Kufuta, kuruhusu na kudhibiti vidakuzi katika Chrome

Unaweza kuchagua kufuta vidakuzi vilivyopo, kuruhusu au kuzuia vidakuzi vyote na kuweka mapendeleo kwenye tovuti fulani.

Muhimu: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, utaona mipangilio mipya ya Chrome ya kudhibiti vidakuzi vya washirika wengine inayoitwa "Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia." Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.

Vidakuzi ni nini

Vidakuzi ni faili zinazoundwa na tovuti unazotembelea. Kwa kuhifadhi maelezo kuhusu shughuli yako ya kutembelea tovuti, vinarahisisha hali yako ya utumiaji mtandaoni. Kwa mfano, tovuti zinaweza kukufanya usalie ukiwa umeingia katika akaunti, kukumbuka mapendeleo yako ya tovuti na kukupatia maudhui muhimu ya eneo ulipo.

Kuna aina 2 za vidakuzi:

  • Vidakuzi vilivyowekwa na vikoa unavyotembelea: Vinaundwa na tovuti unayotembelea. Tovuti inaonyeshwa kwenye sehemu ya anwani.
  • Vidakuzi vya washirika wengine: Vinaundwa na tovuti nyingine. Tovuti unayotembelea inaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo na maandishi. Tovuti zozote zingine kati ya hizi zinaweza kuhifadhi vidakuzi na data nyingine ili kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji.

Futa vidakuzi vyote

Ukiondoa vidakuzi, utaondolewa kwenye tovuti na mapendeleo yako yaliyohifadhiwa yanaweza kufutwa.

  1. Kwenye iPhone au iPad yako, fungua Chrome Chrome.
  2. Gusa More kisha Mipangilio Zaidi Settings.
  3. Gusa Faragha na Usalama kisha Futa Data ya Kuvinjari.
  4. Angalia Vidakuzi, Data ya Tovuti
  5. Batilisha uteuzi wa vipengee vingine.
  6. Gusa Futa Data ya Kuvinjari kisha Futa Data ya Kuvinjari.
  7. Gusa Nimemaliza.

Nyenzo zinazohusiana

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2053981672502974857
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
237
false
false