Ukiingia katika huduma ya Google Darasani, utaona dashibodi iliyowekewa mapendeleo kulingana na jukumu lako. Ukurasa huu wa kwanza unaangazia majukumu yako muhimu zaidi, iwe unafundisha, unajifunza au unasimamia shule yako.
Muhimu: Kwa kuwa ukurasa wako wa kwanza umewekewa mapendeleo kulingana na mipangilio na vipengele vyako, huenda usione kila sehemu iliyoorodheshwa hapa chini.
Kubadilisha kati ya mionekano yako
Ukurasa wako wa kwanza huchagua kwa chaguomsingi jukumu unalotekeleza mara nyingi katika huduma ya Google Darasani. Ikiwa una majukumu mengi (kama vile mwalimu anayesoma kozi ya maendeleo ya kitaaluma), unaweza kubadilisha kwa urahisi dashibodi yako.
Ili ubadilishe mwonekano wako:
- Tembelea classroom.google.com
- Nenda kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa wa kwanza.
- Bofya kitufe cha kubadilisha mwonekano (kwa mfano,
Kufundisha,
Waliojiandikisha au
Msimamizi).
Kubadilisha muundo wako upendavyo
Unaweza kupanga ukurasa wako wa kwanza ili uonyeshe tu maelezo unayohitaji.
- Ili ukunje au upanue sehemu, bofya Kishale cha juu
au Kishale cha chini
katika sehemu ya juu kulia ya sehemu.
- Google Darasani hukumbuka mapendeleo yako, kwa hivyo sehemu zilizokunjwa zitaendelea kufichwa wakati mwingine utakapozitembelea.
Kidokezo: Ikiwa sehemu haina maudhui ya sasa (kama vile hakuna mazoezi yajayo), itafichwa kiotomatiki kwenye ukurasa wako wa kwanza.
Mwonekano wa kufundisha
Walimu wanaweza kutumia ukurasa wa kwanza kufuatilia hatua ambazo wanafunzi wamepiga na kutumia zana za mafunzo. Katika mwonekano wa kufundisha, utapata sehemu hizi:
- Yaliyopaswa Kuwasilishwa Hivi Majuzi: Ina mazoezi yaliyopaswa kuwasilishwa hivi majuzi (inaonyesha hadi mazoezi 5 yaliyopaswa kuwasilishwa siku 7 zilizopita ambayo unahitaji kuyakagua).
- Muhtasari wa darasa: Huonyesha takwimu muhimu kuhusu utendaji wa wanafunzi. Bofya kipengee ili uende moja kwa moja kwenye zana ya kusahihisha au kazi za wanafunzi.
- Vipengele vinavyoangaziwa: Hutoa viungo vya haraka vya kugundua zana za akiliunde, shughuli za video, seti za majaribio na Read Along.
- Madarasa: Huonyesha kadi za madarasa yako yanayoendelea.
Mwonekano wa waliojiandikisha
Wanafunzi wanaweza kutumia ukurasa wa kwanza ili wapange shughuli zao na wafuatilie kazi zao za kozi. Katika mwonekano wa waliojiandikisha, utapata sehemu hizi:
- Yanayopaswa kuwasilishwa hivi karibuni: Huonyesha hadi mazoezi 5 yajayo katika madarasa yote uliyojiandikisha ambayo yanapaswa kuwasilishwa ndani ya siku 7 zijazo. Bofya zoezi ili uende moja kwa moja kwenye kazi yako.
- Kujifunza ukitumia Gemini: Ikiwa unatimiza masharti, wekelea kiashiria juu ya zoezi kisha ubofye "Jifunze ukitumia Gemini" ili uone menyu ya vitendo vya kujifunza kupitia muktadha wa zoezi lako.
- Zana za kujifunza darasani: Ikiwa unatimiza masharti, tumia zana za kujifunza zinazotumia AI ulizokabidhiwa na walimu wako, kama vile madaftari ya NotebookLM na Gemini Gem.
- Madarasa: Huonyesha kadi za madarasa yako yanayoendelea ili uweze kwenda moja kwa moja kwenye kozi mahususi. Ili uone madarasa yaliyofichwa, bofya kishale cha chini katika sehemu ya chini ya sehemu ili uipanue.
Mwonekano wa msimamizi
Wasimamizi na viongozi wa elimu wanaweza kutumia ukurasa wa kwanza kwa usimamizi na udhibiti wa shule nzima. Katika mwonekano wa msimamizi, utapata sehemu hizi:
- Takwimu za shule: Huonyesha vipimo vya kiwango cha juu vya taasisi lako, kama vile viwango vya ukamilishaji wa mazoezi, alama za wastani na asilimia ya wanafunzi wanaoshiriki.
- Vipengele vinavyoangaziwa: Hutoa viungo vya haraka vya kuwasaidia wakufunzi na wanafunzi, kudhibiti shughuli za dashibodi ya msimamizi na kuruhusu wakufunzi wafikie zana.
- Vipengele vipya katika huduma ya Google for Education na Google Darasani: Huangazia vipengele vipya kabisa katika nafasi ya kazi ya Google for Education.