Kuvinjari kwenye Chrome ukitumia hali ya matumizi ya wageni

Muhimu: Ingia tu katika tovuti nyeti kwenye vifaa vya watu unaowaamini. Wamiliki wa vifaa hivyo wanaweza kuwa na uwezo wa kufikia data yako.

Katika Hali ya matumizi ya wageni, hutaona au kubadilisha maelezo yoyote ya wasifu kwenye Chrome. Unapofunga Hali ya matumizi ya wageni, shughuli zako za kuvinjari zitafutwa kwenye kompyuta.

Tumia Hali ya matumizi ya Wageni kwa:

  • Kuruhusu watu wengine kuazima kompyuta yako au unapoazima kompyuta ya mtu mwingine.
  • Kutumia kompyuta ya umma kama iliyo kwenye maktaba au mkahawa.

Ikiwa ungependa kuvinjari katika hali ya faragha kwenye kompyuta yako, tumia Hali fiche. Utaona maelezo na mipangilio yako bila kuhifadhi historia yoyote ya kuvinjari.

Kufungua Hali ya matumizi ya wageni

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Katika sehemu ya juu kulia, bofya WasifuProfile.
  3. Bofya Mgeni.

Vidokezo:

Kuondoka kwenye Hali ya matumizi ya wageni

Funga dirisha la kuvinjari la Hali ya matumizi ya wageni.

Historia yako ya kuvinjari, vidakuzi na data ya tovuti itafutwa.

Wengine wanaweza kuona maelezo fulani

Hali ya wageni huzuia Chrome isihifadhi shughuli zako za kuvinjari kwenye historia ya eneo lako, lakini unapaswa kuingia tu katika tovuti nyeti kwenye vifaa vya watu unaowaamini. Wamiliki wa vifaa wanaweza kufikia data yako, kama vile shughuli zako na mahali uliko. Data hii pia bado inaweza kuonekana kwenye:

  • Tovuti unazotembelea, ikijumuisha matangazo na nyenzo zinazotumiwa kwenye tovuti hizo
  • Tovuti unazoingia katika akaunti
  • Mwajiri wako, shule au yeyote anayeendesha mtandao unaotumia
  • Mtoa huduma wako wa intaneti
  • Mitambo wa kutafuta
    • Mitambo ya kutafuta inaweza kuonyesha mapendekezo ya utafutaji kulingana na eneo uliko au shughuli katika kipindi chako cha sasa cha kuvinjari katika hali fiche. Ukitafuta kwenye Google, kila wakati Google itakadiria eneo la jumla unakotafutia. Pata maelezo zaidi kuhusu eneo unapotafuta kwenye Google.

Nyenzo zinazohusiana

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6529630761574999171
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
237
false
false