Unaweza kuchagua kufuta vidakuzi vilivyopo, kuruhusu au kuzuia vidakuzi vyote na kuweka mapendeleo kwenye tovuti fulani.
Muhimu: Ikiwa unashiriki katika kikundi cha majaribio kinachodhibiti vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, unaweza kupata mipangilio tofauti ya kudhibiti vidakuzi vya washirika wengine. Pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio.
Vidakuzi ni nini
Vidakuzi ni faili zinazoundwa na tovuti unazotembelea. Kwa kuhifadhi maelezo kuhusu shughuli yako ya kutembelea tovuti, vinarahisisha hali yako ya utumiaji mtandaoni. Kwa mfano, tovuti zinaweza kukufanya usalie ukiwa umeingia katika akaunti, kukumbuka mapendeleo yako ya tovuti na kukupatia maudhui muhimu ya eneo ulipo.
Kuna aina 2 za vidakuzi:
- Vidakuzi vilivyowekwa na vikoa unavyotembelea: Vinaundwa na tovuti unayotembelea. Tovuti inaonyeshwa kwenye sehemu ya anwani.
- Vidakuzi vya washirika wengine: Vinaundwa na tovuti nyingine. Tovuti unayotembelea inaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo na maandishi. Tovuti zozote zingine kati ya hizi zinaweza kuhifadhi vidakuzi na data nyingine ili kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji.
Kidokezo: Huenda baadhi ya tovuti zikakuomba ukubali au ukatae vidakuzi.
Kufuta vidakuzi vyote
Muhimu: Ukifuta vidakuzi, unaweza kuondolewa kwenye akaunti katika tovuti zinazokukumbuka na mapendeleo uliyohifadhi yanaweza kufutwa. Hali hii hutokea wakati wowote ukifuta kidakuzi.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Faragha na usalama
Futa data ya kuvinjari.
- Chagua kipindi cha muda, kama vile Saa iliyopita au Kila wakati.
- Chagua Vidakuzi na data ya tovuti na ubatilishe uteuzi wa vipengee vingine vyote.
- Gusa Futa data
Futa.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Nenda kwenye tovuti.
- Kwenye sehemu ya anwani, upande wa juu kushoto, gusa Maelezo ya ukurasa
Vidakuzi na data ya tovuti.
- Karibu na idadi ya vidakuzi vinavyotumika, gusa Futa
.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Mipangilio ya tovuti
Vidakuzi vya washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa unashiriki katika kikundi cha majaribio kinachodhibiti vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio.
- Teua chaguo:
- Ruhusu vidakuzi vya washirika wengine.
- Zuia vidakuzi vya washirika wengine katika Hali ya kutumia faraghani.
- Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
- Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine, vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti zingine vitazuiwa isipokuwa kama tovuti inaruhusiwa kwenye orodha yako ya tovuti zisizofuata kanuni.
Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, bado unaweza kuviruhusu kwenye tovuti mahususi.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Faragha na usalama
Vidakuzi vya washirika wengine.
- Gusa + Weka kwenye orodha ya tovuti zisizofuata kanuni
- Weka anwani ya wavuti.
- Ili uunde orodha ya tovuti zisizofuata kanuni kwenye kikoa kizima, weka [*.] kabla ya jina la kikoa. Kwa mfano, [*.]google.com italingana na drive.google.com na calendar.google.com.
- Unaweza pia kuweka Anwani ya IP au anwani ya wavuti ambayo haianzi na http://.
- Gusa Weka.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya anwani, upande wa juu kushoto:
- Ili uruhusu vidakuzi vya washirika wengine: Gusa Maelezo ya ukurasa
Vidakuzi na data ya tovuti kisha uwashe Vidakuzi vya washirika wengine.
- Ili uzuie au udhibiti vidakuzi vya washirika wengine: Gusa Maelezo ya ukurasa
Vidakuzi na data ya tovuti kisha uzime Vidakuzi vya washirika wengine.
- Ili uruhusu vidakuzi vya washirika wengine: Gusa Maelezo ya ukurasa
Vidokezo:
- Chaguo hili ni la muda na ni la tovuti unayotumia tu.
- Tovuti huwekwa kiotomatiki kwenye orodha ya tovuti zisizofuata kanuni.
- Ukiruhusu kwa muda vidakuzi vya washirika wengine kwenye tovuti, mipangilio hiyo itaendelea hadi katika Hali ya kutumia faraghani na huwezi kuibadilisha kwenye Hali ya kutumia faraghani.
Kampuni inaweza kubainisha kikundi cha tovuti zinazohusiana. Kwa mfano, kampuni inaweza kutaka usalie ukiwa umeingia katika akaunti unapovinjari kati ya acme-music.example
na acme-video.example
.
Ukiruhusu au udhibiti vidakuzi vya washirika wengine: Huruhusu tovuti zinazohusiana zifikie shughuli zako ili ziweke mapendeleo kwenye maudhui au zikufanye usalie ukiwa umeingia katika akaunti kwenye tovuti mbalimbali.
Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine: Mara nyingi hatua hio huzuia aina hii ya uhusiano kati ya tovuti. Unaweza kuzuia vidakuzi vya washirika wengine huku ukiruhusu tovuti katika kikundi sawa ili uboreshe hali yako ya utumiaji.
Unaweza kupata orodha kamili ya kampuni zinazobainisha vikundi vya tovuti zinazohusiana kwenye GitHub. Pata maelezo zaidi kuhusu tovuti zinazohusiana na vidakuzi vya washirika wengine.
Ili uruhusu tovuti zinazohusiana zipate shughuli zako kwenye kikundi:
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Faragha na usalama
Vidakuzi vya washirika wengine
Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
- Kidokezo: Ikiwa unashiriki katika kikundi cha majaribio kinachodhibiti vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio.
- Gusa kishale kando ya "Zuia vidakuzi vya washirika wengine."
- Washa au uzime kipengele cha Ruhusu tovuti zinazohusiana ziangalie shughuli zako kwenye kikundi.
Ili uonyeshe tovuti zinazohusiana kwenye kikundi sawa:
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Mipangilio ya tovuti
Tovuti zote.
- Chagua tovuti.
- Chini ya “Tovuti zinazosimamiwa na [kiungo cha tovuti],” tafuta tovuti katika kikundi sawa.
Dhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio
Kwa kikundi mahususi cha watumiaji, Google hujaribu vipengele kwenye Chrome ambavyo vinazuia kwa kiasi kikubwa tovuti zisitumie vidakuzi vya washirika wengine kukufuatilia unapovinjari. Ikiwa unashiriki katika kikundi cha kujaribu, vidakuzi vya washirika wengine hudhibitiwa kwa chaguomsingi isipokuwa vinapohitajika kuruhusu huduma za msingi za tovuti zifanye kazi.
Ukiamua, unaweza kuzuia kabisa vidakuzi vya washirika wengine katika mipangilio yako. Unaweza kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi vya washirika wengine kwenye mipangilio ya “Faragha na Usalama”.
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Kwenye sehemu ya juu kulia, gusa Zaidi
Mipangilio.
- Gusa Faragha na usalama
Vidakuzi vya washirika wengine.
- Ili kuwekea mapendeleo mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine, unaweza:
- Kuzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine: Unapowasha kitufe hiki, vipengele vilivyo kwenye baadhi ya tovuti huenda visifanye kazi. Chrome huzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti unazotembelea, ikiwa ni pamoja na tovuti zinazohusiana.
- Tuma ombi la "Do not track" kwenye data yako ya kuvinjari: Ukiwasha kitufe hiki, unaomba tovuti zisikufuatilie. Tovuti hutumia hiari yazo ikiwa zitatii ombi. Pata maelezo zaidi kuhusu ombi la "Do Not Track".
- Chagua tovuti unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine: Unaweza pia kuangalia na kubadilisha tovuti zipi unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine chini ya "Tovuti zinazoruhusiwa kutumia vidakuzi vya washirika wengine.” Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuruhusu vidakuzi vya washirika wengine.