Kufuta, kuruhusu na kudhibiti vidakuzi katika Chrome

Unaweza kuchagua kufuta vidakuzi vilivyopo, kuruhusu au kuzuia vidakuzi vyote na kuweka mapendeleo kwenye tovuti fulani.

Muhimu: Ikiwa unashiriki katika kikundi cha majaribio kinachodhibiti vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, unaweza kupata mipangilio tofauti ya kudhibiti vidakuzi vya washirika wengine. Pata maelezo ya jinsi ya kudhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio.

Vidakuzi ni nini

Vidakuzi ni faili zinazoundwa na tovuti unazotembelea. Kwa kuhifadhi maelezo kuhusu shughuli yako ya kutembelea tovuti, vinarahisisha hali yako ya utumiaji mtandaoni. Kwa mfano, tovuti zinaweza kukufanya usalie ukiwa umeingia katika akaunti, kukumbuka mapendeleo yako ya tovuti na kukupatia maudhui muhimu ya eneo ulipo.

Kuna aina 2 za vidakuzi:

  • Vidakuzi vilivyowekwa na vikoa unavyotembelea: Vinaundwa na tovuti unayotembelea. Tovuti inaonyeshwa kwenye sehemu ya anwani.
  • Vidakuzi vya washirika wengine: Vinaundwa na tovuti nyingine. Tovuti unayotembelea inaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo na maandishi. Tovuti zozote zingine kati ya hizi zinaweza kuhifadhi vidakuzi na data nyingine ili kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji.

Kidokezo: Huenda baadhi ya tovuti zikakuomba ukubali au ukatae vidakuzi.

Futa vidakuzi vyote

Muhimu: Ukifuta vidakuzi, unaweza kuondolewa kwenye akaunti katika tovuti zinazokukumbuka na mapendeleo uliyohifadhi yanaweza kufutwa. Hali hii hutokea wakati wowote ukifuta kidakuzi.

  1. Kwenye kompyuta yako, chagua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio Settings.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Chagua Angalia ruhusa na data yote ya tovuti kisha Futa data yote.
  5. Ili uthibitishe, chagua Futa.

Futa vidakuzi mahususi

Futa vidakuzi kwenye tovuti
  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio Settings.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Chagua Angalia ruhusa na data yote ya tovuti.
  5. Katika sehemu ya juu kulia, tafuta jina la tovuti.
  6. Kwenye sehemu ya kulia ya tovuti, chagua Futa Remove.
  7. Ili uthibitishe, chagua Futa.
Futa vidakuzi vya kipindi mahususi
  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Futa data ya kuvinjari.
  3. Katika sehemu ya juu, karibu na "Kipindi cha muda," chagua menyu kunjuzi.
  4. Chagua kipindi, kama vile saa au siku iliyopita.
  5. Angalia Vidakuzi na data nyingine ya tovuti.
  6. Batilisha uteuzi wa vipengee vingine vyote.
  7. Chagua Futa data.

Badilisha mipangilio yako ya vidakuzi

Muhimu: Ikiwa hutaruhusu tovuti zihifadhi vidakuzi, huenda tovuti zisifanye kazi inavyotarajiwa. Ili udhibiti vidakuzi vilivyowekwa na vikoa unavyotembelea, pata maelezo zaidi kuhusu data ya tovuti iliyo kwenye kifaa.

Unaweza kuruhusu au kuzuia vidakuzi kwenye tovuti yoyote.

Ruhusu au uzuie vidakuzi

Unaweza kuruhusu au kuzuia vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi.

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio Settings.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Teua chaguo:
    • Ruhusu vidakuzi vya washirika wengine.
    • Zuia vidakuzi vya washirika wengine katika Hali ya kutumia faraghani.
    • Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
      • Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine, vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti zingine vitazuiwa isipokuwa kama tovuti inaruhusiwa kwenye orodha yako ya tovuti zisizofuata kanuni.
Ruhusu au zuia vidakuzi katika tovuti mahususi
Muhimu: Ikiwa unatumia Chromebook yako kazini au shuleni, huenda usiweze kubadilisha mipangilio hii. Ili upate usaidizi zaidi, wasiliana na msimamizi wako.

Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine kwa chaguomsingi, bado unaweza kuviruhusu kwenye tovuti mahususi.

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Kwenye sehemu ya "Tovuti zinazoruhusiwa kutumia vidakuzi vya washirika wengine," chagua Weka.
  5. Weka anwani ya wavuti.
    • Ili uunde orodha ya tovuti zisizofuata kanuni kwenye kikoa kizima, weka [*.] kabla ya jina la kikoa. Kwa mfano, [*.]google.com italingana na drive.google.com na calendar.google.com.
    • Unaweza pia kuweka Anwani ya IP au anwani ya wavuti ambayo haianzi na http://.
  6. Chagua Weka.

Ili uondoe orodha usiyohitaji tena ya tovuti zisizofuata kanuni, kwenye sehemu ya kulia ya tovuti, chagua Ondoa Remove.

Kuruhusu kwa muda vidakuzi vya washirika wengine katika tovuti mahususi
Ukizuia au udhibiti vidakuzi vya washirika wengine, baadhi ya tovuti huenda zisifanye kazi kama ulivyotarajia. Unaweza kuruhusu kwa muda vidakuzi vya washirika wengine kwenye tovuti mahususi unayotembelea.
  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya anwani, upande wa juu kushoto:
    • Ili uruhusu vidakuzi vya washirika wengine: Chagua vidakuzi vya washirika wengine vinazuiwa au Vidakuzi vya washirika wengine vinadhibitiwa kisha uwashe Vidakuzi vya washirika wengine.
    • Ili uzuie vidakuzi au udhibiti vidakuzi vya washirika wengine: Chagua Vidakuzi vya washirika wengine vinaruhusiwa Preview kisha uzime Vidakuzi vya washirika wengine.
  3. Ili ufunge kidirisha cha mazungumzo kisha upakie upya ukurasa, chagua Funga Close. Unaweza pia kuchagua sehemu yoyote nje ya kidirisha cha mazungumzo ili ukifunge.
  4. Baada ya ukurasa kupakiwa upya, sehemu ya anwani huonyesha "Vidakuzi vya washirika wengine vinaruhusiwa," "Vidakuzi vya washirika wengine vinazuiwa" au "Vidakuzi vya washirika wengine vinadhibitiwa" kulingana na mipangilio yako.

Vidokezo:

Kuruhusu tovuti zinazohusiana zifikie shughuli yako
Kampuni inaweza kubainisha kikundi cha tovuti zinazohusiana. Kwa mfano, kampuni inaweza kutaka usalie ukiwa umeingia katika akaunti unapovinjari kati ya acme-music.example na acme-video.example.
Ukiruhusu au udhibiti vidakuzi vya washirika wengine: Tovuti zinazohusiana zitaruhusiwa kufikia shughuli zako ili kuwekea mapendeleo maudhui au zikufanye usalie ukiwa umeingia katika akaunti kwenye tovuti mbalimbali.
Ukizuia vidakuzi vya washirika wengine: Mara nyingi hatua hio huzuia aina hii ya uhusiano kati ya tovuti. Unaweza kuzuia vidakuzi vya washirika wengine huku ukiruhusu tovuti katika kikundi sawa ili uboreshe hali yako ya utumiaji.
Unaweza kupata orodha kamili ya kampuni zinazobainisha vikundi vya tovuti zinazohusiana kwenye GitHub. Pata maelezo zaidi kuhusu tovuti zinazohusiana na vidakuzi vya washirika wengine.

Ili uruhusu tovuti zinazohusiana zipate shughuli zako kwenye kikundi:

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Chagua Zuia vidakuzi vya washirika wengine.
  5. Washa au uzime kipengele cha Ruhusu tovuti zinazohusiana ziangalie shughuli zako kwenye kikundi.

Ili uonyeshe tovuti zinazohusiana kwenye kikundi sawa:

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine kisha Angalia ruhusa na data yote ya tovuti.
  4. Chagua tovuti.
  5. Ili uonyeshe tovuti kwenye kikundi sawa, chagua kishale cha menyu kunjuzi Down arrow.

Kidokezo: Ili upate tovuti zinazohusiana, kwenye sehemu ya anwani, chagua Angalia taarifa za tovuti Default (Secure) kisha Vidakuzi na data ya tovuti kisha Dhibiti data ya tovuti iliyo kwenye kifaa.

Kuhusu maudhui yaliyopachikwa

Tovuti unazotembelea zinaweza kupachika maudhui kutoka tovuti nyingine, kwa mfano picha, matangazo, maandishi na hata vipengele kama vile kihariri matini au wijeti ya hali ya hewa. Tovuti hizi nyingine zinaweza kuomba ruhusa zitumie taarifa ambazo zimehifadhi kukuhusu (mara nyingi huhifadhiwa kwa kutumia vidakuzi) ili maudhui yake yafanye kazi vizuri.

Kwa mfano, fikiria kwa kawaida unatunga hati kwenye docs.google.com. Unapokamilisha jukumu la shule, unatakiwa ushirikiane na wanafunzi wengine kwenye tovuti ya darasa ya shule yako inayotoa ufikiaji wa moja kwa moja wa Hati za Google. Kupitia ruhusa yako:

  • Hati za Google zinaweza kufikia vidakuzi vyake vya washirika wengine unapotumia tovuti ya shule yako, hivyo kuruhusu muunganisho kati ya tovuti na Hati za Google.
  • Hali hii inaweza kuruhusu Hati za Google zithibitishe wewe ni nani, zipate taarifa zako na zihifadhi mabadiliko unayofanya kwenye hati zako katika tovuti.

Wakati mwingine, taarifa hizi zinaweza kutumika kufuatilia shughuli zako unapovinjari tovuti. Kama kipengele cha faragha, unaweza kuamua wakati wa kuruhusu maudhui yaliyopachikwa yafikie data yako ya tovuti unazoamini.

Kidokezo: Muunganisho hutumia vidakuzi na hudumu kwa siku 30 au ilimradi tu uendelee kuutumia. Unaweza kuacha kuruhusu muunganisho wakati wowote katika Mipangilio.

Kuruhusu au kukataa ruhusa

Unapovinjari tovuti inayoonyesha kidokezo kinachoomba ruhusa ya maudhui yaliyopachikwa kutumia taarifa zilizohifadhiwa kukuhusu:

  • Chagua Ruhusu ili uipe tovuti uwezo wa kufikia taarifa zilizohifadhiwa kukuhusu (kwa kutumia vidakuzi)
  • Chagua Usiruhusu ili ukatae kuipa tovuti uwezo wa kufikia

Vidokezo:

Dhibiti mipangilio ya vidakuzi vya washirika wengine kwa watumiaji wa kikundi cha majaribio

Kwa kikundi mahususi cha watumiaji, Google hujaribu vipengele kwenye Chrome ambavyo vinazuia kwa kiasi kikubwa tovuti zisitumie vidakuzi vya washirika wengine kukufuatilia unapovinjari. Ikiwa unashiriki katika kikundi cha kujaribu, vidakuzi vya washirika wengine hudhibitiwa kwa chaguomsingi isipokuwa vinapohitajika kuruhusu huduma za msingi za tovuti zifanye kazi.

Ukiamua, unaweza kuzuia kabisa vidakuzi vya washirika wengine katika mipangilio yako. Unaweza kudhibiti mapendeleo yako ya vidakuzi vya washirika wengine kwenye mipangilio ya “Faragha na Usalama”.

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Zaidi kisha Mipangilio Settings.
  3. Chagua Faragha na usalama kisha Vidakuzi vya washirika wengine.
  4. Unaweza pia kuchagua ulinzi wa hali ya juu wa faragha:
    • Kuzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine: Unapowasha kitufe hiki, vipengele vilivyo kwenye baadhi ya tovuti huenda visifanye kazi. Chrome huzuia vidakuzi vyote vya washirika wengine kwenye tovuti unazotembelea, ikiwa ni pamoja na tovuti zinazohusiana.
    • Tuma ombi la "Do not track" kwenye data yako ya kuvinjari: Ukiwasha kitufe hiki, unaomba tovuti zisikufuatilie. Tovuti hutumia hiari yazo ikiwa zitatii ombi. Pata maelezo zaidi kuhusu ombi la "Do Not Track".
    • Chagua tovuti unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine: Unaweza pia kuangalia na kubadilisha tovuti unazoruhusu zitumie vidakuzi vya washirika wengine katika sehemu ya “Tovuti zinazoruhusiwa kutumia vidakuzi vya washirika wengine.” Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuruhusu vidakuzi vya washirika wengine.

Nyenzo zinazohusiana

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu