Sasa unaweza kutumia njia ya mkato ya tovuti ya Chrome ili ufikie programu ya Gemini ya wavuti moja kwa moja.
Unachohitaji
Ili utumie programu ya Gemini ya wavuti, unahitaji:
- Kuwa na Akaunti ya Google ya binafsi unayoidhibiti mwenyewe. Bado huwezi kufikia programu ya Gemini ya wavuti ukitumia Akaunti ya Google inayodhibitiwa kupitia Family Link. Soma Ilani ya Faragha kwenye Programu za Gemini.
- Uwe na umri wa miaka 13 (au umri unaoruhusiwa katika nchi uliko) au zaidi.
Maelezo ya ziada kuhusu upatikanaji
- Pata maelezo kuhusu nchi na lugha zinazotumika kwenye programu ya Gemini ya wavuti.
- Pata maelezo kuhusu nchi na lugha zinazotumika kwenye programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi.
- Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Programu za Gemini kwenye Akaunti yako ya Google ya kazini au ya shuleni.
- Ili utumie gemini.google.com, unahitaji kuwa na kivinjari kinachotumika: Chrome, Safari, Firefox, Opera au Edgium.
Kutumia programu ya Gemini ya wavuti kwenye Chrome
Muhimu: Hutaweza kubadilisha, kufuta au kuweka Gemini kuwa mtambo wako chaguomsingi wa kutafuta.
- Katika kompyuta yako, fungua Chrome.
- Kwenye sehemu ya anwani, weka
@gemini. - Bonyeza 'Tab' au 'Space'.
- Pia, unaweza kuchagua Piga Gumzo na Gemini kwenye mapendekezo.
- Weka kidokezo chako.
- Bonyeza Enter.
- Ili upate jibu, utaelekezwa kwenye gemini.google.com.
Kidokezo: Unaweza kuzima njia ya mkato ya tovuti ya Gemini kwenye Mipangilio. Fahamu nama ya kudhibiti mitambo ya kutafuta na njia za mkato za tovuti.