Muhimu: Ingia tu katika tovuti nyeti kwenye vifaa vya watu unaowaamini. Huenda wamiliki wa vifaa hivyo wakawa na uwezo wa kufikia data yako.
Katika hali ya Matumizi ya Wageni, hutapata au kubadilisha maelezo yoyote ya wasifu kwenye Chrome. Ukifunga hali ya Matumizi ya Wageni, shughuli zako za kuvinjari zitafutwa kwenye kompyuta.
Tumia hali ya Matumizi ya Wageni:
- Kuruhusu watu wengine kuazima kompyuta yako au unapoazima kompyuta ya mtu mwingine.
- Kutumia kompyuta ya umma kama iliyo kwenye maktaba au mkahawa.
Ikiwa ungependa kuvinjari katika hali ya faragha kwenye kompyuta yako, Tumia faraghani. Utapata maelezo na mipangilio yako bila kuhifadhi historia yoyote ya kuvinjari.
Kufungua Hali ya matumizi ya wageni
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya Wasifu.
- Bofya Mgeni.
Vidokezo:
-
Ikiwa kuna akaunti ya mtumiaji anayesimamiwa kwenye kompyuta yako, Hali ya matumizi ya wageni haitapatikana wakati wasifu wote usiosimamiwa umefungwa.
-
Hali ya Matumizi ya wageni haipatikani unapotumia Chromebook. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia Chromebook katika hali ya mgeni.
Kuondoka kwenye Hali ya matumizi ya wageni
Funga dirisha la kuvinjari la Hali ya matumizi ya wageni.
Historia yako ya kuvinjari, vidakuzi na data ya tovuti itafutwa.
Wengine wanaweza kuona maelezo fulani
Hali ya wageni huzuia Chrome isihifadhi shughuli zako za kuvinjari kwenye historia ya eneo lako, lakini unapaswa kuingia tu katika tovuti nyeti kwenye vifaa vya watu unaowaamini. Wamiliki wa vifaa wanaweza kufikia data yako, kama vile shughuli zako na mahali uliko. Data hii pia bado inaweza kuonekana kwenye:
- Websites you visit, including the ads and resources used on those sites
- Websites you sign in to
- Your employer, school, or whoever runs the network you’re using
- Your internet service provider
- Search engines
- Search engines may show search suggestions based on your location or activity in your current Incognito browsing session. When you search on Google, Google always estimates the general area that you're searching from. Learn more about location when you search on Google.