Faili ya manukuu ina maandishi ya mambo yanayosemwa kwenye video. Pia inaonyesha muda ambapo kila mstari wa maandishi unapaswa kuonyeshwa. Baadhi ya faili pia zina maelezo ya nafasi na muundo, ambayo ni muhimu kwa watazamaji viziwi au walio na matatizo ya kusikia. Angalia aina za faili zinazoweza kutumika kwenye YouTube hapo chini.
Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuunda faili za manukuu, tunapendekeza utumie mojawapo ya aina zifuatazo za faili:
Jina la muundo | Kiambishi cha faili | Maelezo zaidi |
---|---|---|
SubRip | .srt | Unaweza tu kutumia matoleo ya msingi ya faili hizi. Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi. Ni lazima faili iwe katika maandishi dhahiri ya UTF-8. |
SubViewer | .sbv au .sub | Unaweza tu kutumia matoleo ya msingi ya faili hizi. Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi. Ni lazima faili iwe katika maandishi dhahiri ya UTF-8. |
MPsub (manukuu ya MPlayer) | .mpsub | Kigezo cha "FORMAT=" kinaweza kutumika. |
LRC | .lrc | Maelezo ya muundo (lebo) hayatambuliwi, lakini muundo ulioboreshwa unaweza kutumika. |
Videotron Lambda | .cap | Kimsingi, aina hii ya faili hutumiwa kwenye manukuu ya Kijapani. |
Ikiwa ni mara yako ya kwanza kuunda faili za manukuu, huenda ukahitaji kutumia SubRip (.srt) au SubViewer (.sbv). Miundo hiyo inahitaji tu maelezo ya msingi ya muda na unaweza kuihariri kwa kutumia programu yoyote ya kuhariri maandishi dhahiri.
Tofauti kuu kati ya faili za SubRip na SubViewer ni muundo wa wakati wa kuanza na kukamilika kwa manukuu. Ifuatayo ni mifano ya miundo yote miwili:
Mfano wa SubRip (.srt)1
00:00:00,599 --> 00:00:04,160
>> Fatuma: Hujambo, jina langu ni Fatuma Abdi na huyu ni Juma Hassan
2
00:00:04,160 --> 00:00:06,770
>> Juma: na sisi ndio wamiliki wa Tanuri Mikate ya Abdi.
3
00:00:06,770 --> 00:00:10,880
>> Fatuma: Leo tutawafundisha jinsi ya kutengeneza
biskuti zetu maarufu zenye vipande vya chokoleti!
4
00:00:10,880 --> 00:00:16,700
[muziki wa utangulizi]
5
00:00:16,700 --> 00:00:21,480
Sawa, kwa hivyo tayari tuna viungo vyote hapa
0:00:00.599,0:00:04.160
>> Fatuma: Hujambo, jina langu ni Fatuma Abdi na huyu ni Juma Hassan
0:00:04.160,0:00:06.770
>> Juma: na sisi ndio wamiliki wa Tanuri Mikate ya Abdi.
0:00:06.770,0:00:10.880
>> Fatuma: Leo tutawafundisha jinsi ya kutengeneza
biskuti zetu maarufu zenye vipande vya chokoleti!
0:00:10.880,0:00:16.700
[muziki wa utangulizi]
0:00:16.700,0:00:21.480
Sawa, kwa hivyo tayari tuna viungo vyote hapa
Tumia aina hizi za faili ikiwa ungependa kuwa na udhibiti zaidi wa muundo (lebo) au nafasi ya kuweka manukuu yako.
Jina la muundo | Kiambishi cha faili | Maelezo zaidi |
---|---|---|
SAMI (Synchronized Accessible Media Interchange) | .smi au .sami | Mihuri ya wakati, maandishi na lebo rahisi pekee (<b>, <i>, <u> na color= attribute within a <font>) zinaweza kutumika. Huwezi kuweka nafasi ya manukuu. |
RealText | .rt | Mihuri ya wakati, maandishi na lebo rahisi pekee (<b>, <i>, <u> na color= attribute within a <font>) zinaweza kutumika. Huwezi kuweka nafasi ya manukuu. |
WebVTT | .vtt | Katika utekelezaji wa kwanza. Unaweza kuweka nafasi ya manukuu, lakini unaweza tu kutumia muundo wa <b>, <i>, <u> kwa sababu majina ya aina za vipengee vya CSS bado hayajasawazishwa. |
TTML (Timed-Text Markup Language) | .ttml | Katika utekelezaji usio kamili. Viendelezi vya SMPTE-TT vinaweza kutumika kwenye vipengele vya CEA-608. Unaweza kutumia aina ya faili ya iTunes Timed Text (iTT); iTT ni sehemu ya TTML, Toleo la 1.0. Unaweza kubainisha muundo na nafasi ya manukuu. |
DFXP (Distribution Format Exchange Profile) | .ttml au .dfxp | Aina hizi za faili hufasiriwa kama faili za TTML. |
Kwa kawaida aina hizi za faili hutumiwa kwenye manukuu ya maudhui ya utangazaji (televisheni na filamu) na zinaruhusu viwango vya CEA-608 au EBU-STL. YouTube hujaribu kuonyesha manukuu kutoka kwenye faili hizi kana kwamba yako kwenye runinga — kwa kutumia muundo, rangi na nafasi sawa.
Jina la muundo | Kiambishi cha faili | Maelezo zaidi |
---|---|---|
Manukuu ya Scenarist | .scc | Faili hizi zina uwakilishaji halisi wa data ya CEA-608, ambao ndio muundo unaopendelewa wakati manukuu yanategemea vipengele vya CEA-608. |
EBU-STL (mfumo wa jozi) | .stl | Kiwango cha Shirika la Utangazaji la Ulaya. |
Caption Center (mfumo wa jozi) | .tds | Inaruhusu vipengele vya CEA-608. |
Captions Inc. (mfumo wa jozi) | .cin | Inaruhusu vipengele vya CEA-608. |
Cheetah (maandishi ya ASCII) | .asc | Inaruhusu vipengele vya CEA-608. |
Cheetah (mfumo wa jozi) | .cap | Inaruhusu vipengele vya CEA-608. |
NCI (mfumo wa jozi) | .cap | Inaruhusu vipengele vya CEA-608. |