Unaweza kuhifadhi nakala ya maudhui, data na mipangilio iliyo kwenye simu yako katika Akaunti yako ya Google. Unaweza kurejesha nakala ya maelezo uliyoyahifadhi kwenye simu uliyotumia kuhifadhi au katika simu nyingine ya Android. Huwezi kuhifadhi nakala unapowekea kifaa chako binafsi mipangilio ukitumia wasifu wa kazini au kwa madhumuni ya kazi au unapoweka mipangilio kwenye kifaa kinachomilikiwa na kampuni.
Kurejesha data kunatofautiana kulingana na simu na toleo la Android. Huwezi kurejesha nakala kutoka toleo jipya zaidi la Android hadi kwenye simu inayotumia toleo la awali la Android.
Muhimu: Baadhi ya hatua hizi hutumika tu kwenye Android 9 na matoleo mapya zaidi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia toleo la Android unalotumia.
Mahali data ya simu huhifadhiwa
Jinsi tunavyolinda data yako
Data yako husimbwa kwa njia fiche ili kusaidia ihifadhiwe kwa njia salama.
- Data yote, ikiwa ni pamoja na picha, video, ujumbe na mengineyo husimbwa kwa njia fiche unapoihamisha kati ya kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data.
- Baadhi ya data husimbwa zaidi kwa njia fiche kwa kutumia kipengele cha kufunga skrini kwenye kifaa chako. Picha na video katika huduma ya Picha kwenye Google na maudhui ya MMS uliyopokea kutoka kwa mtoa huduma wako, husimbwa kwa njia fiche kwa kutumia kipengele cha kufunga skrini kwenye kifaa chako.
Kuhifadhi nakala ya data iliyo kwenye kifaa chako kiotomatiki
Muhimu:
- Ili kusaidia kulinda nakala ya data uliyohifadhi, tumia PIN, mchoro au nenosiri kufunga skrini, badala ya kutelezesha kidole au Smart Lock.
- Unaweza kuhifadhi nakala ya hadi GB 15 za nafasi ya hifadhi bila kulipa kwenye akaunti yako ya Google. Unaweza pia kupata nafasi zaidi ya hifadhi ukitumia akaunti ya Google One baadaye.
Unaweza kuwekea simu yako mipangilio ihifadhi nakala za faili zako kiotomatiki.
- Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa chako.
- Gusa Huduma za Google
Huduma zote.
Kidokezo: Chagua data ambayo ungependa kuhifadhia nakala: Picha na video, Data ya kifaa au zote mbili. - Washa au uzime Hifadhi nakala.
Mchakato wa kuhifadhi nakala kwenye Google One unaweza kuchukua hadi saa 24. Data yako ikihifadhiwa, utaona ishara ya “Imewashwa” chini ya aina za data ulizochagua.
Kuweka akaunti ya kuhifadhi nakala
- Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa kwenye kifaa chako cha Android.
- Gusa Google
Huduma zote.
- Katika sehemu ya “Kuhifadhi nakala na kurejesha data,” gusa Hifadhi nakala.
- Utaombwa uingie katika akaunti yako iwapo hukuwa umeingia.
- Iwapo unahifadhi nakala katika akaunti tofauti:
- Gusa Nafasi ya hifadhi ya akaunti.
- Panapohitajika, weka PIN, mchoro au nenosiri la kifaa chako.
- Ingia katika akaunti ambayo ungependa kuweka.
Kubadilisha kati ya akaunti za kuhifadhi nakala
- Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa kwenye kifaa chako cha Android.
- Gusa Google
Huduma zote.
- Katika sehemu ya “Kuhifadhi nakala na kurejesha data,” gusa Hifadhi nakala
Nafasi ya hifadhi ya akaunti.
- Gusa akaunti ambayo ungependa kutumia kuhifadhi nakala.
Nakala ya data ya simu yako huhifadhiwa kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google. Hii ni pamoja na:
- Programu na data ya programu
- Rekodi ya simu zilizopigwa
- Anwani
- Mipangilio kwenye kifaa
- Ujumbe wa MMS na SMS
Nakala ya data ya ziada huhifadhiwa unapotumia programu mahususi ya Google:
- Ujumbe wa RCS unapotumia Google Messages
- Mipangilio ya kupiga simu na namba ulizozuia unapotumia Programu ya Simu kutoka Google
- Picha na video unapotumia huduma ya Picha kwenye Google
Pata maelezo kuhusu kinachotokea unapohifadhi nakala ya picha au video.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuhifadhi nakala ya faili na folda katika Hifadhi ya Google.Kuhifadhi nakala ya data na mipangilio mwenyewe
- Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa kwenye kifaa chako cha Android.
- Gusa Google
Huduma zote.
- Katika sehemu ya “Kuhifadhi nakala na kurejesha data,” gusa Hifadhi nakala
Hifadhi nakala sasa.
Kufuta data yote baada ya kuhifadhi nakala
Kuhamishia data yako kwenye kifaa kipya
Una chaguo la kurejesha ulichokuwa umekihifadhia nakala kwenye Akaunti yako ya Google katika simu ambayo tayari umeiwekea mipangilio unapoweka Akaunti husika ya Google kwenye simu hiyo.
Fuata hatua zilizo kwenye skrini ili urejeshe akaunti uliyohifadhia nakala kwenye simu uliyowekea mipangilio upya. Pata usaidizi kutoka kwa mtengenezaji wa kifaa chako ukihitaji.
Picha na video zako zipo tayari kwenye huduma ya Picha kwenye Google. Lakini unaweza kurejesha data iliyosalia ambayo ulihifadhia nakala wakati unawekea simu yako mipangilio kwa mara ya kwanza au baada ya kurejesha mipangilio iliyotoka nayo kiwandani. Fuata hatua zilizo kwenye skrini urejeshe data yako unapoweka mipangilio.
Mchakato huu unaweza kuchukua hadi saa 24 kukamilika.
Muhimu: Ni lazima vifaa vyote viwili viwe vinatumia toleo lile lile la Android au kifaa chako kipya lazima kiwe kinatumia toleo jipya zaidi la Android. Ikiwa kifaa chako kipya kinatumia toleo la zamani zaidi la Android kuliko kifaa chako cha awali, hali hii inaweza kusababisha mchakato wa kuhamisha data usikamilike. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia na kusasisha toleo unalotumia la Android.
Kuangalia nakala ulizohifadhi za picha, data na mipangilioUnaweza kuangalia data na programu ambazo zimejumuishwa katika nakala uliyohifadhi.
- Fungua programu ya Mipangilio ya kifaa chako.
- Gusa Huduma za Google
Nakala.
- Kagua data uliyohifadhi nakala yake kwenye kifaa chako katika sehemu ya “Maelezo ya nakala”.
Anwani kwenye Google zitasawazisha kiotomatiki iwapo ulikuwa umezihifadhi katika Akaunti yako ya Google. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kurejesha anwani mwenyewe iwapo una anwani nyingine kwenye simu au SIM kadi.
Jinsi Google hushughulikia data yako
Muhimu: Data ambayo Google hukusanya husimbwa kwa njia fiche inapotumwa.
Data unayohifadhia nakala hutumwa kwenye seva za Google na hukuwezesha kuhamisha data kutoka kifaa kimoja hadi kingine. Google hukusanya maelezo fulani ili itekeleze huduma kwenye kifaa chako. Baadhi ya vipengele hivi hutumia huduma za Google Play. Kwa mfano, nakala hukusunya:
- Ujumbe, anwani, mipangilio ya programu na mapendeleo hukusanywa kama sehemu ya nakala yako binafsi.
- Vitambulishi binafsi hukusanywa ili kuhakikisha kuwa nakala unazohifadhi zinahusishwa nawe na akaunti yako.
- Rekodi za matukio ya kuacha kufanya kazi na uchunguzi hukusanywa kwa madhumuni ya uchanganuzi na utatuzi.
Kuzima mipangilio ya kuhifadhi nakala
Ili kuzima kipengele cha kuhifadhi nakala:
- Gusa Mipangilio
Google
Huduma zote.
- Katika sehemu ya “Kuhifadhi nakala na kurejesha data,” gusa Hifadhi nakala.
- Zima Hifadhi nakala kwenye Google One.