Tumia ruhusa ya Ufikiaji wa faili zote (MANAGE_EXTERNAL_STORAGE)

Google Play hudhibiti matumizi ya ruhusa nyeti au zenye hatari kubwa, ikiwa ni pamoja na idhini maalum ya programu inayoitwa Ufikiaji wa faili zote. Hii inatumika tu kwa programu zinazolenga Android 11 (API ya kiwango cha 30) na zinazobainisha ruhusa ya MANAGE_EXTERNAL_STORAGE, ambayo imewekwa kwenye Android 11. Pia, sera hii haiathiri matumizi ya ruhusa ya READ_EXTERNAL_STORAGE

Iwapo programu yako haihitaji idhini ya kufikia ruhusa ya MANAGE_EXTERNAL_STORAGE, ni lazima uiondoe kwenye faili ya maelezo ya programu yako ili kukidhi masharti ya ukaguzi wa sera. Maelezo kuhusu utekelezaji mbadala unaotii sera yanaainishwa pia hapa chini.

Iwapo programu yako inatimiza masharti ya sera ya matumizi yanayokubalika au inaruhusiwa kutofuata kanuni, utatakiwa kubainisha hali hii na ruhusa nyingine zozote za hatari kubwa kwa kutumia Fomu ya Taarifa katika Dashibodi ya Google Play.

Programu ambazo hazitimizi masharti ya sera au hazijatuma Fomu ya Taarifa zinaweza kuondolewa kwenye Google Play.

Unapaswa kuomba ruhusa ya 'Ufikiaji wa faili zote' wakati gani?

Unapaswa tu kuomba ruhusa ya ufikiaji wa faili Zote wakati programu yako haiwezi kutumia vizuri mbinu bora zinazoheshimu faragha ya mtumiaji, kama vile kutumia Mfumo wa Kufikia Hifadhi au API ya MediaStore. Kumbuka kuwa programu yako haipaswi kutoa taarifa kuhusu ruhusa ambazo haihitaji au haitumii.

Utendakazi wa msingi

Mbali na hayo, ni lazima utumiaji wa ruhusa ya programu ukubaliwe, na ni lazima uhusishwe moja kwa moja na utendaji wa msingi wa programu. Utendaji wa msingi hufafanuliwa kuwa lengo kuu la programu. Bila utendaji huu, programu huchukuliwa kuwa "ina hitilafu" au isiyoweza kutumika. Ni lazima utendaji wa msingi, pamoja na vipengele vyovyote vya msingi ambavyo vinajumuisha utendaji huu, vitangazwe na kuonyeshwa kwa njia dhahiri kwenye maelezo ya programu. 

Wakati utendaji wa msingi wa programu unahitaji ruhusa ya kufikia Faili zote, ni sharti msanidi programu akamilishe Fomu ya Taarifa za Ruhusa na kupokea idhini kutoka Google Play.

Kunja Zote Panua Zote

Matumizi yanayokubaliwa ya ruhusa ya ufikiaji wa faili Zote

Kwa programu zinazoomba ruhusa ya ufikiaji wa faili Zote, matumizi yanayokubaliwa na yanayolengwa ni pamoja na vidhibiti vya faili, programu za kuhifadhi na kurejesha nakala, programu za kingavirusi na programu za kudhibiti hati.

Programu zinazopewa ruhusa hii hazipaswi kuendeleza matumizi yake kwa madhumuni yasiyo dhahiri au yasiyo sahihi.

Matumizi

Ruhusa inayotimiza masharti*

Udhibiti wa faili

Madhumuni ya msingi ya programu ni pamoja na ufikiaji, ubadilishaji na udhibiti (ikiwa ni pamoja na udumishaji) wa faili na folda nje ya nafasi ya kuhifadhi ya programu mahususi

MANAGE_EXTERNAL_STORAGE

 

Programu za kuhifadhi na kurejesha nakala

Ni lazima programu ziwe na hitaji la kufikia kiotomatiki saraka nyingi nje ya nafasi ya hifadhi ya programu mahususi kwa madhumuni ya kuhifadhi na kurejesha nakala

Programu za kingavirusi

Madhumuni ya msingi ya programu hii ni kukagua kifaa na kumpa mtumiaji wa kifaa vipengele vya usalama vya kingavirusi

Programu za kudhibiti hati

Programu ambazo ni sharti zibaini, kufikia na kubadilisha aina za faili zinazotumika nje ya hifadhi inayoshirikiwa au ya programu mahususi

Ni lazima programu ibainishe kwenye taarifa yake ya Dashibodi kwa nini suluhisho zinazopatikana kwenye hati ya Fikia faili za programu mahususi au Mfumo wa Kufikia Hifadhi (chaguo linaloheshimu faragha ya mtumiaji) hazitoshi kutekeleza madhumuni yake

Tafuta (Kwenye Kifaa)

Madhumuni ya msingi ya programu ni kutafuta kwenye faili na folda katika hifadhi ya nje ya kifaa

Kufunga na Kusimba Diski/Folda kwa Njia Fiche

Madhumuni ya msingi ya programu ni kusimba faili na folda kwa njia fiche

Uhamishiaji kwenye Kifaa au Simu

Madhumuni ya msingi ya programu ni kusaidia mtumiaji kuhamishia vipengele kwenye kifaa kipya


* Inategemea ukaguzi na idhini ya Google Play.

Hali zisizofuata kanuni

Huenda Google Play itaruhusu kwa muda programu ambazo hazitimizi masharti ya matumizi yanayokubalika kama ilivyobainishwa hapo juu, wakati:

  • Matumizi ya ruhusa huwezesha utendaji wa msingi wa programu.
  • Kwa sasa hakuna njia mbadala ya kutoa utendaji wa msingi, au matumizi ya njia mbadala za kudumisha faragha (kwa mfano, API ya Hifadhi ya Maudhui au Mfumo wa Kufikia Hifadhi) yana athari kubwa kwenye vipengele muhimu vya programu vinavyohusiana na utendaji wa msingi.
  • Athari kwenye faragha ya mtumiaji husuluhishwa na mbinu bora za faragha na usalama.

Ni lazima msanidi programu athibitishe kwenye maelezo yake katika Dashibodi kwa nini Mfumo wa Kufikia Hifadhi au API ya Hifadhi ya Maudhui haitoshi kutekeleza madhumuni ya programu.

Kumbuka: Huenda programu za mtoa huduma na za kampuni inayotengeneza vifaa (OEM) na programu za faragha zinazochapishwa chini ya mfumo wa usambazaji wa Google Play ya Kikazi zikaomba ruhusa za kufikia hali za utumiaji zilizotajwa hapo juu, ikiwa ni pamoja na huduma nyeti zinazoomba uwezo wa kuzifikia.
Matumizi ambayo si sahihi

Katika hali fulani, programu zinaweza kuomba kufikia data nyeti ya mtumiaji kwa madhumuni ambayo kuna njia mbadala iliyo salama zaidi au ambapo hatari za kufichua data ni kubwa kuliko faida ya kuruhusu ufikaji wa data. 

Ifuatayo ni orodha ya matukio ya matumizi ya kawaida ambayo hayaruhusiwi kuomba ruhusa ya MANAGE_EXTERNAL_STORAGE 

  • Ufikiaji wa Faili za Maudhui (angalia Mbinu Mbadala hapa chini)
  • Shughuli zozote za kuchagua Faili ambako mtumiaji anachagua faili mwenyewe (angalia Mbinu Mbadala hapa chini)

Kumbuka: Orodha hii haijagusia kila hali. Ili upate mwongozo wa kina, tafadhali rejelea hati ya Ufikiaji wa Faili Zote na mwongozo wa Mbinu bora za kugawa hifadhi kwa wasanidi programu.

Chaguo mbadala inazopendekezwa zinazoheshimu faragha ya mtumiaji

Matumizi

Mbinu Mbadala

Kufikia Faili za Maudhui

Ukiwa na API ya Hifadhi ya Maudhui, programu zinaweza kuchangia na kufikia maudhui ambayo yanapatikana kwenye hifadhi ya nje bila kuhitaji ruhusa ya ufikiaji wa faili Zote. Kwa kutumia API ya MediaStore, watumiaji wanaweza kurejesha na kusasisha kwa urahisi faili za maudhui. Faili hizi husalia katika hifadhi ya nje kwenye kifaa cha mtumiaji — hata baada ya programu kuondolewa.

Mtumiaji huchagua faili za kutuma/kuhamisha/kuchakata

Wasanidi programu wanapaswa kuzingatia kutumia Mfumo wa Kufikia Hifadhi kama chaguo linaloheshimu faragha ya mtumiaji ili kufikia faili katika hifadhi inayoshirikiwa. Mfumo huu unatumia aina nyingi ya matumizi ya programu ili kutekeleza utendaji kamili.

Muhimu: Ukibadilisha jinsi programu yako hutumia ruhusa hizi zinazodhibitiwa, ni lazima utume fomu tena ikiwa na maelezo sahihi na yaliyosasishwa. Matumizi ya udanganyifu na yasiyotangazwa yanaweza kusababisha kusimamishwa kwa programu yako na/au kufutwa kwa akaunti yako ya msanidi programu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10622770578150419871
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false