekeza uweke wazi jinsi programu yako inavyoshughulikia data ya mtumiaji kwa huduma za akaunti kama sehemu ya uchakataji hati katika kiwango cha akaunti na mchakato wa kujisajili.

Je, huduma za Mfumo ni nini?

Huduma za mfumo ni programu zilizosakinishwa mapema zinazotumia utendaji wa msingi wa mfumo. Huduma za mfumo zinaweza kutuma maombi ya kutojaza Fomu ya Usalama wa Data.

Uwasilishaji wa Sehemu ya Usalama wa Data wa programu yangu uliidhinishwa lakini hivi karibuni nimepokea arifa kuhusu sasisho. Je, ninawezaje kuangalia hali ya sasa ya uwasilishaji wangu na kama si ya kudumu?

Unaweza kuangalia hali ya uwasilishaji wako kwenye ukurasa wa Maudhui ya programu(Sera > Maudhui ya programu) kwenye Dashibodi ya Google Play. Ikiwa uwasilishaji wako unatii masharti, utaona alama ya kijani ya kuteua kwenye sehemu ya “Usalama wa Data”.

Kumbuka: Sera zetu zinatekelezwa kupitia mifumo na michakato ambayo inaendelea kuboreshwa kadiri muda unavyopita. Pia, mabadiliko na masasisho kwenye sera zetu yanaweza kuonekana kwenye programu ambazo ziliidhinishwa mapema ili kutekelezwa baadaye baada ya uwasilishaji wa kwanza kutotii.

Google Play itawaarifu wasanidi programu kuhusu sasisho lolote. Unaweza kuangalia Sera yetu ya Data ya Mtumiaji na makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili uhakikishe kuwa unafahamu mwongozo uliosasishwa hivi karibuni.

Ninawezaje kubainisha mkusanyiko wa data ambayo inatumika kwa njia ya muda mfupi kupakia kurasa na huduma katika muda halisi kabla ya data hiyo kuingizwa kwenye seva zetu na kutumika kwa madhumuni mengine?

Ikiwa utumiaji huu ni wa muda mfupi, huna haja ya kuujumuisha kwenye majibu ya fomu yako. Hata hivyo, ni lazima ubainishe matumizi yoyote ya data ya mtumiaji zaidi ya uchakataji wa muda mfupi, ikijumuisha madhumuni yoyote ambayo unatumia data ya mtumiaji unayoweka. Tafadhali kagua ufafanuzi wa uchakataji wa muda mfupi kwenye sehemu ya Ukusanyaji wa data hapo juu.

Je, kuna tofauti gani kati ya orodha ya ruhusa na Sehemu ya Usalama wa Data ya programu?

Google hukusanya maelezo ya orodha ya ruhusa kulingana na ruhusa ya wakati wa kusakinisha ambayo programu inabainisha katika faili ya maelezo.

Sehemu ya Usalama wa Data hushiriki data ambayo programu hukusanya na kushiriki na washirika wengine.

Kumbukumbu ya mabadiliko

Unaweza kurejelea kifungu hiki ili uone historia ya mabadiliko ya makala haya, ili uendelee kufuatilia mabadiliko katika kipindi fulani. Tutaongeza tarehe hapa wakati wowote tunapofanya mabadiliko makubwa kwenye makala haya baadaye.

Tarehe 5 Desemba, 2023 Tarehe 31 Machi 2023

Tumesasisha sehemu ya Ni wasanidi gani wa programu wanahitaji kujaza Fomu ya usalama wa data kwenye Dashibodi ya Google Play? ili kutoa maelezo yaliyosasishwa kuhusu masharti ya Sehemu ya Usalama wa Data na majaribio ya ndani. Tumeondoa pia kifungu kinachohusiana na hili kwenye mabadiliko tuliyofanya tarehe 24 Agosti 2022, kwa kuwa maelezo hayo hayatumiki tena na hatungependa kuwakanganya wasanidi programu wanaotafuta maelezo kuhusu tatizo hili.

Tumebadilisha makala kote ili kuondoa marejeleo ya tarehe mahususi; marejeleo haya awali yalijumuishwa (na kusasishwa mara kwa mara) kabla ya, wakati wa na baada ya uzinduzi wa Sehemu ya Usalama wa Data katika Dashibodi ya Google Play ili kuwasaidia wasanidi programu waelewe masharti yaliyokuwepo kila wakati mahususi. Kwa kuwa Sehemu ya Usalama wa Data inapatikana kwenye Google Play sasa, tumeondoa kumbukumbu halisi na marejeleo kwenye tarehe mahususi.

Tumeongeza maelezo ya ziada kwenye aina ya data "Mitagusano ya programu" (sasa hali hii inajumuisha "picha za skrini zilizopigwa").

Tarehe 24 Agosti, 2022

Tumesasisha sehemu ya Ni wasanidi gani wa programu wanapaswa kujaza Fomu ya usalama wa data katika Dashibodi ya Google Play? ili kuonyesha kwamba, kuanzia tarehe 24 Octoba, 2022, vikundi vinavyotumika kwenye toleo la jaribio la ndani havitajumuishwa katika sehemu ya usalama wa data. Hutakiwi kujaza fomu ya taarifa kwa programu zinazotumika kwenye kikundi hiki pekee.

Tarehe 20 Julai, 2022

Tulisasisha taarifa za Maelezo ya ratiba kwenye sehemu ya "Kutayarisha maelezo yako" ili kufafanua kuwa masasisho na mawasilisho mapya ya programu yasiyotii masharti yatapokea onyo kuwa yatakataliwa katika Dashibodi ya Google Play ikiwa kuna hitilafu ambazo hazijatatuliwa kwenye fomu. Pia, tulisasisha sehemu hii na maelezo ya kitakachofanyika baada ya kipindi hiki cha onyo kuisha tarehe 22 Agosti, 2022.

Katika sehemu ya Maelezo ambayo wasanidi programu wanatakiwa kufumbua katika Fomu ya usalama wa data, tulifanya mabadiliko yafuatayo kwenye sehemu ndogo ya Ukaguzi huru wa usalama (sasa yanapatikana kwa programu zote):

  • Tulibadilisha jina kutoka "Ukaguzi huru wa usalama (toleo la beta litapatikana kuanzia mwezi Machi 2022, na upatikanaji wa jumla unakuja hivi karibuni) " hadi "Ukaguzi huru wa usalama (sasa inapatikana kwa wasanidi programu wote)," kwa kuwa kipengele hiki sasa kinapatikana kwa programu zote.
  • Tulisasisha sehemu ndogo ili kujumuisha maelezo ya wasanidi programu ambao wanapendelea kushiriki kwenye ukaguzi huru wa usalama.

Tulifanya mabadiliko yafuatayo katika sehemu ya Maswali yanayoulizwa sana:

  • Tulisasisha jibu la swali, "Je, ninahitaji kuweka mbinu ya kufuta data? Je, ni sharti utaratibu uwe wa data yoyote na data yote ya mtumiaji?"
  • Moja kwa moja chini ya swali hili, tuliongeza pia maswali matatu na majibu mapya yanayotoa maelezo ya kina kuhusu taratibu za kufuta data na Fomu ya usalama wa data.
  • Tuliongeza swali moja jipya kuhusu tofauti kati ya orodha ya ruhusa na Sehemu ya usalama wa data ya programu. Tuliondoa swali kuhusu programu zinazolenga matoleo ya zamani ya Android.
28 Juni, 2022

Katika sehemu ya Muhtasari, tuliongeza sentensi kuwahimiza wasanidi programu kuangalia Faharasa ya SDK ya Google Play ili kuona iwapo mtoa huduma wao ametoa kiungo cha mwongozo. Unaweza kusoma makala ya Kituo cha Usaidizi ya Fanya uamuzi sahihi ukitumia Faharasa ya SDK ya Google Play ili upate maelezo zaidi.

Katika sehemu ya Kutayarisha maelezo mapya, tuliongeza pendekezo ili kutazama video ya Mwongozo wa Fomu ya usalama wa data ya PolicyBytes ya Google Play, ambayo inakuongoza kupitia nyenzo na hatua zote zinazohitajika ili ujaze Fomu ya usalama wa data.

Tarehe 26 Aprili, 2022

Katika sehemu ya Muhtasari, tuliongeza sentensi kuwahimiza baadhi ya wasanidi programu kurejelea maelezo ya usalama wa data yaliyochapishwa na mtoa huduma wa SDK ili kupata taarifa kama vile, Firebase na AdMob.

Tulisasisha taarifa za Maelezo ya ratiba kwenye sehemu ya "Kutayarisha maelezo yako" kwa kutumia marejeleo ya ujumbe watakaouona watumiaji kwenye Google Play katika ingizo la Julai 2022 (awali, ilisomeka "Hakuna data inayopatikana," ambayo imesasishwa kuwa "Hakuna maelezo yanayopatikana")

Katika sehemu ya Maswali Yanayoulizwa Sana, tulifanya mabadiliko yafuatayo:

  • Tuliongeza maswali na majibu mapya kuhusu huduma za mfumo.
  • Tuliongeza maswali na majibu mapya kuhusu chaguo za utatuzi endapo hutaona masasisho mapya ya Usalama wa Data kwenye Google Play.
  • Tulisasisha majibu yaliyopo kulingana na muda unaotumika kwa masasisho ya Usalama wa Data kuonekana kwenye Google Play na kwenye usimamizi wa akaunti.
Tarehe 8 Aprili, 2022

Mnamo tarehe 8 Aprili, 2022, tulisahihisha jina la aina ya data "Picha na video" (ambapo awali liliorodheshwa kama "Picha au video").

Tarehe 24 Februari, 2022

Mnamo tarehe 24 Februari, 2022, tulifanya mabadiliko kadhaa kwenye makala haya, ambayo yamebainishwa hapa chini.

Mabadiliko ya maelezo ya ratiba

Tulisasisha taarifa za Maelezo ya ratiba kwenye kifungu cha "Kutayarisha maelezo yako" kama ifuatavyo:

  • Awali, tulisema kwamba kuanzia Februari 2022, sehemu ya Usalama wa data itapatikana kwenye Google Play kwa watumiaji wote. Tarehe hii imesasishwa kuwa mwishoni mwa mwezi Aprili, 2022.
  • Awali, tulisema kwamba kuanzia Aprili 2022, masasisho na programu mpya zinazotumwa zitakataliwa katika Dashibodi ya Google Play ikiwa kuna hitilafu ambazo hazijatatuliwa kwenye fomu. Tarehe hii imesasishwa kuwa tarehe 20 Julai, 2022.
  • Hapo awali, tulisema kwamba kuanzia Aprili 2022, programu ambazo hazitii masharti zinaweza kuathiriwa na hatua za ziada za utekelezaji katika siku zijazo. Tarehe hii imesasishwa kuwa baada ya tarehe 20 Julai, 2022.

Tulisasisha marejeleo mengine ya tarehe kwenye makala ili yalingane na tarehe zilizorekebishwa hapo juu.

Ufafanuzi kuhusu maelezo ambayo wasanidi programu wanatakiwa kufumbua katika aina za data

Katika sehemu ya "Maelezo ambayo wasanidi programu wanatakiwa kufumbua katika Fomu ya usalama wa data", tulifanya mabadiliko yafuatayo kwenye sehemu ndogo ya "Maelezo ambayo wasanidi programu wanatakiwa kufumbua katika aina za data":

Aina za data na madhumuni ya masasisho

Tulifanya mabadiliko madogo ya mfumo wa majina kwenye aina zetu za data:

  • "Vitambulishi binafsi" vya aina ya data vilibadilishwa jina kuwa "Vitambulisho vya Mtumiaji."
  • Aina ya data ya "kadi ya mikopo, kadi ya malipo au nambari ya akaunti ya benki" ilibadilishwa jina kuwa "Maelezo ya malipo ya mtumiaji."
  • Aina ya data ya "Maelezo ya mikopo" ilibadilishwa jina kuwa "Alama ya kuweza kulipa mikopo."
  • Tuliongeza mfano wa mshahara au madeni ya mtumiaji kwenye aina ya data ya "maelezo mengine ya kifedha".
  • Aina ya data ya "Maelezo ya afya" ilibaki kuwa "Maelezo ya afya."
  • Aina ya data ya "Maelezo ya siha" ilibaki kuwa "Maelezo ya siha."
  • Aina ya data ya "Ujumbe wa SMS au MMS" ilibadilishwa jina kuwa "SMS au MMS."
  • Aina ya data ya "Mara ambazo ukurasa ulitazamwa na kuguswa katika programu" ilibadilishwa jina kuwa "Matumizi ya programu," na maelezo yake yalisasishwa.
  • Maelezo ya aina ya data ya "Maudhui mengineyo yaliyozalishwa na watumiaji" na "vitendo vinginevyo" yalisasishwa.
  • Aina ya data ya "taarifa binafsi nyinginezo" ilibadilishwa jina kuwa "Maelezo mengineyo."
  • Kipengele cha "Kifaa au vitambulishi vinginevyo" kilibadilishwa jina kuwa "Kifaa au Vitambulisho vinginevyo."

Tulitoa ufafanuzi kwenye madhumuni ya data zetu:

  • Mfano wa “Mawasiliano ya msanidi programu” ulisasishwa.
  • Mfano wa "Utangazaji au uuzaji" ulisasishwa.
  • Mfano wa "Usimamizi wa akaunti" ulisasishwa.

Mabadiliko mengine

Kwenye kifungu cha Muhtasari, tuliongeza picha za ziada ili kuonyesha kile ambacho watumiaji wataona kama programu yako haitashiriki data yoyote ya mtumiaji.

Tuliongeza Maswali mapya Yanayoulizwa Sana yakijumuisha mada zinazohusiana na usimamizi wa akaunti, vitendo vilivyoanzishwa na mtumiaji, mifumo ya matumizi ya malipo na usimbaji fiche.

Tulisasisha ufafanuzi wa uchakataji wa muda mfupi kwenye sehemu ya Ukusanyaji wa data na tuliongeza maswali mapya yanayoulizwa sana kuhusu mada hii.

Tarehe 14 Desemba, 2021

Tarehe 14 Desemba 2021, tulisasisha aina ya data ambayo awali ilijulikana kama "Mwelekeo wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia."  Aina hii ya data sasa inajulikana kama "Mwelekeo wa kijinsia" na inarejelea mwelekeo wa kijinsia pekee.

Tulisasisha pia aina ya data inayojulikana kama "Taarifa zingine binafsi" ili kujumuisha utambulisho wa kijinsia kama mfano wa taarifa zingine binafsi.

Nyenzo zingine

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2421333677663978974
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false