Mtambo wako wa kutafuta hukuwezesha kutafuta kwenye wavuti katika skrini ya kwanza au kivinjari chako. Pata maelezo kuhusu skrini ya uteuzi kwenye Android
Kubadilisha mtambo wako wa kutafuta
Kwenye kifaa cha Pixel
Muhimu: Maagizo yaliyo hapa chini yanatumika tu kwenye Nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA).
- Kwenye Simu ya Pixel au kishikwambi chako, gusa na ushikilie upau wa kutafutia katika skrini yako ya kwanza.
- Gusa Mipangilio
Mtambo wa kutafuta.
- Chagua programu ya mtambo wa kutafuta ambao ungependa kutumia.
Kwenye kifaa cha Android
- Kwenye kifaa chako cha Android, gusa na ushikilie nafasi tupu katika skrini yako ya kwanza.
- Gusa Wijeti
.
- Chagua programu ya mtambo wako wa kutafuta unaopendelea.
- Gusa na ushikilie kisha uburute mtambo huo wa kutafuta hadi kwenye skrini yako ya kwanza.
- Ikiwa hutapata mtambo wa kutafuta unaotaka kutumia, uweke kutoka kwenye Duka la Google Play.
Kwenye kifaa cha Android kupitia mipangilio ya Chrome
- Kwenye kifaa chako cha Android, fungua Chrome
.
- Gusa Zaidi
Mipangilio
.
- Katika sehemu ya “Mambo msingi,” chagua Mtambo wa kutafuta.
- Chagua mtambo wa kutafuta unaotaka kutumia kwenye Chrome.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mtambo chaguomsingi wa kutafuta.