Kutumia programu ya Gemini ya wavuti ili kupata majibu kwenye Chrome

Sasa unaweza kutumia njia ya mkato ya tovuti ya Chrome ili ufikie moja kwa moja programu ya Gemini ya wavuti.

Unachohitaji

Ili uweze kutumia programu ya Gemini ya wavuti, unapaswa:

  • Akaunti ya Google ya binafsi ambayo unaidhibiti mwenyewe. Hutaweza kufikia programu ya Gemini ya wavuti ukitumia Akaunti ya Google inayodhibitiwa na Family Link. Soma Ilani ya Faragha ya Programu za Gemini.
  • Utimize kiwango cha chini cha masharti ya umri ili utumie programu ya Gemini ya wavuti:
    • Kwa nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA), Uswizi na Uingereza: Ni sharti uwe na miaka 18 au zaidi.
    • Kwa nchi nyingine ambapo programu ya Gemini ya wavuti inapatikana: Ni sharti uwe na miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi uliko) au zaidi. Iwapo una chini ya miaka 18, kwa sasa unaweza kutumia programu ya Gemini ya wavuti kwa Kiingereza pekee.

Pata maelezo zaidi kuhusu lugha na nchi ambako unaweza kutumia programu ya wavuti ya Gemini.

Kutumia programu ya Gemini ya wavuti kwenye Chrome

Muhimu: Hutaweza kubadilisha, kufuta au kuweka Gemini kuwa mtambo wako chaguomsingi wa kutafuta.

  1. Kwenye kompyuta yako, fungua Chrome.
  2. Kwenye sehemu ya anwani, weka @gemini.
  3. Bonyeza Tab au Space.
    • Pia, unaweza kuchagua Piga Gumzo na Gemini kwenye mapendekezo.
  4. Weka kidokezo chako.
  5. Bonyeza Enter.

Kidokezo: Unaweza kuzima njia ya mkato ya tovuti ya Gemini kwenye Mipangilio. Jifunze kudhibiti mitambo ya kutafuta na njia za mkato za tovuti.

Nyenzo zinazohusiana

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9603560553633467218
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
237
false
false