Unaweza kuchagua kufuta vidakuzi vilivyopo, kuruhusu au kuzuia vidakuzi vyote na kuweka mapendeleo kwenye tovuti fulani.
Muhimu: Iwapo umejiunga katika kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, utapata mipangilio mipya ya Chrome ya kudhibiti vidakuzi vya washirika wengine inayoitwa "Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia." Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
Vidakuzi ni nini
Vidakuzi ni faili zinazoundwa na tovuti unazotembelea. Kwa kuhifadhi maelezo kuhusu shughuli yako ya kutembelea tovuti, vinarahisisha hali yako ya utumiaji mtandaoni. Kwa mfano, tovuti zinaweza kukufanya usalie ukiwa umeingia katika akaunti, kukumbuka mapendeleo yako ya tovuti na kukupatia maudhui muhimu ya eneo ulipo.
Kuna aina 2 za vidakuzi:
- Vidakuzi vilivyowekwa na vikoa unavyotembelea: Vinaundwa na tovuti unayotembelea. Tovuti inaonyeshwa kwenye sehemu ya anwani.
- Vidakuzi vya washirika wengine: Vinaundwa na tovuti nyingine. Tovuti unayotembelea inaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo na maandishi. Tovuti zozote zingine kati ya hizi zinaweza kuhifadhi vidakuzi na data nyingine ili kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji.
Futa vidakuzi vyote
Muhimu: Ukifuta vidakuzi, unaweza kuondolewa kwenye akaunti katika tovuti zinazokukumbuka na mapendeleo uliyohifadhi yanaweza kufutwa. Hali hii hutokea wakati wowote ukifuta kidakuzi.
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio .
- Bofya Faragha na usalama vidakuzi vya Washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, chagua mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
- Bofya Angalia data na ruhusa zote za tovuti Futa data yote.
- Ili uthibitishe, bofya Futa.
Futa vidakuzi mahususi
Futa vidakuzi kwenye tovuti- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio .
- Bofya Faragha na usalama vidakuzi vya Washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, chagua mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
- Bofya Angalia data na ruhusa zote za tovuti.
- Katika sehemu ya juu kulia, tafuta jina la tovuti.
- Kwenye sehemu ya kulia ya tovuti, bofya Futa .
- Ili uthibitishe, bofya Futa.
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Futa data ya kuvinjari.
- Katika sehemu ya juu, karibu na "Kipindi cha muda," bofya menyu kunjuzi.
- Chagua kipindi, kama vile saa au siku iliyopita.
- Angalia Vidakuzi na data nyingine ya tovuti.
- Batilisha uteuzi wa vipengee vingine vyote.
- Bofya Futa data.
Badilisha mipangilio yako ya vidakuzi
Muhimu: Ikiwa hutaruhusu tovuti zihifadhi vidakuzi, tovuti nyingi zinazohitaji uingie katika akaunti hazitafanya kazi na mapendeleo uliyohifadhi huenda yasihifadhiwe.
Unaweza kuruhusu au kuzuia vidakuzi kwenye tovuti yoyote.
Ruhusu au uzuie vidakuziUnaweza kuruhusu au kuzuia vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi.
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio .
- Bofya Faragha na usalama Vidakuzi vya washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, fuata maagizo ya mipangilio ya “Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia”.
- Teua chaguo:
- Ruhusu vidakuzi vya washirika wengine.
- Zuia vidakuzi vya washirika wengine katika Hali ya kutumia faraghani.
- Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
- Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine, vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti zingine vinazuiwa isipokuwa kama tovuti inaruhusiwa kwenye orodha yako ya tovuti zisizofuata kanuni.
Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, bado unaweza kuviruhusu kwenye tovuti fulani.
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio.
- Bofya Faragha na usalama Vidakuzi vya washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, chagua mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
- Karibu na "Tovuti zinazoruhusiwa kutumia vidakuzi vya washirika wengine," bofya Weka.
- Weka anwani ya wavuti.
- Ili uunde orodha ya tovuti zisizofuata kanuni kwenye kikoa kizima, weka
[*.]
kabla ya jina la kikoa. Kwa mfano,[*.]google.com
italingana nadrive.google.com
nacalendar.google.com
. - Unaweza pia kuweka Anwani ya IP au anwani ya wavuti ambayo haianzi na
http://
.
- Ili uunde orodha ya tovuti zisizofuata kanuni kwenye kikoa kizima, weka
- Chagua Weka.
Ili uondoe orodha ya tovuti zisizofuata kanuni usizohitaji tena, kwenye sehemu ya kulia ya tovuti, bofya Ondoa .
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Kwenye sehemu ya anwani iliyo juu:
- Ili uruhusu vidakuzi vya washirika wengine: Chagua Vidakuzi vya washirika wengine vilivyozuiwa au mipangilio ya Ulinzi dhidi ya tovuti zinazokufuatilia kisha uwashe Vidakuzi vya washirika wengine.
- Ili uzuie vidakuzi vya washirika wengine: Chagua Vidakuzi vya washirika wengine vilivyoruhusiwa au mipangilio ya Ulinzi dhidi ya tovuti zinazokufuatilia kisha uzime Vidakuzi vya washirika wengine.
- Ili ufunge kidirisha cha mazungumzo kisha upakie upya ukurasa, chagua Funga . Unaweza pia kuchagua sehemu yoyote nje ya kidirisha cha mazungumzo ili ukifunge.
- Baada ya ukurasa kupakiwa upya, sehemu ya anwani huonyesha "Vidakuzi vya washirika wengine vinaruhusiwa," "Vidakuzi vya washirika wengine vimezuiwa" au "Vidakuzi vya washirika wengine ni vichache" kulingana na mipangilio yako.
Vidokezo:
- Chaguo hili ni la muda na la tovuti unayotumia tu.
- Tovuti huwekwa kiotomatiki kwenye orodha ya tovuti zisizofuata kanuni.
- Ukiruhusu kwa muda vidakuzi vya washirika wengine kwenye tovuti, mipangilio hiyo itaendelea hadi katika Hali ya kutumia faraghani na huwezi kuibadilisha kwenye Hali ya kutumia faraghani.
acme-music.example
na acme-video.example
.Ili uruhusu tovuti zinazohusiana zipate shughuli zako kwenye kikundi:
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio.
- Bofya Faragha na usalama Vidakuzi vya washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, fuata maagizo ya mipangilio ya “Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia”.
- Chagua Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
- Washa au uzime kipengele cha Ruhusu tovuti zinazohusiana ziangalie shughuli zako kwenye kikundi.
Ili uonyeshe tovuti zinazohusiana kwenye kikundi sawa:
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio.
- Bofya Faragha na usalama Vidakuzi vya washirika wengine Angalia data na ruhusa zote za tovuti.
- Kidokezo: Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, chagua mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
- Chagua tovuti.
- Bofya Zaidi Onyesha tovuti katika kikundi sawa.
Kidokezo:
- Ili upate tovuti zinazohusiana, karibu na sehemu ya anwani, bofya Angalia maelezo ya tovuti Vidakuzi na data ya tovuti Angalia tovuti zinazohusiana.
- Ikiwa wewe ni sehemu ya kikundi cha majaribio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia, chagua mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
Tovuti unazotembelea zinaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo, maandishi na hata vipengele kama vile kihariri matini au wijeti ya hali ya hewa. Tovuti hizi nyingine zinaweza kuomba ruhusa zitumie taarifa ambazo zimehifadhi kukuhusu (mara nyingi huhifadhiwa kwa kutumia vidakuzi) ili maudhui yake yafanye kazi vizuri.
Kwa mfano, fikiria kwa kawaida unatunga hati kwenye docs.google.com
. Unapokamilisha jukumu la shule, unatakiwa ushirikiane na wanafunzi wengine kwenye tovuti ya darasa ya shule yako inayotoa ufikiaji wa moja kwa moja wa Hati za Google. Kupitia ruhusa yako:
- Hati za Google zinaweza kufikia vidakuzi vyake vya washirika wengine unapotumia tovuti ya shule yako, hivyo kuruhusu muunganisho kati ya tovuti na Hati za Google.
- Hali hii inaweza kuruhusu Hati za Google zithibitishe wewe ni nani, zipate taarifa zako na zihifadhi mabadiliko unayofanya kwenye hati zako katika tovuti.
Katika baadhi ya matukio, taarifa hizi zinaweza kutumika kufuatilia shughuli zako unapovinjari tovuti. Kama kipengele cha faragha, unaweza kuamua wakati wa kuruhusu maudhui yaliyopachikwa yafikie data yako ya tovuti unazoamini.
Kidokezo: Muunganisho hutumia vidakuzi na hudumu kwa siku 30 au ilimradi tu uendelee kuutumia. Unaweza kuacha kuruhusu muunganisho wakati wowote katika Mipangilio.
Kuruhusu au kukataa ruhusa
Unapovinjari tovuti inayoonyesha kidokezo kinachoomba ruhusa ya maudhui yaliyopachikwa kutumia taarifa zilizohifadhiwa kukuhusu:
- Chagua Ruhusu ili uipe tovuti uwezo wa kufikia taarifa zilizohifadhiwa kukuhusu (kwa kutumia vidakuzi)
- Chagua Usiruhusu ili ukatae kuipa tovuti uwezo wa kufikia
Vidokezo:
- Ili uzime kipengele cha kuruhusu uwezo wa kufikia, pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti ruhusa za mipangilio ya tovuti.
- Unaweza pia kudhibiti uwezo wa kufikia kwa kubofya "Angalia maelezo ya tovuti" kwenye upande wa kushoto wa sehemu ya anwani kisha uwashe au uzime Maudhui yaliyopachikwa .
Kudhibiti mipangilio yako ya ulinzi dhidi ya tovuti zinazokufuatilia
Mipangilio ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia inapowashwa huzuia kwa kiasi kikubwa tovuti zisitumie vidakuzi vya washirika wengine kukufuatilia unapovinjari, isipokuwa katika hali chache ili kuruhusu huduma za msingi zifanye kazi. Ukiamua, unaweza kuzuia kabisa vidakuzi vya washirika wengine katika mipangilio yako. Unaweza kudhibiti mapendeleo yako ya Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia katika mipangilio yako ya "Faragha na Usalama".
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Zaidi Mipangilio .
- Bofya Faragha na usalama Ulinzi Dhidi ya Tovuti Zinazokufuatilia.
- Unaweza pia kuchagua ulinzi wa hali ya juu wa faragha:
- Kuzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine: Unapowasha kitufe hiki, vipengele vilivyo kwenye baadhi ya tovuti huenda visifanye kazi. Chrome huzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti unazotembelea, ikiwa ni pamoja na tovuti zinazohusiana.
- Tuma ombi la "Do not track" kwenye data yako ya kuvinjari: Ukiwasha kitufe hiki, unaomba tovuti zisikufuatilie. Tovuti hutumia hiari yazo ikiwa zitatii ombi. Pata maelezo zaidi kuhusu ombi la "Do Not Track".
- Chagua tovuti unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine: Unaweza pia kuangalia na kubadilisha tovuti unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine chini ya “Tovuti zinazoruhusiwa kutumia vidakuzi vya washirika wengine.” Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuruhusu vidakuzi vya washirika wengine.