Unaweza kubadilisha picha yoyote kwenye intaneti ukitumia Gemini kwenye Chrome.
Unachohitaji
Ili uhariri picha kutoka kwenye wavuti katika Gemini kwenye Chrome katika kompyuta yako, unahitaji:
- Kujijumuisha katika Gemini kwenye Chrome. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupata Gemini kwenye Chrome.
- Kutumia toleo jipya kabisa la Chrome. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kusasisha Chrome.
- Kuingia katika Chrome. Kipengele hiki hakipatikani Faraghani. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuingia katika Chrome.
- Ili utayarishe picha, ni sharti uwe na umri wa miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi uliko) au zaidi.
- Ili uhariri picha, ni sharti uwe na umri wa miaka 18 au zaidi.
Muhimu:
- Tunazindua kipengele hiki kwa utaratibu, kwa hivyo huenda usiweze kukitumia kwa sasa.
- Kwa sasa, huwezi kutumia kipengele hiki ikiwa umeingia katika Akaunti ya Google ya kazini au ya shuleni.
- Ikiwa ungependa kubuni picha zilizowekewa mapendeleo kikamilifu, pata maelezo kuhusu jinsi ya kubuni picha zilizowekewa mapendeleo ukitumia Programu za Gemini.
Kabla ya kutumia kipengele hiki
Unapobuni picha ukitumia Programu za Gemini, kumbuka kuwa ulikubali Sheria na Masharti ya Google, ikiwa ni pamoja na Sera Dhidi ya Matumizi Yasiyokubalika. Hakikisha hukiuki haki za faragha au hakimiliki za wengine. Kuwa mwangalifu kabla ya kutegemea, kuchapisha au kutumia maudhui yanayotayarishwa na Programu za Gemini. Huenda watumiaji walio na akaunti ya kazini au ya shuleni wakasimamiwa na masharti tofauti kulingana na aina ya leseni. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Programu za Gemini kwenye Akaunti yako ya Google ya kazini au ya shuleni.
Kuhariri picha ukitumia Nano Banana
- Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
- Tafuta picha ambayo ungependa kuhariri.
- Bofya kulia kwenye picha
Buni picha ukitumia Gemini.
- Ikiwa hutaona “Buni picha ukitumia Gemini” kwenye picha mahususi, huenda picha hiyo inalindwa au haitumiki.
- Katika Gemini kwenye Chrome, fafanua picha ambayo ungependa kubuni au uchague pendekezo.
Kidokezo: Ili uhifadhi au unakili picha iliyobuniwa, bofya kulia kwenye picha Hifadhi picha kama… au Nakili picha.
Mifano
- Buni upya picha hii bila watu wowote katika mandharinyuma.
- Buni upya picha hii ya kikombe changu kilichotengenezwa kwa mikono kama picha ya kitaalamu ya bidhaa.
- Buni upya picha hii ili uondoe mkwaruzo mdogo kwenye uso wa mjukuu wangu.
- Buni upya picha hii iwe nembo ya vekta kutokana na mchoro huu wa mkono.
Maelezo kuhusu vidokezo vya kubuni picha
- Anza kidokezo chako ukitumia maneno kama vile chora, buni na tayarisha.
- Fafanua muundo wa picha unaopendelea. Ifuatayo ni mifano michache: michoro ya katuni, michoro ya rangi za maji, michoro ya mkaa, inayoonekana kuwa halisi.
- Jumuisha maelezo ya kina ya michoro ambayo ungependa yawe kwenye picha. Maelezo yanaweza kujumuisha kilicho kwenye picha, kitendo kinachofanyika na mandharinyuma au mazingira.