Mara ya mwisho kusasishwa: Tarehe 24 Machi, 2025
Yaliyomo
- Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini
- Data yako kwenye Programu za Gemini
- Ni data ipi inakusanywa na ainatumika vipi
- Jinsi wahakiki wanadamu wanavyoboresha Akiliunde ya Google
- Kuweka mipangilio yako
- Jinsi Shughuli kwenye Programu za Gemini hufanya kazi na huduma na mipangilio mingine
- Kuomba kuondolewa kwa maudhui na kuhamisha taarifa zako
- Kutumia Gemini kama kiratibu kwenye kifaa chako cha Android
- Mambo unayohitaji kujua
- Sheria na Masharti
- Maswali kuhusu faragha
- Jumla
- Programu za Gemini ni nini?
- Ninawezaje kupinga uchakataji wa data yangu au kuomba data isiyo sahihi kwenye majibu ya Programu za Gemini isahihishwe?
- Je, misingi ya kisheria ambayo Google hutumia kuchakata data ya Programu za Gemini chini ya sheria ya ulinzi wa data ya Umoja wa Ulaya (EU) au Uingereza (UK) ni ipi?
- Je, data gani hukusanywa? Inatumika kwa kusudi gani?
- Je, unatumia mazungumzo yangu ya Programu za Gemini kunionyesha matangazo?
- Ni nani aliye na idhini ya kufikia data ya mazungumzo yangu na Programu za Gemini?
- Je, ninaweza kufikia na kufuta data yangu kwenye Akaunti yangu ya Google?
- Ni kwa nini mazungumzo yangu kwenye Programu za Gemini, maoni na data inayohusiana yanahitaji kuhakikiwa na binadamu?
- Ni kwa nini Google huhifadhi mazungumzo yangu baada ya mimi kuzima Shughuli kwenye Programu za Gemini na Google hutumia data hii kufanya nini?
- Je, Google inatumiaje maoni yangu?
- Je, inamaanisha nini tunaposema kuwa Gemini ni teknolojia mpya na inayobadilika?
- Ni nini hutokea ninapoziomba Programu za Gemini zihifadhi taarifa?
- Maelezo kuhusu ruhusa ya mahali na ruhusa nyinginezo
- Faili zilizopakiwa
- Picha zilizozalishwa
- Programu zilizounganishwa katika Gemini
- Gemini Live
- Gem
- Jumla
Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini
Mara ya mwisho kusasishwa: Tarehe 6 Machi, 2025
Data yako kwenye Programu za Gemini
Ilani hii pamoja na Sera yetu ya Faragha inaelezea jinsi Google inavyoshughulikia data yako wakati unatumia Gemini, kiratibu chako cha binafsi kinachotumia AI kutoka Google, kupitia programu na huduma zilizoorodheshwa hapa (“Programu za Gemini” au “Gemini” kwa ufupi).
Kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya na Uswisi, Programu za Gemini zinatolewa na Google Ireland Limited. Kwingineko, Programu za Gemini zinatolewa na Google LLC. Tunarejelea Google Ireland Limited na Google LLC hapa chini kama Google.
Ni data ipi inakusanywa na ainatumika vipi
Google hukusanya magumzo yako (ikiwa ni pamoja na rekodi za jinsi unavyotumia na Gemini Live), unachoruhusu Programu za Gemini zifikie (kama vile faili, picha na skrini), maelezo yanayohusiana ya matumizi ya bidhaa, maoni yako na maelezo kuhusu mahali ulipo. Maelezo kuhusu mahali ulipo yanajumuisha eneo kwa jumla lilivyo kwenye kifaa chako, anwani ya IP au anwani yako ya Nyumbani au ya Kazini iliyo katika Akaunti yako ya Google. Pata maelezo zaidi kuhusu data ya mahali katika g.co/privacypolicy/location.
Google hutumia data hii, kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha, ili kutoa, kuboresha na kubuni bidhaa, huduma pamoja na teknolojia za mashine kujifunza za Google, ikijumuisha bidhaa za Google za biashara kama vile Wingu la Google.
Kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini huwa kimewashwa kwa chaguomsingi ikiwa una umri wa miaka 18 au zaidi. Watumiaji walio na umri wa chini ya miaka 18 wanaweza kukiwasha. Iwapo umewasha mipangilio ya Shughuli kwenye Programu za Gemini, Google huhifadhi shughuli yako ya Programu za Gemini katika Akaunti yako ya Google kwa hadi miezi 18. Unaweza kubadilisha muda huu uwe miezi 3 au 36 katika mipangilio yako ya Shughuli kwenye Programu za Gemini.
Jinsi wahakiki wanadamu wanavyoboresha Akiliunde ya Google
Ili kusaidia kuboresha na kuimarisha bidhaa zetu (kama vile mifumo zalishi ya mashine kujifunza inayoendesha Programu za Gemini), wahakiki wanadamu (ikiwa ni pamoja na washirika wengine) husoma, hufafanua na kuchakata mazungumzo yako kwenye Programu za Gemini. Tunachukua hatua ili kulinda faragha yako kama sehemu ya mchakato huu. Hatua hizi ni pamoja na kutenganisha mazungumzo yako kwenye Programu za Gemini na Akaunti yako ya Google kabla ya wahakiki kuyaona au kuyafafanua. Tafadhali usiweke taarifa za siri katika mazungumzo yako au data yoyote ambayo hungependa mhakiki aone au Google itumie ili kuboresha bidhaa, huduma na teknolojia zetu za mashine kujifunza.
Kuweka mipangilio yako
Nenda kwenye Akaunti yako ya Google ili ufikie mipangilio na zana zinazokuwezesha kulinda data na faragha yako.
Ili uzuie mazungumzo ya siku zijazo yasihakikiwe wala kutumiwa kuboresha teknolojia za Google za mashine kujifunza, zima kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini. Unaweza pia kukagua na kufuta mazungumzo ya awali katika Shughuli kwenye Programu za Gemini.
Mazungumzo ambayo yamehakikiwa au kufafanuliwa na wahakiki wanadamu (pamoja na data inayohusiana kama vile lugha, aina ya kifaa, maelezo ya mahali au maoni) hayafutwi unapofuta data ya shughuli zako kwenye Programu za Gemini kwa sababu huwa yamehifadhiwa kando na hayahusishwi na Akaunti yako ya Google. Badala yake, huhifadhiwa kwa hadi miaka mitatu.
Hata wakati umezima kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini, mazungumzo yako yatahifadhiwa katika akaunti yako kwa hadi saa 72. Hali hii huiruhusu Google kukupatia huduma na kuchakata maoni yoyote. Shughuli hii haitaonekana katika Shughuli zako kwenye Programu za Gemini. Pata maelezo zaidi.
Jinsi Shughuli kwenye Programu za Gemini hufanya kazi na huduma na mipangilio mingine
Ukizima mipangilio hii au kufuta shughuli zako kwenye Programu za Gemini, mipangilio mingine ya Google haitabadilika. Mipangilio hiyo, kama vile Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu au Kumbukumbu ya Maeneo Yangu inaweza kuendelea kuhifadhi data ya mahali na data nyingine wakati unatumia huduma nyingine za Google. Pia unaweza kuunganisha na kutumia Programu za Gemini pamoja na huduma nyingine za Google. Ukifanya hivyo, huduma hizo huhifadhi na kutumia data yako ili kukuhudumia na pia kuboresha huduma zinazotoa, kwa mujibu wa sera husika pamoja na Sera ya Faragha ya Google. Ukitumia Programu za Gemini kutangamana na huduma za wengine, huduma hizo zitachakata data yako kwa mujibu wa sera yazo zenyewe za faragha.
Kuomba kuondolewa kwa maudhui na kuhamisha taarifa zako
Unaweza kuomba maudhui yaondolewe kwa kuzingatia sera zetu au sheria zinazotumika. Pia unaweza kuhamisha taarifa zako.
Kutumia Gemini kama kiratibu kwenye kifaa chako cha Android
- Ushughulikiaji wa data wa ziada. Ikiwa kiratibu kwenye kifaa chako, Gemini pia huchakata, kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha, taarifa kutoka kwenye vifaa na huduma zako ili kukuelewa, kukujibu na kukusaidia kutekeleza mambo. Kwa mfano, Gemini hufikia data na ruhusa fulani za mfumo (ikiwa ni pamoja na kupitia Kiratibu cha Google), kama vile kipiga simu, kumbukumbu za simu na ujumbe pamoja na anwani (ili kukusaidia uendelee kuwasiliana), programu zilizowekwa kwenye kifaa kama vile Saa, mapendeleo ya lugha (ili kukusaidia uzungumze na Gemini) na maudhui yaliyo kwenye skrini (ili kukusaidia uyashughulikie). Pia inafikia maelezo ya muktadha kutoka kwenye vifaa na huduma unazotumia katika Gemini na Kiratibu cha Google (kama vile orodha na majina ya vifaa mahiri vya nyumbani). Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti ruhusa zako za programu (kama vile maelezo ya mahali kifaa kilipo, maikrofoni na kamera) kwa matumizi ya Gemini.
- Usaidizi wa Kiratibu cha Google. Wakati Gemini inapata usaidizi wa Kiratibu cha Google kwa vitendo fulani, mipangilio inayofaa ya Kiratibu cha Google kama vile Matokeo Binafsi hutumika. Wakati Gemini inashughulikia vitendo kupitia programu zilizounganishwa, mipangilio hiyo ya Kiratibu cha Google haitumiki. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Gemini na Kiratibu cha Google hufanya kazi pamoja. Ili kusaidia kuboresha mawasiliano unapohamia Gemini kutoka kwenye Kiratibu cha Google, historia ya maombi yako ya hivi majuzi ya mawasiliano kwenye Kiratibu cha Google (kwa mfano, “Mtumie Sakina ujumbe”) inaweza kuhamishiwa katika Shughuli kwenye Programu za Gemini katika baadhi ya maeneo. Pata maelezo zaidi.
- Kuzungumza na Gemini. Iwapo huduma za “Ok Google” na Voice Match (zinazoendeshwa na Kiratibu cha Google) zimewashwa katika mipangilio yako, unaweza kuzungumza na Gemini au Kiratibu cha Google (yoyote inayofanya kazi) bila kugusa kifaa. Huenda Gemini ikawaka bila wewe kukusudia. Hali hii inaweza kutokea, kwa mfano, iwapo kuna kelele inayofanana na “Ok Google” au ukiiwasha kwa kuigusa bila kukusudia. Gemini ikijibu, itachukulia kitendo chako kama kidokezo cha kawaida. Iwapo umewasha mipangilio ya Shughuli kwenye Programu za Gemini, data hii hutumiwa kwa mujibu wa ilani hii pamoja na Sera ya Faragha ya Google, kwa madhumuni mbalimbali yakiwemo kuboresha Akiliunde ya Google kwa usaidizi wa wahakiki wanadamu.
Vipengele vya Ziada
Unaweza kutumia vipengele kadhaa vya ziada (kama vile Gem) katika Programu za Gemini. Wakati unatumia vipengele hivi vya ziada, data ya ziada unayotoa (kama vile majina ya Gem na maagizo maalum) hukusanywa na kutumiwa kwa mujibu wa ilani hii pamoja na Sera yetu ya Faragha, kwa madhumuni mbalimbali yakiwemo kuboresha Akiliunde ya Google kwa usaidizi wa wahakiki wanadamu.
Mambo unayohitaji kujua
- Programu za Gemini zinaendelea kubadilika mara kwa mara na wakati mwingine zinaweza kutoa maelezo yasiyo sahihi, yanayokera au yasiyofaa, ambayo hayawakilishi maoni ya Google.
- Usitegemee majibu ya Gemini kama ushauri wa kimatibabu, kisheria, kifedha au ushauri mwingine wa kitaalamu.
- Maoni yako yatasaidia kuboresha Gemini.
Angalia Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Programu za Gemini na Kituo cha Usaidizi wa Faragha kwenye Programu za Gemini ili upate maelezo zaidi.
Sheria na Masharti
Kumbuka: Masharti ya Google pamoja na Sera dhidi ya Matumizi Yasiyokubalika ya AI Zalishi vinatumika kwenye Programu za Gemini.
Ikiwa wewe ni mtumiaji uliye nchini Korea, pia unakubali kuwa utumiaji wako wa Programu za Gemini unasimamiwa na Sheria na Masharti ya Matumizi ya Data ya Mahali ya Korea.
Maswali kuhusu faragha
Mara ya mwisho kusasishwa: Tarehe 24 Machi, 2025
Jumla
Programu za Gemini ni nini?Programu za Gemini zinazorejelewa katika Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini na Kituo cha Faragha cha Programu za Gemini ni pamoja na:
- Programu ya Gemini ya wavuti kwenye gemini.google.com
- Programu za Gemini za vifaa vya mkononi, ambazo zinajumuisha:
- Programu ya Gemini, ikiweza pia kuwa kiratibu chako kwenye kifaa cha mkononi, katika Android
- Programu ya Gemini kwenye iOS
- Gemini kwenye programu ya Google Messages katika maeneo mahususi
“Programu za Gemini” pia wakati mwingine hujulikana kama “programu ya Gemini” au “Gemini.” Iwapo una Akaunti ya Google ya kazini au ya shuleni, huenda matumizi yako ya Programu za Gemini yakasimamiwa na masharti tofauti ya kushughulikia data. Pata maelezo zaidi kuhusu AI Zalishi katika Kituo cha Faragha cha Google Workspace.
Algoriti za LLM (Ikiwa ni pamoja na Programu za Gemini) zinaweza kuota na kuwasilisha taarifa zisizo sahihi kana kwamba ni ukweli.
Chini ya sheria fulani za faragha, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data katika Umoja wa Ulaya (EU), unaweza kuwa na haki ya:
- Kupinga uchakataji wa data yako binafsi au
- Kuomba data binafsi isiyo sahihi kwenye majibu ya Programu za Gemini isahihishwe.
Ili utumie haki hizi, unaweza kuanzisha ombi kwenye Kituo chetu cha Usaidizi.
Unaweza pia kuanzisha ombi moja kwa moja kwenye Programu za Gemini. Chini ya jibu la Programu za Gemini, chagua Zaidi
Ripoti tatizo la kisheria.
Nyenzo za ziada
Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia haki zako zinazohusiana na data tuliyokusanya, soma Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
Iwapo sheria ya ulinzi wa data ya Umoja wa Ulaya (EU) au Uingereza (UK) inatumika katika uchakataji wa taarifa zako, tafadhali soma maelezo yaliyo hapa chini kwa makini.
Unapotumia Programu za Gemini, Google huchakata taarifa zako kwa madhumuni na sababu za kisheria zilizoelezwa hapa chini.
Tunaporejelea “data yako ya Programu za Gemini” hapa chini, tunamaanisha yote yafuatayo: (i) mazungumzo yako kwenye Programu za Gemini (ikiwa ni pamoja na maagizo yoyote maalum uliyoweka), maelezo yanayohusiana ya matumizi ya bidhaa (ambayo ni pamoja na maelezo ya mahali ulipo) na maelezo yoyote ya ziada yanayochakatwa wakati Gemini ni kiratibu kwenye kifaa chako cha mkononi; na (ii) maoni yako.
Misingi ya kisheria ambayo Google hutumia ni:
- Utekelezaji wa mkataba. Tunachakata data yako ya Programu za Gemini na taarifa zako nyingine zozote unazozipatia ruhusa Programu za Gemini kuchakata unapounganisha Programu za Gemini na huduma nyingine ili tuweze kukupatia na kudumisha huduma ya Programu za Gemini uliyoomba kulingana na Sheria na Masharti ya Google. Kwa mfano, tunachakata taarifa zako kwenye Programu za Gemini ili kujibu hoja zako na kutoa utendaji na vipengele mbalimbali vya Programu za Gemini kama vile uzalishaji wa misimbo.
- Sababu halali za Google na washirika wengine zilizo na ulinzi stahiki kwa faragha yako.
- Tunachakata taarifa kutoka vyanzo vinavyoweza kufikiwa na umma na data yako ya Programu za Gemini ili tuweze kutoa, kudumisha, kuboresha na kuunda bidhaa na huduma za Google pamoja na teknolojia za mashine kujifunza.
- Uchakataji wa taarifa hizi kwa madhumuni haya ni muhimu kwa sababu halali za Google na kwa watumiaji wetu katika:
- Kutoa, kudumisha na kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wetu (kama vile kutumia mazungumzo kurekebisha mifumo na kuboresha majibu ya Programu za Gemini ili yawe salama na sahihi).
- Kubuni bidhaa na vipengele vipya vinavyowafaa watumiaji wetu (kama vile kujifunza jinsi ya kuelekeza maombi kwenye mifumo mipya mikubwa ya lugha ambayo ni bora katika kujibu swali fulani au kufunza mifumo mipya jinsi ya kushughulikia maombi hayo).
- Kuelewa jinsi watu wanavyotumia huduma zetu ili kuhakikisha na kuboresha utendaji wa huduma zetu (kama vile kuzalisha vipimo ili kuelewa jinsi watumiaji wanavyotumia Programu za Gemini ili kutoa hali ya kipekee ya utumiaji).
- Kuwekea huduma zetu mapendeleo ili kuwapatia watumiaji hali bora zaidi ya utumiaji (kama vile kutumia maelezo ya mahali ulipo na mazungumzo yako ya zamani ili Programu za Gemini zitoe majibu yanayokufaa zaidi).
- Uchakataji wa taarifa hizi kwa madhumuni haya ni muhimu kwa sababu halali za Google na kwa watumiaji wetu katika:
- Pia, tunachakata taarifa zako za Programu za Gemini ili tuweze kudumisha utendaji, usalama na hali ya kutegemewa kwa Programu za Gemini, ikiwa ni pamoja na kutambua, kuzuia na kushughulikia masuala ya ulaghai, matumizi mabaya, hatari kwa usalama na matatizo ya kiufundi yanayoweza kuathiri Google, watumiaji wetu au umma.
- Uchakataji wa taarifa hizi kwa madhumuni haya ni muhimu kwa sababu halali za Google, watumiaji wetu na umma katika:
- Kutambua, kuzuia au vinginevyo kukabiliana na ulaghai, matumizi mabaya, masuala ya usalama au matatizo ya kiufundi katika huduma zetu (kama vile kurekebisha hitilafu na kushindwa kutatua matatizo).
- Kulinda dhidi ya ukiukaji wa haki, madhara kwa mali au usalama wa Google, watumiaji wetu au umma jinsi inavyotakiwa au kuruhusiwa na sheria (kama vile kusasisha viainishi vya usalama na vichujio vya miundo).
- Kufanya utafiti unaoboresha huduma zetu kwa watumiaji wetu na kunufaisha umma.
- Kutekeleza madai ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuchunguza ukiukaji wa sheria na masharti yanayotumika unaoweza kutokea (kama vile kukagua shughuli na mitagusano ambayo imetiwa alama kuwa ina matatizo).
- Uchakataji wa taarifa hizi kwa madhumuni haya ni muhimu kwa sababu halali za Google na washirika wetu wa kibiashara katika kutekeleza wajibu kwa washirika wetu kama vile wasanidi programu na wamiliki wa haki (kama vile kutimiza maombi ya kuondoa maudhui kutoka kwa wenye haki za uvumbuzi).
- Uchakataji wa taarifa hizi kwa madhumuni haya ni muhimu kwa sababu halali za Google, watumiaji wetu na umma katika:
- Ili kujibu ombi lako, kwa mfano kufupisha barua pepe kutoka kwa mtu aliye na jina kwenye anwani zako, tunachakata data binafsi kuhusu anwani nyingine ulizozipatia Programu za Gemini (kama vile unapounganisha Programu za Gemini na huduma nyingine kama Google Workspace).
- Tunachakata taarifa kutoka vyanzo vinavyoweza kufikiwa na umma na data yako ya Programu za Gemini ili tuweze kutoa, kudumisha, kuboresha na kuunda bidhaa na huduma za Google pamoja na teknolojia za mashine kujifunza.
- Wajibu wa kisheria. Pia, tunachakata taarifa zako za Programu za Gemini ili tuweze kutii sheria, kanuni, mchakato wa kisheria au ombi lolote la serikali linaloweza kutekelezwa (kama vile tukipokea ombi la kisheria la kutaka taarifa kutoka kwenye chombo cha dola).
- Idhini yako. Tunategemea idhini yako unapotumia vipengele fulani kama vile Voice Match. Programu za Gemini zinavyoendelea kuimarika, huenda tukakuomba idhini ili kuchakata taarifa yako kwa madhumuni mahususi. Pale ambapo tunategemea idhini yako ili kuchakata taarifa, utakuwa na haki ya kuondoa idhini hiyo wakati wowote.
Aina ya data inayokusanywa
Soma Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini ili uelewe aina ya data inayokusanywa unapotumia Programu za Gemini. Mihtasari muhimu imeainishwa hapa chini.
Unapotumia Programu za Gemini, Google hukusanya:
- Data ya mazungumzo
- Data ya mahali
- Maoni
- Maelezo ya matumizi
Wakati Gemini ni kiratibu kwenye kifaa chako cha mkononi, Google huchakata maelezo ya ziada (kama vile maelezo kwenye vifaa na huduma, ruhusa, muktadha wa skrini, programu ulizoweka kwenye kifaa chako) ili ielewe kidokezo chako, ikujibu na ikupe usaidizi bila wewe kugusa kifaa.
Unapounganisha programu na Gemini, ufikiaji wa data yako huruhusiwa kati ya Gemini na programu na huduma nyingine, ili Gemini iweze kukujibu vizuri zaidi. Pata maelezo kuhusu data yako wakati programu nyingine zimeunganishwa na Gemini.
Ukitumia Programu za Gemini kufikia huduma za wengine, huduma hizo zitachakata data yako kwa mujibu wa sera husika za faragha.
Jinsi Google inavyotumia data hii
Data hii hutusaidia kutoa, kuboresha na kubuni bidhaa, huduma na teknolojia za mashine kujifunza za Google, kama zile zinazoziwezesha Programu za Gemini. Kwa maelezo zaidi, soma Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
Ifuatayo ni mifano michache:
- Programu za Gemini hutumia mazungumzo yako ya awali, data ya mahali ulipo na maelezo yanayohusiana ili kuzalisha jibu.
- Tunakagua maoni yako na kuyatumia kusaidia kuzifanya Programu za Gemini ziwe salama zaidi. Pia, tunayatumia kusaidia kupunguza matatizo ya kawaida ya mifumo mikubwa ya lugha.
Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi tunavyohifadhi data yako kwa faragha na usalama katika kanuni za faragha za Google.
Iwapo una Akaunti ya Google ya kazini au ya shuleni, huenda matumizi yako ya Programu za Gemini yakasimamiwa na masharti tofauti ya kushughulikia data. Pata maelezo zaidi kuhusu AI Zalishi katika Kituo cha Faragha cha Google Workspace.
Mazungumzo yako na Programu za Gemini hayatumiwi kukuonyesha matangazo. Ikiwa hali hii itabadilika, tutawasiliana nawe kwa uwazi.
Ili ufahamu kuhusu namna tunavyohifadhi data ya watumiaji wetu kwa njia salama na ya faragha, soma Kanuni zetu za Usalama na Faragha.
Tunazingatia faragha yako kwa umakini na hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. Ili kusaidia kuboresha huduma ya Gemini huku tukilinda faragha yako, huwa tunachagua vijisehemu vya mazungumzo na kutumia zana za kiotomatiki kusaidia kuondoa taarifa zinazomtambulisha mtumiaji (kama vile anwani za barua pepe na namba za simu). Sampuli hizi za mazungumzo zinahakikiwa na wahakiki waliohitimu (ambao wanajumuisha washirika wengine) na kuhifadhiwa kwa hadi miaka mitatu, kando na Akaunti yako ya Google. Soma Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini ili upate maelezo zaidi.
Jinsi unavyoweza kudhibiti kinachotumwa kwa wahakiki
Ukizima Shughuli kwenye Programu za Gemini, mazungumzo ya baadaye hayatatumwa kuhakikiwa na binadamu au kutumiwa kuboresha mifumo yetu zalishi ya mashine kujifunza.
Tafadhali usiweke taarifa za siri katika mazungumzo yako na Programu za Gemini au data yoyote ambayo hungependa mhakiki aone au Google itumie kuboresha bidhaa, huduma na teknolojia zetu za mashine kujifunza.
Ndiyo, unaweza kupata kiungo cha Shughuli Zako kwenye Programu za Gemini katika Programu za Gemini, ambapo unaweza kudhibiti na kufuta data yako.
Unaweza pia kufuta gumzo kwenye magumzo uliyobandika na ya hivi karibuni. Unapofanya hivi, hatua hii pia hufuta shughuli zinazohusiana katika kipengele cha Shughuli Zako kwenye Programu za Gemini. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti magumzo.
Kuhusu udhibiti wako wa Shughuli kwenye Programu za Gemini
Ukiwasha Shughuli kwenye Programu za Gemini , Google huhifadhi shughuli zako kwenye Programu za Gemini (kama vile vidokezo, majibu na maoni yako) katika Akaunti yako ya Google.
Hata wakati kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini kimezimwa, mazungumzo yako yatahifadhiwa kwenye akaunti yako kwa hadi saa 72 ili kuturuhusu kutoa huduma na kuchakata maoni yoyote.
Shughuli hii haitaonekana kwenye data ya Shughuli zako kwenye Programu za Gemini.
Jinsi ya kudhibiti shughuli zako kwenye Programu za Gemini
Katika kipengele cha Shughuli Zako kwenye Programu za Gemini, wakati wowote unaweza:
- Kuzima Shughuli kwenye Programu za Gemini
- Kukagua vidokezo vyako
- Kufuta Shughuli zako kwenye Programu za Gemini
- Kubadilisha mipangilio ya kipengele cha futa kiotomatiki
Pata maelezo zaidi kuhusu Shughuli kwenye Programu za Gemini.
Unaweza pia kuhamisha taarifa zako, kama ilivyoelezwa kwenye Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
Jinsi uhakiki unaofanywa na binadamu unavyosaidia kuboresha mifumo
Google hutumia mazungumzo (pamoja na maoni na data inayohusiana) kutoka kwa watumiaji wa Programu za Gemini kuboresha huduma za Google ili kuzifanya ziwe salama, zifae zaidi na zifanye kazi vizuri kwa watumiaji wote. Hii inajumuisha mifumo zalishi ya mashine kujifunza inayowezesha Programu za Gemini na teknolojia zinazosaidia kupunguza vitendo visivyokusudiwa vya kuwashwa kwa Programu za Gemini. Uhakiki unaofanywa na binadamu ni hatua muhimu katika mchakato wa kuboresha mfumo huu. Kupitia uhakiki, ukadiriaji na uhariri wanaofanya, wahakiki wanadamu (ambao wanajumuisha washirika wengine) husaidia kuboresha mifumo zalishi ya mashine kujifunza kama ile inayowezesha Programu za Gemini.
Jinsi tunavyolinda faragha yako katika mchakato huu
Tunachukua tahadhari kadhaa ili kulinda faragha yako wakati wa mchakato huu wa uhakiki unaofanywa na binadamu:
- Mazungumzo (pamoja na maoni na data inayohusiana kama vile lugha, aina ya kifaa chako au maelezo ya mahali ulipo) ambayo wahakiki huona na kufafanua hayahusishwi na akaunti zozote za watumiaji.
- Tunachagua sampuli bila utaratibu wowote ili ifanyiwe uhakiki huo unaofanywa na binadamu na ni sehemu tu ya mazungumzo yote na Programu za Gemini ambayo huhakikiwa.
Jinsi mchakato unavyofanya kazi
- Wahakiki wetu waliohitimu huangalia mazungumzo ili kutathmini ikiwa majibu ya Programu za Gemini ni ya ubora wa chini, si sahihi au ni hatari.
- Kisha, wahakiki waliohitimu hupendekeza majibu yenye ubora wa juu zaidi.
- Kisha majibu haya hutumiwa kuunda seti bora ya data ili mifumo zalishi ya mashine kujifunza ijifunze kutokana nayo ili mifumo yetu iweze kutoa majibu bora zaidi hapo baadaye.
Muda ambao data iliyohakikiwa huhifadhiwa
Mazungumzo yako na Programu za Gemini ambayo yamehakikiwa au kufafanuliwa na wahakiki wanadamu (pamoja na maoni na data inayohusiana kama vile lugha, aina ya kifaa chako au maelezo ya mahali ulipo) hayafutwi unapofuta shughuli zako kwenye Programu za Gemini kwa sababu yamehifadhiwa kando na hayahusishwi na Akaunti yako ya Google. Badala yake, yanahifadhiwa kwa hadi miaka 3.
Jinsi unavyoweza kudhibiti kinachotumwa kwa wahakiki
Ukizima Shughuli kwenye Programu za Gemini, mazungumzo ya baadaye hayatatumwa kuhakikiwa na binadamu au kutumiwa kuboresha mifumo yetu zalishi ya mashine kujifunza.
Usiweke chochote ambacho hungependa mhakiki mwanadamu aone au Google itumie. Kwa mfano, usiweke taarifa unazochukulia kuwa za siri au data ambayo hungependa itumiwe kuboresha bidhaa, huduma za Google na teknolojia za mashine kujifunza.
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuzima, kudhibiti na kufuta shughuli zako kwenye Programu za Gemini wakati wowote. Pia, unaweza kudhibiti uhifadhi wa Google wa shughuli kwenye Programu za Gemini katika sehemu ya Shughuli Zangu wakati wowote.
Google inahitaji mazungumzo haya ili kukujibu na iyatumie kama muktadha wa maoni unayochagua kutuma ili kusaidia kudumisha na kuboresha Programu za Gemini na kuwapa watumiaji wote hali salama na bora zaidi ya utumiaji.
Yafuatayo ni maelezo zaidi kuhusu mazungumzo yanayohifadhiwa kwenye akaunti yako hata ukishazima kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini:
Kabla ya kutoa maoni kwenye Programu za Gemini
- Ukizima kipengele cha Shughuli kwenye Programu za Gemini, Google huhifadhi mazungumzo yako kwenye akaunti yako kwa hadi saa 72. Shughuli hii haitaonekana katika Shughuli zako kwenye Programu za Gemini na hutumiwa ili:
- Kujibu mazungumzo yako kwa kuzingatia muktadha. Kwa madhumuni haya, Programu za Gemini hutumia data ya saa 24 pekee.
- Kudumisha ulinzi na usalama wa Programu za Gemini na kuboresha Programu za Gemini. Kwa madhumuni haya, Google huhitaji kipindi cha kuhifadhi cha saa 72 ili kusaidia kuhakikisha kwamba data kutoka kwenye michakato ya nyuma ya mifumo au programu inapatikana endapo kutakuwa na hali ya mifumo kushindwa kufanya kazi.
- Ukizima Shughuli kwenye Programu za Gemini, Google haitumii mazungumzo yako mapya yaliyohifadhiwa kwenye akaunti yako ili kuboresha teknolojia zake zalishi za mashine kujifunza, isipokuwa ukituma maoni kuhusu mazungumzo.
Baada ya kutoa maoni kwenye Programu za Gemini
Ukiamua kutuma maoni kwa Google, mifumo ya Google itakusanya maelezo yafuatayo:
- Maoni yako.
- Maudhui yoyote yaliyojumuishwa, kama vile faili na picha unazopakia, pamoja na maudhui yako binafsi ambayo Programu za Gemini hupata kutoka kwenye programu zilizounganishwa.
- Muktadha unaoweza kutusaidia kuelewa vyema maoni yako. Hii ni pamoja na saa 24 zilizopita za data ya mazungumzo inayopatikana, kama vile vidokezo vyako na majibu ya Programu za Gemini.
Maoni yako, maudhui yoyote yaliyojumuishwa (kama vile faili au maudhui yako binafsi kutoka kwenye programu zilizounganishwa), mazungumzo yanayohusishwa (kama vile vidokezo na majibu ya Programu za Gemini) pamoja na data inayohusiana:
- Huhakikiwa na timu maalum zilizohitimu. Uhakiki unaofanywa na binadamu ni muhimu ili kusaidia kutambua, kushughulikia na kuripoti matatizo yanayoweza kuwepo ambayo yametumwa kupitia maoni. Katika hali fulani, uhakiki huu unahitajika kisheria.
- Hutumiwa kulingana na Sera ya Faragha ya Google. Google hutumia data hii ili kutoa, kuboresha na kubuni bidhaa na huduma zake pamoja na teknolojia za mashine kujifunza. Hatua hii imeelezwa kwa kina katika Sera yetu ya Faragha.
- Kwa mfano, tunatumia data hii ili kusaidia kuzifanya Programu za Gemini ziwe salama zaidi. Hutusaidia kutambua na kuepuka maombi au majibu yasiyo salama katika siku zijazo.
- Huhifadhiwa kwa hadi miaka 3. Maoni yaliyohakikiwa, mazungumzo na data inayohusiana huhifadhiwa kwa hadi miaka 3, bila kuhusishwa na Akaunti yako ya Google.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutuma maoni au kuripoti tatizo kuhusu Programu za Gemini.
Programu za Gemini (hapo awali iliitwa Bard) huendeshwa na mifumo mikubwa ya lugha, kama ilivyofafanuliwa katika muhtasari huu wa Bard na James Manyika (Makamu Rais Mwandamizi wa Google, anayesimamia Teknolojia na Jamii). Kama ilivyo katika mifumo mingi mikubwa ya lugha (LLM), mifumo inayoendesha Programu za Gemini zilifunzwa mapema kwa kutumia aina mbalimbali za data kutoka vyanzo vinavyopatikana kwa umma.
Jinsi Mifumo Mikubwa ya Lugha (LLM) inavyofanya kazi
Kupitia mafunzo ya mapema, mifumo ya LLM hutafuta mitindo katika lugha na huitumia kutabiri neno au maneno yenye uwezekano wa kufuata katika mfuatano. Hata hivyo, ikiwa mfumo wa LLM utachagua neno moja tu lenye uwezekano zaidi wa kufuata, majibu yasingekuwa ya ubunifu zaidi. Ndio maana LLM huruhusiwa kuwa nyumbufu. Inaweza kuchagua kutoka kwenye chaguo kadhaa za maneno yenye uwezekano mdogo kiasi kufuata, ili kuzalisha majibu yanayovutia zaidi.
Kwa nini majibu si sahihi kila wakati
Wakati mwingine LLM hutekeleza vyema hoja za ukweli na huonekana kana kwamba inatafuta taarifa, lakini si hifadhidata za taarifa au mifumo ya upataji taarifa. Unapowasilisha hoja kwenye hifadhidata, unaweza kutarajia jibu lile lile kila wakati. Lakini, unapotoa kidokezo hicho hicho kwenye LLM, si lazima kwamba utapata jibu lile lile kila wakati au taarifa halisi ambazo zilitumiwa kufunza LLM. Hii ni kwa sababu Mifumo Mikubwa ya Lugha (LLM) imefunzwa kutabiri neno lenye uwezekano zaidi wa kufuata na si kupata taarifa.
Hiki pia ni kigezo muhimu kuhusu kwa nini LLM huweza kuzalisha majibu yanayoonekana kuwa mazuri lakini si sahihi kuhusu watu na mada nyingine. Hata hivyo, huenda hali hii isifae iwapo ukweli ndio kigezo kikuu, lakini inaweza kuwa muhimu katika kuzalisha majibu ya kibunifu au yasiyotarajiwa.
Kwa nini Programu za Gemini ni mpya na zinabadilika mara kwa mara
Programu za Gemini ni sehemu ya juhudi zetu za muda mrefu na zinazoendelea za kubuni LLM kwa kuwajibika. Katika kipindi kizima cha kazi hii, tumegundua na kujadili mipaka kadhaa inayohusishwa na LLM, ikijumuisha vipengee vitano tunavyoendelea kuvifanyia kazi:
- Usahihi: Majibu ya Programu za Gemini kuhusu watu au mada nyingine huenda yakawa si sahihi hasa zinapoulizwa masuala changamano au ya kweli.
- Upendeleo: Majibu ya Programu za Gemini yanaweza kuonyesha upendeleo au mitazamo kuhusu watu na mada nyingine ilivyo kwenye data iliyotumika kuzifunza.
- Hulka: Majibu ya Programu za Gemini yanaweza kuonyesha kuwa zina maoni au hisia za binafsi.
- Usahihi usio kweli na ukosefu usio kweli: Programu za Gemini huenda zisijibu hoja fulani zinazofaa na zikatoa majibu yasiyofaa kwa baadhi ya hoja.
- Kuwepo katika hatari ya kupatiwa udokezaji hasidi: watumiaji watatafuta njia za kuzifanyia Programu za Gemini jaribio la kutatiza zaidi. Kwa mfano, wanaweza kuziomba Programu za Gemini ziote na zitoe maelezo yasiyo sahihi kuhusu watu au mada nyingine.
Tumezingatia kushughulikia vipengee hivi kabla ya kuzindua Programu za Gemini. Kwa kushirikiana na tasnia pana, tunaendelea kuvitafutia suluhisho. Hapa Google, tumejitolea kufanya kazi ili kuwa bora kadiri muda unavyosonga. Pata maelezo zaidi.
Taarifa ulizoiomba Gemini ihifadhi (kwa mfano, “Kumbuka kuwa …”) hutumiwa kukupatia majibu maalum zaidi katika Programu za Gemini.
Taarifa huhifadhiwa hadi utakapozifuta na unaweza kuzima mipangilio hii wakati wowote. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta taarifa ulizohifadhi au kuzima mipangilio hii.
Maelezo kuhusu ruhusa ya mahali na ruhusa nyinginezo
Ni maelezo ipi ya mahali hukusanywa na Programu za Gemini, kwa nini na inatumiwa vipi?Data ya mahali hukusanywa ikiwa unatumia Programu za Gemini ili ziweze kukupatia majibu ambayo yanafaa hoja yako. Kwa mfano, ili kujibu hoja kama vile "Je, hali ya hewa ikoje?", Programu za Gemini zinahitaji kujua mahali ulipo.
Programu za Gemini zinapopata data ya mahali na jinsi inavyotumika
Chanzo cha data ya mahali ambayo Programu za Gemini hukusanya hutofautiana. Kwa chaguomsingi, Programu za Gemini hutumia maelezo ya eneo kwa jumla kutoka kwenye anwani yako ya IP au anwani yako ya Kazini au ya Nyumbani ilivyo kwenye Akaunti yako ya Google ili kutoa majibu yanayofaa kwa hoja kama vile “Je, hali ya hewa ikoje?”
Kwa ruhusa yako, Programu za Gemini pia huchakata data ya eneo mahususi ilivyo kwenye kifaa chako ili kutoa majibu yanayofaa zaidi. Kwa mfano, Programu za Gemini zinaweza kutumia data ya eneo mahususi uliko ili kujibu kwa usahihi zaidi vidokezo kama vile "je, mgahawa wa kahawa ulio karibu nami zaidi uko wapi?
Pia, Google hutumia data ya mahali ulipo, ikiwa ni pamoja na data ya eneo lako mahususi, kwa madhumuni na kulingana na sababu za kisheria iliyoelezewa kwenye Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini. Pata maelezo zaidi kuhusu data ya mahali katika g.co/privacypolicy/location.
Jinsi data ya eneo mahususi inavyotumwa
Ikiwa inapatikana, Programu za Gemini zinaweza kuruhusu data ya eneo mahususi uliko ifikiwe na huduma nyingine ya Google, kama vile Ramani za Google, ili kutekeleza ombi lako. Huduma ya Google inayokusanya data ya mahali ulipo inaitumia kulingana na Sera ya Faragha ya Google.
Jinsi data ya mahali inavyohifadhiwa
- Data ya eneo mahususi haihifadhiwi katika Shughuli zako kwenye Programu za Gemini.
- Data ya mahali inayochakatwa na Programu za Gemini hufanywa kuwa ya eneo kwa jumla kabla ya kuhifadhiwa pamoja na Shughuli zako kwenye Programu za Gemini. Eneo kwa jumla ni kubwa kuliko kilomita 3 za mraba na lina angalau watumiaji 1000 ili maelezo ya eneo kwa jumla ya hoja yako yasitumike kukutambua, hali inayosaidia kulinda faragha yako. Hii inamaanisha kuwa eneo kwa jumla kwa kawaida huwa kubwa kuliko kilomita 3 mraba nje ya miji mikuu.
Jinsi ya kudhibiti data yako
Wakati wowote, unaweza:
- Kubadilisha mipangilio yako ya mahali. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti data ya mahali ulipo.
- Kudhibiti ruhusa za mahali za programu yako ya vifaa vya mkononi ya Gemini kwa kubadilisha mipangilio ya mahali ya kifaa ya programu ya Google (Gemini inapatikana kwenye programu hiyo). Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti mipangilio ya mahali kwenye kifaa na udhibiti ruhusa za kifaa cha mkononi wakati Gemini ni kiratibu kwenye kifaa chako.
- Kukagua na kufuta Shughuli zako kwenye Programu za Gemini. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti Shughuli zako kwenye Programu za Gemini.
Programu ya wavuti ya Gemini
Programu ya wavuti ya Gemini huonyesha vipengee vya kiolesura katika sehemu ya chini ya Menyu vinavyotoa uwazi unaoendelea kuhusu data ya mahali inayochakatwa na programu.
Ili uangalie ikiwa gemini.google.com inafikia na inatumia data ya eneo lako mahususi:
- Nenda kwenye gemini.google.com.
- Katika sehemu ya juu kulia, gusa Menyu
.
- Katika sehemu ya chini ya menyu, kagua nukta karibu na maelezo ya mahali.
- Ikiwa nukta ni ya rangi ya bluu, gemini.google.com inaweza kufikia na inatumia data ya eneo lako mahususi.
- Ikiwa nukta ni ya rangi ya kijivu, gemini.google.com haitumii data ya eneo lako mahususi.
Programu ya vifaa vya mkononi ya Gemini (kwenye Android)
Gemini inapangishwa na programu ya Google, hata kama unapakua Programu ya Gemini . Ili uangalie ikiwa Gemini inafikia na inatumia data ya eneo lako mahususi:
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua programu ya Mipangilio.
- Gusa Mahali
ruhusa ya mahali katika Programu.
- Gusa Google
.
- Angalia ikiwa "Tumia data ya eneo mahususi" imewashwa
.
- Ikiwa imewashwa
, Gemini na huduma zingine katika programu ya Google (kama vile Tafuta) zinaweza kufikia na kutumia data ya eneo lako mahususi.
- Ikiwa imezimwa
, Gemini na huduma zingine katika programu ya Google (kama vile Tafuta) haziwezi kufikia na kutumia data ya eneo lako mahususi.
- Ikiwa imewashwa
- Chagua ufikiaji wa eneo wa programu: Ruhusu kila wakati, Ruhusu programu inapotumika tu, Omba idhini yako kila wakati, au Usiruhusu.
Programu ya vifaa vya mkononi ya Gemini (kwenye iOS)
Ili kuangalia kama Gemini katika programu ya Google inafikia na kutumia data ya eneo lako mahususi:
- Kwenye iPhone yako, fungua programu ya Mipangilio.
- Gusa Usalama na Faragha
Huduma za Mahali.
- Gusa Google
.
- Angalia ikiwa "Tumia data ya eneo mahususi" imewashwa
.
- Ikiwa imewashwa
, Gemini na huduma zingine katika programu ya Google (kama vile Tafuta) zinaweza kufikia na kutumia data ya eneo lako mahususi.
- Ikiwa imezimwa
, Gemini na huduma zingine katika programu ya Google (kama vile Tafuta) hazitumii data ya eneo lako mahususi.
- Ikiwa imewashwa
- Chagua ruhusa ya programu ya kufikia maelezo ya mahali: Kila wakati, Programu Inapotumika Tu, Omba Idhini Wakati Mwingine Au Ninapotuma au Usiruhusu Kamwe.
Gemini kwenye Google Messages
Gemini kwenye Google Messages haiwezi kufikia data ya eneo mahususi uliko. Fahamu mahali ambako Gemini kwenye Google Messages inapatikana.
Pata maelezo zaidi kuhusu data ya mahali ulipo na jinsi ya kuidhibiti.
Programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi (kwenye Android)
Gemini inapatikana kwenye programu ya Google, hata ikiwa utapakua programu ya Gemini . Gemini na programu ya Google vinaweza kutumia uwezo na vipengele mbalimbali kwenye kifaa chako (kama vile kamera, maikrofoni, anwani au data ya mahali uliko) kulingana na ruhusa za programu yako ya Google. Ili ukague na udhibiti ruhusa hizi:
- Gusa na ushikilie programu ya Google
.
- Gusa Maelezo ya Programu
Ruhusa.
- Ili ubadilishe mipangilio ya ruhusa, iguse, kisha uchague Ruhusu au Usiruhusu.
Faili zilizopakiwa
Ninaweza kukagua na kudhibiti kwa namna gani faili nilizopakia?Ambapo unaweza kukagua faili unazopakia
Unaweza kukagua faili unazopakia, kama vile picha, hati na picha za skrini katika magumzo uliyobandika na ya hivi majuzi kwenye Programu za Gemini.
Jinsi ya kudhibiti faili unazopakia
Unaweza kufuta vidokezo ambako ulipakia faili katika Shughuli kwenye Programu za Gemini. Kulingana na mahali ulipotoa faili ulizopakia, faili hufutwa au kuacha kutumiwa tena kukujibu.
- Ikiwa faili ilipakiwa kutoka kwenye kifaa chako, faili hiyo hufutwa unapofuta kidokezo kinachohusiana.
- Ikiwa faili ilipakiwa kutoka kwenye Hifadhi yako ya Google, haitumiwi tena kukujibu katika gumzo linalohusiana, lakini bado inapatikana katika Hifadhi yako.
Jinsi picha kwenye vidokezo hufanya kazi
Unapoweka picha kwenye kidokezo chako au picha ya skrini ukitumia kipengele cha "Uliza kuhusu skrini hii," Programu za Gemini pia hutumia teknolojia ya Lenzi ya Google kuelewa kilicho kwenye picha na kusoma maandishi. Kwa mfano, Lenzi ya Google inaweza kutambua pikseli zilizo kwenye picha na kubaini kuwa ni paka anayeruka. Programu za Gemini huongeza taarifa hii kwenye kidokezo chako ili kuelewa ombi lako vyema. Google hutumia taarifa hii kwa namna sawa na kidokezo kingine chochote, kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
Jinsi tunavyodhibiti matumizi ya picha zako halisi
Kwa wakati huu, hatutumii picha halisi unazopakia au pikseli za picha hizo kuboresha teknolojia zetu zalishi za mashine kujifunza, isipokuwa zijumuishwe kwenye maoni. Ukituma maoni kuhusu jibu la Programu ya Gemini, picha ya mwisho iliyopakiwa katika mazungumzo yale yale kabla ya jibu hilo hujumuishwa kama sehemu ya maoni yako, isipokuwa uchague kutoituma. Google hutumia data hii sawa na maoni mengine yote unayotoa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia maoni yako.
Kadiri tunavyotoa vipengele vipya na kuboresha huduma zetu, tutawasiliana nawe kwa uwazi ikiwa tutatumia picha zako kwa njia tofauti.
Unapopakia faili kwenye kidokezo chako, Programu za Gemini zinaweza kuifasiri kwa kuihusisha na kidokezo chako. Hii inaweza kujumuisha kuchanganua faili hiyo ili kutoa maelezo kuihusu kwenye jibu.
Kwa sasa Google haifundishi mifumo yake ya AI zalishi kwa kutumia faili unazopakia, isipokua ukizijumuisha kwenye maoni yako.
Kadiri tunavyotoa vipengele vipya na kuboresha huduma zetu, tutawasiliana nawe kwa uwazi ikiwa tutatumia kwa njia tofauti faili unazopakia.
Picha zilizozalishwa
Unaweza kukagua picha zako zilizozalishwa katika magumzo yako yaliyobandikwa, magumzo ya hivi majuzi na Shughuli kwenye Programu za Gemini. Unaweza kufuta vidokezo vyako, hatua ambayo pia hufuta picha zozote zilizozalishwa kwenye majibu ya vidokezo hivyo, katika Shughuli kwenye Programu za Gemini.
Google hutumia data hii, kulingana na Ilani yetu ya Faragha ya Programu za Gemini, ili kutoa, kuboresha na kubuni bidhaa na huduma za Google pamoja na teknolojia za mashine kujifunza.
Unapotuma maoni kuhusu majibu kutoka kwenye Programu za Gemini, Google hutumia data hii kwa namna sawa na maoni mengine unayotoa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotumia maoni yako.
Programu zilizounganishwa katika Gemini
Nini hutokea katika data yangu ambayo Gemini huruhusu programu zilizounganishwa zifikie?Gemini inaweza kuunganisha na huduma zinazoitwa programu ili kukusaidia kutekeleza mambo vizuri zaidi, kama vile:
- Kutafuta maelezo yanayofaa ili kukujibu
- Kukufanyia vitendo
Pata maelezo zaidi kuhusu programu zinazoweza kuunganisha na Gemini.
Data inayofikiwa
Ili kushughulikia maombi yako, Gemini inaweza kuruhusu programu zilizounganishwa zifikie data ifuatayo:
- Maelezo kutoka kwenye kifaa na mazungumzo yako
- Mapendeleo kama vile lugha
- Maelezo ya mahali
Pia, kwa ruhusa yako, Gemini huziambia programu fulani wewe ni nani. Hii inahitajika ili kuunganisha Programu za Gemini na taarifa binafsi pamoja na maudhui yako katika huduma nyingine ili ziweze kushughulikia maombi yako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti programu kwenye Gemini.
Muhimu: Ukiziomba Programu za Gemini zibadilishe maudhui unayofikia pamoja na wengine au zidhibiti vifaa unavyotumia pamoja na wengine kwenye huduma nyinginezo, vitendo hivyo vinaweza kuonekana kwa mtu yeyote anayeweza kufikia kifaa au maudhui hayo ya pamoja.
Jinsi data inayoweza kufikiwa inavyotumiwa na huduma nyingine za Google
Maelezo yanayoruhusiwa kufikiwa na huduma nyingine za Google yanatumika kulingana na Sera ya Faragha ya Google ili:
- Kukupa huduma na kushughulikia ombi lako
- Kudumisha teknolojia za Google zinazowezesha shughuli za Gemini na programu, kama vile API
- Kuboresha huduma hizo ili kukujibu ipasavyo pamoja na watumiaji wengine wa Google
Jinsi data inayoweza kufikiwa hufutwa na huduma nyingine za Google
Huduma za Google zinaporuhusiwa kufikia data, zitafuta kiotomatiki taarifa hizi zinazofikiwa wakati hazihitajiki tena kwa madhumuni yaliyoorodheshwa hapo juu, kama ilivyoelezwa kwenye Jinsi Google inavyohifadhi data inayokusanya. Ukifuta mazungumzo husika katika Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, hatua hiyo haifuti taarifa zinazoweza kufikiwa katika huduma nyingine.
Jinsi data inayoweza kufikiwa inavyotumiwa na kufutwa na huduma pamoja na programu za wengine
Huduma na programu za wengine hutumia data inayoweza kufikiwa mara kwa mara kwa mujibu wa sera yazo zenyewe za faragha. Tafadhali zikague kwa makini kabla ya kutumia huduma au programu za wengine.
Jinsi ya kudhibiti data yako
- Unaweza kudhibiti programu zinazounganisha na Gemini wakati wowote kwenye ukurasa wa Programu katika mipangilio ya Gemini.
- Ukizima kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, programu huzimwa. Ukiwasha kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, programu zozote zilizounganishwa huwashwa upya.
Unaweza kutumia programu ili kusaidia Programu za Gemini kuunganisha na:
- Taarifa zako binafsi na maudhui kwenye kifaa chako na katika zana, programu na huduma nyingine ili Programu za Gemini ziweze kukujibu vyema zaidi.
- Huduma nyingine za Google ili Programu za Gemini ziweze kutekeleza vitendo unavyoomba kwenye huduma hizo.
Pata maelezo zaidi kuhusu programu zinazoweza kuunganisha na Gemini.
Jinsi data inavyotumika
Gemini huchakata data binafsi inayoifikia kwenye programu zilizounganishwa, kama vile jina, anwani ya barua pepe na maudhui yako binafsi kisha kuitumia ili:
- Kukupatia vipengele vya Programu za Gemini wakati unaviomba. Kwa mfano:
- Kwa kutumia Google Workspace, kuandaa muhtasari wa barua pepe zako na kutuma maudhui
- Kupata maelezo zaidi kuhusu programu nyingine zinazoweza kuunganisha na Gemini
- Kudumisha huduma za Programu za Gemini. Kwa mfano:
- Kurejesha hali ya kawaida baada ya huduma kuacha kufanya kazi
- Kupima hali ya jumla ya utumiaji
Maudhui yako binafsi ambayo Programu za Gemini hufikia kwenye huduma za Google:
- Hayaruhusiwi kufikiwa wala kuhakikiwa na wahakiki wanadamu
- Hayatumiwi ili kuboresha teknolojia zalishi za mashine kujifunza zinazoendesha Programu za Gemini
- Hayatumiwi na Programu za Gemini kukuonyesha matangazo
- Hayahifadhiwi ikipita kipindi cha muda unaohitajika kutoa na kudumisha huduma za Programu za Gemini
Jinsi ya kudhibiti data yako
- Unaweza kudhibiti programu zinazounganisha na Gemini wakati wowote kwenye ukurasa wa Programu katika mipangilio ya Gemini.
- Ukizima kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, programu huzimwa. Ukiwasha kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, programu zozote zilizounganishwa huwashwa upya.
Data inayokusanywa na kuchakatwa
Ukiunganisha Gemini na programu za kutuma ujumbe au kupiga simu ili ikusaidie kutuma ujumbe au kupiga simu, programu za Gemini za vifaa vya mkononi hukusanya na kuchakata:
- Shughuli zako kwenye Programu za Gemini
- Kumbukumbu za simu na ujumbe kwenye kifaa
- Maelezo ya mawasiliano
- Maelezo na mipangilio ya kifaa
Iwapo ulitumia programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi kupiga simu au kutuma ujumbe kwa usaidizi wa Mratibu wa Google, historia ya hadi siku 90 ya maombi ya mawasiliano yaliyohifadhiwa ya Mratibu wa Google (kwa mfano, "Mtumie Sasha ujumbe") inaweza kupakiwa kutoka kwenye Historia yako ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu hadi kwenye Shughuli zako kwenye Programu za Gemini. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi Shughuli za Programu za Gemini hutumika na huduma na mipangilio mingine.
Jinsi data inavyotumika
Ili upige simu au utume ujumbe ukitumia programu zilizounganishwa, programu za Gemini za vifaa vya mkononi hutumia data yako:
- Kuchagua programu ya kupiga simu au kutuma ujumbe inayofaa zaidi na
- Kukusaidia kuwasiliana na mtu sahihi.
Jinsi ya kudhibiti data yako
- Ikiwa hungependa programu za Gemini za vifaa vya mkononi zitumie shughuli zako kupiga simu au kutuma ujumbe, unaweza kufuta shughuli zako wakati wowote katika Shughuli Zako Kwenye Programu za Gemini.
- Unaweza kuzima programu za kupiga simu na kutuma ujumbe wakati wowote katika ukurasa wako wa Programu kwenye mipangilio ya Gemini. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti programu kwenye Gemini.
Muhimu: Mipangilio ya Kiratibu cha Google, kama vile Mipangilio ya Kiratibu kwenye skrini iliyofungwa na Matokeo binafsi haitumiki kwenye programu zilizounganishwa na Gemini.
Gemini Live
Google hutumiaje data ya Gemini Live?Rekodi na manukuu ya jinsi unavyotumia Gemini Live, pamoja na maudhui yote unayoiruhusu ifikie, huchakatwa kwa mujibu wa Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini na kuhifadhiwa katika Shughuli kwenye Programu za Gemini ikiwa umewasha. Unaweza kudhibiti na kufuta shughuli zako kwenye Programu za Gemini wakati wowote.
Iwapo umezima kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, magumzo yako na Gemini Live huhifadhiwa katika Akaunti yako ya Google kwa hadi saa 72 ili Google iweze kutoa huduma na kuchakata maoni yoyote. Pata maelezo zaidi.
Iwapo umewasha kipengele cha Shughuli zako kwenye Programu za Gemini, manukuu ya Magumzo yako ya moja kwa moja hutumiwa kuboresha Akiliunde ya Google. Pata maelezo zaidi kuhusu chaguo ulizonazo.
Kwa wakati huu, rekodi za sauti za Live hazitumiwi kuboresha Akiliunde ya Google. Tutakufahamisha iwapo hilo litabadilika.
Tafadhali heshimu faragha ya wengine na uombe ruhusa kabla ya kurekodi au kuwajumuisha kwenye Gumzo la moja kwa moja.
Gem
Nini hufanyika kwenye data yangu ninapotumia Gem?Jinsi data inavyotumika
Unaweza kubuni na kuhifadhi Gem ili uwekee mapendeleo majibu ya Programu za Gemini. Programu za Gemini hutumia maelezo uliyotoa ili kutayarisha majibu yanayokufaa. Jina la Gem yako, maagizo maalum na maelezo yanayohusiana yanatumika kwa mujibu wa Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini na Sera ya Faragha ya Google, kwa madhumuni mbalimbali yakiwemo kuboresha Akiliunde ya Google kwa usaidizi wa wahakiki wanadamu.
Ukizima Shughuli zako kwenye Programu za Gemini:
- Gem zozote utakazobuni bado zitahifadhiwa katika Programu za Gemini.
- Mazungumzo yoyote na Gem hayatahifadhiwa isipokuwa kama ilivyobainishwa kwenye Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
Iwe umewasha au kuzima Shughuli kwenye Programu za Gemini, magumzo ya kukagua yanayotayarishwa wakati wa kuunda Gem mpya hayatahifadhiwa.
Jinsi unavyoweza kufuta Gem
Gem hufutwa unapozifuta katika programu ya Gemini ya wavuti. Unaweza kufuta Gem katika ukurasa wa kidhibiti cha Gem kwenye programu ya Gemini ya wavuti.
Jinsi ya kudhibiti data yako
Unaweza kudhibiti Gem zako katika ukurasa wa kidhibiti cha Gem kwenye programu ya Gemini ya wavuti.