Unaweza kutumia zana ya uthibitishaji inayopatikana kwenye Programu ya Gemini kwa watumiaji walioingia katika akaunti, ili kusaidia kutambua picha, video na sauti zilizotayarishwa au kuhaririwa kwa mifumo ya AI.
Kuna teknolojia mbili zinazotumiwa kukagua ikiwa maudhui yametayarishwa kwa AI katika Programu za Gemini:
- SynthID: Hutumia alama maalum zisizoonekana ili kubaini iwapo picha, video na sauti zimetayarishwa au kuhaririwa mahususi na mifumo ya AI kutoka Google.
- Vitambulisho vya Maudhui: Teknolojia inayofanya kazi kama pasipoti dijitali kwa kurekodi chanzo na historia ya maudhui dijitali na inatumiwa kwenye maudhui yaliyotayarishwa na ambayo hayakutayarishwa kwa AI.
Unachohitaji
Ili utumie uthibitishaji wa AI, unahitaji:
- Akaunti binafsi au akaunti ya Workspace inayotimiza masharti
- Toleo jipya kabisa la Programu ya Gemini ikiwa unatumia programu kuthibitisha maudhui.
- Uwe umeingia katika Programu za Gemini. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuingia katika Programu za Gemini.
Kupakia maudhui yako ili yathibitishwe
Muhimu:
- Unaweza tu kuchagua picha, video au faili moja ya sauti ya kuthibitisha kwa wakati mmoja na inapaswa kuwa na ukubwa wa faili usiozidi MB 100.
- Kila video haipaswi kuzidi sekunde 90 na kila faili ya sauti haipaswi kuzidi saa 1
- Ikiwa unapiga picha ya skrini ya picha ili uthibitishe, hakikisha kuwa umepunguza picha hiyo kwa usahihi ili upate usahihi wa hali ya juu na usipakie kolagi ya picha nyingi tofauti.
- Kwenye kompyuta yako, nenda katika https://gemini.google.com.
- Bofya Weka faili
.
- Ili upakie faili inayotumika iliyo kwenye kifaa chako bofya Pakia Faili
.
- Ili upakie faili inayotumika kutoka kwenye Maktaba yako ya picha bofya Upakiaji Zaidi
Picha
.
- Ili uweke faili inayotumika iliyo kwenye Hifadhi yako ya Google bofya Hifadhi
.
Kidokezo: Ili uweke faili iliyo kwenye Hifadhi yako, unahitaji kuwasha mipangilio ya Kuhifadhi Shughuli na uunganishe Google Workspace na Programu za Gemini. Ikiwa haijaunganishwa, utapata chaguo la kuiunganisha. Pata maelezo kuhusu Programu za Gemini na data yako ya Google Workspace.
- Ili upakie faili inayotumika iliyo kwenye kifaa chako bofya Pakia Faili
- Uliza swali la uthibitishaji kama vile:
- "Je, picha au video au sauti hii ilitayarishwa au kuhaririwa kwa Google AI?"
- "Je, maudhui haya yametayarishwa kwa AI?"
- "Je, hii ni video halisi?"
Kuhusu matokeo ya uthibitishaji
Muhimu:
- Ingawa kampuni nyingine zimeanza kutumia alama maalum za SynthID, kwa sasa Gemini inaweza tu kutambua maudhui yaliyotayarishwa kwa kutumia zana za akiliunde kutoka Google.
- Vitambulisho vya Maudhui vinaweza kusaidia kutoa maelezo kuhusu chanzo na historia ya maudhui na iwapo zana za akiliunde zilitumiwa kuyatayarisha au kuyahariri.
Baada ya mchakato wa uthibitishaji kukamilika, Gemini itatoa jibu kulingana na matokeo ya uthibitishaji.
Kwa SynthID
- Ikiwa alama maalum ya SynthID itatambuliwa, inamaanisha kuwa picha au video nzima au sehemu yake ilibuniwa au kuhaririwa kwa mifumo ya AI kutoka Google.
- Ikiwa alama maalum ya SynthID haitatambuliwa, inamaanisha kuwa picha au video haikubuniwa au kuhaririwa kwa Google AI, lakini huenda ilibuniwa kwa mifumo mingine ya AI.
- Katika hali fulani, si dhahiri ikiwa picha au video ilitayarishwa au kuhaririwa kwa kutumia Google AI au la. Baadhi ya sababu za kawaida zinazosababisha hali hii ni:
- "Hakuna maelezo ya kutosha ya kuweka alama maalum" (k.m., maudhui rahisi sana au dhahania).
- "Huenda mabadiliko ni madogo mno" (huenda mabadiliko madogo yasiwe na alama maalum inayotambulika).
Kwa faili za video, Gemini itabainisha sehemu za video ambazo alama maalum ya SynthID ilitambuliwa. Hii haimaanishi kuwa ilitambuliwa katika sehemu zote za sehemu hiyo ya video.
Kwa Vitambulisho vya Maudhui
Ikiwa maudhui yana Vitambulisho vya Maudhui, unaweza kuangalia muhtasari wa:
- Muundo wa maudhui.
- Historia ya mabadiliko.
- Iwapo AI ilitumika au la.
Njia nyingine za kutambua maudhui yaliyotayarishwa kwa AI
Ingawa uthibitishaji wa maudhui kwenye programu ya Gemini unaweza kuwa zana muhimu, unaweza pia kutumia mbinu nyingine kutambua maudhui ambayo huenda yamebuniwa kwa AI:
- Kutafuta vizalia vya picha: Kagua picha na video ili ubaini hitilafu au makosa ambayo ni ya kawaida katika maudhui yaliyotayarishwa kwa AI. Hii inaweza kujumuisha:
- Maandishi yasiyolingana au yaliyoharibika kwenye picha au video.
- Makosa katika vipengee fulani, kama vile mikono, meno au vipengele vya mandharinyuma.
- Vivuli na mwangaza usio sawa.
- Miundo inayojirudia ambayo inaonekana kuwa si ya kawaida.
- Utafutaji kupitia picha: Tumia zana za utafutaji kupitia picha (k.m., Picha za Google) ili upate vyanzo halisi au picha zinazofanana. Kufanya hivyo kunaweza kukusaidia kubaini ikiwa maudhui yanatokana na chanzo kinachojulikana au ikiwa ni mapya na hayajabuniwa au kubadilishwa kwa AI.
- Uchanganuzi wa metadata: Ikiwa unaweza kufikia faili halisi (si picha ya skrini), unaweza kuangalia maelezo yaliyopachikwa. Kwa picha, hii inaweza kujumuisha data ya EXIF yenye miundo ya kamera, tarehe na mipangilio.
- Dalili za kutumiwa kwa programu ya kuhariri: Wakati mwingine metadata inaweza kuonyesha ikiwa programu ya kitaalamu ya kuhariri ilitumika.
Maswali yanayoulizwa sana kuhusu SynthID
Maswali yanayoulizwa sana kuhusu Vitambulisho vya Maudhui
Mambo ambayo Vitambulisho vya Maudhui hufanya
- Kutoa maelezo kuhusu asili na historia ya maudhui kupitia kiwango kinachotumika kwenye vifaa na programu mbalimbali kutoka kampuni tofauti.
- Kutoa maelezo kutoka kwa mtengenezaji wa programu au kifaa kuhusu zana za akiliunde au zisizo za akiliunde zilizotumiwa kutayarisha au kuhariri faili ya picha, video au sauti.
Mambo ambayo Vitambulisho vya Maudhui havifanyi
- Hukufahamisha iwapo faili ya picha, video au sauti imetayarishwa kwa AI, lakini unaweza kutumia maelezo ya chanzo na historia pamoja na maudhui yenyewe ili ufanye maamuzi sahihi.
- Vitaonyesha kampuni iliyotoa na kutia sahihi maelezo kwa njia fiche. Kwa mfano, “Maelezo kutoka Google LLC” inaonyesha kuwa Google ilitoa maelezo hayo.
- Huenda matokeo yakaorodhesha zaidi ya kampuni moja.
- Vimehaririwa vibaya: Vitambulisho vya Maudhui vinategemea historia inayodumishwa na kuthibitishwa na kila mtu anayehariri faili. Hitilafu hutokea ikiwa historia ya maudhui imehaririwa au kuharibiwa bila kusasisha data ya C2PA ipasavyo.
- Havitumiki au havioani: Programu za Gemini zinatumia matoleo ya 2.2 na matoleo mapya zaidi ya Vitambulisho vya Maudhui, kutoka kwenye bidhaa katika Orodha ya Bidhaa Zinazotii C2PA. Huenda vitambulisho kutoka kwenye bidhaa zisizo kwenye orodha hiyo visizingatiwe kuwa sahihi au kuaminika. Pia, baadhi ya programu za wengine za Vitambulisho vya Maudhui huhifadhi metadata kwenye seva za mbali, tofauti na faili ya picha, video au sauti; Programu za Gemini hazitumii metadata ya mbali.
- Haijatambuliwa: Huenda faili ikawa na Vitambulisho vya Maudhui vilivyoharibika wakati programu iliyotayarisha faili ilipata hitilafu. Programu za Gemini zinaweza kubaini Vitambulisho, lakini haziwezi kuvitafsiri katika baadhi ya hali.