Kutumia SDK za wengine katika programu yako

Pindi SDK za wengine zinapojumuishwa kwenye programu yako, zinaweza kuwa na athari kubwa katika uoanifu, utendaji, usalama na ubora wake.

Mabadiliko kuhusu SDK za wengine

Ili kusaidia kuhakikisha kuwa programu yoyote ya wengine inayotumiwa na programu yako inatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu za Google Play na inachangia kwa njia bora katika hali yako ya utumiaji, Google Play itaanza kuripoti matatizo yanayojulikana kwenye SDK maarufu katika Dashibodi ya Google Play.

Ili kufahamu SDK inayotumiwa na programu yako, sisi hutumia faili ya vitegemezi iliyo kwenye programu yako. Faili ya vitegemezi huorodhesha matoleo yote kwenye maktaba ambayo programu hutegemea. Programu zinazotumia Android App Bundle hutoa faili za vitegemezi kwa chaguomsingi. Programu zilizoundwa kabla ya Agosti 2021 kwa kutumia muundo wa uchapishaji wa APK hujumuisha faili za vitegemezi kuanzia Programu jalizi ya Android Gradle, toleo la 4.0.

Kufahamu matatizo kwenye SDK za wengine katika programu yako

Panapotumika, matatizo ya matoleo ya SDK zinazotumiwa na programu yako yamefafanuliwa kwenye Dashibodi ya Google Play katika sehemu ya juu ya ukurasa wa Toleo la umma, au kwenye ukurasa wa Muhtasari wa toleo.

Ikiwa programu yako inatumia toleo la SDK ambalo linaweza kusababisha isitii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu za Google Play, matoleo mapya ya programu yanayotumia toleo hilo la SDK yanaweza kukataliwa. Kulingana na aina ya ukiukaji, utaelekezwa kuhakikisha matumizi yako ya SDK yanatii sera zetu za Data ya Mtumiaji, badilisha utumie toleo tofauti ambalo linapendekezwa na mtoaji, au ondoa SDK.

Ikiwa programu yako inatumia toleo la SDK ambalo muda wake umeisha au lina matatizo makuu, utapokea onyo ambalo linaweza kuhitaji uchukue hatua zaidi. Kwa mfano, iwapo mtoa huduma za SDK ametufahamisha kuwa muda wa toleo la SDK unalotumia umeisha, bado unaweza kuchapisha programu yako. Hata hivyo, hutaweza kuchapisha toleo lingine la programu yako ukitumia toleo la SDK ambalo muda wake umeisha; utahitaji kutumia toleo jipya la SDK. Iwapo programu yako inatumia toleo la SDK ambalo mtoa huduma za SDK ameripoti kuwa lina matatizo makuu, utaona onyo linalofafanua aina ya tatizo, kama ilivyoelezwa na mtoa huduma za SDK.

Iwapo una maswali kuhusu toleo la SDK ambalo muda wake umeisha au lina matatizo makuu, tunakushauri uwasiliane na mtoa huduma za SDK.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9930433660797445129
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false