Zana na huduma za mshirika mwingine

Kumbuka: Huduma zilizo kwenye orodha hii zinatolewa na mshirika mwingine, Google haiwezi kukuhakikishia ubora wa huduma wala kukusaidia kuhusu mzozo wowote unaoweza kutokea kati yako na mtoa huduma. Pia, orodha hii si ya kina na haionyeshi kuwa Google ina uhusiano wowote rasmi na watoa huduma hawa. Ni hiari kushiriki katika orodha hii ya watoa huduma.

Unaweza kudhibiti manukuu, tafsiri na mahitaji yako ya manukuu ukitumia zana na huduma za wengine. Zana na huduma hizi za wengine zinasimamiwa na sheria na masharti yao ambayo unapaswa kusoma na kuelewa.

Watoa huduma za manukuu

Kampuni Maelezo
3Play Media 3Play Media ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya 3Play Media ili upate maelezo zaidi.
Amara Amara ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video (Amara On Demand) na zana zinazosaidia kudhibiti michango ya jumuiya (Amara Community). Angalia makala haya kwenye tovuti ya Amara ili upate maelezo zaidi.
Cielo24 Cielo24 ni mtoa huduma za manukuu yenye maelezo na huduma za ufikivu wa video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Cielo24 ili upate maelezo zaidi.
Rev

Rev ni mtoa huduma za manukuu na huduma za ufikivu za video za mtandaoni. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Rev ili upate maelezo zaidi.

Amberscript Amberscript hutoa huduma za manukuu yenye maelezo, manukuu yaliyotafsiriwa, maelezo ya sauti na kuweka sauti nyingine kwenye maudhui. Kwa kujumuisha akiliunde na timu ya zaidi ya wataalamu 1000 wa lugha, Amberscript hutoa manukuu ya kitaalamu kwa gharama ndogo tu. Angalia hapa ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuweka manukuu kwenye video yako ya YouTube au angalia tovuti ya Amberscript ili upate huduma za ziada.

Watoa huduma za kuweka sauti nyingine kwenye maudhui

Kampuni Maelezo
Creator Global CreatorGlobal ni mtoa huduma za kuweka sauti nyingine iliyotafsiriwa kwenye maudhui inayowasaidia watayarishi kuwa magwiji wa kimataifa kwa kujanibisha maudhui yao na kukuza chaneli zao katika masoko mapya. Angalia tovuti ya Creator Global ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Air.io

AIR hutoa huduma tofauti za tafsiri na ujanibishaji kwa WanaYouTube katika zaidi ya lugha 50: kuanzia manukuu yenye maelezo, tafsiri, ujanibishaji, uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui unaofanywa na binadamu au AI hadi chaneli za YouTube ambazo zimeshatafsiriwa na kujanibishwa. Angalia makala haya kwenye tovuti ya AIR ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.

Papercup Teknolojia ya Papercup ya uwekaji sauti nyingine iliyotafsiriwa kwenye maudhui inayotumia AI hutoa huduma za uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui kwa bei nafuu na ubora wa huduma hizo hukaguliwa na wafsiri. Sauti za Papercup zilizobuniwa na kompyuta zimechangia utazamaji wa mamilioni ya maudhui kwenye YouTube. Angalia tovuti ya Papercup ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
VITAC

VITAC, Kampuni ya Verbit, ni mtoa huduma za uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui, manukuu na tafsiri katika sekta ya vyombo vya habari. Inatoa huduma hizo kwa kampuni zote kuu za utayarishaji wa maudhui ya televisheni, Chaneli na Watayarishi wa Maudhui ya YouTube kote duniani. Angalia tovuti ya VITAC ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.

Vidby Vidby ni programu inayotumia AI ili kutafsiri na kuweka sauti nyingine katika video kwa haraka, kwa bei nafuu na usahihi wa asilimia 100 katika lugha 75 na lahaja 65. Ina maktaba ya sauti mbalimbali (ikijumuisha za watoto, vijana, watu wazima na wakongwe) unazoweza kuchagua. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Vidby ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
WellSaid Labs WellSaid Labs ni mtoa huduma wa sauti zilizobuniwa na kompyuta anayeongoza kwenye sekta, ambaye anaaminiwa na maelfu ya kampuni kote duniani. Angalia tovuti ya WellSaid Labs ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Shorthand Studios Shorthand Studios ni mtoa huduma za kisasa kwa watayarishi wanaoangazia dijitali kwanza walio na uwezo wa hali ya juu wa kutafsiri. Studio hiyo inatoa huduma za kuweka sauti nyingine kwenye maudhui katika zaidi ya lugha 20 kwenye chapa maarufu za kisasa. Angalia tovuti ya Shorthand Studios ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Deep Media Deep Media hutoa huduma za tafsiri na uwekaji sauti nyingine kwenye maudhui bila malipo kwa kutumia DubSync. Zana hii ya kimapinduzi inayotumia AI huondoa vizuizi vya lugha kwa haraka na urahisi katika zaidi ya lugha 20. Angalia tovuti ya Deep Media ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
XTracks XTracks hutoa huduma za ubora wa juu za Kuweka sauti nyingine na Maelezo ya Sauti kwenye maudhui ili kujanibisha maudhui yako na kuyafanya yafikiwe na hadhira za vipofu na wenye uwezo mdogo wa kuona. Angalia tovuti ya XTracks ili upate maelezo zaidi.
Ollang Ollang ni mfumo unaotoa huduma zote za ujanibishaji. Unatoa huduma za manukuu ya kawaida, manukuu yenye maelezo, uwekaji wa sauti nyingine kwenye maudhui kwa ubora wa juu unaofanywa kwenye studio na kwa kutumia AI kwa watayarishi, televisheni, filamu na mifumo ya mafunzo ya kielektroniki. Angalia tovuti ya Ollang ili upate maelezo zaidi na utume maswali hapa.
Dubverse

Dubverse.ai hutoa huduma ya muda halisi inayotumia AI ya Uwekaji Sauti Nyingine kwenye Video na Manukuu katika zaidi ya lugha 30 na mfumo wa kujihudumia, kuanzia toleo la BILA MALIPO lililoubuniwa kwa ajili ya watayarishi. Angalia makala haya kwenye tovuti ya Dubverse.ai ili upate maelezo zaidi.

Camb.AI Camb.AI hutumia teknolojia inayomiliki na yenye hakimiliki inayotumia AI kunasa na kuhamisha, katika muda halisi, urekebishaji wa sauti na muktadha wa matamshi, ili kuhakikisha hali za utumiaji ambazo ni halisi na rahisi kwa uhamishaji kamili wa utendaji kwenye video za wazungumzaji wengi, hata katika mazingira yenye sauti tulivu. Ikiwa na zaidi ya lugha 100, lafudhi 30 na lahaja 40, Camb.ai inatumika kama mbinu ya kuwawezesha watayarishi wa maudhui kufikia hadhira ya kimataifa. Angalia tovuti ya Camb.AI ili upate maelezo zaidi au utume maswali hapa.
Dubly.AI Dubly.AI huwapa watayarishi wa maudhui na biashara suluhisho bora zaidi la kutafsiri video zao kwa usahihi wa asilimia 100. Dubly.AI hutoa mpango wa punguzo maalum kwa watayarishi wa YouTube. Tembelea tovuti ya Dubly.AI ili upate maelezo zaidi au tuma swali lako hapa.
ElevenLabs ElevenLabs hushirikiana na kampuni za burudani na watayarishi maarufu kutafsiri na kuweka sauti nyingine kwenye maudhui, ili kuhakikisha kuwa yanaweza kufurahiwa katika lugha yoyote huku yakidumisha mtindo wa sauti asili. ElevenLabs hutoa uwekaji wa kiotomatiki wa sauti nyingine kwenye maudhui katika lugha 29 na hutoa usaidizi mahususi kwa WanaYouTube maarufu. Ijaribu leo bila malipo katika tovuti ya ElevenLabs au ujisajili ili upate usaidizi wa kipekee na wa kiwango cha juu hapa.
MadLove MadLove inajikita katika masuala ya lugha, ufikiaji na uunganishaji. Inatoa maelezo ya sauti yanayolenga wasioona, uwekaji wa sauti kwenye maudhui unaoiga maneno na unaozingatia tamaduni na kuunganisha hadhira za kimataifa na maudhui yenye maana na yanayozingatia muktadha. Ili upate maelezo zaidi kuhusu mradi wako, angalia tovuti ya MadLove au utume maswali hapa.

Kuondoa ufikiaji wa washirika wengine

Ikiwa hutaki tena ufikiaji wa washirika wengine kwenye akaunti yako ya Google, unaweza kuuondoa wakati wowote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5211953197933647866
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false