Iwapo una msongo wa mawazo au mawazo ya kutaka kujiua, tumia maelezo ya mawasiliano yaliyo hapa chini ili upate usaidizi.
- Marekani: Wasiliana na Shirika la Kitaifa la Kuzuia Matukio ya Kujiua (Lifeline) kupitia 1-800-273-TALK (8255). Wahudumu wanaoshughulikia dharura wanapatikana wakati wowote na simu ni ya siri. Nchi nyingine: Tembelea tovuti ya Shirika la Kimataifa la Kuzuia Matukio ya Kujiua Ili upate kituo cha dharura katika eneo uliko.
Kumsaidia mtu mwingine
Iwapo unaamini kuwa mtu mwingine yupo katika hatari ya kujiua (na una maelezo ya mawasiliano ya mtumiaji huyu), wasiliana na taasisi ya sheria katika eneo uliko ili upate usaidizi wa papo hapo.
Unaweza pia kumhimiza mtu huyo apige simu ya moja kwa moja ya huduma ya kuzuia matukio ya kujiua kwa kutumia taarifa zilizo hapo juu.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kumsaidia mtu anayezungumza kuhusu kujiua:
- Marekani: Shirika la Kitaifa la Kuzuia Matukio ya Kujiua
- Nchi nyingine: Befrienders Worldwide